Kesi ya mjane wa bilionea Msuya: Miriam, Mwendesha Mashtaka walivyochuana mahakamani

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Mrita, ameingia katika hatua ya pili ya utetezi wake katika kesi ya mauaji ya wifi yake inayomkabili yeye na mwenzake, ya kuhojiwa maswali ya dodoso.

Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Agosti 7, 2013, anakabiliwa na shtaka la mauaji ya wifi yake Aneth Elisaria Msuya; yeye na mwenzake Revocatus Everist Muyella.

Aneth aliuawa Mei 26, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo), jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, inasikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya utetezi wake akiongozwa na wakili wake Peter Kibatala, sasa ameingia katika hatua ya pili, ambapo katika hatua hiyo anahojiwa maswali ya dodoso na upande wa mashtaka.

Katika hatua hiyo upande wa mashtaka umeanza kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maelezo yake aliyoyatoa katika ushahidi wake mkuu kwa lengo la kuutikisa ushahidi wake na kuufanya usiwe na thamani.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano baina ya mshtakiwa huyo na kiongozi wa jopo la waendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Paul Kimweri.

SSA P. Kimweri: Shahidi tukumbushe majina yako

Shahidi: Miriam Steven Mrita

Kimweri: Una kiwango gani cha elimu?

Shahidi: Elimu yangu ni darasa la saba

Kimweri: Uliolewa lini na Erasto Msuya?

Shahidi: Mwaka 1996

Kimweri: Utakubaliana nani wakati unaolewa hukuwa na ajira rasmi au uliolewa kama mama wa nyumbani?

Shahidi: Sijaelewa

Kimweri: Narudia mara ya mwisho (3) ili sasa kama hujaolewa tupate mwongozo wa Mahakama.

Shahidi: Nilikuwa sina ajira rasmi.

Kimweri: Kwenye ushahidi ulioutoa mrefu umetaja biashara kubwa SG Hotel machimbo ya madini ya Tanzanite kabla hujaolewa haujawahi kuwa nazo?

Shahidi: Nilikuwa bado.

Kimweri: Kwa maneno mengine ulijihusisha na biashara hii baada ya kuolewa na Erasto Msuya?

Shahidi: Sio kweli Mheshimiwa

Kimweri: Baada ya kuolewa na Erasto Msuya kwa muda wote ambao ulikaa na familia hiyo uliwahi kufahamu baba mkwe wako Elisaria Elia Msuya alikuwa akimiliki migodi?

Shahidi: Alikuwa mchimbaji wa Tanzanite na alikuwa na mgodi na walikuwa wanachimba pamoja na Erasto, kama ni wa kwake au si wa kwake hilo sijui.

Kimweri: Huo mgodi unaitwaje? Au kama umesajiliwa kwa jina gani?

Shahidi: Huo waliokuwa wanachimba Elisaria Msuya na Erasto Msuya sijui umesajiliwa kwa jina gani.

Kimweri: Katika maisha yenu mlikuwa mnamiliki magari kadhaa, ni sahihi?

Shahidi: Ndio.

Kimweri: Unaweza kutukumbusha haya magari yalikuwa ni magari gani namba za usajili, aina. Ngoja nikukimbushe, kuna Range Rover Evoque T429 BYY.

Shahidi: Nakumbuka mume wangu alikuwa na Range Rover Evoque lakini sikumbuki namba.

Kimweri: Vipi kuhusu T677 BNM Landcruiser?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Sikumbuki mheshimiwa Jaji.

Kimweri: Vipi kuhusu T307 CBH aina ya Ford Ranger?

Shahidi: Ndio, hilo limesajiliwa kwa jina langu.

Kimweri: Vipi kuhusu T800 CKF Range Rover?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Ni magari gani katika hayo unakumbuka ni lipi marehemu alikuwa anaendesha siku anafariki?

Shahidi: Sikumbuki

Kimweri: Lakini tukio hilo unalikumbuka kuwa mwili wake ulipokutwa pembeni kulikutwa gari aliloendesha siku hiyo?

Shahidi: Simkumbuki.

Kimweri: Kwa hiyo kwa ujumla wakati marehemu anafariki mlikuwa mnamiliki magari mangapi kwa ujumla?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Sasa kuna gari hapa la mwisho kukutajia umelikumbuka sababu lilikuwa limesajiliwa kwa jina lako, sasa hii ni ripoti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uchunguzi wa magari, shika hii. Kwenye huo ukrasa huo kuna wamiliki mbalimbali (wa gari T800 CKF) mmiliki wa mwisho ni nani?

Shahidi: Miriam Steven Mrita

Kimweri: Kwa hiyo sasa baada ya kusoma umekumbuka kuwa mmiliki wa mwisho wa T800 CKF Range Rover ni wewe?

Shahidi: Nimekumbuka

Kimweri: Sasa tarehe 12/12/2013 ndio tarehe ya kwanza wewe kumiliki hili gari kwa kujibu wa ripoti hii, ndivyo inavyoonekana?

Shahidi: Ndio

Kimweri: Marehemu Erasto Msuya alifariki lini?

Shahidi: Tarehe 7/8/2013

Kimweri: Kwa hiyo kuanzia tarehe 7/8/2013 mpaka wewe unafanya transfer (uhamisho) hii tarehe 12/12/2013 ilikuwa imepita miezi mingapi?

Shahidi: Miezi mitano.

Kimweri: Unakumbuka kwamba hii ndio gari ambayo marehemu Erasto Msuya aliloendesha kwa mara ya mwisho kabla ya kuuawa?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sikumbuki.

Kimweri: Wakati hii transfer ya hili gari inafanyika kwenda kwenye jina lako ulikuwa umeshateuliwa kuwa msimamizi wa mirathi?

Shahidi: Ndio

Kimweri: Na wakati hii transfer inafanyika kwenye gari hili ulikuwa bado hujapeleka mrejesho mahakamani kama msimamizi wa mirathi, niko sahihi?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Uliteuliwa lini kuwa msimamizi wa mirathi?

Shahidi: Tarehe 5/11/2013.

Kimweri: Na wakati unateuliwa kuwa msimamizi wa mirathi Mahakama ilikuelekeza ndani ya muda gukani uwe umepeleka mrejesho (wa orodha) ya mali za marehemu?

Shahidi: Ilielekeza hivyo.

Kimweri: Ndani ya kipindi cha muda gani?

Shahidi: Miezi Sita

Kimweri: Wakati unakamatwa kwa tuhuma hizi tarehe (5/8/2016) ulikuwa bado hujapeleka hiyo orodha?

Shahidi: Ndio

Kimweri: Kwa sababu hiyo wakati inafanyika hiyo transfer ya hii gari ni wakati ambao ulikuwa bado hujapeleka mrejesho mahakamani?

Shahidi: Sikumbuki

Kimweri: Hukumbuki nini?

Shahidi: Usinilazimishe nijibu jibu lako?

Kimweri: Mimi nakulazimisha ujibu swali langu siyo jibu lako?

Kimweri: Nilikuwa bado.

Kimweri: Wewe kama msimamizi wa mirathi wakati huo unafahamu baada ya kufanya hayo yote na mahesabu kupeleka mahakamani ndipo mali yote inagawiwa?

Shahidi: Nilifahamu.

Kimweri: Kwa hiyo wakati unagawa hizi maana uliniambia Mahakama uligawa Sh250 milioni kwa wazazi na watoto na Sh73 milioni kwa ndugu wa marehemu, wakati unafanya huu mgawanyo uliufanya kutoka kwenye mahesabu gani ya mali za marehemu?

Shahidi: Nilikuwa bado.

Kimweri: Utakubaliana nami kwamba hata ushahidi wa nyaraka wa huo mgawo kwamba ulimgawia nani na akasaini haujauleta hapa mahakamani kama kielelezo?

Shahidi: Kama kielelezo hakikupokelewa.

Kimweri: Ulisema kuna kesi mbalimbali zilifunguliwa kupinga wewe kuwa msimamizi wa mirathi, hizo kesi zilianza lini?

Shahidi: Baada ya kusoma kielelezo (uamuzi wa moja ya shauri la maombi ya kumpinga kuwa msimamizi wa mirathi) mwaka 2013.

Kimweri: Wakati huo wewe ulikuwa wapi? Gerezani au wapi?

Shahidi: Nilikuwa Arusha.

Kimweri: Kuna shauri lolote uliwahi kupeleka mahakamani kuhusiana na mirathi hii kwa suala la wewe kutokupeleka mrejesho kabla hujaenda gerezani, uliwahi kuomba Mahakama ikuongezee muda wa wewe kupeleka mrejesho?

Shahidi: Sikumbuki mheshimiwa jaji.

Kimweri: Ulishawahi kupeleka shauri la maombi mchanganyiko namba 217 la mwaka 2015 mbele ya Jaji Masengi kuomba kuongezewa muda?

