Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Ooh my Gosh!! My country is swing like a poor drunk man, why zis hapening these days and not those days???? Mungu Ibarika Tz,Mungu Ibarik Africa.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Huyo Prof Mukandara atalegea tu.hana uwezo huo wa kukataa maamuzi ya magamba.
 
Mukandala anahusika vipi na matokeo ya olevel? au wameenda kuomba ushauli senet ya udsm? Hueleweki!

Mkuu vipi tena, mbona hujasoma mwanzo wa uzi? Prof. Mukandala amekataa kubadili matokeo kama MWENYEKITI wa NECTA na siyo kama VC wa UDSM. Umeelewa sasa?
 
Nitashangaa sana kama Prof. Atakubali mapendekezo ya KILAZA LUkuvi.
Akikubali nitaamini kweli " AKILI NDOGO inaongoza AKILI KUBWA"
 
Ooh my Gosh!! My country is swing like a poor drunk man, why zis hapening these days and not those days???? Mungu Ibarika Tz,Mungu Ibarik Africa.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Ndugu yanatokea hivyo kwa sababu tumekubali Akili Ndogo kuongoza Akili Kubwa.
 
nime 'like' post yako maana unawakilisha mawazo ya Watz walio wengi.
Wamekataza kuongea mambo ya udini na ubaguzi lakini kwa mnaoishi Dar es Salaam angalieni masaa fulani ya watoto kurejea kutoka mashuleni kuna mabasi yameandikwa kabisa 'INDIAN SCHOOL', ukiwafuatilia hawa watototoambao kweli wengi wana asili ya Asia wote ni Watanzania.
Unavyolalamika hapa huenda wenyewe hawana hata habari kama mitihani 'inasahihishwa' upya maana wao hata hayawahusu. Kinachowahusu wao katika nchi hii ni pale tunapokuja kwenye issue ya kushare cake ya taifa, nani anabisha kuwa mgawanyo hapa unakuwa na utata!? Na ukumbuke pia kuwa 'wagawaji' wa keki ni sisi wenyewe!!
Kwa maana hiyo tutakavyoendelea kuwabeba watu waliofeli ili waonekane wamepass ndivyo tutakavyoendelea kuwa vibarua wa wageni. Ni ukweli mchungu.
Mkuu Kikwajuni one, ukikubali kuona Division 2 zikifika 70% ya watainiwa na wewe unachekelea wakati ukisahau kuwa hao wote hawajui ni kwa nini maji yote ya mto Rufiji, Ruvu nk yanamwagika baharini na watu wanatumia maji machafu ya chooni kunywa haitasaidia chochote. Uwe na 95% waliopasi wakati hakuna hata mwenye uelewa wa ni kwa nini kampuni ambayo rais haifahamu (Richmond/Dowans) inalipwa capacity charge ya shs. 160m kwa siku, au nchi yenye kila kitu inasaidiwa dola laki saba!
Kuna haja sana ya kubadilisha our traditional ways of thinking wakuu!
Hebu tupeaneni ushauri,inauma sana kumuona ndugu yako,mtanzania mwenzako,yuko kwenye ajira ya kunyanyasika,au akawa kibaka,tuwasaidie hawa watoto,ni wengi,nilifurahi serekali iliposhisha kiwango cha ufaulu darasa la saba,angalau tupunguze ajira za watoto za u house girl na u house boy nk,pamoja na vibaka.bila kazi maisha magumu ndugu zanguni,wa Tanzania wenzangu.
 
Punguza hasira Oduko. Ila nakubaliana na wewe kuwa njia sahihi hapa ni kuachia ngazi kwa hawa viongozi wasomi uchwara ambao wameshindwa kusimamia taasisi ya kusahihisha mitihani na kutangaza matokeo. Haiwezekani mtu asifanye mtihani kisha apewe maksi kana kwamba amefanya.

