Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Watzn wote wakijua kinachofanywa na magamba hii inchi hitakalika. Haya ya vuta nkuvute kwa faida ya wachache madarakani hayakubaliki hata kid'ogo!!! Nakubaliana na msemo "hakili ndogo kuingoza hakili kubwa' ni chimbuko la haya yote. I support Prf Mkandara and Ndarichako though I am not sure how serious they are maana jk lazima hatawaelewa.
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba kada wa chama chetu Prof. Mukandala anaweza kuivimbia serikali yake ya ccm.
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba Dr. Ndalichako anaweza kuivimbia serikali yake ya ccm.
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba kada wa chama chetu Prof. Mukandala na Dr. Ndalichako wanaweza kujiuzulu nyadhifa zao huko NECTA.


Mkuu, hivi kisheria mtumishi wa umma anaweza kukiuka maamuzi ya baraza la mawazi? Lakini hata Mkandara mwenyewe ashalalamikiwa siku nyingi na vijana wetu UDSM wakitaka aondolewe bila mafanikio.
 
Nafikiri hujasoma majibu ya msemaji wao John Nchimbi kuwa wanafanya kazi masaa 24 ili kubadilisha maana yake wamekubali sasa wewe unabisha nn mzee wa Vuta nikuvute ha ha ha ha ha hakuna kujiuzulu wewe kashindwa Kawambwa na maghembe sembuse huyu mama ndalichako nani ambae hataki ulaji HUU NI UPEPO TU UTAPITA
 
Anakataa kwa sheria ipi?

Sheria yetu (mbovu) ndio inayompa mamlaka waziri kutoa maagizo (hata ya kisiasa kwenye mambo ya taaluma) kwa baraza la mitihani na kwa mujibu wa sheria hiyo (s 20, Necta Act 1973) baraza linalazimika kutekeleza maagizo hayo!

kazi ipo kwa kweli! Magamba kwa magamba, yetu macho na masikio
 
  • Thanks
Reactions: SMU
kama haitoshi eti safari hii wamekuja navijimeza vyao vya maabara (sijui wanafunzi 40 watajifunzaje practical ? hivi kweli tunajua tunachofanya kwenye elimu)
wametawanya hizi meza nchi nzima na inaonekana serikali imetumia hela nyingi bila sababu kwa kuwa fedha za meza moja zingeweza kununa vifaa vya kutosha vya maabara za shule badala ya hivyo vimeza.
 
Hivi kwanini waandishi hwajawafuata tangu mwanzo ili kusikia opinion yao? Kipindi kile dr Ndalichako alikuwa anatembea na zombe zilizochorwa na wanafunzi, kuonyesha jinsi watoto wetu hao wanavyo fanya mzaha. Leo hii akikaa kimya bila kutueleza kama yeye ndo alibadilisha pasi mark, nitamshangaa sana!! Credibility yake ipo kwenye mtihani mgumu, hapo ndo maamuzi ya msomi na mchumia tumbo yatatoa tofauti.
Jambo la pili kama watabadilisha bila , Dr Ndalichako kutoa yake ya moyoni kwa watazania, na mwenyekiti wa board akaridhia mabadiliko hayo, na waziri wa elimu Dr. Kawambwa na Mlugo wakatangaza tena, na wakaendelea kuwepo kwenye nafasi hizo, mimi nitawa-standardize credibility zao woote!!! toka waziri, n/waziri, Prof Mkandala, Dr. Ndalichako, TEA mkurugenzi na mwenyekiti wa board, katibu wa wizara, etc hadi mfagizi na wadau wote wa elimu
SP
 
Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.TUSUBIRI TUONE.
 
Matokeo lazima yabadilishwe kwasababu necta wamechangia kuwa mabaya, sababu wametumia viwango vipya bila kuhusisha wadau wote
 
Akiachia ngazi Ndalichako itakuwa sawa na Kuvuja kwa Pakacha. Huyu mama amelalamikiwa sana, hata kama ni mtendaji mzuri lakini lawama zikizidi ni bora kutafuta ustaarabu mwingine. Mbona elimu yake ni nzuri tu aachane na hiyo kazi ya NECTA ni kama imemshinda vile. Sifa ya kiongozi mzuri ni pamoja na ku_manage Public Relations

Elimu yake nzuri lakini mazoea ndiyo yanayowaponza kaka , wanapenda sana kuwa viongozi hawa watu kaka , kwa Lawama alizotupiwa huyu Ndalichako hakutakiwa kuwepo pale hadi leo .
 