Shahidi: Nakumbuka mbele ya Jaji Moshi.

Jaji Kakolaki: aliyefungua ni nani?

Shahidi: Elisaria Elia Msuya na Eater Msuya, dhidi ya Miriam Steven Mrita.

Kimweri: Utakubaliana na mimi kuwa sababu moja wapo ni pamoja na wewe kutokupeleka mrejesho?

Shahidi: Sababu ilikuwa ni hiyo.

Kimweri: Ulisema wakati wanakukamata (Askari Polisi) miongoni mwa vitu walivyochukua ni pamoja na hati ya kusafiria, sawa?

Shahidi: Ndio

Kimweri: Na wakati unatoa ushahidi hapa mahakamani hujawahi kutaja namba ya hiyo passport?

Shahidi: Wewe ulizipata kutoka Mamlaka ipi?

Shahidi: Uhamiaji

Kimweri: Uliwahi kutoa taarifa kwenye mamlaka hiyo kuwa kuna passport yangu namba hii walinichukua Polisi lakini hawakuileta mahakamani?

Shahidi: Sikuweza kutoa taarifa kwa sababu nilikuwa gerezani.

Kimweri: Lakini ukiwa gerezani mambo mengine yalikuwa yanaendelea kupitia kwa mawakili wako?

Shahidi: Ndio zilikuwa zinaendelea.

Kimweri: Ulisema kwamba David (Mhanaya) kwa Sasa RCO Arusha, aliyekuwa kiongozi wa timu ya wapelelezi wa kesi hiyo hakukupa haki zako na hata kosa lako hakukueleza lakini hujaiambia Mahakama kwamba ulipofika mbele ya mkuu wa kituo hukumhoji sababu za kukamatwa.

Shahidi: Nilipofikishwa kituoni sikupewa nafasi ya kujieleza nilifikishwa tu nikaanza kuhojiwa kama nawafahamu watu mbalimbali. Awali nilipokamatwa niliuliza kosa nikaambiwa kuwa natuhumiwa kwa kosa linalohusiana na madini.

Kimweri: Umeeleza hapa kuhusiana na kuteswa ili ukiri utakubaliana nami kwamba katika wote uliowataja kukupiga aliyeandika maelezo yako WP Mwajuma hujamlalamikia kukupiga?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji hakuwepo katika mateso yale, hivyo hakunipiga.

Kimweri: Wakati hayo maelezo ya onyo yanatolewa hapa mahakamani uliyapinga unakumbuka sababu za kuyapinga?

Shahidi: Kwamba nililazimishwa na nilipigwa ili nikiri makosa.

Kimweri: Katika hizo sababu ulizozitoa, sababu kwamba saini iliyopo katika maelezo hayo si ya kwako si miongoni mwa sababu ulizozitoa wakati wa mjadala wa kupokea maelezo hayo?

Shahidi: Nilipinga, sababu hiyo pia ilikuwepo.

Kimweri: Mheshimiwa Jaji tunaomba mwenendo wa Novemba 30, 2021 ukurasa wa 6 na 7, sababu za pingamizi la kupokewa kwa maelezo, umkumbushe shahidi ili tumhoji maswali.

Jaji: Sababu ya kwanza maelezo hayo yalichukuliwa ni ya muda, ya pili, maelezo yale yalichukuliwa baada ya kuteswa bila utashi wake na sababu ya tatu ni kwamba hakuelezwa haki zake ikiwemo haki ya kuwa na Wakili, ndugu au rafiki wakati wa kuchukuliwa maelezo.

Kimweri: Sasa shahidi katika hizo sababu tatu hakuna sababu ya kupinga saini yako?

Shahidi: Nililalamika kwamba nililazimishwa kusaini lakini hapo haipo.

Kimweri: Na katika sababu hizo tatu ambazo Mheshimiwa Jaji amezisoma ipo sababu ya kwamba WP Mwajuma, shahidi wa kwanza hakukuandika maelezo?

Shahidi: Kwenye hizo sababu hamna.

Kimweri: Shahidi baada ya simulizi yako ya mateso mahakamani ulipelekwa lini kwa mara ya kwanza?

Shahidi: Tarehe 23/8/2016

Kimweri: Ndio tarehe hiyo ambayo wakili wako alikuombea itoke amri ya Mahakama upelekwe hospitali kwa uchunguzi?

Shahidi: Siyo hiyo.

