Bubu Msemaovyo
Platinum Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,552
Huyu jamaa maelezo yake yanaonesha wakati akisoma alikua ni wale ambao combination aliitafuta kwa tochi (kama alifanikiwa kufikia hatua ya kupata hiyo combination), vinginevyo namuona kama alifanikiwa kuipata angalau div IV ni kwa bahati sana. Kwa upande mwingine namuona ni walewale wenye kulalamikia Baraza la mitihani la Taifa (NECTA) na mambo ya kimfumo.
Hizo seminary anazozitaja kwamba watoto wa Ndalichako au Mkandala wanasoma!!!, ni seminary zipi? mbona kuna shule zenye majina ya seminary zinaangukia pua kuliko hata zisizo na majina hayo? au anataka kutuaminisha kwamba wamiliki wa hizo ''seminary'' zingine zinazoangukia pua walijaribu kuziita kwa majina ya seminary wakifikiri zingeweza kufanya vizuri? Kama ni suala la seminary naamini hata yeye anaweza kumpeleka mtoto wake, kwa sababu zipo nyingi tu na zimetawanyika karibu nchi nzima.
Masanja Mkandamizaji akivaa gauni akajiremba saaaana bado jina lake halisi ni Emmanuel Mgaya. Shule hizi za Seminary ufanisi wake si jina "Seminary" bali uthubutu wa kweli wa kuinua elimu.
Big up Mkuu Ng'wale