Kesi ya Mbowe Novemba 4, 2021: Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Sebastian Madembwe atoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Novemba 5, 2021

Leo shahidi wa sita naye kapita na mazaga zaga yake kama yale yale, ya wale wa awali.

Shahidi huyu anadai alipata barua ikimtaka kukagua silaha kama ilikuwa imesajiliwa nchini 25/11/2020. Akaijibu barua hiyo 15/3/2021, miezi 5 baadaye.

Maajabu yapate vipi kukoma?

Tumeona hukumu zikitolewa katika hatua mbali mbali za shauri hili.

Tumeona Hati ya Mashtaka ikibadilishwa ndani ya shauri. Tumeona na mengi mengine.

Siyo siri kuwa pana ukakasi wa kutosha unaoligubika shauri hili.

View attachment 1998796

Ukweli ni pumzi ya wapenda haki.

Maisha ya wenye haki yako mashakani kutokana na idadi ya waongo kuongezeka kila kukicha.

Hata hivyo yote kheri kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli.
Substitution au amendment ya charge ni kitu cha kawaida s.234 CPA,labda kwasababu wewe ni mgeni mahakamani. hati ya mashitaka huwa inabadilisha na sheria inaruhusu hivyo.
 
Objectively speaking, shahidi wa leo lengo lake ni kuonesha kuwa silaha waliyokamatwa nayo watuhumiwa haikuwa halali.

Ninavyoona watuhumiwa watakutwa na kesi ya kujibu, kama watafungwa au la itategemea na ushahidi wa upande wa utetezi.
Je silaha iliingiaje mikononi mwa washtakiwa,je huyu msajili ana uhakika gani kama silaha aliyokuwa anaisearch ndio hii inayozungumziwa
 
Biblia. Mithali 16:27
[27]Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara;
Katika midomo yake mna moto uteketezao.

( Hakuna jipya chini ya jua tuwe na subira wacha waropoke yote for records)
 
Mawakili wa Utetezi wamejipanga kusawasawa. Toka mwanzo wanawagalagaza wa upande wa mashitaka .hii Kesi kama hakimu ataifutilia mbali Basi anaweza kuukwaa umaarufu kwa kuwa hodari na shujaa wa nyakati hizi. Akionekana ndy Mbana matumizi ya kodi za wananchi na mtunza heshima za Wasomi!!
 
Hakuwa na barua ya mwanzo aliyoandikiwa
Details za silaha na nini alitakiwa kuchunguza. Je mahakama itajuaje report aliyotoa
Miezi 5 baade ndiyo ya silaha waliyokamatwa nayo?

Ila sahihi zaidi ni kuwa mahakama itajuaje silaha aliyohakiki ilikuwa ni hii hii inayoongelewa?

Haupo uthibitisho kuwa walikamatwa na silaha.
 
substitution au amendment ya charge ni kitu cha kawaida s.234 CPA,labda kwasababu wewe ni mgeni mahakamani. hati ya mashitaka huwa inabadilisha na sheria inaruhusu hivyo.
Lakini kwenye hii kesi Jaji ndio aliagiza ibadilishwe bila Jamhuri kuleta Ombi hilo
 
Leo shahidi wa sita naye kapita na mazaga zaga yake kama yale yale, ya wale wa awali.

Shahidi huyu anadai alipata barua ikimtaka kukagua silaha kama ilikuwa imesajiliwa nchini 25/11/2020. Akaijibu barua hiyo 15/3/2021, miezi 5 baadaye.

Maajabu yapate vipi kukoma?

Tumeona hukumu zikitolewa katika hatua mbali mbali za shauri hili.

Tumeona Hati ya Mashtaka ikibadilishwa ndani ya shauri. Tumeona na mengi mengine.

Siyo siri kuwa pana ukakasi wa kutosha unaoligubika shauri hili.

View attachment 1998796

Ukweli ni pumzi ya wapenda haki.

Maisha ya wenye haki yako mashakani kutokana na idadi ya waongo kuongezeka kila kukicha.

Hata hivyo yote kheri kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli.
Shahidi wa sita au wa tano
1. Kingai
2.
3.
4.
5.
6.
 
Objectively speaking, shahidi wa leo lengo lake ni kuonesha kuwa silaha waliyokamatwa nayo watuhumiwa haikuwa halali.

Ninavyoona watuhumiwa watakutwa na kesi ya kujibu, kama watafungwa au la itategemea na ushahidi wa upande wa utetezi.
Umeangalia na uzito wa silaha yenyewe kuhusu matumizi! Kwa kifupi ni silaha ya jikoni na risasi tatu! Za kutendea ugaidi! Yaani ukilipua risasi moja tu vituo viwili vya mafuta vinalipuka.
FROM RAU MADUKANI WITH LOVE.
 
Naam, hiyo sasa itakuwa ni kazi ya mawakili wa upande wa utetezi kuonesha kwamba hakukua na njama zozote za kutenda ugaidi
 
Je silaha iliingiaje mikononi mwa washtakiwa,je huyu msajili ana uhakika gani kama silaha aliyokuwa anaisearch ndio hii inayozungumziwa
Haikuwa kazi yake- yeye alitakiwa kujibu swali moja tu- imesajiliwa au haijasajiliwa?
Sasa ni kazi ya Kibatala atajapokuwa anauomgoza ADAMOO
1.aje na usajili wa hiyo silaha
2. akane kuwa hajakamatwa na silaha
3. hajawahi kuiona wala haijui
4. au ni ya marehemu
 
Mawakili wa Utetezi wamejipanga kusawasawa. Toka mwanzo wanawagalagaza wa upande wa mashitaka .hii Kesi kama hakimu ataifutilia mbali Basi anaweza kuukwaa umaarufu kwa kuwa hodari na shujaa wa nyakati hizi. Akionekana ndy Mbana matumizi ya kodi za wananchi na mtunza heshima za Wasomi!!
Binafsi naona kama mawakil wa jamhuri ndio wamekua wakiwabwaga mawakili wa utetezi.hata pingamiz lao la jana kuhusu shahid wa jana kuwa batil pia lilionekana halina mashiko na hii ukiachilia mbali kesi ndogo walioshindwa vibaya sana.Japo wanajitahid kuuliza maswal ila naona kama wanacheza na jukwaa badala ya kutafuta point..
 
Haikuwa kazi yake- yeye alitakiwa kujibu swali moja tu- imesajiliwa au haijasajiliwa?
Sasa ni kazi ya Kibatala atajapokuwa anauomgoza ADAMOO
1.aje na usajili wa hiyo silaha
2. akane kuwa hajakamatwa na silaha
3. hajawahi kuiona wala haijui
4. au ni ya marehemu
Uko sahihi ila i guess atasema haijui wala hajakamatwa nayo biashara imeisha
 
Back
Top Bottom