Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kama ni kutazama hiyo habari moja tu iliyopostiwa hapo juu, hicho si kigezo cha kutosha kupinga au kuunga mkono suala la Tz kujiunga OIC. Msingi mkubwa wa kupinga ama kuunga mkono hoja ya OIC ni madhumuni ya hiyo taasisi, na kama Tanzania kama nchi inayakubali kimsingi. Hebu tujadili misimamo, malengo na madhumuni ya hiyo taasisi, na tuone kama Tanzania kama nchi inapaswa ama inaweza kukubaliana nayo bila kuathiri misingi yetu ya utaifa.
 
[/COLOR]

Asante sana Ngereja kwa charter hii muhimu.
Siku zote kumekuwa na mjadala kuhusu Tanzania kujiunga au kutokujiunga na OIC.Sikupenda sana kujiingiza ktk mjadala ila nilichangia kwa kuwaqtaka wana JF na watanzania wote kuweka itikadi za kidini pembeni na kujadili suuala hili katika sura ya kitaifa ili kuona:
- Nini hasa OIC kwa maana ya malengo, mtizamo n.k
- Nini faida za kujiunga na OIC kama taifa kwa ujumla wetu na siyo kikundi fulani tu
- Nini zimekuwa hasara kwa upande wetu kwa muda wote ambao hatujawa wanachama waOIC.
n lazima iwepo tafakari yakinifu juu ya kujiunga OIC.Tusiyumbishwe na imani ya mtu kwa namna yoyote ile.

Kwa kuitazama charter hii naona kuna haja kujiuliza kama kweli Tanzania ya waislamu,wakristo ,wabudha,wahindu na wale wote wenye dini na wasiokuwa na dini wanabebwa katika vipengele hivi vya charter ya OIC.

RESOLVED to preserve Islamic spiritual, ethical, social and economic values, which will remain one of the important factors of achieving progress for mankind;

DETERMINED to consolidate the bonds of the prevailing brotherly and spiritual friendship among their people, and to protect their freedom, and the common legacy of their civilization restoring particularly on the principles of justice, tolerance and non-discrimination;A) Objectives:
The objectives of the Islamic Conference shall be:

* to promote Islamic solidarity among Member States;
* to consolidate cooperation among Member States in the economic, social, cultural, scientific and other vital fields of activities, and to carry out consultations among Member States in international organizations;
* to endeavor to eliminate racial segregation, discrimination and to eradicate colonialism in all its forms;
* to take necessary measures to support international peace and security founded on justice;
* to coordinate efforts for the safeguarding of the Holy Places and support of the struggle of the people of Palestine, to help them regain their rights and liberate their land;
* to back the struggle of all Muslim people with a view to preserving their dignity, independence and national rights;* to create a suitable atmosphere for the promotion of cooperation and understanding among Member States and other countries

Kwa mtizamo wangu nashawishika kusema kuwa mambo niliyoyaweka rangi ya dark brown hayagusi ustawi wa watanzania wote bila kujali mipaka ya dini zao.Tupendetusipende OIC kama chombo kinavyojieleza ni jumuiya ya nchi za Kiislamu na inatambua uanachama wa nchi nyingine zisizokuwa za kiislamu kwa kigezo cha kuwepo kwa waislamu katika nchi hizo.

Tanzania kama taifa hatuna sababu ya msingi kujiunga OIC na vilevile hatuna sababu ya kujiunga na jumuiya ya nchi za kikristo au za kihindu kama zipo.Umoja wetu na mshikamano wetu unajengwa na utadumishwa hata kama hatupo OIC.

Ndugu zetu waganda wanazo sababu za kujiunga OIC na wala hazina uhusiano na misaada ya kiuchumi.Ni suala la kihistoria na iliwalazimu kufanya hivyo kwa wakati ule.

Tukijadiliana kwa fikra pana tutafika,tusishupE


Nadhani viongozi wetu wamtegemee Mungu na sio hii oic maana sasa wanatutakia majanga pindi taifa lolote likimkataa Mungu na kufata njia zake lenyewe ukubwa na madhara nadhani viongozi wamtegemee Mungu nae hatawapa ufahamu ni vipi nchi iendeshwe na uchumi utakuwa.
kujiunga mwishoe tutaanza kujiunga na umoja wakila kitu.

Tanzania isimame kama Tanzania.
 
Tujiunge OIC itatusaidia kupata misaada mingi, mfano; nyama ya mbyzi, tende na pia itatusaidia kuimarisha chuo kikuu morogoro
 
Kama ni kutazama hiyo habari moja tu iliyopostiwa hapo juu, hicho si kigezo cha kutosha kupinga au kuunga mkono suala la Tz kujiunga OIC. Msingi mkubwa wa kupinga ama kuunga mkono hoja ya OIC ni madhumuni ya hiyo taasisi, na kama Tanzania kama nchi inayakubali kimsingi. Hebu tujadili misimamo, malengo na madhumuni ya hiyo taasisi, na tuone kama Tanzania kama nchi inapaswa ama inaweza kukubaliana nayo bila kuathiri misingi yetu ya utaifa.

Je! hii oic wakiomba msaada kwetu ni ya ngapi hesabu sasa, Tatizo watu ni wavivu wakutafuta Data.
Sasa sisi tulio ambiwa eti tujiunge tutasaidiwa je hizo dolla watatoa wapi au kiini macho.


Source
With the advent of the holy month of Ramadan, the Organization of the Islamic Conference (OIC) intensifies its efforts to assist the Palestinian people in the Gaza Strip. The OIC has launched a second aid campaign by freighting medication, food supplies and other medical supplies, currently on their way from Jordan to the Gaza Strip.

On the occasion of this holy month rife with Muslim sentiments of goodness and mercy, the OIC appeals to all philanthropists and benevolent organizations across the Muslim Ummah to contribute generously to kick-start a third aid campaign that will hopefully have a palpable impact in alleviating the suffering of the Palestinian people in the Gaza Strip due to the unjust embargo.

Contributions can be made into the following bank accounts:

Number of dollar-denominated bank account: 5600...
Swift code: SAMB...
Samba Banking Group - main branch
Al-Andalus Street Jeddah


kwanini waombe msaada nadhani na sisi tukijiunga tutaambiwa tuchangie sasa hiyo itakuwa faida au hasara?
 
Polisi Z`bar wavamia wanaokula mchana

2008-09-25 13:28:33
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Polisi wa kituo cha Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, wamevamia nyumba ya mama lishe na kuwanyang\'anya sahani za wali watu waliokutwa wakila chakula mchana wakati huu wa Mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Tukio hilo lilitokea juzi mchana baada ya vibarua na mafundi wa kampuni ya ujenzi ya S.S. Mehta kwenda kupata huduma ya chakula nyumbani kwa mama lishe.

Taarifa kutoka katika eneo la tukio, zilisema baada ya polisi kuingia katika nyumba iliyozungushiwa uzio, waliwaweka chini ya ulinzi wateja wote na kuwataka kusalimisha sahani zao za vyakula walizokuwa nazo mkononi.

Mfanyakazi wa kampuni ya S.S. Mehta, Simoh Joseph, alisema alilazimika kusalimisha sahani ya wali pamoja na wenzake baada ya polisi kuvamia eneo hilo.

Alisema wafanyakazi wa kampuni hiyo walikuwa wana kawaida ya kula chakula nyumbani kwa mama liche huyo.

Alisema hakuna mtu aliyepewa nafasi ya kujitetea kwa kuwa wateja wote walitakiwa kusalimisha sahani za wali na wale waliowahi kumaliza chakula, sahani zao zilichukuliwa kama kielelezo.

Alisema baada ya hapo, askari waliondoka na mama lishe aliyekuwa akitoa huduma ndani ya nyumba yake kwa tuhuma za kuuza chakula wakati wa mchana.

Mhandisi wa kampuni hiyo, Josepha Marwa, alithibitisha kukamatwa kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kula chakula wakati wa mchana na chakula chao kuchukuliwa na polisi.

Je hapo Ofisi ya Kadhi itakapowekwa kwenye katiba mambo yatakuwaje na hao waliokamatwa watapelekwa kwenye mahakama ipi. Hakuna sheria ya nchi inayosema mtu asile mchana na watu wenyewe kazi yao ndio hiyo - unatakiwa ushibe. Na hiyo hasara ya contractor atagharimia nani. Lo, kazi kweli kweli.
 
Polisi Z`bar wavamia wanaokula mchana

2008-09-25 13:28:33
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Je hapo Ofisi ya Kadhi itakapowekwa kwenye katiba mambo yatakuwaje na hao waliokamatwa watapelekwa kwenye mahakama ipi. Hakuna sheria ya nchi inayosema mtu asile mchana na watu wenyewe kazi yao ndio hiyo - unatakiwa ushibe. Na hiyo hasara ya contractor atagharimia nani. Lo, kazi kweli kweli.

Ofisi ya kadhi itakapowekwa, itaangalia pia haki za wale wasio kuwa waislam, kutokana na maonevu kama hayo ya askari wenye kutumiwa na watu wenye chuki zisizo na msingi. Kwa maana ofisi ya kadhi ni kwa waislam na si kwa wale wasio waumini wa dini ya kiislam.

Hao watu hawana kosa kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, kwani sheria zilizopo zinakataza watu kula adharani wakati wa mfungo wa ramadhani. Hao polisi wamevunja haki ya msingi ya raiya halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya serikari ya Mapinduzi Zanzibar.

Kula Mchana kwa mujibu wa sheria za kiislam, kunaruhusiwa kwa watu wenye matatizo na maradhi mbali mbali amabayo yanaweza kumsababishia mfungaji madhara, pia kufunga kumesamehewa kwa wasafiri. Wasio kuwa waislam kwao si lazima na wala sheria ya kutokula mchana haiwahusu, as long as wanakula ndani ya majumba yao.

Hao askari wangefanya jambo la maana sana kama wangekwenda kule kwenye mahoteli ya kitalii, na kukamata kila mtalii na mfanyakazi anaye kula na kuuza pombe wakati wa mfungo wa ramadhani. Lakini kutokana na unafiki wa viongozi wa serikali ya znz hawayafanyi haya, wamekalia ufisadi na kuonea wanyonge na kuwaacha wengie.

