Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kwa kweli maamuzi yaliyofanywa na kamati ilyoundwa kufuatilia suala la matokeo mabovu ya kidato cha nne yalikuwa ni ya kukurupuka, na yalifanywa bila kufikiriwa sawasawa. Najaribu kuwaza concept ya kustandardize matokeo, ni kwa faida ya nani? Kujifurahisha kwa kuona tunarekodi za vijana wengi waliofaulu bila kuzingatia ubora wa elimu na uwezo wa hao wanafunzi wenyewe? Si haya aliyosema Richard Mabala kuwa ni sawa na kupanua goli ili mtu afunge!!! Haya ni Maamuzi yasiyo na tija. Nampongeza sana Prof. Mkandala kama kweli atasimamia msimamo huo.

Tatizo la matokeo mabaya haliko kwenye kustandardize wala hizo grades mpya, tatizo ni mfumo mbovu wa elimu nchini. Na matatizo haya si mageni, maana yalishazungumzwa sana. Matatizo ni kama kukosa nyenzo za kufundishia, uhaba wa walimu, uhaba wa vifaa vya maabara, maslahi duni ya walimu, mazingira magumu ya kufundishia, ukosefu wa majengo ya kutosha, ubovu na uchakavu wa madarasa na nyumba za walimu, nk nk
Serikali ilipaswa iyatatue haya na si kukimbilia kkwenye kufuta matokeo na kustandardize matokeo maana matokeo haya ni kuwa na WASOMI wasio wasomi ambao kimsingi NDIYO hao wanaotuletea MATATIZO kwenye hii SERIKALI yetu ya sasa. Baadhi ya viongozi wetu ni vihiyo wa kutupwa, wana PHD ama Masters za magumashi na matokeo yake ndiyo haya kukurupuka kutoa maamuzi ambayo hayana tija kwa watanzania.

mkuu umenifanya nicheke sana hapo kwenye bold!!!ndiyo tanzania,yani vitu vinafanyika kwa kuangalia leo tuu,ya kesho yatapangwa muda huo huo ukifika
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)
Kwa hiyo tunafurahi hawa watoto wakafanye kazi za u house girl na house boy,na shamba boy?Na pia waew vibaka ,ukipaki gari yako uibiwe vitu vya gari?fikirieni sana.
 
Wakikubali matakwa ya Serikali yatimie hawa ndg tena wasomi wazuri hatakuwa wamewatendea haki watanzania na pia watakuwa hawajazitendea haki elimu/taaluma zao walizonazo, labda wakubali kuachia hizo nafasi walizonazo ili aje mtu mwingine mbadala afanye huo ushenzi wa kukachachua elimu.

Ni upuuzi mtu, hata mahakamani unapokata rufaa juu ya hukumu ya kesi usiyolizika na maamuzi yake shauri linapelekwa mahakama ya juu kuliko ile iliyoamua awali na huko hupangiwa hakimu ama jaji mwingine ili aweze kuwa huru kufanya uamuzi sahihi, ifikie hatua kwenye elimu hawa serikali walijue hilo pia.

Hata appeal za mitihani ya hao baraza japo wasihihishaji ni walimu, lakini hutafutwa walimu ambao hakushiriki zoezi la awali na hata vyuo vya elimu ya juu inapokuwepo appeal anatafutwa mwl mwingine tofauti na yule ambaye ni subject master na mara nyingine hadi mwalimu toka chuo tofauti.

Kama serikali wangetaka maana wanajua kutumia ovyo pesa zetu za kodi kwa vile wameshindwa kuwa na imani na Baraza la mtihani la taifa ambalo sisi watanzania wa kawaida tuna imani nalo bado watumie watangaze tenda kimataifa baraza lolote ta taifa lolote litakaloshinda lije kufanya huo upuuzi wanaoulazimisha ufanyike kwa maslahi ya kisiasa.

CCM mnaleta siasa hadi kwenye elimu, kweli mmefilisika kabisa, fanyenyi kazi zenu za siasa, na mwacheni wataalamu/wanataaluma wafanye kazi zao, msiwaingilie, bali mwawezeshe wafanye kazi zao kwa maslahi ya umma wa Tanzania.

