Chimbo la Vitunguu Lumuma

Chimbo la Vitunguu Lumuma

EVIGT

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
589
Reaction score
561
Salaam
Kama unaitaji kununua kitunguu, nenda Lumuma, hata upeleke semi 10 zitajaa kwa wakati mmoja.

Lumuma ni kijiji kinachopatikana wilaya ya Kilosa kwa upande wa Morogoro na Mpwapwa upande wa Dodoma, yaani kipo mpakani.

Sasa hapa kijijini kuna bonde kubwa lenye acres za kutosha, linatumika kwa kilimo cha vitunguu,,

Mteja wangu ambaye nilienda kumchimbia kisima nyumban kwake ni mkulima ananidadavulia kuwa bonde hilo wanalima kitunguu mwaka mzima, chanzo cha maji ni kijimto na mifereji inapitisha maji kutoka kwenye chemchem milimani huko inatililika mwaka mzima bila kujali majila.
Kufika Lumuma ni rahisi sana, ukitokea morogoro mjini, gari zipo hadi Lumuma, ukitokea Dodoma mjini pia zipo gari hadi Lumuma.

Kama unaitaji kununua kitunguu, nenda Lumuma, hata upeleke semi 10 zitajaa kwa wakati mmoja.
Siku njema.
👇
Video
 
Attachments

  • 20260728_164512.mp4
    59.6 MB
Hilo bonde lina utajiri sana, vitunguu maji, vitunguu saumu, mpunga, nyanya vinalimwa hapo

Moja ya mabonde ambayo hadi kiangazi maji yapo ni mwendo wa irrigation tu mifereji kama yote

Wana stoo kama zote za kuhifadhia vitunguu
 
Kuna miwa pia ya kutosha,,
 
Matapeli nao wametega mitego
Wakuja tukienda kutafuta fursa ya mashamba watupige
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom