Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Erick_Otieno

JF-Expert Member
Mar 28, 2010
627
1,000
10-2-Raw-vs.-Cooked-Garlic-and-Onions-for-Blood-Thinning-1200x675.jpeg

Wakuu salamu,

Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!
Kilimo Kwanza!

BAADHI YA WADAU WANAOHITAJI KUELEWA KILIMO HIKI
Wadau,

Napenda kufanya kilimo cha vitunguu ila sina data za kutosha kuhusu hili swala. Nimesikia kuna sehemu inaitwa mang`ola wanalima ila sijawahi fika,sehemu nyingine ni Iringa ila sasa nashindwa kujua ni wapi kati ya sehemu hizo mbili nimzuri na cheap.

Then: ingependa kujua mashamba yanakodishwa shiling ngapi? Mbegu kwa heka ni sh ngapi? Gharama ya kulima pamoja na kuweka matuta? Kupanda? Mtu wakulinda shamba ni sh ngapi?na vitu vingine ambavyo sivijuwi.

Wadau haya yote yametokana na hali mbaya ya wategemeawo mwisho wa mwezi.naombeni mawazo yenu wadau.

Naomba kuwakilisha hoja.
Wandugu nimeamua kuingia kwenye kilimo,ninawaza kuanza na kitunguu saumu,..naomba mnijuze wapi panafaa kulima?gharama ya kutunza hekari 1,muda mpaka kukomaa, . Pili nafikia pia maharage ya kijivu(ya mbeya) detail zake pia,, asanteni.
Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo.napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1

MICHANGO YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI
ABC's ZA KILIMO CHA VITUNGUU
UTANGULIZI
Vitunguu saumu ni zao ambalo lipo katika jamii ya vitunguu na hufanana sana na vitunguu maji, zao hili linatumika sana duniani kama kiungo cha chakula na wengine hutumia kama dawa.

ASILI YAKE
Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na China, Asia lakini pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA ZA VITUNGUU SWAUMU
Vitunguu swaumu vipo vya aina mbalimbali nazo ni:=

i) Antichoke – Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea

ii) Soft neck – Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani

iii) Silver skin – Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

HALI YA HEWA & UDONGO
Vitunguu saumu hulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba linapaswa kutayarishwa mapema kabisa, lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda.

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Mbegu ya kitunguu swaumu ni ile punje (vikonyo) inayokuwa imebanguliwa kutoka kwenye kitunguu au tunguu iliyokomaa kabisa, kiasi cha kilo 300 – 500 hutumika kwa hekari moja na inatakiwa uchague mbegu isio na magonjwa au isio dhaifu.

UPANDAJI
Tabia ya mmea wa Vitunguu swaumu humea huanza kuota kipindi cha baridi ( miezi yenye baridi), kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August, Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 .
Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.

MBOLEA
Mbolea huwekwa baada ya palizi, tumia mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi.

UPALILIAJI
Kuwa na juhudi ya kupalilia ili kuipa uhuru mimea kumea vizuri na kulifanya shamba lako kuwa safi, Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza ndipo weka mbolea.

Unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi. Mmea unapoendelea kukua na kutoa maua yaache majani yarefuke mpaka yajikunje, ndipo utayakata ili kuongeza uzalishaji.

MAGONJWA & WADUDU
MAGONJWA

Vitunguu swaumu havishambuliwi sana na magonjo, ila magongwa yake ni kama:=

i) Fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna

ii) Kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia

iii) Kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi

iv) Baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao

v) Muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa.

WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

UVUNAJI
Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja.

SOKO
Soko lipo kwasababu Vitunguu Swaumu ni kiungo kinacho tumika na wengi, kwa bei ya shiling 3,000 – 3800 kwa kilo.
GHARAMA ZA KULIMA KITUNGUU KILOSA
Kwa Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua

Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
GHARAMA ZA KULIMA KITUNGUU MBEYA
Mbeya
Kukod shamba 50000
Mbegu gram 400-500
Gram 100-25000
Kulima 50000
Vitalu kwa ajur ya kupanda 50000
Kupanda 100000
Dawa ya palizi 40000
Paluz 3
Mbolea 150000
Madawa tote 150000
Kuvuna 100000
Hapo unaweza kuvuna gunia had 90 hakuna migogoro ya maji yapo kubao unwagiria SAA yeyote ukitaka coll me 0759185832
KITUNGUU NI ZAO LENYE MANUFAA
Habari ndugu zangu,

Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.

Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.

Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com

Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.
UHUDUMIAJI WA KITUNGUU
Kwa kilimanjaro.