Habari ndio hiyo matumaini umenielewa
 
mtoto akizaliwa pale zanzibar atakuwa mwislamu, akizaliwa kule rombo atakuwa mkatoliki, akizaliwa mzake pale dodoma atakuwa mu anglikan, akizaliwa marangu mtoni atakuwa mlutheri, akizaliwa kipera kule iringa atakuwa mu-orthodox, akizaliwa kule kandete tukuyu atakuwa monrovian, ugomvi wa nini? kuna aliyechagua azaliwe mahali hapo na kujikuta na dini hiyo? ngozi yetu na utaifa letu ndo muhimi zaidi

Mwikimbi hapa umesema ukweli hasa!
 
Badala ya Tanzania kujiunga na OIC kwanini muungano wa waislam wote Tanzania usiungane na OIC?
Ama kuna something i am missing?
Kama sivyo then i think ni politics.
 
Vatican ni nchi, ndio maana wana ubalozi wao hapa Tanzania na nchi nyingine. Nchi nyingine zinazoongozwa kidini pia zina ubalozi Tanzania. Hakuna aliyebaguliwa mpaka hapo. OIC ni muungano wa nchi za kiislamu, si muungano wa nchi ZENYE waislamu. Na hata OIC haiwezi kufananishwa na WCC (World Council of Churches), maana ile si baraza la nchi za kikristo, ni baraza la makanisa, kwa hiyo kinachojiunga kule ni makanisa si nchi. Kwa hiyo ndani ya WCC pia kuna makanisa yaliyoko katika nchi ambako wakristo ni minority kama China na Indonesia. Kama ingekuwa OIC ni muungano unaohusu waislamu peke yao bila kulazimisha nchi nzima kuwa wanachama mimi ningeona haihitaji kuuliza wasio waislamu, maana ni mambo ya imani ya waislamu. Kwa hiyo kusingekuwa na tatizo kwa waislamu wa Tanzania kujiunga na shirika lolote la kiulimwengu la waislamu. Tatizo la OIC linataka tuingizwe humo wote kama nchi, sasa hiyo kwangu ndio haikubaliki.

Kuna mifano mingi. Umoja wa makanisa ya Sabato duniani, Tanzania (kama dola) si mwanachama, lakini wasabato wa Tanzania ni wanachama huko, na ndio wanaohudhuria vikao na kuwaletea waumini wao kilichojiri, hatutumi waziri huko au mwakilishi wa Rais. Sasa hii OIC ukisoma charter yake, ni tofauti kabisa, ni muungano wa kidola, na una vikao vya wakuu wa nchi, nk. Sasa kitu kama hii huwezi kujiunga kama nchi si ya kiislamu kikatiba. Na kama kuna nchi ambazo si za kiislamu kikatiba lakini zimejiunga huko (kwa sababu zao mbalimbali), hiyo si sababu ya sisi pia kuvunja katiba yetu. "Two wrongs do not make a right"!
 
VIONGOZI WA DINI WENYE CHOYO NA HUSUDA!

UMEZUKA mtindo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini kuingilia masuala ya dini zingine kwa kisingizio hiki au kile. Ninadhani hiki sio kitu chema na mahusiano kati ya dini hiyo na watu wa dini nyingine yanaweza yakalikokota taifa kule tusikotaka.

Katiba ya nchi inasemaje kuhusu suala la Imani za watu? Hapa chini ni nukuu ya kifungu Na.19 ambacho ndicho kinachozungumzia suala la imani:

"19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
"

Uchaguzi hapa tunachukulia sio tu ni maamuzi bali utekelezaji wa yale yote muumini wa dini fulani anayoamini kwamba ni lazima yawepo ili aijenge imani yake kikamilifu.

Kwa mantiki hii Waislamu wana haki sio tu ya kudai haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi kama sehemu muhimu ya kukamilisha Uislamu wao bali pia na kushirikiana na wale wote ambao wanaweza wakasaidia kuupeleka Uislamu mbele ndani na nje ya nchi.

Hili liko wazi katika katiba: '20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi aukuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.'


Kama Wakatoliki nchini wanavyosaidiwa na Vatican ni muhimu vivyo hivyo kwa Waislamu kusaidia na vyombo kama IOC ili kuupeleka Uislamu wao mbele.

Ilivyo sasa ni kwamba serikali inaelekea kusema na kuendesha mambo yake kama vile Wakatoliki na madhehebu nyingine wana haki ya kupata misaada kutoka nje lakini eti Waislamu hawastahili kupata msaada wowote toka nje kwa sababu ya kusingiziwa kuwa wao Waislamu ni 'magaidi'!

Ieleweke kwamba katika nadharia za Uwezo na Mamlaka katika nchi vikundi mbalimbali vya watu vinahodhi kiasi fulani cha 'units of power' na hatari kubwa kwa nchi ni kikundi kimoja kupora 'units of power' za vikundi vingine au vikundi fulani kushisrikiana ili kupora vikundi vingine 'units of power'! Kinachotokea sio tu kwamba wanasiasa wanawapora Waislamu 'units of power'! bali pia Wakatoliki wanawapora moja kwa moja na vile vile kwa kushirikiana na serikali hiyo ambayo tayari inawapora Waislamu haki zao.

Hili haliashirii mema katika kuendelea kuwepo umoja na amani katika taifa hili.

Roho mbaya ya baadhi ya viongozi wa dini inawafanya washinikize serikali kuwanyima watu wa dini zingine haki zao za msingi na ushiriki wao katika kulea 'balance of power' ambayo ndiyo inayowezesha nchi kuwa na umoja na amani ya kweli.

Kinachoonekana hapa kwa kuwa kuna dini ina uongozi mkuu wa kimataifa na inasimamiwa katika misingi bora ya menejimenti na utawala; ina hazina kubwa inayotoka ndani na nje ya nchi; ina uwezo wa kifedha hata kurubuni viongozi wa kisiasa na serikali; ina waumini wake wengi kwenye nfafasi za maamuzi ya fedha, uchumi na maendeleo; ina taasisi zenye uwezo wa kujenga na kubadili fikira za wananchi; ina Ubalozi wa Kidni unaosaidia mambo yake; una mashirikiano na wenye fedha ndani na nje ya nchi kufanya mambo yao yaende vyema; na una wasomi na wataalamu wa kuweka misingi ya kuhodhi uwezo na mamlaka zaidi siku zijazo BASI DINI HIYO HAITAKI DINI NYINGINE nazo zipate fursa kama hiyo. Hii ni husuda, huu ni wivu, hii ni choyo na wala hakuna ajenda yoyote ya kidini kuingiliana na siasa hapa. Bali walio nacho wanataka wasio nacho waendelee kutokuwa nacho!

MIMI sina dini. Lakini kwa uchungu uliosababishwa na unafiki wa viongozi wa Kanisa la Katoliki imebidi niseme lile ninaloliona ndilo kwa hakika la ukweli na haki na sio vinginevyo!


sasa wewe huoni kama kuweka mahakama ya kadhi kutacontradict katiba yetu amabayo inasema watu wote ni sawa before the law. sasa leo iweje mwingine ahukumiwe kwa kupigwa mawe mpaka kufa na mwingine vinginevyo. mi naona kwenye maswala ya kuendesha inchi mambo ya dini yaachwe pembeni. la sivyo kila mtu akisema anataka ahukumiwe au aongozwe kutokana na dini yake yake, sijui kama patakalika hapa.
yani sis wenzetu wanaenda mbele, sis tunarudi nyuma alafu tunasema tunataka maendeleo. Maendeleao yatakujaje kama hatufuati mtiririko mmoja? Mfano mzuri, ni pale shule watu wanavyoruhusiwa kuvaa nguo zinazoonyesha imani zao.
Mi nafikiri Nyerere alitujengea msingi mzuri, kwamba mtu anapokuwa kwenye public school au public area yeyote awe neutral Ama sivyo aende shule za seminari ambako anaweza kuishi kutokana na imani yake.

Kwakweli inasikitisha kuona tunaingizwa OIC bila ya kushirikishwa sis wananchi. Mswala ya Ubalozi wa Vatican kuwa hapa, hayafanani wala kuhusiana na membership ya OIC. Vatican is a state ambayo kiongozi wake ni Pope, kama ambavyo kuna balozi za nchi nyingine, Vatican nayo ina haki ya kuwakilishwa hapa. Mfano nchi kama Islamic republi of Iran ina ubalozi hapa nchini na inafanana tu na iyo ya Vatican.

Nafikiri nimeeleweka maana I am not a very good Swahili writer.
asanteni
 
What you have said makes sense! Ila kwenye masuala ya dini / imani jamaa wengi huleta jazba zaidi na kuachana na mantiki, hivyo rahisi sana kutoelewana!

for your information, misaada ya Vatican siku hizi hamna, na hata iyo michache iliyobaki inawanufaisha Watanzania wote kwani shule, hospital n.k zinatoa huduma kwa watanzania wote bila kijali imani zao.

Misaadaya Vatican pia, ni misaada tu na haina masharti. wakati uko OIC tunaenda kuomba mikopo ambayo masharti yake hatujui yatakuwaje. inawezekana kabisa wakasema nchi yetu ni lazima itawaliwe kwa Sharia..... tutakubali???
mbona umaskini unatupeleka pabaya????
mi nafikiri tufike mahali tujipange tujikwamue wenyewe. I dont think anybody from outside Tanzania is interested to help us for real. nia yao ni kutubana kwenye kona ambapo we will reach a point where we will have no choice zaidi ya kutekeleza matakwa yao.

kwakweli I am so disappointed na watanzania hasa hao viongozi wetu!!!!!! lol
 
Masuala yanayohusu dini yabaki kuwa ni masuala ya waumini wa dini husika kujiunga au kuanzisha vyama au kujiunga na shirikisho lolote mradi hawaendi kinyume na sheria za nchi. Kulazimisha mabadiliko ya katiba ya nchi ili cheo cha kadhi kitambulike na kubadili katiba ya nchi kuruhusu Tanzania iwe mwanachama wa OIC haya ni mambo ya ajabu kabisa.
 