Tata yalikuwa ni makosa ya kiundishi tu nazani nimesharekebisha pamoja sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
HII SERKALI ni ya KISE-la sana!!!!! sasa kustandardize ndio makalio gani kwa hiyo watastandardize kila mwaka au hii ni maana ya kupunguza Uhalisia wa maana ya elimu na ubora wake ili ufanane na ujinga wa watoto wetu...Tunafuga mitoto mijinga kwa upumbavu wa serikali ya kikwete>>>>serikali gani inashindwa maono hata na ka NGO kama Haki Elimu!

ni jitiada za kujipendekeza kwa wananchi wapumbavu!watoto waRESEAT TUU.
nDALICHAKO NI MTENDAJI bora SANA TUU SEMA HII MISISIEM INAENDEKEZA SIASA ZA MAJI MACHAFU Mpaka kwenye issue za msingi.....
HAKUNA KUSTANDARDIZE WALA NINI
CCM MAKALIO BORESHENI ELIMU KIUTENDAJI PUMBAVU NYINYI:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:
 
Mukandala anahusika vipi na matokeo ya olevel? au wameenda kuomba ushauli senet ya udsm? Hueleweki!

Wewe pia mitihani yako irudiwe kusahishwa, mleta mada kasema Mwenyekiti wa balaza la mitihani na unajua fika nchi hii mtu mmoja anaweza kuwa na nyadhifa zaidi ya moja.
 
Msimamo mzuri sana kwa maslahi ya Taifa
 
Wanasiasa, wasio na integrity, wajinga na wenye njaa huwa hawaachii ngazi. Mkuu kwa mtu mwenye akili timamu, hsa Profesa na Dr, 1+1=2, haiwezi kuwa 3 wala nne. Kama watoto wamefeli, ukiwaongezea alama 20 au zaidi bado watakuwa wamefeli tu. Kama serikali inafanya ujinga wasibebeshwe mzigo wengine, kimsingi ni kuwa Mh Pinda na Kawambwa wanatakiwa kutoa maelezo ya maana na yenye akili na kuchukua hatua za kweli, and not lipsticking a pig.

Katika ngazi kwa Tanzania ni ngumu sana, na hata ukianza utaratibu wa kujiuzuru Rais atakuwa kila siku anahangaika kuteua hebu chukulia mtu kama Mulugo akiachia ngazi, ana kibarua cha kuteua mtu mwingine ndani ya CCM, usisahau kwamba watu makini ndani ya CCM walio wengi wanawekwa pembeni kwasababu wanaikosoa Serikali, usitarajie watateua watu kama akina Filikunjombe, Mpina au Lugola no watateua wale wafia chama kama akina Lusinde na akina Serukamba ambao hawachelewi kuwaambia wananchi Fukyuu na kuboronga maofisini na kulazimika kujiuzuru mara kwa mara
 
:angry::angry::angry::angry: KWELI KABISA ME MWENYEWE NNA WANGU HUMO ME ATARESEAT TUU
nime 'like' post yako maana unawakilisha mawazo ya Watz walio wengi.
Wamekataza kuongea mambo ya udini na ubaguzi lakini kwa mnaoishi Dar es Salaam angalieni masaa fulani ya watoto kurejea kutoka mashuleni kuna mabasi yameandikwa kabisa 'INDIAN SCHOOL', ukiwafuatilia hawa watototoambao kweli wengi wana asili ya Asia wote ni Watanzania.
Unavyolalamika hapa huenda wenyewe hawana hata habari kama mitihani 'inasahihishwa' upya maana wao hata hayawahusu. Kinachowahusu wao katika nchi hii ni pale tunapokuja kwenye issue ya kushare cake ya taifa, nani anabisha kuwa mgawanyo hapa unakuwa na utata!? Na ukumbuke pia kuwa 'wagawaji' wa keki ni sisi wenyewe!!
Kwa maana hiyo tutakavyoendelea kuwabeba watu waliofeli ili waonekane wamepass ndivyo tutakavyoendelea kuwa vibarua wa wageni. Ni ukweli mchungu.
Mkuu Kikwajuni one, ukikubali kuona Division 2 zikifika 70% ya watainiwa na wewe unachekelea wakati ukisahau kuwa hao wote hawajui ni kwa nini maji yote ya mto Rufiji, Ruvu nk yanamwagika baharini na watu wanatumia maji machafu ya chooni kunywa haitasaidia chochote. Uwe na 95% waliopasi wakati hakuna hata mwenye uelewa wa ni kwa nini kampuni ambayo rais haifahamu (Richmond/Dowans) inalipwa capacity charge ya shs. 160m kwa siku, au nchi yenye kila kitu inasaidiwa dola laki saba!
Kuna haja sana ya kubadilisha our traditional ways of thinking wakuu!
 
