Kumbe ninachokonoa watu wazito na wanaitika basi ni nyota kubwa sana mm

Haya nitakucheki mkuu, nami Nile mema ya nchi
 
Linaripoti gazeti la New york post(Marekani): Mshawishi maarufu wa mitandao ya kijamii anayeishi Santa Monica nchini Marekani na mwenye zaidi ya wafuasi milioni 10, anadai katika kesi mpya kwamba akaunti zake za mitandao ya kijamii zilifutwa baada ya kampuni ya Meta kudaiwa kukubali shinikizo kutoka Serikali ya Tanzania.

Mwanaharakati Mange Kimambi, mwenye umri wa miaka 46, anasema aligeuka kuwa mlengwa wa viongozi wa Tanzania baada ya kutumia Instagram na WhatsApp kufichua madai ya mauaji na kuhamasisha maandamano ya amani kufuatia uchaguzi wa urais wa mwaka jana ambao ulipingwa na baadhi ya watu.

Kimambi anadai katika kesi yake kwamba Meta ilifuta akaunti zake za mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kukubali shinikizo kutoka Serikali ya Tanzania.

Anasema pia alikuwa amelipia huduma ya Meta Verified ili kupata huduma ya moja kwa moja kwa wateja, lakini hakupata msaada wakati akaunti zake zilipoondolewa.

“Badala yake, Serikali ya Tanzania iliigeukia Meta, na Meta ikaipa kile ambacho serikali haikuweza kukipata yenyewe,” inaeleza kesi hiyo ambayo imeripotiwa kupatikana na California Post.

Kesi hiyo inaendelea kueleza:

“Kampuni ya Marekani, iliyojengwa katika misingi ya uhuru wa kujieleza unaolindwa na sheria za Marekani, ilichagua mapato yake nchini Tanzania badala ya haki za binadamu, uhuru na demokrasia.”

Kimambi anadai kuwa alilengwa baada ya kutumia akaunti zake zilizokuwa na watazamaji wengi kumkosoa na kufichua madai mbalimbali kuhusu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mawakili wa Kimambi wanadai Meta ilitoa kile ambacho Tanzania haikuweza kupata yenyewe — yaani kumyamazisha — kwa kufunga akaunti zake duniani kote, baada ya serikali kudaiwa kutishia kuzuia majukwaa ya kampuni hiyo nchini Tanzania.

Kimambi amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali ya Tanzania baada ya kuhamia Marekani mwaka 2012. Baadhi ya wafuasi wake nchini Tanzania humtambua kwa jina la “dada wa taifa.”

 
Kaka naomba connection basi mtu mzito
 
Mange HAWEZI kushinda hii kesi. Na asipokuwa makini atajikuta yeye ndio anabembeleza kuifuta. Kifupi, ameshauriwa vibaya kufungua kesi! Subiri muone!
Mahakama za US sio za maelekezo kaka, hamna makada wa chama mle

Wenzetu kampuni kama meta na zingine they are very sensitive na publick relation zao, any shred ya uchafu wanajua ita wa cost hela.
 
Mahakama za US sio za maelekezo kaka, hamna makada wa chama mle

Wenzetu kampuni kama meta na zingine they are very sensitive na publick relation zao, any shred ya uchafu wanajua ita wa cost hela.
Kwahiyo unafikiri hao META walikurupuka kufunga hizo accounts sio? Kwamba kampuni inaendeshwa na "chawa" sio?
 
Moto hapa unazidi kuchemka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…