Ukitaka kuona jazba ya wabongo taja mambo yanayohusu dini, utashangaa katika mada nyingine wanajenga hoja vizuri lakini ikifika dini tatizo. Punguzeni jazba na zijengwe hoja kama kukubaliana au kupingana basi hoja ndio ziamue na si jazba wala uchoyo.

Ni kweli Tanzania haina dini lakini watanzania wana dini na serikali inaowajibu wa kuwasaidia wananchi kuabudu katika dini wanazotaka, serikali pia ni watu. Kama katika ibada na sikukuu za kidini serikali inatoa ulinzi kuhakikisha waumini wanaabudu kwa imani zao basi ni sahihi kusema serikali inasaidia waumini kuabudu kwa gharama za walipa kodi bila kujali imani za walipa kodi.

Sidhani kama kuna tatizo lolote katika hili la serikali kusaidia waumini wa dhehebu fulani. Kama Membe amesema ruksa kujiunga OIC kwa faida ya waislamu wa Tanzania na haitaathiri uhuru wa dini zingine hiyo safi, hata kama ingekuwa Wasabato pia ingekuwa safi hakuna haja ya kuogopa.

Labda tu siku hizi kinachoonekana kuna baadhi ya dini lazima zitoke na misimamo yao baada ya serikali kuamua jambo. Hii sio safi, waacheni watu waabudu wanavyoona wao sahihi na halivunji sheria za nchi hata kama linawakera. Haikutokea na haita tokea watu wote tukawa na imani sawa, na dunia inapendeza zaidi watu wakawa na imani tofauti.

Tukumbuke pia dini zenyewe tumeletewa kwa malengo na madhumuni ya walio tuletea, kubeba bango na kuona wengine hawako sahihi sio poa tujenge hoja maisha yaendelee, kwa wasio waislamu mnapoteza nini Tanzania ikijiunga OIC. Isijekuwa mtu mwenyewe anachukia kusikia dini flani na anatumia dini yake kusema hisia zake.

Kauli mbiu ya Forum Hii izingatiwe katika kila jambo linaloletwa mbele, acheni woga wa kujadili dini zenu na viongozi wa dini zenu. Inapojengwa hoja nao wanapata mwongozo wa kwenda mbele na wenyewe ni binadamu na wanakosea pia, sio kila wanalo sema basi ndio msimamo wenu.

Vatican City [ˈvætɪkən ˈsɪti] (help·info), officially the State of the Vatican City (Italian: Stato della Città del Vaticano), is a landlocked sovereign city-state whose territory consists of a walled enclave within the city of Rome. At approximately 44 hectares (110 acres), and with a population of around 800, it is the smallest independent state in the world by both population and area.[2][3][4]

Vatican City is a city-state. It came into existence only in 1929. It is thus clearly distinct from the central authority of the Roman Catholic Church, known as the Holy See, which existed long before 1929. Ordinances of Vatican City are published in Italian. Official documents of the Holy See are issued mainly in Latin. The two entities even have distinct passports: the Holy See, not being a country, only issues diplomatic and service passports; the state of Vatican City issues normal passports. In both cases the number of passports issued is extremely limited.

The Lateran Treaty in 1929, which brought the city-state into existence, spoke of it as a new creation (Preamble and Article III), not as a vestige of the much larger Papal States (756-1870) that had previously encompassed central Italy. Most of this territory was absorbed into the Kingdom of Italy in 1860, and the final portion, namely the city of Rome with a small area close to it, ten years later, in 1870.

Vatican City is a non-hereditary, elected monarchy that is ruled by the Bishop of Rome — the Pope. The highest state functionaries are all clergymen of the Catholic Church. It is the sovereign territory of the Holy See (Sancta Sedes) and the location of the Pope's residence, referred to as the Apostolic Palace.

The Popes have resided in the area that in 1929 became the Vatican City only since the return from Avignon in 1377. Previously, they resided in the Lateran Palace on the Caelian Hill on the opposite side of Rome, which was out of repair in 1377. The signing of the agreements that established the new state took place in the latter building, giving rise to the name of Lateran Pacts, by which they are known.
Source Vatican City - Wikipedia, the free encyclopedia

OIC
The Organization of the Islamic Conference (OIC) is an international organization grouping fifty seven States which have decided to pool their resources together, combine their efforts and speak with one voice to safeguard the interests and secure the progress and well-being of their peoples and of all Muslims in the world.

The Organization was established in Rabat, Kingdom of Morocco, on 12 Rajab 1389H (25 September 1969) when the First meeting of the leaders of the Islamic world was held in the wake of the criminal Zionist attempt to burn down the Blessed Al-Aqsa Mosque on 21 August 1969 in the occupied city of Al-Quds.
Under the Charter, the Organization aims to:
1. Strengthen:
a) Islamic solidarity among Member States;

b) Cooperation in the political, economic, social, cultural and scientific fields;

c) The struggle of all Muslim people to safeguard their dignity, independence and national rights.


2. Coordinate action to:

a) Safeguard the Holy Places;

b) Support the struggle of the Palestinian people and assist them in recovering their rights and liberating their occupied territories.


