mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
Niambie msiba hata mmoja ambao Magufuli alihudhuria. Hata wewe mleta uzi usipokuwa na tabia ya kwenda kwa misiba ya majirani utasusiwa pale utakapopata msiba. Malipo ni hapa hapa.Nchi yetu ilifikwa na msiba wa kufiwa na rais, baada ya kufiwa immediately tulipokea salamu za rambirambi kutoka kwa maraisi wa jumuia ya Afrika mashariki akiwemo mzee Museveni, Rais Kenyata, Rais Ndaishimiye, Lakini Kagame ilimchukua siku nyingi sana takriban miezi miwili kabla ya kuwapa pole Watanzania.
Rais Kenyata alikuja nchini kuhani Msiba, Mzee Museveni alihani msiba huko kwao na tuliona picha zake, Lakini Kagame alikuwa Mkavu bila hata kuonyesha feelings zozote hata za kuzugia kipindi hicho.
Sasa swali ninalopenda kumuuliza Samia, Unakwenda Rwanda kipindi hiki kufanya nini? Huyu Kagame ambaye hakututakia hata salamu ya rambirambi kwa wakati ndiye Kagame yuleyule aliyemtishia maisha rais wetu mwingine aliyetutangulia. Sasa unakwenda huko kufanya nini kwa sasa?.
Ninafahamu tuna ishu za kibiashara na hiyo nchi naam hayo ni mambo ya msingi, na yako palepale, lakini Je kwa nini sisi tusionyeshe kukasirishwa na kutoheshimiwa kidiplomasia na Kagame baada ya kufiwa na rais wetu?