Kutekwa kwa Paul Manzi, raia wa Rwanda nchi Tanzania kunaichafua nchi kidiplomasia

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
๐™ˆ๐˜ผ๐™…๐˜ผ๐™Ž๐™๐™Ž๐™„ ๐™’๐˜ผ ๐™๐™’๐˜ผ๐™‰๐˜ฟ๐˜ผ ๐™†๐™๐™„๐™‰๐™‚๐™„๐˜ผ ๐™‰๐˜พ๐™ƒ๐™„๐™‰๐™„ ๐™‰๐˜ผ ๐™†๐™๐™ˆ๐™๐™€๐™†๐˜ผ ๐™‹๐™–๐™ช๐™ก ๐™ˆ๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™ž ๐˜ฝ๐™ฎ๐™–๐™—๐™–๐™œ๐™–๐™ข๐™—๐™– ๐™๐˜ผ๐™„๐˜ผ ๐™’๐˜ผ ๐™๐™’๐˜ผ๐™‰๐˜ฟ๐˜ผ ๐˜ผ๐™‡๐™„๐™”๐™€๐™†๐™๐™’๐˜ผ ๐˜ผ๐™‰๐˜ผ๐™„๐™Ž๐™ƒ๐™„ ๐™‰๐˜พ๐™ƒ๐™„ ๐˜ฝ๐˜ผ๐˜ผ๐˜ฟ๐˜ผ ๐™”๐˜ผ ๐™†๐™๐™‹๐˜ผ๐™๐˜ผ ๐™ƒ๐™„๐™๐˜ผ๐˜ฟ๐™ƒ๐™„ ๐™”๐˜ผ ๐™๐™†๐™„๐™ˆ๐˜ฝ๐™„๐™•๐™„ ๐™’๐˜ผ ๐™†๐™„๐™Ž๐™„๐˜ผ๐™Ž๐˜ผ ๐™‰๐™„ ๐™๐™•๐™€๐™ˆ๐˜ฝ๐™€ ๐™’๐˜ผ ๐™‘๐™”๐™Š๐™ˆ๐˜ฝ๐™Š ๐™‘๐™”๐™€๐™๐™ ๐™‘๐™”๐˜ผ ๐™๐™‡๐™„๐™‰๐™•๐™„ ๐˜ผ๐™ ๐™†๐™๐™‰๐˜ผ ๐™๐™Ž๐™ƒ๐™„๐™๐™„๐™†๐˜ผ?

Wakati wapigania haki wa Africa Mashariki tukiendelea kuomboleza msiba mzito wa mwanaharakati wa Rwanda mwanamama Anne Rwigara aliyefia Gerezani kwa kuwekewa sumu na serikali ya Rwanda, kumetokea tukio lingine la kutekwa kwa familia ya Paul Manzi Byabagamba aliyekuwa anaishi nchini kama mkimbizi wa kisiasa.

Kukiwa bado kuna maswali mengi juu ya kifo cha mwanamama machachari Anne Rwigara huko gerezani kunaibuka tukio lingine lenye utata kutekwa kwa familia ya Paul Manzi. Mwaka 2015 baba mzazi na tajiri mkubwa katika nchi ya Rwanda alikufa katika kifo cha ajali ya kutatanisha baada ya kutoa maoni juu ya utawala wa Kagame. Mzee Rwigara kabla ya kifo chake alikuwa ni mfadhili mkuu wa kikundi cha waasi wa RPF chini ya Kagame ambaye baadaye alikuja kuwa Rais.

Miaka mwili baada ya kifo cha Mzee Rwigara mtoto wake mpendwa Anne Rwigara anatangaza nia ya kugombea uRais uchaguzi mkuu nchini Rwanda. Kagame kwa hofu alimkamata binti huyu yeye na familia nzima akiwemo mama yake mzazi na kuwafunga jela kisha kuwanyang'anya na kutaifisha mali za familia vikiwemo viwanda huku tume ya uchaguzi ikiondoa jina lake. Binti Anne Rwigara akiwa gerezani anakufa baada ya kuwekewa sumu. Kiufupi ni kwamba hizi ndio fadhila ambazo Kagame ameilipa familia hii ambayo ina mchango mkubwa katika harakati zao za msituni wakipigania haki katika taifa lao la Rwanda.

Tukiwa bado tunatafakari roho ya Kagame dhidi ya tukio la Familia ya mzee Rwigara ghafla familia ya Paul Manzi Byabagamba ambayo ilikuwa ikiishi Tanzania baada ya kupata hifadhi ya kisiasa inatekwa na majasusi wa Rwanda kisha kurudishwa Rwanda.