Mnasosoneka nini ili hali hakuna mtoto wenu aliyefeli, waliofeli ni watoto wa walalahoi acheni tuwahukumu, maana mnachotaka kufanya ni kuendelea kuwaibia watanzania maskini kwa udanganyifu kuwa kulikuwa na makosa, ili hata mtoto aliyepata div IV kwa matokeo ya awali ionekane ana II, ama III, na ataendelea na masomo ya juu baada ya miaka miwili tena anafanya mtihani wa kidato cha sita anapata ziro, pesa ya mzazi imepotea, muda umepotea, kodi za wananchi zimepotea, na umasikini unazidi kwa familia husika.

Msiwaongezee watanzania mzigo kwa maamuzi ya kipuuzi kama hayo.

Prof. Mkandala linda heshima kidogo uliyonayo kwa jamii, wewe ni Prof wa ukweli, popote pale duniani unafanya kazi, kuwa Mtanzania mzalendo, usiamua kisiasa bali kitaaluma zaidi.

Dr. Ndalichako, jamii ya watanzania walio wengi, wako nyuma yako, hata wenye watoto wenye ziro kitaaluma wanajua hilo, msiyumbishwe na siasa, timiza wajibu wako, ukiona yanakushinda bwaga manyanga waachie baraza lao, wakikunyima kazi serikalini hata walipokutoa, zipo sekta binafsi kwa fani yako ndani na nje ya nchi, utapokelewa.

...ndo kwaaaanza mziki unaanza,hata korasi bado kabisaaa....
 
Ingawa huyu Prof simkubali kwa jinsi anavyoifanya UDSM, lakini kwa hili niko naye 100%! I salute him for this kama ni kweli.

kwa hiyo unafurahi ndugu na watoto wetu,wawe ma house girl na houseboy,kwenye majumba ya wenye nazo?Mbona ziko nchi hawakubali kwa njia yoyote watoto na ndugu zao kuwa na kazi hizi?Wanaagiza wafanyakazi wa ndani toka nchi nyongine?
Au twataka tuongeze idadi ya vibaka?mkivamiwa msilalmike,mtu asiyekuwa na shughuli au kazi ya kufanya,lazima atajiingiza kwenye makundi mabaya.
 
Tupo ngomani na inabidi kucheza mwisho wa siku wachezaji watakuwa hooooi!ccm mnatupeleka wapi kielimu
 
Kwa hiyo tunafurahi hawa watoto wakafanye kazi za u house girl na house boy,na shamba boy?Na pia waew vibaka ,ukipaki gari yako uibiwe vitu vya gari?fikirieni sana.

Mkuu mpaka sasa hatuko salama,maana huko ndiko serikali ya ccm imeamua kutupeleka,kwani
ukimpeleka mtoto mbele wakati hastahili utakuwa umemsaidia?ningewaona wana akili kama wangeshauri hawa
waliofeli warudie mwaka kwa ada ileile then wakafundishwa kwa uangalifu na usimamizi mzuri ingesaidia
 
Mukandala anahusika vipi na matokeo ya olevel? au wameenda kuomba ushauli senet ya udsm? Hueleweki!
......mbona Huelewi wewe! ushaambiwa mukandala ni mwenyikiti wa baraza.ndo mana mnafeli mitihani unakurupuka tu kucomment bila kuzingatia content ya uzi.
 
Akiachia ngazi Ndalichako itakuwa sawa na Kuvuja kwa Pakacha. Huyu mama amelalamikiwa sana, hata kama ni mtendaji mzuri lakini lawama zikizidi ni bora kutafuta ustaarabu mwingine. Mbona elimu yake ni nzuri tu aachane na hiyo kazi ya NECTA ni kama imemshinda vile. Sifa ya kiongozi mzuri ni pamoja na ku_manage Public Relations

Hapo umejichanganya......ila ni vizuri ajiuzulu kulinda heshima yake
 
Anakataa kwa sheria ipi?