3. Work to:

a) Eliminate racial discrimination and all forms of colonialism;

b) Create a favourable atmosphere for the promotion of cooperation and understanding between Member States and other countries.
sOURCE www.oic-un.org/about_oic


HEBU WASOMI WETU WAKRISTO KWA WAISLAMU KABLA YA KUCHANGIA HOJA HAKIKISHA UNAELEWA JAMBAO UNALOTAKA KULISEMEA. KWA WALE WASIOJUA VATICAN BASI FAHAMUNI JAMANI HII NI NCHI, CITY STATE. HIVYO KUWA NA UBALOZI NA KUSAIDIA INAOWATAKA NI RUKSA. KAMA VILE TUNAVYOONA MATAIFA MBALI MBALI YAKISAIDIA MAENEO WANAYOTAKA. HATA BAADHI YA BALOZI NA MATAIFA YA KIARABU YAMEKUWA YAKISAIDIA MISIKITI, MASHULE NA TAASISI MBALI MBALI ZA KIISLAMU. HIYO NI RUKSA!

NA KAMA NI KUPATA MAHAKAMA YAO YA KADHI NI SAHIHI MRADI ISITUNGIWE SHERIA MAANA TANZANIA NI SECULAR STATE! WAO WANAOPENDA NA KUHESHIMU DINI YAO, WASULUHISHANE KWENYE VIKAO VYAO VYA DINI. WAKRISTO NAO WASULUHISHANE KATIKA MAKANISA YAO. WAPAGANI WAITANE KATIKA VIKAO VYAO VYA UKOO MBELE ZA MIUNGU YAO YA ASILI. KWA NINI MUNGU ASAIDIWE NA SHERIA YA NCHI WAKATI NI HIARI MTU KUMFUATA. KAMA WAKITOKEA WAISLAMU WASIOTAKA KUFUATA VIZURI MISINGI YA UISLAMU NAO WAPATE HAKI YA KUTOAMINI UISLAMU (HATA WAKI RETADI WASIBUGHUDHIWE!) WABAKI NA HAKI YA KUCHAGUA IMANI YAO WANAYOTAKA KUIFUTA AU KUTOIFUTA. KAMA MKRISTO, MWISLAMU AU MPAGANI ASIPORIDHIKA NA UTARATIBU WA DIN YAKE AENDE MAHAKAMA YA WATU WOTE ISIYOJARI DIN YA MTU. LAKINI KUWEKA SHERIA ITAKAYOMBANA MTU KWENYE SUALA LA IMANI SI SAWA. NA KUWABURUTA WANANCHI WOTE NDANI YA OIC NAYO SI SAWA. KWA NINI IFIKIRIWE KUWA TANZANIA NI NCHI YA KIISLAMU WAKATI SIO? HUU UTAKUWA UTAPELI! MAANA OIC INATAMBUA KUWA NCHI WANACHAMA NI NCHI ZA KIISLAMU ZINAZOTAFUTA MSHIKAMANO KATIKA KUTETEA MASLAHI YA UISLAMU NA KUENDELEZA MATAIFA YAO. HIVI WAISLAMU TWAMBIENI TANZANIA NI NCHI YA KIISLAMU? HATA KAMA TUTAPOTEZA MISAADA LAKINI LAZIMA TUWE WAKWELI TANZANIA HAINA SIFA YA KUJIUNGA NA OIC. KAMA WAGANDA NA MOZAMBIQUE WALITAPELI LAZIMA NASI TUWAIGE?
 
Date::10/23/2008
Waziri Membe akana kuubeba msalaba OIC
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

WAZIRI wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, amekuja juu akisema baadhi ya watu wamekuwa wakimtwisha mzigo kwamba, ameingiza Tanzania katika Jumuiya ya nchi za Kiislam Duniani (OIC), kitu ambacho si kweli.

Kauli hiyo ya Membe ni ya kwanza kuitoa hadharani tangu kuibuka kwa kasi kwa mjadala huo, ambao unaonekana kuigawa nchi katika misingi ya kiitikadi.

Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam jana, Membe alisema si kweli kwamba Tanzania imekwishajiunga na OIC na wala yeye hajasema lazima ijiunge.

Membe akifafanua huku akionekana kuguswa na tuhuma hizo dhidi yake kutokana na kutamka hilo bunge katika hotuba ya bajeti ya wizara yake, alisema uamuzi wa kujiunga au la, uko kwa wananchi.

"Nimekuwa kimya, kuachia na kusikiliza watu waseme, jamani, Tanzania haijajiunga na OIC wala sijasema lazima ijiunge," alisema na kuongeza:

"Uamuzi wa kujiunga au kutojiunga utakuwa chini ya wananchi, wasomi, NGOs na ninyi waandishi wa habari, ndiyo mtakaoamua."

Membe alikuwa akifafanua kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Iran, ambao unaonekana na baadhi ya watu kama wenye nia ya kuingiza nchi OIC.

Akifafanua zaidi, alisema watu wasiingize vitu visivyokuwa na msingi kwa ajili ya kutunga na kuzungumzia hisia, na kushauri wasome historia kufahamu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Membe huku akionekana kuchukizwa na fikra mbovu za kupandikiza udini katika nchi, alisema Watanzania ni watu wanaoheshimika duniani kwa umakini wao, ni aibu na haipendezi kujadili udini.