Tukio la kutekwa kwa familia ya Paul Manzi Byabagamba kunazua maswali mengi ambayo kwa kiasi kikubwa maswali hayo yanavua nguo vyombo vyetu vya dola hasa idara yetu ya usalama wa taifa TISS.

Watanzania tunauliza ilikuwaje mkimbizi wa kisiasa ambaye yupo nchini na anayelindwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa zinazohusu hadhi ya wakimbizi anatekwa na majasusi wa nchi nyingine bila vyombo vyetu kujua?

Kwamba majasusi wanatoka Rwanda wanavuka pale border na kuingia nchini bila usalama wa nchi yetu kujua? Sasa kazi ya wale maafisa wa TISS, Polisi na Uhamiaji nini nini pale mpakani?

Kwamba baada ya kuteka familia nzima wakarudi tena wakapita mpaka/border hiyohiyo na kurudi Rwanda bila usalama wetu kujua?

Ama usalama wa nchi yetu ulijua na ulitoa ushirikiano kutekwa kwa familia hiyo kinyume na sheria za nchi na zile za kimataifa?

Suala lingine ni kwamba kwanini serikali ya Tanzania haijatoa tamko lolote kuhusiasa na tukio hilo? Hii ilikuwa lazima serikali ya Tanzania iwajibike kwa kuchukua hatua kwa sababu ndiyo ilipewa dhamana ya kuilinda familia hii kwa mujibu wa sheria za kimataifa kama ambavyo Ubelgiji ilihakikisha Tundu Lissu anakuwa salama. Mfano ni Uturuki ilipoamua kuichukulia hatua Saudia baada ya kifo cha Jamal Khashogi mwanaharakati na mwandishi wa habari aliyekuwa akikosoa utawala wa familia ya ufalme wa Saudia aliyeuliwa ndani ya ubalozi wa Saudia pale Uturuki. Hatua hizo zilifanya Saudia kuwageuka na kuwachukulia hatua za kuwahukumu kifo maafisa wake waliotumwa kumuuwa Jamal ndani ya ubalozi kule Uturuki. Lakini kwa Tanzania imekuwa kimya sijui ni kwa sababu ya serikali imekuwa Corrupted.

Kwa maoni yangu juu ya tukio hili sidhani kama kuna ushirika wowote wa serikali kuisaidia Rwanda kuteka raia wa Rwanda ambayo serikali ya Tanzania yenyewe imewapa hifadhi. Nashawishika kusema kwamba ni uzembe wa vyombo vyetu na tumezidiwa pakubwa katika masuala ya ujasusi/Usalama na Rwanda.

Mfano hai unatoka kwangu mwenyewe Mdude Mpaluka Nyagali. Novemba 2017 nilipokuwa nashikiliwa kituo cha polisi cha kati Posta Dar es Salaam nilikutana na raia mmoja wa Rwanda aliyeniambia amekamatwa kwa kuingia nchini bila kibali yani hakuwa na passport. Raia huyo ambaye majina yake niliyasau umri wake ulikuwa miaka 29 na dini yake alikuwa mkristo Msabato na alikuwa ameoa miezi kadhaa kabla ya kufanya safari Tanzania na kudakwa.

Jamaa huyo nilikaa naye selo moja pale shimoni Central Posta Dar na baadaye nilianza kumtilia mashaka baada ya kuwa anauliza sana mambo ya siasa za Tanzania na mara nyingi simlizi zake zinahusu uzuri wa Kagame na kuhalalisha vifo vya wapinzani wa Kagame kwamba wao ndio wenye makosa. Nililazimika kuanza kumchimba huyu jamaa kwa sababu pia mimi mwenyewe nilikaa kituoni hapo takribani mwezi mmoja bila kufikishwa mahakamani kwa kesi ya uchochezi lakini yeye kuvuka mpaka bila passport amekaa miezi 6 bila kufikishwa mahakamani.

Siku moja askari wa zamu alipoingia kuita majina ya mahabusu wote aliniomba nimshikie daftari moja ya register ya mahabusu. Kiufupi ni kwamba kila mahabusu anayeingizwa rock up lazima asajiliwe kwenye hiyo register ya mahabusu kuanzia majina yake, umri wake, dini na kesi iliyomleta polisi. Kwa hiyo nilichokifanya nilikaa karibu na askari huyo huku nikiwa nimemshikia daftari moja la register wakati akiwa anasoma majina ya mahabusu. Sasa nilikuwa nasubiri jina la jamaa nilichungulie kesi yake ni ipi haiwezekani kesi ya uhamiaji hapelekwi mahakamani wakati waethiopia wanaletwa kama leo kesho wanapelekwa mahakamani.