Sheria yetu (mbovu) ndio inayompa mamlaka waziri kutoa maagizo (hata ya kisiasa kwenye mambo ya taaluma) kwa baraza la mitihani na kwa mujibu wa sheria hiyo (s 20, Necta Act 1973) baraza linalazimika kutekeleza maagizo hayo!
Mkuu, kwanza Mukandala hawezi kukataa hata kama kungekuwa hakuna sheria.
Hawezi, nasema hawezi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Sawa willy
 
Wabongo macho yanazidi kututoka juu ya hili, Kama wanataka kutoa max za bure inafuta maana ya kuwa na mitihani na kupoteza rasilimali kibao zinazohusu uandaaji, usahihishaji mpaka kuyatoa kama hali ndio hii.

Hata hivyo Tanzania wataalamu hao hao kina Mukandala ndio waliokubali kutumiwa kisiasa kwa miaka kadhaa leo wanagoma nini, na kama hawakutaka kutumiwa hivyo kwa nini walikuwa mstari wa mbele. Akamuulize Kitilya amekuwa na msimamo kwa maswala yote yanayoenda kinyume bila kujali msemaji ni nani na kwa maslahi ya nani.
 
Hapo umejichanganya......ila ni vizuri ajiuzulu kulinda heshima yake
Mkuu kusema ''hata kama ni mtendaji mzuri'' ina maanisha sina uhakika. Maoni yangu yametokana na kiwango kikubwa cha yeye kulalamikiwa, sifahamu sana juu ya utendaji wake.

Na wenzangu wale wa Kwa Mtoro ndio hawataki kabisa kumsikia
 
kwa hiyo unafurahi ndugu na watoto wetu,wawe ma house girl na houseboy,kwenye majumba ya wenye nazo?Mbona ziko nchi hawakubali kwa njia yoyote watoto na ndugu zao kuwa na kazi hizi?Wanaagiza wafanyakazi wa ndani toka nchi nyongine?
Au twataka tuongeze idadi ya vibaka?mkivamiwa msilalmike,mtu asiyekuwa na shughuli au kazi ya kufanya,lazima atajiingiza kwenye makundi mabaya.

Mkuu get the BIG PICTURE, hao watoto hawajui, wanahitaji kuelimishwa/kufundishwa na kuweza kufaulu. So kuwaongezea marks sio solution. Kwani huwaoni mtaani wewe hawa vijana wa siku hizi. Serikali is working on the wrong goal post badala ya kutatua tatizo la msingi. I cant believe kwamba Serikali is that stupid not to see the basic problem.
 
Aksante Prof.Mukandara,huo ndo msimamo wa kiongozi anaejiamini aisee..tusilete masihala kwene sekta ya Elimu,kama mnaona matokeo yanashusha hadhi ya nchi mngelifanyia kazi kabla!! Tujifunze kuprevent na sio kutibu akati uwezo tulikua nao aisee.....

"Tusitaniane kwene elimu nyakati kama hizi"
 
Mkuu get the BIG PICTURE, hao watoto hawajui, wanahitaji kuelimishwa/kufundishwa na kuweza kufaulu. So kuwaongezea marks sio solution. Kwani huwaoni mtaani wewe hawa vijana wa siku hizi. Serikali is working on the wrong goal post badala ya kutatua tatizo la msingi. I cant believe kwamba Serikali is that stupid not to see the basic problem.
Hebu tupeaneni ushauri,inauma sana kumuona ndugu yako,mtanzania mwenzako,yuko kwenye ajira ya kunyanyasika,au akawa kibaka,tuwasaidie hawa watoto,ni wengi,nilifurahi serekali iliposhisha kiwango cha ufaulu darasa la saba,angalau tupunguze ajira za watoto za u house girl na u house boy nk,pamoja na vibaka.bila kazi maisha magumu ndugu zanguni,wa Tanzania wenzangu.
 
Hoja kuu mwanzo ilikuwa ni UJANGILI, jamaa wakatuamisha ghafla mpaka kwenye hoja ya MATOKEO YA KIDATO CHA IV na hatimaye wote tukailukia kwa nguvu zote, Baad ya hapo tukahamia hoja ya UGAIDI WA ARUSHA na tukasahua hoja ya matokeo ya kidato cha IV, sasa baada ya serkali kuboronga hoja ya Arusha na kuwataja wagalitia ndo wamehusika, Basi Jamaa wameamua tena kutuhamishia tena kuhusu NECTA na Mkandara.

Hii nchi hadi raha kwa bongo movie zake.
 
Back
Top Bottom