Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Haya wale walokua wanasema haina haja ya kununua mbegu..mbegu ni unapanda zile zile ulizovuna mko wpiii?...
Simara njoo uone wkulima wa kisasa hapa...sio mnalima mradi umelima...
Kubalini mktae mbegu bora hutoa matokeq mazuri..hizo zenu za kupanda ten na tena huwa mazao hafifu...
NAPOLEON
 
Wakati mwingine nyie wafanyakazi wa serikali muwe mnajifunza toka kwa wenzenu unasubiri mpaka miaka kumi inapita ndio unaanza kulima.presha ya uzeeni hiyo unajitakia halafu eka tatu ni ya chakula hiyo
 
Nimevuna gunia 30 za mahindi msimu huu. Kwa kuwa bei imeshuka ya kuuza mahindi nawaza niyaweke dawa au nitumie njia gani nzuri kwenye kuyahifadhi.
Napenda maoni yenu wakuu kwani nimechelewa kuufatilia uzi huu.
Tutajiane na bei za viwatilifu hivyooo maana ss wa vijijini tukienda mjini huwa tunapigwa sana bei.
 
Msaada tafadhali, maandiko mengi ni ya maelezo ambayo hayana figures.

Naomba nisaidiwe kwamba kwa ekar moja inaweza fika shilingi ngapi na kwa ekar 10 shilingi ngapi, shamba langu sikodi.

Kwamba:
1. Kuandaa
2. Kupanda
3. Mbegu hybrid
4. Mbolea za kisasa bei
5. Palizi
6. Trekta
7. Madawa nk.

Nawategemea sana wakuu ndugu zanguni.
 
Kilimo cha mahindi inabidi ulime karibu na mto ili kama utatokea ukame unakodi pampu na unamwalia kama kawaida.
Kulima mbali na mto ni kupata au kukosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na wapi umelimia kuna mikoa ambayo ni lazima tu mahindi yatafika. Mvua yaweza kuwa pungufu misimu mingine ila si kwa kiasi cha kutokukomaza mahindi. Eneo hili linajumuisha sehemu kubwa ya mikoa ya nyanda za juu kusini kama mbeya, njombe, songea, iringa, songwe na rukwa.
 
Ilikua heka ngapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heka 3 na nusu. Na mvua zilikuwa nyingi mashamba mengi yalizama kwenye maji.
Ila changamoto kwenye bei imenifanya nisiuze mahindi. Nitulie tuu hadi wakat wa mwez wa 10
 
Hayo mahindi ya laki kwa gunia ni mahindi ya kuchoma?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…