Alisema kama ni kujiunga na OIC ni jambo la kuamua, kwani Uganda ambako kuna Waislam asilimia 10 imeweza kujiunga huku Wakristo wakiwa ni asilimia 66 na wengine wapagani.

"Sasa jamani, msitake kunichinganisha na watu wangu, nawaambieni tena na tena, Tanzania haijajiunga na OIC na haitaweza kujiunga uamuzi huo ni ridhaa ya wananchi," alisisitiza.

Kwa ufafanuzi, alisema aliwahi kuzungumzia ripoti ya utafiti ya Juni mwaka 1993, ambayo inatoa mapendekezo matatu ambayo ni pamoja na kuingia kuwa kama mwangalizi kisha wananchi wataamua.

Akizungumzia zaidi uhusiano huo na Iran, Membe alisema ziara yake ya hivi karibuni ililenga kuomba kupunguziwa au kufutiwa deni la zaidi ya sh 270 bilioni, ambazo Tanzania inadaiwa.

"Sasa mtu anapohoji urafiki wetu na Iran, ana maana gani, anataka hizi fedha tuzilepeje, kama taifa lina matatizo yake sisi hayatuhusu, tunasimamia maslahi ya taifa," alisema.

Katika hatua nyingine, Membe alionya mwamko wa demokrasi ya mgawanyo wa madaraka baada ya uchaguzi na kwamba, mfumo huo unaojengeka ni wa hatari.

Alisema haiwezekani kuruhusu utaratibu huo kwani utazidi kuhatarisha demokrasi katika bara la Afrika na kuongeza kwamba, ni vema demokrasi ikaheshimika wakati wa uchaguzi.

"Huu mtindo wa baada ya uchaguzi watu kuanza kupiga kelele, sijui siridhiki, kisha wagawane madaraka asilia 40, ni wa hatari, lazima ukomeshwe na usiendelee," alionya Membe.

Hivi karibuni kumeibuka mtindo, ambao chama tawala hugawana madaraka na vyama vingine vya upinzani kama ilivyofanyika baada ya uchaguzi mkuu wa Desemba 27 mwaka jana nchini Kenya, kati ya ODM na PNU na sasa Zimbabwe kati ya ZANU-PF na MDC.
 
Membe awashangaa wanaoihofu OIC
Mwandishi Wetu
Daily News; Thursday,October 23, 2008 @20:15

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ameeleza kushangazwa na hatua ya baadhi ya Watanzania kuogopa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC).

Membe ambaye alilazimika kuzungumzia suala hilo baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wanahabari aliozungumza nao Dar es Salaam jana alifafanua kuwa Tanzania bado haijajiunga na OIC bali iko kwenye mchakato wa kufanya hivyo.
Mwandishi huyo alihoji uhusiano wa Tanzania na Iran kuwa unaleta wasiwasi kwa kuwa nchi hiyo iliwahi kuisaidia Tanzania huku misaada hiyo ikiwa inaambatana na Koran.

Alihoji kama uhusiano huo sio mwanzo wa Tanzania kuingia OIC. Membe ambaye alionyesha kuchukizwa na swali hilo alijibu; "Jamani twende wapi kutafuta misaada, nikienda Marekani mnapiga kelele kuna jambo, tumeenda Iran unatoa hoja zao, twende wapi, Yemen? "Naomba sasa wewe mwandishi unayepinga tusiwe na uhusiano na Tehran niletee nchi mbili ambazo unaona hazina matatizo ndizo tushirikiane nazo kiuchumi," alisema Membe.

Waziri huyo alifafanua kuwa hata hivyo suala la Tanzania kujiunga ama kutojiunga na OIC liko mikononi mwa Tanzania. Alisema makundi yote ya wananchi yatatoa mawazo yao hivyo kwa sasa hakuna haja ya kuogopa wala kuzusha mijadala isiyokuwa na manufaa kwa nchi.

Katika mazungumzo yake hayo Membe alionyesha kushangazwa na woga wa baadhi ya watu baada ya Tanzania kutangaza kuanzisha mchakato wa kujiunga na jumuiya hiyo.

"Woga wa Watanzania unatoka wapi kujiunga na OIC? Mbona tunaaminiwa duniani, iweje leo tuogope kitu hiki?" alihoji Membe na kuongeza; "Kama kuna shetani ana fedha zake kwa nini tusiende kuzichukua? "Hata kama wewe ni Mwislamu una njaa na kuna nyumba ambako kuna nyama ya nguruwe na ng'ombe, iweje ugome kuingia, kwa nini usiingie uchukue nyama ya ng'ombe na kuondoka?" alisema.

Waziri huyo alitolea mfano wa Uganda kuwa nchi hiyo yenye asilimia 60 ya Wakristo na asilimia 10 ya Waislam huku asilimia 30 wakiwa Wapagani bado haijageuzwa nchi ya Kiislamu na wala hakuna misikiti iliyosambaa katika taifa hilo ingawa ni mwanachama wa OIC.

Alisema badala yake nchi hiyo imekuwa inafaidika kwa kiasi kikubwa na misaada kutoka katika jumuiya hiyo licha ya kuwa haina Waislam wengi kama ilivyo kwa Tanzania. Akizungumza namna Watanzania watakavyoshirikishwa katika mchakato huo alisema wataamua hali ibaki kama ilivyo sasa lakini pia kuna baadhi ya watu wataenda kuangalia katika nchi zingine ambazo zimejiunga na jumuiya hiyo.

