Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Nchi hii! Sijui tulirogwa na nani?? Serikali inatoa maamuzi ya kipuuzi na watu wanalala na kuamka kama kawaida! Inashangaza, inahuzunisha!
 
Kwa hiyo tunafurahi hawa watoto wakafanye kazi za u house girl na house boy,na shamba boy?Na pia waew vibaka ,ukipaki gari yako uibiwe vitu vya gari?fikirieni sana.

Mkuu sisi watz ni wanafiki hakuna mfano, Hao hao pale mwanzo ndio waliokuwa wakilalamimika kuwa hawa vijana waliofeli tutawapeleka wapi? Lakin sasa kumbe solution imepatikana tena kutokana na uchunguzi wa watalamu na sasa bado wanalalamika tu.
 
Uamuzi mzuri maana sasa serikali inataka kuwadhalilisha
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Maoni na Mtazamo wangu
Kama taarifa hii ni ya kweli na kama Prof. Mkandala atasimamia msimamo wake na akaachia ngazi ya Cheo Chake NECTA basi BIFU kati yake na Serikali itakuwa kubwa sana na itambidi ajiandae kuachishwa huo U Vice Chancellor hapo Mlimani. He may be correct kwenye msimamo wake but kwa namna mambo yalivyo yaweza kumgharimu Cheo Chake pale Mlimani.
Ni maoni tu wadau msijenge chuki.
 
selikari ni nan? na kwanini akatae so kama mtu kaumizwa kwanin selikali isiingilie kati? maamuz ya selikali ni mazur na yana tija kwa baadae wala sio siasa kama kuna sababu maalum acha haki itendeke.

Karibu JF...bila shaka uu miongoni mwa wale asilimia 60...pole sana.
Join Date : 7th May 2013

Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received 0

Likes Given 0

Hebu tupeaneni ushauri,inauma sana kumuona ndugu yako,mtanzania mwenzako,yuko kwenye ajira ya kunyanyasika,au akawa kibaka,tuwasaidie hawa watoto,ni wengi,nilifurahi serekali iliposhisha kiwango cha ufaulu darasa la saba,angalau tupunguze ajira za watoto za u house girl na u house boy nk,pamoja na vibaka.bila kazi maisha magumu ndugu zanguni,wa Tanzania wenzangu.

Nakuunga mkono by 100000000000000%,
 
Maoni na Mtazamo wangu
Kama taarifa hii ni ya kweli na kama Prof. Mkandala atasimamia msimamo wake na akaachia ngazi ya Cheo Chake NECTA basi BIFU kati yake na Serikali itakuwa kubwa sana na itambidi ajiandae kuachishwa huo U Vice Chancellor hapo Mlimani. He may be correct kwenye msimamo wake but kwa namna mambo yalivyo yaweza kumgharimu Cheo Chake pale Mlimani.
Ni maoni tu wadau msijenge chuki.

Nadhani haya ni maoni tu ya VUTA-NKUVUTE...Nitakuwa wa mwisho kuamin kuwa hawa aliowataja hapa wana guts za kuigomea serikali though hiyo ilipaswa kuwa ndio Reaction yao.
 
Last edited by a moderator:
Hebu tupeaneni ushauri,inauma sana kumuona ndugu yako,mtanzania mwenzako,yuko kwenye ajira ya kunyanyasika,au akawa kibaka,tuwasaidie hawa watoto,ni wengi,nilifurahi serekali iliposhisha kiwango cha ufaulu darasa la saba,angalau tupunguze ajira za watoto za u house girl na u house boy nk,pamoja na vibaka.bila kazi maisha magumu ndugu zanguni,wa Tanzania wenzangu.

Mkuu, I hear you so straight kabisa. Naelewa frustrations ulizonazo na si wewe tuu watanzania wengi wako nazo. Ni kweli kabisa ndugu zetu wako mtaani etc etc etc...lakini hata wakiongezewa marks wakaonekana wamefaulu wakaenda mpaka vyuoni, haisaidii hili taifa. At the end of the day, hawata pata ajira au hawatapata ajira nzuri au hawataweza kujiajiri na hivyo tutaishia kule kule. Tutaishia kulalamika kwamba wageni tu ndo wanaopata ajira ilhali uhalisia ni kwamba mfumo wetu unazalisha VILAZA ama watu ambao hawajaiva kufanya au kujiajiri. Kwa hiyo mm naona ni bora tutatue tatizo la msingi tusitumie hizi short cut. Inauma lakini tutatue tatizo msingi...
 
Naunga hoja jirani yangu mkandara, hata kama wakibebwa vip matokeo ya fom 6 yatawaumbua, pumba zitabaki kuwa pumba na mchele utabaki kuwa mchele. BasI na waliomaliza 2010 na 2011 wafanyiwe standardization kama hawa wa 2012
 
Prof. Mukandala, Dr. Ndalichako Vs Mh. Lukuvi (questionable education)

Nami nina mtoto anasali usiku na mchana yarekebishwe maana amepata points 34.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Mukandara and Ndalichako have only two options:
1) Redo the marking as instructed by the government, else
2) Resign from their posts (ie pack and go)
Period
 
wanabadilisha matokeo ili wamfurahishe nani?

njia pekee ya kuepuka hii aibu kwa viongozi wa necta ni kuachia ngazi ingawa kwa Tanzania hii kitu kujiuzuru imekuwa ni kitendawili kisichotegulika
 
Mitoto imekuwa mizembe sana siku hizi ikingojea vya bure kazi kuchezea simu tu kutwa nzima na kushinda fb. unakuta katoto kadogo kutwa nzima kanashinda fb huku kamerundika picha kibao halafu kanasubiri kufaulu bure wakati wengine tulikesha na taa za chemli. Kuanzisha chuo kikuu cha dodoma kumemeza mpaka makapi nayo yamo. Vyuo inabidi viimarishe mitihani kwani watu wengi sasa hawasomi kazi ni fb tu.
 
Mukandara and Ndalichako have only two options:
1) Redo the marking as instructed by the government, else
2) Resign from their posts (ie pack and go)
Period

Marking??....MHhhhhhhh..
 
Karibu JF...bila shaka uu miongoni mwa wale asilimia 60...pole sana.
Join Date : 7th May 2013

Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received 0

Likes Given 0

Mkuu acha kuumbua wenzako sio fair..
 
Lakini usomi wao pembeni. Hivi ni nini hasa kulichotokea mpaka watoto ambao hawakufanya mtihani wakapata maksi nzuri na wale ambao walifanya wakafeli?Kwa nini ripoti yote ya uchunguzi isiwekwe wazi wananchi tujue mwanzo na mwisho wa matatizo ya NECTA? Kutakuwa na tatizo kubwa sana NECTA ambalo nadhani wanasiasa wanataka kufunika kombe mwanaharamu apite ili kuepusha aibu ya kuweka wazi uozo ulioonekana NECTA.
 
wanabadilisha matokeo ili wam----hishe nani?

njia pekee ya kuepuka hii aibu kwa viongozi wa necta ni kuachia ngazi ingawa kwa Tanzania hii kitu kujiuzuru imekuwa ni kitendawili kisichotegulika

Punguza hasira Oduko. Ila nakubaliana na wewe kuwa njia sahihi hapa ni kuachia ngazi kwa hawa viongozi wasomi uchwara ambao wameshindwa kusimamia taasisi ya kusahihisha mitihani na kutangaza matokeo. Haiwezekani mtu asifanye mtihani kisha apewe maksi kana kwamba amefanya.
 
Back
Top Bottom