Ulivyoanza kuandika kama ningekuwa ni walewale wa kukurupuka kusoma ningekupinga kwa sauti ya juu lakini ulivyofika hapo nilipo-bold nikakuunga mkono though pia kama ikaonekana imeshindikana hata hao wenye nafuu kidogo wasilazimishe kuwapeleka form 5 bali na kuja na kama crash programme ya kuangalia namna ya kuwasaidia ili wawe vizuri kitaaluma maana si kosa lao na ikiwezekana hata hao matokeo yao yaliyorekebishwa wanapoingia form 5 wapigwe paper la kiana ambalo linaweza likawa GENERAL KNOWLEDGE kuwajaribu kama wana deserve kweli kuendelea na masomo.

Wadau wengi wana hofu na hii serikali sikivu huenda ikawa sikivu mpaka ikapitiliza kupunguza idadi ya wanafunzi waliopata division 0 kutoka 65% mpaka 6% kitu ambacho kitakuwa ni kutudanganya wananchi maana ili ufaulu upate division 4 unatakiwa upate kiwango cha D katika masomo mawili tu kitu ambacho hata kama kuna matatizo ya grading na kama mwanafunzi amefundishwa vizuri lazima atapata masomo mawili kati ya saba na kuchomoka lakini kwa kundi hili kubwa lililopata zero lazima kuna sehemu tumejikwaa inabidi tuangalie namna ya kutatua

Mapendekezo yako ni ya msingi sana, kuna haja ya kuangalia kwa kuwapima na hiyo mitihani kama ile ya matriculation ili kuwachuja na kuzuia tatizo la ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kidato cha sita watakayo fanya.
 
Mukandala hana Lolote , hao wasiasa ndiyo anaowategemea kumpandisha vyeo , hana ujanja wa kuwapinga , Mukandala plus Dr Bhana ni madudu matupu , ni walamba miguu ya wanasiasa tu !
 
Serikali ya kinafiki...Haki Elimu walishasema siku mingi tu habari ya qualify ya elimu na ufaulu kwa ujumla. Wakaishia kuambiwa kuwa sijui sample ndogo mara ni uzushi oooh wanatumiwa kisiasa nk...kiko wapi? Angalia minister alivyokuwa disconnected na reality.
 
selikari ni nan? na kwanini akatae so kama mtu kaumizwa kwanin selikali isiingilie kati? maamuz ya selikali ni mazur na yana tija kwa baadae wala sio siasa kama kuna sababu maalum acha haki itendeke.
karibu sana JF!
 
Hongera Prof. Mukandara, this is what is expected from a Professor. The issues are technical yet the government is providing political solution. For whose interest are the results being modified? Excellent question from a well educated fellow.
 
Kama ni kweli ni safi sana.

Actually nashangaa sana kwa wasomi, hasa walimu wa vyuo vikuu, kufumbia macho uozo huu!! Hivi ni sawa wanasiasa (kama wakina Lukuvi ambao ni ex-seven) kusimamia ubora wa elimu yetu?? Wako wapi UDASA, MUHASA, UDOMASA, etc??? Shame on them!!
 
Matokeo ya darasa la saba pass mark ilishushwa mpaka 70 eti madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi yasikose wanafunzi nadhani na hapa mchezo ni huo huo na ukizingatia 2015 inakaribia kwa kasi. Ipo siku mawaziri watasema mitihani ya wanafunzi wa chuo kikuu isahihishwe na walimu wa shule za msingi kwa kuwa waziri husika au rais ana mamlaka juu ya taasisi hizo. Viongozi wetu wamefika mwisho wa uwezo wao wa kufikiri. Wapumzike
 
Tutajikongoja mwishowe tutafika

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Aisee sisi ni madodoki kweli tunapokea tu, wanataka kutusahaulisha kilichotokea Arusha,Kesho utasikia vyombo vya habari vyote vimerukia kwa Mkandalla.Hii ndio nchi yangu inaweza kutawaliwa na yeyote yule hata kama hamnazo.
 
Ingawa huyu Prof simkubali kwa jinsi anavyoifanya UDSM, lakini kwa hili niko naye 100%! I salute him for this kama ni kweli.
 
Back
Top Bottom