Kimweri: Ni tarehe ngapi alikuja kukuombea amri upelekwe hospitalini?

Shahidi: Siikumbuki.

Kimweri: Kwa hiyo katika hiyo tarehe nyingine wakili wako aliwahi kukuombea na kupata amri ya kupelekwa hospitali?

Shahidi: Aliniombea Wakili wangu Kibatala kutokana na majeraha niliyokuwa nayo na Mahakama ikatoa maelekezo kuwa nipelekwe hospitalini kutibiwa.

Kimweri: Uliwahi kupelekwa hospitalini kutibiwa?

Shahidi: Ndio nilipelekwa.

Kimweri: Hapa mahakamani hujawahi kutoa cheti chochote cha hospitali hiyo kama ushahidi kwamba ulitibiwa huko, niko sahihi?

Shahidi: Sijatoa.

Kimweri: Mara ya mwisho wewe kupigwa kabla hujapelekwa mahakamani ilikuwa ni lini?

Shshidi: Tarehe 10/8/2016

Kimweri: Kwa hiyo kuanzia tarehe 10/8/2016 mpaka baada ya tarehe 23/8/2016 siku zote hizi hukuwahi kupelekwa kufanyiwa matibabu?

Shahidi: Hawakunipeleka maana nilikuwa chini yao na hao hao ndio walikuwa wananipiga.

Kimweri: Katika siku zote hizi 13 Bado ulikuwa katika hali hiyohiyo ya maumivu na vidonda kama ulivyoeleza hapa?

Shahidi: Ndio maana nilikuwa chini yao.

Kimweri: Uliiambia mahakama kuwa lengo la kuteswa ilikuwa ili ukiri ukiri kumuua Aneth, sawa?

Shahidi: Ndio

Kimweri: Ile tarehe uliyolazimishwa kuchukuliwa maelezo yako ilikuwa tarehe ngapi?

Shahidi: Mimi najua tarehe 12/8/2016 ndio nililazimishwa nisaini maelezo hayo.

Kimweri: Mheshimiwa tunaomba kielezo PE1 (kielelezo cha kwanza upande wa mashtaka-maelezo yanayodaiwa kuwa yake mshtakiwa) anamuonesha.mshtakiqa na Anauliza. Upande wa mashtaka wanadai kuandika lini maelezo hayo ambayo umeyakataa?

Shahidi: Tarehe 7/8/2016

Kimweri: Sasa tuchukulie kama ulikubali maelezo hayo, baada ya tarehe hiyo (ya kuandika maelezo hayo) walikuwa wanakupiga ili iweje?

Shahidi: Siwezi kuyasemea haya maelezo kwa sababu siyajui.

Kimweri: Baada ya hiyo tarehe waliendelea kukupeleka porini ili iweje?

Shahidi: Kunilazimisha nikubali kumuua Aneth.

Kimweri: Sasa umesema hata baada ya kufikishwa mahakamani umeieleza mahakama kuwa hukuwahi kutibiwa gerezani, sawa?

Shahidi: Nilikuwa natibiwa

Kimweri: Ulikuwa unatibiwa nini?

Shahidi: Majeraha niliyoyapata.

Kimweri: Yaliyotokana na nini?

Shahidi: Kupigwa

Kimweri: Ulikuwa unatibiwa wapi?

Shahidi: Huko Magereza.

Kimweri: Wakati unatibiwa Hilo kwenye hiyo hospitali ya gerezani ulitoa cheti au nyaraka yoyote kuthibitisha kuwa ulikuwa unatibiwa hilo?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji hapa Sijatoa lakini alikuja daktari wa Magereza kutoa ushahidi.

Jaji: Wakati gani huó?

Kimweri: Wakati wa total within trial (kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, ya kupinga maelezo yake kupokewa)

Kimweri: Ulikuwepo wakati daktari wa maagereza anatoa ushahidi?

Shahidi: Nilikuwepo

Kimweri: uliona alitoa kielelezo chochote hapa?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Mshtakiwa wa pili unayeshtakiwa naye kabla ya kukamatwa ulimfahamu?

Shahidi: Ndio.

Kimweri: Mlifahamiana wapi?

Shahidi: Arusha

Kimweri: Sehemu kubwa sana ushahidi wako ulijikita katika malalamiko ya kuteswa unakumbuka uliwahi kuleta mashahidi na upande wa mashtaka ulileta mashahidi kutatua hiyo hoja (katika kesi ndogo), unakumbuka hilo?