Kilichonishangaza ni kwamba jina la Jamaa huyo wa Rwanda lilipoitwa nilichungulia sehemu ya kesi yake nikakuta imeandikwa Taske Force kwa biki nyekundu. Nikajiuliza mbona hakuna kosa linaitwa Taske Force nchini? Baadaye nikajua jamaa kayakanyaga kwa wale wasiojulikana. Baada ya uchunguzi mwingine nikaambiwa jamaa aliingia rock up hapo tangu mwezi june 2017 akachukuliwa na jamaa zetu wa Taske Force wakaenda kumtesa kule kusikojulikana akateswa kama mimi then baada ya wiki 4 akarudishwa hapo Central akiwa hatembei kwa kipigo cha jamaa zetu wa Taske Force. Na hata baada ya suala lake kuwa wazi kwangu jamaa alishangaa nilipomsimulia aina ya watesaji wa Taske Force na aina ya mateso yao akatabasamu na kuniambia wewe Mdude ni mwanaume kama ulipitia mikono ya wale jamaa na hujaacha siasa.

Sasa tukirudi mwanzo ni kwamba jamaa alikamatwa kwa kosa la traffic barabarani akiwa na gari dogo ambalo ndani yake kulikuwa na Kapten mmoja wa jeshi la Rwanda ambaye aliasi jeshi la Rwanda na kukimbilia nchini na akawa anaishi ubungo bila vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kujua. Huyo Kapten akapata passport ya Tanzania na anasafiri kwenda nchi mbalimbali katika shuguli zake akitumia passport ya Tanzania.

Serikali ya Rwanda ilipojua ikamtuma huyo jamaa na sijui huyo kapten alifanywa nini lakini alijikuta yuko ndani ya gari akiwa amefungwa pingu na gari inatembea. Inadaiwa askari wa Usalama barabarani au Traffic barabara kuu ya Dar - Moro waliikamata gari hiyo kwa makosa ya kukiuka sheria barabarani sasa wakati Jamaa huyo kutoka Rwanda akitaka kutoa rushwa ili askari huyo awaruhusu waendelee na safari yule kapten akaamua kumwaga ugali na kupiga kelele. Askari waliposikia kelele inabidi wasogee na wakakuta kuna mtu anasafirishwa kijasusi na alipoulizwa inabidi aseme ukweli kwamba yeye ni kapten wa jeshi la Rwanda na alitoroka Rwanda na kuishi Dar anamekamatwa na anarudishwa Rwanda ili akauawe. Ndipo askari hao wakapiga simu kwa wakubwa na hapo ukawa mwanzo wa jamaa na Kapten wake kukamatwa.

Sasa kukamatwa kwa yule jamaa na Kapten wake kulipelekea mwenyekiti wa mtaa na maafisa wengine waliosaidia kapten huyo wa Rwanda kupata Passport ya Tanzania kukamatwa ijapo hawakufikishwa mahakamani waliachiwa baadaye. Kwamba bila traffic kusimamisha na kukagua gari hiyo pengine jamaa angekamilisha misheni yake bila kushtukiwa.

Jamaa nilimwacha rock up akiwa amekaa miezi 6 ya polisi posta bila kufikishwa mahakamani. Muda mwingi anaamka usiku kusali na wakati mwingine alikuwa analaumu ubalozi wa Rwanda nchini kwamba walifika hapo mara moja na waliahidi kulimaliza kidipromasia ili jamaa aachiwe lakini anaona kimya. Muda mwingi alijiona kama ni mtu aliyekufa na alikataa tamaa maana hata chakula ni mpaka tumpe sisi tuliokuwa tunakaa naye selo moja.

Sasa katika mazingira haya katika ulimwengu wa kijasusi ni matusi makubwa sana majasusi wa nchi nyingine kuingia nchi yenu na kufanya chochote wanachotaka bila nyie kujua. Bado nasisitiza kwamba nchi yetu imekuwa Corrupted karibia taasisi zote na inahitaji mabadiliko makubwa sana ya kimfumo, kisela, kisheria na kiutawala. Idara ya usalama wa taifa iliyoheshimika enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa leo imejaa vijana wa Green Gard kutoka Uvccm. Hakuna wanachojua zaidi ya kuteka, kuuwa na kuvuruga chaguzi. Idara imepoteza sifa na heshima ya kikanda na kimataifa.

Katika ulimwengu wa kidipromasia ni makosa makubwa sana serikali ya Tanzania kukaa kimya katika tukio la kutekwa kwa familia ya Paul Manzi Byabagamba katika ardhi ya Tanzania ambako alikuwa amepewa hifadhi ya ukimbizi. Nadhani Rais Samia anapaswa kujua kuwa jambo hili halimjengi katika ulimwengu wa kidipromasia bali linambomoa.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
20231229_150101.jpg
20231229_150105.jpg
 
labda kama wameruhusu icho kitu kifanyike. ila kama hajaruhusu, sasaivi samia alitakiwa awe amemfukuza balozi wa Rwanda.
Samia huyu huyu aliyechekelea kuuawa kijana wa kitanzania pale Palestina na sasa Balozi wa Palestina anazunguka misikitini akihamasisha ndugu zetu wawaunge mkono HAMAS ikiwemo kuandaa vijana wa kwenda kujiunga na HAMAS na anaangaliwa tu.
 
Samia huyu huyu aliyechekelea kuuawa kijana wa kitanzania pale Palestina na sasa Balozi wa Palestina anazunguka misikitini akihamasisha ndugu zetu wawaunge mkono HAMAS ikiwemo kuandaa vijana wa kwenda kujiunga na HAMAS na anaangaliwa tu.
sasa kama hatachukua hatua, yeye usalama wake upo wapi? kama kagame ataingia nchini na kufanya chochote na kutoka bila yeye kujua, siku akiamua kufanya chochote juu yake atashindwa? au anafikiria nini?
 
๐™ˆ๐˜ผ๐™…๐˜ผ๐™Ž๐™๐™Ž๐™„ ๐™’๐˜ผ ๐™๐™’๐˜ผ๐™‰๐˜ฟ๐˜ผ ๐™†๐™๐™„๐™‰๐™‚๐™„๐˜ผ ๐™‰๐˜พ๐™ƒ๐™„๐™‰๐™„ ๐™‰๐˜ผ ๐™†๐™๐™ˆ๐™๐™€๐™†๐˜ผ ๐™‹๐™–๐™ช๐™ก ๐™ˆ๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™ž ๐˜ฝ๐™ฎ๐™–๐™—๐™–๐™œ๐™–๐™ข๐™—๐™– ๐™๐˜ผ๐™„๐˜ผ ๐™’๐˜ผ ๐™๐™’๐˜ผ๐™‰๐˜ฟ๐˜ผ ๐˜ผ๐™‡๐™„๐™”๐™€๐™†๐™๐™’๐˜ผ ๐˜ผ๐™‰๐˜ผ๐™„๐™Ž๐™ƒ๐™„ ๐™‰๐˜พ๐™ƒ๐™„ ๐˜ฝ๐˜ผ๐˜ผ๐˜ฟ๐˜ผ ๐™”๐˜ผ ๐™†๐™๐™‹๐˜ผ๐™๐˜ผ ๐™ƒ๐™„๐™๐˜ผ๐˜ฟ๐™ƒ๐™„ ๐™”๐˜ผ ๐™๐™†๐™„๐™ˆ๐˜ฝ๐™„๐™•๐™„ ๐™’๐˜ผ ๐™†๐™„๐™Ž๐™„๐˜ผ๐™Ž๐˜ผ ๐™‰๐™„ ๐™๐™•๐™€๐™ˆ๐˜ฝ๐™€ ๐™’๐˜ผ ๐™‘๐™”๐™Š๐™ˆ๐˜ฝ๐™Š ๐™‘๐™”๐™€๐™๐™ ๐™‘๐™”๐˜ผ ๐™๐™‡๐™„๐™‰๐™•๐™„ ๐˜ผ๐™ ๐™†๐™๐™‰๐˜ผ ๐™๐™Ž๐™ƒ๐™„๐™๐™„๐™†๐˜ผ?

Wakati wapigania haki wa Africa Mashariki tukiendelea kuomboleza msiba mzito wa mwanaharakati wa Rwanda mwanamama Anne Rwigara aliyefia Gerezani kwa kuwekewa sumu na serikali ya Rwanda, kumetokea tukio lingine la kutekwa kwa familia ya Paul Manzi Byabagamba aliyekuwa anaishi nchini kama mkimbizi wa kisiasa.
Huyo aliyeuwawa huko USA nako.unasemaje?
 
Back
Top Bottom