Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)
 
Ngoja tuone mwisho wa senema hii. Director wa movie za Tanzania, so creative.
 
Akiachia ngazi Ndalichako itakuwa sawa na Kuvuja kwa Pakacha. Huyu mama amelalamikiwa sana, hata kama ni mtendaji mzuri lakini lawama zikizidi ni bora kutafuta ustaarabu mwingine. Mbona elimu yake ni nzuri tu aachane na hiyo kazi ya NECTA ni kama imemshinda vile. Sifa ya kiongozi mzuri ni pamoja na ku_manage Public Relations
 
Anakataa kwa sheria ipi?

Sheria yetu (mbovu) ndio inayompa mamlaka waziri kutoa maagizo (hata ya kisiasa kwenye mambo ya taaluma) kwa baraza la mitihani na kwa mujibu wa sheria hiyo (s 20, Necta Act 1973) baraza linalazimika kutekeleza maagizo hayo!

Minister may give directions:
20.
The Minister may give the Council directions of a general or specific character and the council shall give effect to every such direction.
 
Gamba bwana!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wakikubali matwaka ya cabinet basi watakuwa wamekubali kubebeshwa zigo la lawama ambalo lilitakiwa libebwe na wizara ya elimu..
 
Mukandala anahusika vipi na matokeo ya olevel? au wameenda kuomba ushauli senet ya udsm? Hueleweki!
 
ni bora PROF NA DR NDALICHAKO WALINDE HESHIMA YAO prof mukandala ni msomi mzuri ila ana tabia ya kuyumbishwa na wanasiasa na kama atalisimamia msimamo wake basi itakuwa ushindi ata kwa wanafunzi wa UDSM pia Dr JOYCE NDALICHAKO bingwa wa mathematics mwenye msimamo na asiyeyumbishwa ata kidogo anaweza akajiuzulu kama serikali itaendelea na msimamo wao cha msingi WAWE NA MSIMAMO MOJA ILA NAMWOFIA PROF ANAWEZA AKALEGEZA MSIMAMO.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne. Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala. Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo. Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Kwa kweli maamuzi yaliyofanywa na kamati ilyoundwa kufuatilia suala la matokeo mabovu ya kidato cha nne yalikuwa ni ya kukurupuka, na yalifanywa bila kufikiriwa sawasawa. Najaribu kuwaza concept ya kustandardize matokeo, ni kwa faida ya nani? Kujifurahisha kwa kuona tunarekodi za vijana wengi waliofaulu bila kuzingatia ubora wa elimu na uwezo wa hao wanafunzi wenyewe? Si haya aliyosema Richard Mabala kuwa ni sawa na kupanua goli ili mtu afunge!!! Haya ni Maamuzi yasiyo na tija. Nampongeza sana Prof. Mkandala kama kweli atasimamia msimamo huo.

Tatizo la matokeo mabaya haliko kwenye kustandardize wala hizo grades mpya, tatizo ni mfumo mbovu wa elimu nchini. Na matatizo haya si mageni, maana yalishazungumzwa sana. Matatizo ni kama kukosa nyenzo za kufundishia, uhaba wa walimu, uhaba wa vifaa vya maabara, maslahi duni ya walimu, mazingira magumu ya kufundishia, ukosefu wa majengo ya kutosha, ubovu na uchakavu wa madarasa na nyumba za walimu, nk nk
Serikali ilipaswa iyatatue haya na si kukimbilia kkwenye kufuta matokeo na kustandardize matokeo maana matokeo haya ni kuwa na WASOMI wasio wasomi ambao kimsingi NDIYO hao wanaotuletea MATATIZO kwenye hii SERIKALI yetu ya sasa. Baadhi ya viongozi wetu ni vihiyo wa kutupwa, wana PHD ama Masters za magumashi na matokeo yake ndiyo haya kukurupuka kutoa maamuzi ambayo hayana tija kwa watanzania.
 
Kuachia ngazi?!!!
Not in Tanzania yet...

Wanasiasa, wasio na integrity, wajinga na wenye njaa huwa hawaachii ngazi. Mkuu kwa mtu mwenye akili timamu, hsa Profesa na Dr, 1+1=2, haiwezi kuwa 3 wala nne. Kama watoto wamefeli, ukiwaongezea alama 20 au zaidi bado watakuwa wamefeli tu. Kama serikali inafanya ujinga wasibebeshwe mzigo wengine, kimsingi ni kuwa Mh Pinda na Kawambwa wanatakiwa kutoa maelezo ya maana na yenye akili na kuchukua hatua za kweli, and not lipsticking a pig.
 
Kwa hili ni bora serikali ikawawajibisha wote waliosababisha kadhia hii lakini kitendo cha kubatilisha matokeo ni aibu sana. Nakubaliana na hiyo tetesi ikiwa ni kweli basi inafaa Prof na Dr wajiuzulu kwa heshima zao na vyombo vyao.
 
Back
Top Bottom