CHADEMA: 'Tulipiga Kura za Wazi kwasababu Kulikuwa na dalili za Rushwa'

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1689147511664.png

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Ruth Mollel amesema katika mkutano wa baraza kuu uliofanyika Mei 11 mwaka jana, walilazimika kupiga kura za wazi kwa kuwa kulikuwa na dalili za rushwa.

Mollel alieleza hayo jana wakati akihojiwa maswali ya dodoso na Wakili Ipilinga Panya katika kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama, iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18 baada ya kuomba kuihoji bodi ya wadhamini.

Mdee, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dar es Salaam, wakipinga kufukuzwa uanachama kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama.

Mdee na wenzake walivuliwa uanachama Novemba 27, 2020 kwa tuhuma za mbalimbali ikiwemo kukisaliti na kujipeleka bungeni kuapishwa. Walikata rufaa Baraza Kuu kupinga uamuzi huo wa Kamati Kuu lakini Baraza katika uamuzi wake wa Mei 11, mwaka jana lilitupilia mbali rufaa yao hiyo.

Jana, akiongozwa na Wakili Panya, Mollel alipoulizwa katiba inasemaje kuhusu mamlaka za nidhamu kuwa ni siri, alisema suala la kupiga kura ni uamuzi wa kikao, lakini kikao cha baraza kuu kilichosikiliza rufaa zao kulikuwa na mambo ya rushwa. Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili Panya na Mollel.

Wakili: Waleta maombi wanadai hawakupewa haki ya kusikilizswa na baraza kuu na kamati kuu.

Shahidi: Walipewa na waliitwa lakini walisema wanaogopa. Mkutano ukabadilishwa kwenda Bahari Beach na kwenye baraza kuu pia walipewa nafasi.

Wakili: Wewe ni mjumbe wa Baraza Kuu?

Shahidi: Hapana

Wakili: Ulijuaje kama walipewa nafasi?

Shahidi: Tulipewa taarifa na mwenyekiti kama wajumbe wa bodi ya wadhamini.

Wakili: Kwenye baraza kuu ulikuwepo?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Kama nani?

Shahidi: Mjumbe wa bodi

Wakili: Mjumbe wa bodi anakuwaje kwenye baraza kuu?

Shahidi: Tulialikwa kama watu wengine lakini hatukupiga kura.

Wakili: Ni sahihi kuwepo kwenye mkutano?

Shahidi: Ndio mimi ni mdhamini wa chama.

Wakili: Katiba inaeleza hivyo ?

Shahidi: Tulienda pale kama waalikwa

Wakili: Unaifahamu katiba ya chama?

Shahidi: Naifahamu lakini siwezi kusema nafahamu kila kitu.

Wakili: Kuna kipengele cha kushughulikia mashauri ya chama, unakifahamu?

Shahidi: Nimesema siwezi kufahamu kila kitu.

Wakili: Unafahamu kuhusu dharura?

Shahidi: Ndio

Wakili: Ukishaapa unakuwa mbunge?

Shahidi: Ndio

Wakili: Baada ya kuapa ilihitajika kuchunguzwa walikuwaje wabunge?

Shahidi: Unakuwaje mbunge wakati mchakato haukufuatwa.

Wakili: Udharura mliouchukulia ni upi?

Shahidi: Kuapa kuwa wabunge kinyume na utaratibu wakati chama hakikupeleka majina.

Jaji Cyprian Mkeha aliiahirisha kesi hadi Julai 26, kwa ajili ya mawakili wa waleta maombi kuendelea kuhoji maswali ya dodoso.
 
Hao wabunge ni hirizi la chama dola, hawawez achiliwa asilani...

Hizi Dana Dana zitaenda had uchaguzi mkuu wa 2025.... labda muujiza utokee... ila hali ilivyo CCM hawathubutu kubaki wenyewe pale Dodoma.
 
Huyu anaeongea ni Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa Chadema.

--

Chanzo: Mwananchi

My Take
Eti Hawa ndio Wanawaambia Watanzania Wawachague watawaletea Maendelea 🤣🤣🤣🤣
 
Eti Hawa ndio Wanawaambia Watanzania Wawachague watawaletea Maendelea
Haisaidii kutuondoa Bandarini.
 
Back
Top Bottom