Kwanza mbegu kwa eka utatakiwa kusia kilo tatu mpaka nne. Ukinunua mbegu dukani hiyo ni 400,000
Kuandaa kitalu, kusia na kutunza mbegu kwa angalau mwezi mmoja na nusu lazima uwe na angalau 300,000
Kupandikiza ekari moja yenye majaruba yasiyopungua 330= 330,000
Utatakiwa ukishapandikiza uwe na mifuko angalau 12 ya mbolea kila mwezi utatia mbolea (yaani mifuko minne kwa eka) 45,000x12.

Utatakiwa kupiga dawa kila wiki ya kuua wadudu, buster, ya kuondoa baridi etc..dawa pekee itakugharimu si chini ya 80,000 kwa ekari moja kila wiki. Utatakliwa either kupiga dawa ya kuua mbegu za magugu yasiote ambayo ni tsh 17,000-27/ lita kwa ekar unaweza kuhitaji lita mbili. au kungolea majani angalau mara nne tangu kupandikiza mpaka kuvuna.

Kwa eka kila wiki utahitaji kumwagilia. Kwa ekari moja angalau uwe na lita 30 za dizeli/petroli kama pumb unayo.

NB: Omba Mungu utakapovuna Mang'ora au Ngage usiwe msimu wa kuvuna vitunguu maana utapata pressure. wengi wamepata hasara kubwa na wengine wamepoteza maisha. Bei kwa sasa kwa gunia la vitunguu haizidi elfu 60,000. Mimi binafsi nimelima na nimepata hasara isiyo kifani.

Kwa ekar kuanzia kusia mpaka kuvuna angalau uwe na tsh 3mil - 4mil. Lakini usitengee kuwa utavuna upate faida kama story zilivyo. Kama unapesa hivyo nakushauri uiwekeze kwa mambo mengine. Mzunguko wa pesa kwa sasa hakuna. Kitunguu hakilipi kwa sababu kinalimwa kila mahali Tanzania kwa sasa. Weka pesa zako hata fixed deposit.

Nazungumza kutokana na uzoefu. Nitumia zaidi ya mil13 kulima. Nilipovuna nikauza kila gunia kwa 40,000 nikapata hasara zaidi ya milion 10. Usisikie story. The truth is terrifying. Na usije ukachukua mkopo ukitegemea kilimo cha kitunguu kitakulipa.

Kabla benki hawajakufikia utakuwa umeshakufa kwa pressure. Nenda ngage, kileo, chekereni, mawala, na sehemu zingine za mkoa wa kilimanjaro utapata story za watu waliokufa kwa pressure mwaka huu kutokana na vitunguu kushuka bei na kutofikia hata gharama za uzalishaji.

unaweza kuja inbox kwa maelezo zaidi. lakini kwa sasa kilimo cha vitunguu is not ideal
 
King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema !!!!!!!

Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),

Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu,watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.

Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
Mkuu huko Kipatimu ni wapi haswa???
 
Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
1,225
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema !!!!!!!

Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),

Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu,watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.

Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
Pia unaweza kujaribu Nar (Bashnet) Wilaya ya Babati au Bashay kwa Mh. Marmo
 
King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Kipatimu ipo wilaya ya Kilwa,ukitoka Dsm kwenda Lindi,unaweza kuingilia Somanga au Njia Nne na ukiwa usafiri wako unaweza toka Dsm asubuhi na jioni uko Dsm bila taabu.
Mkuu huko ni kuzuri zaidi maana ni karibu na DSM ngoja nifanye mipango angalau niweze kufika huko
 
King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
Mkuu nikitaka kufika huko nafikaje Kilosa npafahamu na nimeshawahi kufika ila huiko mwega/malolo ndio sipajui nipe direction mkuu
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,605
2,000
ni km ngapi kutoka bandari iliyo salama mpaka kipatimo,labda tunaweza tia miguu mafuta tukaja wekeza
Nakadiria kama km 300 as maxmum,kwa sababu Dsm mpaka Somanga ni km 220, kisha unaingia kulia. Ngoja nimuulize dogo mmoja anipe uhakika kwa kupitia Kinjumbi ni km ngapi toka Somanga.
 
CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
566
225
Nashukuru sana kwa taarifa kama hii.
Ekari moja wanakodisha au wanauza kwa bei gani?
Gharama za kulima, kutunza shamba la ekari moja hadi kuvuna ni sh. ngapi?
Ekari moja inatoa gunia ngapi?
Naweza kupata eneo zuri lenye maji yasiyokauka nilime kilimo cha umwagiliaji kwa mashine ya kuvta maji?
Contacts zangu ni: 0767 919923, 0784 593005, 0716 889705, richkety@yahoo.co.uk
 
CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
566
225
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
Nashukuru sana kwa taarifa kama hii.
Ekari moja wanakodisha au wanauza kwa bei gani?
Gharama za kulima, kutunza shamba la ekari moja hadi kuvuna ni sh. ngapi?
Ekari moja inatoa gunia ngapi?
Naweza kupata eneo zuri lenye maji yasiyokauka nilime kilimo cha umwagiliaji kwa mashine ya kuvta maji?
Contacts zangu ni: 0767 919923, 0784 593005, 0716 889705, richkety@yahoo.co.uk
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,605
2,000
Nashukuru sana kwa taarifa kama hii.
Ekari moja wanakodisha au wanauza kwa bei gani?
Gharama za kulima, kutunza shamba la ekari moja hadi kuvuna ni sh. ngapi?
Ekari moja inatoa gunia ngapi?
Naweza kupata eneo zuri lenye maji yasiyokauka nilime kilimo cha umwagiliaji kwa mashine ya kuvta maji?
Contacts zangu ni: 0767 919923, 0784 593005, 0716 889705, richkety@yahoo.co.uk
Mkuu kuna eneo lina maji mengi sana yasiyo kauka na kijito kizuri, unaweza kulima kilimo cha umwagiliaji. Eneo hili lipo km 75 toka Dsm njia ya Mkuranga. Udongo ni mzuri na barabara ipo. Eneo hilo linafaa pia kwa mifugo mbalimbali.
 
Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,789
1,500
Wakuu ; baada ya tukio la ajali kesi yangu ilipangiwa wilayani Kilosa; na hivyo nililazimika kusafiri hadi mjini Kilosa.......naweza kusema safari yangu ya Kilosa was a blessing in disguise............njiani nimekutana na mabonde mengi sana na mambwawa kedede yaliyojaa maji mapaka sasa pia ardhi nzuri kwa kilimo cha nyanaya na vitunguu na hasa katika vijiji vya Kilangali na Lyamuhaa (Kama sijakosea jina)................natafuta wasaa wa kwenda tena Kilosa na kama kuna mdau analifahau vizuri eneo hilo atujuze zaidi.
 
Kwanza pole kwa ajali mkuu,
Nilibanwa hadi nikasahau kuuliza habari za afya yako tangu siku ile. Kuna jamaa yangu ana makazi huko Kilosa,nitajaribu kumchimba ili asaidie ni maeneo gani sugu kwa mafuriko, ugomvi kt ya wafugaji na wakulima, na yepi yamechukuliwa na wakubwa. Akinipa jibu nitakupasha ili usiingie matatizoni. Ila safari ya Iringa ilikuwa na matunda kwangu na wenzangu.
 
Asante!

Nasikitika kuwa ajali ilinizuia nisijiunge nanyi huko Iringa; Mungu atatupatia wasaa mwingine tena! Namalizia kujipanga ili nirudi mstari wa mbele
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,605
2,000
Asante!

Nasikitika kuwa ajali ilinizuia nisijiunge nanyi huko Iringa; Mungu atatupatia wasaa mwingine tena! Namalizia kujipanga ili nirudi mstari wa mbele
Natarajia desember tuwe na trip mbili za Iringa, ya mwisho itakuwa baada ya x-mass hivi,naamini hii utashiriki mkuu. Nitakuwa na vijana wa jf baadhi.
 
kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,007
1,500
Wakuu nilikuwa na-review hii thread, nikaona jinsi wazee mlivyomwaga nondo. sasa kwa wanaofahamu vizuri kilimo cha vitunguu. Je vitunguu vinakubali ardhi ya mkuranga na Bagamoyo? hasa ukichukulia case ambapo kuna mto usiokauka, au vinalimwa sehemu zenye ubaridi kama Iringa?- au kikubwa ni maji ya kumwagilia. nitashukuru kwa taarifa!!
 
123

Member
Feb 16, 2011
82
70
Wadau,

Napenda kufanya kilimo cha vitunguu ila sina data za kutosha kuhusu hili swala. Nimesikia kuna sehemu inaitwa mang`ola wanalima ila sijawahi fika,sehemu nyingine ni Iringa ila sasa nashindwa kujua ni wapi kati ya sehemu hizo mbili nimzuri na cheap.

Then: ingependa kujua mashamba yanakodishwa shiling ngapi? Mbegu kwa heka ni sh ngapi? Gharama ya kulima pamoja na kuweka matuta? Kupanda? Mtu wakulinda shamba ni sh ngapi?na vitu vingine ambavyo sivijuwi.

Wadau haya yote yametokana na hali mbaya ya wategemeawo mwisho wa mwezi.naombeni mawazo yenu wadau.

Naomba kuwakilisha hoja.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom