Samahani wakuu naomba mtu mwenye kujua kuhusu garlic anisaidie requirement ya mbengu kwa heka, output yake inakuwaje plus masoko nataka nijaribu hiki kilimo.
 
baadhi ya jf members tunafanya projects zetu pamoja lakini kila mtu anamiliki kivyake. Unakuta kwa mfano huko kwenu Iringa tunawekeza pamoja kila mtu kwa kadri ya uwezo alio nao. Lakini kuna mambo tunashirikiana ili kupunguza gharama fulani fulani. Na sio kwenu tu, hata huku Pwani pia tunashirikiana ktk miradi mingine. Nakuletea mail.

Sawa mkuu! nadhani nami nastahili katika hilo.Hivyo nikitaka kuunga mkono juhudi hizo mmeweka utaratibu gani ili tuweze badilishana mitizamo mkuu, niweke sawa mkuu sitaki kuchelewa
 
sawa mkuu! nadhani nami nastahili katika hilo.Hivyo nikitaka kuunga mkono juhudi hizo mmeweka utaratibu gani ili tuweze badilishana mitizamo mkuu, niweke sawa mkuu sitaki kuchelewa

Kabla hujawa nasi ni lazima uielewe project tunayoifanya ili uone kama inakufaa au la,kisha nitakwambia inafanywaje kuanzia mwanzo mpaka mwisho,hapo ndio unakuwa na ujasiri wa kuingia. Project ziko nyingi tunazofanya kwa pamoja.
 
wazee naomben ushaur wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu,kuanzia maeneo yanayotoa vitunguu kwa wingi,muda wa kuanza kulima,gharama ya kulima heka moja na heka moja inatoa gunia ngapi na bei ya shambani kwa kila gunia ni kiasi gani
 
Unataka kulima sehemu gani? Gharama zinatofautiana sana kati ya eneo na eneo
 
wazee naomben ushaur wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu,kuanzia maeneo yanayotoa vitunguu kwa wingi,muda wa kuanza kulima,gharama ya kulima heka moja na heka moja inatoa gunia ngapi na bei ya shambani kwa kila gunia ni kiasi gani

Hata mimi nasubiria kupata huo ushauri, mimi nategemea kuanza hicho kilimo kati ya mwezi wa nane hadi wa 12 maeneo ya Wami. Kuna mtu kaniambia maeneo hayo yanafaa.

Nangojea ufafanuzi zaidi.
 
Jamani mnataka vitunguu Twahumu au vitunguu maji?

Mbona hamsomeki? kwanza nyinyi mnajua nini kuhusu vitunguu? labda tuanzie hapo.
 
Kwenye hii blog mtapata kilimo na ufugaji wa vitu vingi sana, kikubwa ukitaka ufanikiwe kwa kitu chochote unachofanya ni kuamua kutafuta information.
 
wadau mwenye utaalam wa jinsi ya kulima vitunguu swaum anijuze tafadhali. Tayari ninalo shamba mkoani mbeya hivyo ni kuanzia uandaaji wa shamba, mbegu na muda mpaka kuwa tayari kuvuna.
 
jamaa yangu anafanya hiyo kitu ila analima too local, sasa sijui kitaalam ikoje ili kuongeza mavuno.
 
Kwani hilo shamba lina mfumo gani wa umwagiliaji ni kilimo cha kutegemea mvua au mfumo gani.
 
Wandugu nahitaji maelezo ya kina kuhusu kilimo cha vitunguu tafadhali. nina shamba la hela 5 Mlandizi nimepata wazo la kulima vitunguu ila sina ujuzi wa aina yoyote.msaada please.
 
Sweetdada,

Lets share ideas, mimi nasikia vitunguu vinahitaji sana maji sasa hapo kwako upo karibu na kijito?
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom