Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Erick_Otieno, Aug 11, 2010.

 1. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Wakuu salamu.
  Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.

  Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!
  Kilimo Kwanza!

  ===============================================
  MCHANGANUO WA KILIMO HIKI.
  ===============================================
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 0
  Realtor

  Jaribu Mang'ola kaka, Iringa kuna maeneo wanalima sana vitunguu pia-nimesahau ni kijiji gani along BY road.

  Kilimo Kinalipa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Realtor,'

  Kuna sehemu fulani inaitwa ruaha mbuyuni, hapo bwana kilimo hakitegemei mvua, kitunguu kinakubali sana hapo mpendwa, vilevile uzuri wa hapo ni kwamba unawezakulima vitunguu marambili kwa mwaka, ukitoa kitunguu unaweza kulima mahindi mara mbili na maharage mwaka huo huo mmoja. Yaani ardhi ya hapo inakubali karibu kila kitu na serikali imeshapaendeleza.

  Ukiweza kupapata hapo utafaidika sana lkn bei sio zile za elfu 50 kwa hekari,bei hapo ni kubwa na ni vigumu kidogo kupata eneo maana tayari mabebari tumeshayakamata,,(kidding).

  ni-PM kama unataka maelezo ya zaidi naweza kukusaidia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  cheusimangala

  Seconded.

  Kijiji kinaitwa msosa to be precise. ni tarafa ya mahenge i think Wilaya ya Kilolo. Au ukiwa unatokea Dar kwenda Iringa opposite aljazeera hotel on your left. Kuna mifereji kabisa ya umwagiliaji. Nilikuwa huko last month, it's terrific, we nenda utapata mashamba ya kukodi and it pays.

  Good luck.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Shukrani Cheusimangala...Hawa mabebari:smile-big: tutabanana nao!
   
 6. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  This is great information....thanks!
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema !!!!!!!

  Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),

  Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu,watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.

  Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
   
 8. D

  Dick JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pamoja na maeneo yote yaliyotajwa hapo juu, jaribu Kiloosa maeneo ya Mzaganza hadi Mpwapwa Dodoma. Kila la kheri!
   
 9. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pia jatribu kwenda mkoa wa pwani. Ukivuka daraja la mto ruvu mbele kama 1 kilomita (nadhani zamani palikuwepo na ranch ya napco) pinda kulia - nenda kama kilometere kumi hivi/pia ulizia wakazi utakutana na wanakijiji amabao watakuelekeza wapi hasa pana mashamba ya kukodi au kununua. ila chunga matapeli. kila la kheri
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  Well said bro ( hapo pekundu)

  Maeneo hayo ni hatari,kama hela zako ni za kuungaunga,yaani kama unanunua eneo kisha upate muda mwingine wa kutafuta uwezo wa kuliendeleza,utaishia kulia. Ruvu kwa sasa inatakiwa uwe na uwezo,unanunua na kuendeleza eneo lako mara moja.

  Ila usiogope,ni ushauri tu.
   
 11. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Hii ya matapeli ni tatizo kubwa sana kwenye kununua ardhi....nilishawahi kuuziwa heka 8 na serikali ya kijiji pale mlandizi ukienda ndani karibu na reli ya kati, baadae likawa na kesi kati ya vijiji viwili wanaligombania. Nashindwa kuelewa ni namna gani tunaweza kuudhibiti huu utapeli......
   
 12. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Cheusimangala nime-PM kama unaweza kunisaidia zaidi!
   
 13. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 629
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Malila unaweza kunipa mwanga kidogo kuhusu bei za hayo maeneo ya Ruaha na hayo mengine kama unafahamu. Nataka nikasurvey na angalau kabla sijaenda huko nijue bei ya kununua kwa eka au ya kukodi kwa eka.

  Kilimo Kwanza!
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  check inbox yako kaka nimeshafanya.
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  Kwa maeneo hayo sijapata kutafiti bei zikoje,ila naona dada Cheusi anaweza kukusaidia kupata bei hizo kwa maeneo yale. Mimi nitapita maeneo ya Ruaha,nitajaribu kuuliza bei zikoje.
   
 16. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Malila hongera kaka kwa juhudi zako Mungu atakusaidia ndugu yangu nakuombea lakheri nimekukubali nimtaftaji hakuna sehem usoijua na malezoyako niuwazi bilashaka mtuasipo kuelewa atkua namatatizo naham yakukuona hoja zako zimenipa faraja na kujiamini, nisikupendele sana kuna wengi manyusi, cheusimangala, Dick, nawshukuru sana nifaidika sana na ushauri wenu bila ya ninyi kujua mungu awalinde kwa afianjema muiwezeshe jamii.

  Malila naomba mualiko katika vikao vyenu mkuu.

  Mbarikiwe sana
   
 17. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu Malila naomba na mini nisiwe mchoyo wa kutoa shukrani zangu!

  Kwa kweli nimekuwa nafurahia sana mchango wako.....na umekuwa muwazi sana.....na hivi ndo wajasiriamali wa Tanzania tunatakiwa tuwe! big up saaaanaaaaa!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  kasopa

  Asante ndugu yangu.

  Kama uko DSM niambie ili siku nikifika dar nikutafute, leo niko nje ya dar. Unaweza kushiriki vikao vyetu bila taabu. Hakuna kiingilio na hatumfichi mtu kitu tunachofanya. Tunajadili namna ya kushiriki uchumi wa nchi yetu na sio kuwa watazamaji.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashkuru mkuu kwasasa sipo nchini nategemea kurud mwisho wamwezi ujao ntakujulisha
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  Poa,tuombe Mungu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...