Kwa kweli maamuzi yaliyofanywa na kamati ilyoundwa kufuatilia suala la matokeo mabovu ya kidato cha nne yalikuwa ni ya kukurupuka, na yalifanywa bila kufikiriwa sawasawa. Najaribu kuwaza concept ya kustandardize matokeo, ni kwa faida ya nani? Kujifurahisha kwa kuona tunarekodi za vijana wengi waliofaulu bila kuzingatia ubora wa elimu na uwezo wa hao wanafunzi wenyewe? Si haya aliyosema Richard Mabala kuwa ni sawa na kupanua goli ili mtu afunge!!! Haya ni Maamuzi yasiyo na tija. Nampongeza sana Prof. Mkandala kama kweli atasimamia msimamo huo.

Tatizo la matokeo mabaya haliko kwenye kustandardize wala hizo grades mpya, tatizo ni mfumo mbovu wa elimu nchini. Na matatizo haya si mageni, maana yalishazungumzwa sana. Matatizo ni kama kukosa nyenzo za kufundishia, uhaba wa walimu, uhaba wa vifaa vya maabara, maslahi duni ya walimu, mazingira magumu ya kufundishia, ukosefu wa majengo ya kutosha, ubovu na uchakavu wa madarasa na nyumba za walimu, nk nk
Serikali ilipaswa iyatatue haya na si kukimbilia kkwenye kufuta matokeo na kustandardize matokeo maana matokeo haya ni kuwa na WASOMI wasio wasomi ambao kimsingi NDIYO hao wanaotuletea MATATIZO kwenye hii SERIKALI yetu ya sasa. Baadhi ya viongozi wetu ni vihiyo wa kutupwa, wana PHD ama Masters za magumashi na matokeo yake ndiyo haya kukurupuka kutoa maamuzi ambayo hayana tija kwa watanzania.

km kweli chanzo cha kufeli huku kwa 60% kumesababishwa na sababu ulizo zianisha,Je shule za private pia zina uhaba wa walim??je zina maslahi duni kwa walim??je hazina maabara na vifaa vya kufundishia vya kutosha?je walim wa shule za private pia wana mgogoro na serikali???

Nimeuliza hivyo ni kwasababu tumeshuhudia pia anguko la kutisha kwenye shule za private ambapo miaka yote huishia divishen 3 lkn mwaka jana shule hizo zimetoa zero za kutosha!!...mfano Jitegemee sec wana ziro 410 hali ambayo haijawah kutokea tangu shule ianzishwe!
 
Kama kweli habari hii ni sahihi

Mawazo yangu:
Mosi niwape pongezi Mwenyekiti na Katibu yaani, Profesa Mukandala na Dkt. Ndalichako kwa kuijali elimu yetu ya Tanzania huu ni ujasiri wa kupongezwa na kusifiwa kwa hali na mali.
Serikali ya chama cha mapinduzi imejiingiza kwenye doa kubwa baada ya kukubaliana na maamuzi ya Tume njaa, lengo lao halikuwa kuchunguza kuporomoka kwa elimu bali kuisafisha Serikali, huu ni udhaifu ambao Ndg. Pinda ameuonyesha pamoja na Rais wetu mpendwa.
Elimu ya Tanzania inajulikana kwa madhaifu yake, tume zimeshaundwa wadau wameshasema, tukirudi kwenye suala la matokeo ni dhahiri Serikali ilijipaka kinyesi walipoamua kutangaza matokeo, maana mfumo uko wazi, lazima Serikali iridhie kabla ya kutangazwa, au walikuwa wanatafuta nini kuruhusu kutangazwa kwa matokeo yale?

Nini Kifanyike
Kwanza Waziri wa Elimu na timu yake ya mipango wizarani watoke, au waondoshwe hapa Ndg Pinda usipapase macho wala kununa, TEKELEZA, Sababu kubwa wamekosa mikakati ya kuelemisha jamii ya watanzania, wametuletea aibu Tanzania, wameleta hasara kwenye bujeti ya nchi. LAZIMA WAONDOKE.

Mbili, uteuzi wa Waziri mpya uzingatie historia yake katika elimu sio kumpa zawadi mtu wa karibu au rafiki fulani, Ndugu Rais tafadhali sikia kilio changu na teua mtu atakaye kusadia kurudish elimu mahala pake, usikomaze shingo, WATOTO ndio TAIFA LA KESHO, objective isiwe kuokoa pesa, bali kuelimisha JAMII.

Tatu
Wadau muhimu wa elimu waje na mikakati ya kusaidia waliopo kidato cha nne sasa nakushuka kuhakikisha janga hili halijirudii, hata kama itamaanisha kurudia budget ya Wizara ya Elimu chini ya WAziri mpya

Mkifanya haya mtarudisha heshima ya Serikali, na chama

Nitasikitika sana kama Ndugu Raisi na Ndugu Pinda hawatatekeleza haya, maisha ya watoto waliofeli yatakuwa juu yao na vizazi vyao. Mungu mjaalie zaidi hekima Rais wa JMT, Mungu ibariki Tanzania
 
Wanasiasa, wasio na integrity, wajinga na wenye njaa huwa hawaachii ngazi. Mkuu kwa mtu mwenye akili timamu, hsa Profesa na Dr, 1+1=2, haiwezi kuwa 3 wala nne. Kama watoto wamefeli, ukiwaongezea alama 20 au zaidi bado watakuwa wamefeli tu. Kama serikali inafanya ujinga wasibebeshwe mzigo wengine, kimsingi ni kuwa Mh Pinda na Kawambwa wanatakiwa kutoa maelezo ya maana na yenye akili na kuchukua hatua za kweli, and not lipsticking a pig.

Heshima mbele Mkuu........maneno kamili kabisa hayo.......hivi sijui hawa viongozi wanalipeleka wapi Taifa hili.......waliusoma ushauri wa Mzee Mwanakijiji vibaya and out of context......hivi kuna sehemu yeyote naweza kupata ripoti ya kamati iliyoundwa.......
 
Last edited by a moderator:
Bora waachie ngazi - kwani tunajua fika hata Mh. Kawambwa atapata pakuanzia kuachia ngazi.
 
Kama kweli habari hii ni sahihi

Mawazo yangu:
Mosi niwape pongezi Mwenyekiti na Katibu yaani, Profesa Mukandala na Dkt. Ndalichako kwa kuijali elimu yetu ya Tanzania huu ni ujasiri wa kupongezwa na kusifiwa kwa hali na mali.
Serikali ya chama cha mapinduzi imejiingiza kwenye doa kubwa baada ya kukubaliana na maamuzi ya Tume njaa, lengo lao halikuwa kuchunguza kuporomoka kwa elimu bali kuisafisha Serikali, huu ni udhaifu ambao Ndg. Pinda ameuonyesha pamoja na Rais wetu mpendwa.
Elimu ya Tanzania inajulikana kwa madhaifu yake, tume zimeshaundwa wadau wameshasema, tukirudi kwenye suala la matokeo ni dhahiri Serikali ilijipaka kinyesi walipoamua kutangaza matokeo, maana mfumo uko wazi, lazima Serikali iridhie kabla ya kutangazwa, au walikuwa wanatafuta nini kuruhusu kutangazwa kwa matokeo yale?

Nini Kifanyike
Kwanza Waziri wa Elimu na timu yake ya mipango wizarani watoke, au waondoshwe hapa Ndg Pinda usipapase macho wala kununa, TEKELEZA, Sababu kubwa wamekosa mikakati ya kuelemisha jamii ya watanzania, wametuletea aibu Tanzania, wameleta hasara kwenye bujeti ya nchi. LAZIMA WAONDOKE.

Mbili, uteuzi wa Waziri mpya uzingatie historia yake katika elimu sio kumpa zawadi mtu wa karibu au rafiki fulani, Ndugu Rais tafadhali sikia kilio changu na teua mtu atakaye kusadia kurudish elimu mahala pake, usikomaze shingo, WATOTO ndio TAIFA LA KESHO, objective isiwe kuokoa pesa, bali kuelimisha JAMII.

Tatu
Wadau muhimu wa elimu waje na mikakati ya kusaidia waliopo kidato cha nne sasa nakushuka kuhakikisha janga hili halijirudii, hata kama itamaanisha kurudia budget ya Wizara ya Elimu chini ya WAziri mpya

Mkifanya haya mtarudisha heshima ya Serikali, na chama

Nitasikitika sana kama Ndugu Raisi na Ndugu Pinda hawatatekeleza haya, maisha ya watoto waliofeli yatakuwa juu yao na vizazi vyao. Mungu mjaalie zaidi hekima Rais wa JMT, Mungu ibariki Tanzania

KULA TANO MKUU!!.....heshima mbele.....
 
Back
Top Bottom