Shahidi: Nakumbuka

Kimweri: Na unakumbuka baada ya mahakama kusikiliza mashahidi wa pande zote ilitupilia mbali hiyo hoja na kupokea kielelezo (maelezo yanayodaiwa ya kwake ya onyo)?

Shahidi: Ndio Mheshimiwa

Kimweri: Katika ushahidi wako wakili wako alikuongoza akakuhoji kuhusu maelezo ya ungamo (kukiri kosa mbele ya Mlinzi wa Aman- Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo) ulisema hukupelekwa kwa Mlinzi wa Amani, unakumbuka hilo?

Shahidi: Nakumbuka sikupelekwa.

Kimweri: Pia unakumbuka uliyapinga maelezo hayo kuwa aliyemtaka kuyatoa yaani shahidi wa pili (Mlinzi wa Amani) kuwa aliyetaka kukitoa kielelezo hicho siyo mtu sahihi?

Shahidi: Sikumbuki.

Kimweri: Anaiomba Mahakama inasoma Mwenendo wa kesi ndogo kupinga kupokewa maelezo hayo kisha anauliza:

Shahidi kuna sababu ya wewe kupinga kupelekwa kwa Mlinzi wa Amani kwamba hajawahi kuandika maelezo ya ungamo?

Shahidi: Sijasikia (wakati Jaji akisoma sababu).

Kimweri: Na katika hoja ambazo wakili wako aliziibua kupinga maelezo hayo umesikia hoja kwamba mlinzi wa Amani hakukupa haki zako za msingi?

Shahidi: Hiyo haikuwa hoja iliyotolewa hapo.

Kimweri: Uliwahi kuwa na mgogoro na shahidi wa pili, Leonia Kajumlo (Mlinzi wa Amani)

Shahidi: Siwezi kuwa na mgogoro na mtu ambaye Simfahamu.

Kimweri: Uliieleza mahakama kwamba siku Mahakama ilipohamia Chang'ombe Polisi (kuangalia vielelezo, gari aina ya Rangerover Ivoque) ulisema haina plate number, ni sahihi?

Shahidi: Ndio.

Kimweri: Zaidi ya plate namba hakuna mahali ambako uliona namba za usajili?

Shahidi: Mimi sikuoneshwa.

Kimweri: Lakini ni moja ya magari yaliyokamatwa?

Shahidi: Hiyo gari mimi sijui maana gari ya mume wangu wakati nakamatwa ilibaki nyumbani na taarifa nilizo nazo ni kwamba ilishagawiwa mirathi na nilisema hizi gari aina ya Range Rover ziko nyingi (watu wengine wanazo).

Kimweri: Kwa hiyo ni kwamba hiyo gari iliyoko Chang'ombe haihusiki, je aligawiwa nani?

Shahidi: Watakuja wenyewe wataeleza.

Kimweri: Shahidi umesema ulikabidhiwa marehemu Aneth umlee kama mtoto wako ilikuwa ni lini?

Shahidi: Tangu akiwa Anasoma shule ya msingi.

Kimweri: Pamoja na hayo yote kwamba ulimlea lakini anafariki anazikwa wewe hukuhudhuria msiba wake?

Shahidi: Si kweli

Kimweri: Haya twambie tarehe ngapi mwili ulisafirishwa kutoka wapi na kwenda wapi?

Shahidi: Mwili ulikuwa uko Dar es Salaam ukapelekwa Mererani

Kimweri: Lini hiyo?

Shahidi: Tarehe sikumbuki.

Kimweri: Wakati huo wewe ulikuwa wapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji msiba ulikuwa wa ndugu na uligawanyika sehemu mbili Mererani na Arusha Mjini nilitoka Arusha mjini nikaenda Mererani na Arusha kuna watu walikuwa wanakuja kunisalimia kama mama mlezi.

Kimweri: Hiyo tarehe aliyozikwa ilikuwa ni lini?

Shahidi: Sikumbuki tarehe aliyozikwa.

Kimweri: Ulisema kuwa kwa sababu ulimlea tangu utoto usingeweza kumuua, katika umri wako wote hujawahi kusikia mzazi kamuua mtoto au mtoto kamuua mzazi?

Shahidi: Nimewahi kusikia lakini kunakuwa na sababu fulani.

Kesi hiyo itaendelea kesho ambapo mshtakiwa huyo ataendelea kuhojiwa na waendesha mashtaka maswali ya dodoso.


Credit: Mwananchi
 
Back
Top Bottom