"Watanzania wana uchaguzi wa kufanya, kujiunga ama la, lakini nashangazwa na hoja hizi zinatoka wapi wakati tunaaminiwa duniani kwa jeuri yetu…jamani hakuna haja ya kuogopa," alisema Membe. Waziri huyo alisisitiza kuwa msimamo huo wa Tanzania wataelezwa pia kwa upande wa Zanzibar.

Alisema mwaka 1993 kilichotokea ni kutokuwapo kwa utafiti kuangalia iwapo Tanzania itajiunga na jumuiya hiyo itafaidikaje na athari zake ni zipi. Tanzania ilitangaza nia yake ya kuanzisha mchakato wa kujiunga na OIC katika kipindi cha bajeti ya mwaka huu wakati Waziri Membe alipokuwa anawasilisha mapato na matumizi ya wizara yake bungeni.
 
Membe kachemsha sana kwa sababu hajui Uganda ilingiaje OIC na nani aliingiza Uganda OIC na kwa sababu zipi. Kumbuka Wapalestina na Walibya waliwaunga mkono jeshi la Uganda kwenye uvamizi wa Idi Amin Tanzania. Hebu soma hapa chini :-

Elizabeth Namazzi
Kampala


IT comes as a surprise to many Ugandans that our country is a member state of the Organisation of Islamic Conference (OIC).

With Christians making up 80% of the population and Muslims accounting for only 12 %, it is indeed a surprise that Uganda belongs to a Muslim body. Delegates from the OIC member states met in Kampala from June 16 to June 20 to discuss issues affecting them. How Uganda found herself in the same block with Arab countries can be traced to one ambitious leader.

His dream was to be a life president, but it was slipping out of his grasp pretty fast. He had to find a way to strengthen his weakening political base. He did not look further than the Muslim world, which was sympathetic to his political woes.

The year was 1974, and Idi Amin Dada placed Uganda in the fold of OIC. His hope was that in any eventuality of war, his brothers in faith would offer their support to ensure his stay in power. It never happened. Instead, when Amin was overthrown in 1979 and Saudi Arabia did the next best thing - they offered him asylum.

He welcomed their offer and enjoyed Saudi Arabia's hospitality up to the time of his death in 2003. But 29 years after Amin's overthrow, Uganda is still a member of the OIC. Many Christian leaders are not amused by this, and have tried several times to cut Uganda's ties with the body.


The Muslims, however, have resisted any such attempts. There was an uproar within the Muslim community when Christian leaders called for Uganda's withdrawal from OIC in 2002. One of their arguments against Uganda's withdrawal was that Islam was here before Christian missionaries even heard of the country, and they are right.
 
Najiuliza nashindwa kuelewa kuna nini hapa! 1990's enzi za Hassan mwinyi nchi iliingia kwenye sakata la IOC, bahati likapita...na sasa enzi hi za Jakaya Kikwete limerudi tena! mbona enzi za Benjamin Mkapa halikujitokeza? Hivi hili swala linauhusiano na imani/dini ya rais?Jamani huu si udini tu? Kweli ni analysis za kiuchumi ndio zinaleta haya au imani ya kidini?
Mungu aepushe...hili linaonekana ni la kidini zaidi ya manufaa mengine. Kikwete ana mtumia kibaraka wake Membe kufanikisha hili ili kujiondoa kwenye lawama! Jazba alitokuwa nayo Membe mbele ya waandishi wa habari ni wazi kuna something "fishy" about the whole issue. Alionekana dhahiri dhamira inamsuta. Jumuiya ya kiislamu wakati nchi yetu sio ya kiislamu! Nadhani watanzania tusimame kidete nchi isifanyiwe maamuzi ya 'kinduli' kama ilivyotokea Uganda.
 
Hivi hii debate ya OIC siyo imewekwa kutufanya tuache kuwaza na kufuatilia kesi za EPA na tuhuma nyingine za ufisadi kweli??!!
 
Hii ya OIC kama JK atatuningiza huko naamini rais atakayefuata atakuwa na jambo rahisi la kuitoa nchi huko! Kama JK alivyofuta baadhi mambo ya Mungai na Mkapa katika elimu ndivyo ambayo rais ajaye atakavyotutoa huko OIC! Yaani hawa jamaa wameishiwa ya kuwaza mpaka wanawaza OIC! Nchi na raslimali zote hizi watu bado wanafikiria kwenda kuomba tu!!!!!! Hivi tuko sawa kweli!
 
..nani alisema IOC ndio muarubaini wa matatizo yetu????...hii tabia ya kulelewa kwa kutegemea kukinga mikono kwa mamwana tunaitoa wapi?..nchi iliyosheni madini ,wanyama,mabonde ya kilimo yanayotririka maji siku zote...tunataka Mungu atupe nini basi ,kiasi cha kujiunga na taasisi ambayo wengi wa wananchi hawaitaki....

...kama wanataka na wajiunge na nchi haitatawalika!!!
 
Back
Top Bottom