Kagame hakuja msibani kumzika rais wetu, na alikaa miezi siku nyingi sana kabla hajatupa pole, Rais Samia unakwenda Rwanda kufanya nini?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,129
2,000
Nchi yetu ilifikwa na msiba wa kufiwa na rais, baada ya kufiwa immediately tulipokea salamu za rambirambi kutoka kwa maraisi wa jumuia ya Afrika mashariki akiwemo mzee Museveni, Rais Kenyata, Rais Ndaishimiye, Lakini Kagame ilimchukua siku nyingi sana takriban miezi miwili kabla ya kuwapa pole Watanzania.

Rais Kenyata alikuja nchini kuhani Msiba, Mzee Museveni alihani msiba huko kwao na tuliona picha zake, Lakini Kagame alikuwa Mkavu bila hata kuonyesha feelings zozote hata za kuzugia kipindi hicho.

Sasa swali ninalopenda kumuuliza Samia, Unakwenda Rwanda kipindi hiki kufanya nini? Huyu Kagame ambaye hakututakia hata salamu ya rambirambi kwa wakati ndiye Kagame yuleyule aliyemtishia maisha rais wetu mwingine aliyetutangulia. Sasa unakwenda huko kufanya nini kwa sasa?.

Ninafahamu tuna ishu za kibiashara na hiyo nchi naam hayo ni mambo ya msingi, na yako palepale, lakini Je kwa nini sisi tusionyeshe kukasirishwa na kutoheshimiwa kidiplomasia na Kagame baada ya kufiwa na rais wetu?
 

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,237
2,000
Ukimuangalia tolu pichani unaeza sema kama mnyonge fulani asiyejua kitu ila sasa...

59453A5E-C27E-4348-9BCB-F68229CD3F51.jpeg
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,975
2,000
Inanibidi niyaseme haya kwenye mada hii kuhusu mleta mada:

Umekuwa mzalendo kuliko nilivyowahi kukusoma hapa JF. Kuna kitu gani kimebadilika?

Nauliza hivi kwa moyo safi kabisa bila ya hiana yoyote moyoni mwangu; kwani maslahi ya Tanzania mbele ya jambo jingine lolote ndiyo lengo la waTanzania (wote?)

Naunga mkono hoja yako.

"Maza Mizinguo" ana kazi kubwa sana ya kunyoosha "learning curve" yake kuhusu haya mambo. Inaonekana hata huko ndani ya Ikulu yake, kama ushahidi unavyoonyesha waziwazi, kuna upungufu mkubwa sana wa utambuzi wa mambo yanayohusu maslahi ya nchi hii.

Hii inadhihirisha kwamba taifa letu kwa sasa hivi tupo uchi wa mnyama.
 

Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
378
1,000
Yeye anadai kuwa anaenda kudumisha mausiano, sjui hayo , mausiano yalipotea lin....ukwel nikwamba kuna mambo anayoyafata na anayajua yeye na hao anaoshirikiana nao.

Huko jamuhur ya twitter na viunga vyake, kuna mjuba akadai kuwa mamayenu kaenda kwa jasusi kununua mtambo wa kuhack simu za wabongo machakunaku walio kinyume na utawala dharimu wa huyu mzenjibar......Nothing more she's doing but nonsense
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,877
2,000
Nchi yetu ilifikwa na msiba wa kufiwa na rais, baada ya kufiwa immediately tulipokea salamu za rambirambi kutoka kwa maraisi wa jumuia ya Afrika mashariki akiwemo mzee Museveni, Rais Kenyata...
Mkuu, wajitahidi sana kuwasilisha mawazo ila hii imekaa kushoto zaidi.

Kwa mfano we hapo jiulize kwanini PK hakuja , yaani ulitegemea PK aruke angani wakati ule?

Halafu wafahamu pale Kigali ni refuge point?

Kuna mambo mengi sana yapo nyuma ya pazia hii mada itakuwa yazunguka tu bila kwenda CenterPoint.

Yaani pale penye kiini pale.

Nadhani utanielewa nimetumia codes.
 

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,171
2,000
Kagame is so much cunning and wicked in his own ways. He has a very strange annoying character. Pure mercilessly capitalist. He is a self centered brutal autocratic dictator.
🤣 🤣🤣sentensi fupi lakini umetupa shida wenzio do!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom