Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 4, 2006.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 4, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa mara nyingine tena hoja ya Bunge kupitisha sheria ya kurudisha ofisi ya Kadhi Mkuu linajitokeza tena huku waislamu wakitaka Bunge litunge sheria ya kutambua uwepo wake na wakristu wakipiga kelele kuwa kufanya hivyo ni kuvunja Katiba. Hoja yangu leo ni kuwa, Waislamu hawahitaji kibali cha serikali kuanzisha ofisi ya Kadhi Mkuu kushughulikia mambo yao yanayoendana na sheria za Kiislamu.

  Waislamu wakae wao wenyewe wapitishe uwepo wa ofisi hiyo na kuendelea na shughuli zao. Ilimradi tu, maamuzi ya ofisi yao hiyo hayaingilii uhuru wa Mtanzania mwingine au utendaji kazi wa sheria zetu za makosa ya uhalifu na jinai. Pia waelewe ya kwamba uwepo wa ofisi ya Kadhi Mkuu ni subject ya Katiba ya Muungano na Mtanzania yeyote kimbilio lake la mwisho ni mahakama ya Kiraia. Zaidi ya yote, watakapoanzisha ofisi hiyo, wajue kuwa isiwalazimishe waislamu wote kutatua matatizo yao kupitia ofisi hiyo isipokuwa wale ambao kwa hiari yao wanataka kufanya hivyo.

  Kanisa Katoliki kwa mfano linayo mahakama yake na sheria zinazoliongoza kanisa hilo (Canon Law) na mahakama yake hiyo ina ngazi za rufaa hadi Vaticano. Hata hivyo Mkatoliki ana haki ya kutumia sheria hizo kuhusu masuala mbalimbali ya kanisa lake, lakini anapofanya kosa la jinai, sheria za kiraia (civil law) zinakuwa na mamlaka. Hivyo basi, waislamu wasisubiri Bunge kupitisha ofisi ya Kadhi Mkuu bali waianzishe wao wenyewe huku wakiweka bayana kabisa kuwa ofisi hiyo haitahusika na makosa ya jinai au kupingana na Katiba ya nchi. Then, hakutakuwa na haja ya kugongana!!!
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Aug 5, 2006
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,777
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,
  Zanzibar waliomba warejeshewe Ofisi ya Kadhi Mkuu, SMZ iliitikia wito huo. Kitu cha ajabu ni malalamiko yaliyojitokeza kwamba kwanini Kadhi Mkuu ateuliwe na Raisi wa Zanzibar. Vilevile wengine walilalamika kwamba kwanini Kadhi Mkuu awe chini ya mamlaka ya Waziri ambaye ni Mkristo, Bw.Adam Mwakanjuki.

  Kuleta nafasi ya Kadhi Mkuu kupitia Bunge na Katiba kutaleta migogoro isiyo ya lazima kati ya serikali na Waislamu. Naunga mkono mapendekezo yako kwamba Waislamu waungane wamchague Kadhi Mkuu bila kuishirikisha serikali na vyombo vyake.

  Ikiwa Wamaasai wameweza kuwa na mfumo na utaratibu wao wa mila na uongozi sioni kwanini Waislamu washindwe kuwa kitu kimoja na kumchagua Kadhi Mkuu. Wamaasai wana utaratibu wa kuchagua Laigwanan ktk jumuiya ndogo ndogo, halafu kutokana na hao huchaguliwa kiongozi wa Laigwanan wote.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 5, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wanaotaka tuamini kuwa suala la Kadhi linawahusu waislamu wao peke yao. Ukweli wa mambo ni kuwa suala hili ni la Watanzania wote na tuna haki ya kulizungumzia. Ninazichambua hoja dhaifu za kina Ponda Issa Ponda, Khalifa Khamisi na Mufti. KLH News... yote yanazungumzika!!!

  Back with a vengeance... www.mwanakijiji.podomatic.com
   
 4. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2006
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tume ya Kurekebisha Sheria yakabidhiwa jukumu
  *Wananchi na wadau wote watakiwa kutoa maoni
  *Waziri Nagu awaomba Watanzania waache malumbano
  *Aonya yanaweza kuipeleka nchi yetu mahali pabaya


  Na Julius Samwel

  BAADA ya malumbano ya kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi Mkuu Tanzania Bara kupanda moto, serikali sasa imeamua kuirejesha hoja hiyo kwa wananchi ili waijadili na kutoa maoni yao kama inafaa kuwepo au la.

  Hoja ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo imezua mvutano mkubwa baina ya viongozi na waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu kwa miezi kadhaa sasa.

  Wakati waislamu wamekuwa wakipigania kutaka serikali ianzishe mahakama hiyo kupitia sheria ya Bunge, Wakristo kwa upande wao wamekuwa wakiipinga kwa maelezo kuwa itasababisha madhara makubwa katika jamii siku zijazo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk Mary Nagu, alisema serikali imeamua kulipeleka suala hilo kwa wananchi kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria, kutokana na malumbano juu yake kuelekea katika kuleta mvutano na mpasuko miongini mwa Watanzania.

  "Serikali imeiagiza Tume ya Kurekebisha Sheria kuifanyia kazi hoja hii ili baadaye tume hii iishauri serikali kuhusu ufumbuzi halisi wa suala hili kwa kuzingiatia maslahi ya taifa, historia ya nchi yetu na matakwa ya wananchi," alisema.

  Alisema wakati suala hilo linafanyiwa kazi na tume ya kurekebisha sheria, wananchi wote watashirikishwa kwa uwazi mkubwa wakati wote wa mchakato wa huo.

  Waziri Nagu alisema serikali itahakikisha inatumia busara na hekima katika kulishughulikia suala hilo na wadau wote watashirikishwa kutoa mawazo yao.

  Aliwataka wananchi kuacha malumbano yanayoendelea kwa sasa kuhusu suala hilo na waliachie serikali ilifanyie kazi kwanza.

  "Ndugu wananchi, kwa unyenyekevu mkubwa, ninawaomba kwamba malumbano yanayoendelea na yanayoelekea kuleta mvutano na mpasuko miongoni mwetu, tuyaache na kuyaacha kwa maslahi ya taifa letu, ninawaomba sana," alisema.

  Alisema ni wajibu wa serikali kushughulikia mambo ambayo yanayonekana kuwa kero, likiwamo suala la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi kama ilivyoanishwa katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005.

  Nagu alisema historia ya jambo hili inaonyesha jinsi ambavyo serikali ilivyolipokea na hatua ilizozichukua na inazoendelea kuzichukua ili kulitafuatia ufumbuzi na kwamba mchakato wa kulitafuatia ufumbuzi bado unaendelea.

  Suala la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi mkuu nchini lilianza 1999 na lilitolewa na na Waislamu kwa Rais Benjamin Mkapa katika kilele cha Sikukuu ya Idd el-fitr na Rais aliahidi kulifanyia kazi.

  Baadaye suala hilo liliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2002 kama hoja binafsi na aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya.

  Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo, Spika wa Bunge, kwa kutumia kanuni za Bunge aliliwasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Sheria na Katiba, ambayo iliunda kamati ndogo kwa ajili ya jambo hilo.

  Nagu alisema kamati hiyo ilifanya ziara katika nchi za Kenya, Uganda, Musumbiji na Afrika Kusini ili kujifunza namna suala la kadhi linavyoshughulikiwa katika nchi hizo.

  Alisema ikiwa Kenya, kamati hiyo iliambiwa kuwa mahakama ya kadhi inatambuliwa na katiba ya nchi na kwamba kuna sheria maalum iliyotungwa ambayo inampa madaraka Rais kuanzisha mahakama hiyo.

  Alisema mahakama hiyo ina madaraka ya kusikiliza mashauri ya yanayohusu hadhi binafsi, ndoa, talaka na mirathi pale ambapo wahusika wote ni waislam. Hata hivyo, mahakama hiyo inafanya kazi katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

  Alisema nchi za Uganda na Msumbiji hazijaanzisha mahakama ya kadhi na kwamba Afrika Kusini inatambua ndoa za Kiislamu na wanaoshughulikia masuala hayo ni viongozi wa kidini wanaoitwa Amir.

  Malumbano kuhusu kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi yalianzishwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki katika mkutano wao na Rais Jakaya Kikwete miezi michache iliyopita.

  Katika mkutano huo, maaskofu hao walimweleza Rais kuwa wamepata taarifa za kuandaliwa kwa muswada wa kuanzisha mahakama ya kadhi na wakaiomba serikali ichukue tahadhari kubwa katika suala hilo.

  Siku chache baadaye, viongozi wengine wa kanisa hilo waliitisha mkutano na waandishi wa habari, nao wakieleza kwa kina athari zinazoweza kutokea iwapo mahakama hiyo itaanzishwa kwa sheria ya Bunge, wakisema inaweza kuleta madhara makubwa dhidi ya watu wasiokuwa Waislamu.

  Hata hivyo, viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakisisitiza waachiwe hoja hiyo kwa kuwa inawahusu wao na si waumini wa dini nyingine.

  Mbali na Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiinjili la Kiluthari Tanzania (KKKT), nalo limetoa tahadhari ya kaunzishwa kwa mahakama hiyo, likisema iwapo sheria itapitishwa na Bunge, inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii ya Kitanzania katika siku za baadaye.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi kama Waislam watakosa Mahakama yao na CCM ilisha wapa ahadi je mwaka 2010 CCM watakuwa na lugha gani juu ya ahadi hii ?Hebu Mzee Es nipe mawazo yako maana ni Chama chako abacho kimevamia sera hii .
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Sep 18, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hili wala halihitaji mtu uwe mwana Sayansi kulitafutia ufumbuzi... Serikali ijiondoe na iwape baraka zote waislamu kuanzisha mahakama hiyo!!
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Serikali acheni kupoteza pesa za wananchi, toeni tamko tu kwamba seriakli haina dini, na suala la mahakama ya kadhi liko juu ya uwezo wenu (waislamu), maadamu haitapingana na katiba ya nchi.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 18, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ila wakifanya hivyo hawatapa msosi...! so lazima wale na kumegeana!
   
 9. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2006
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Mahakama ni sehemu ya serikali. Serikali ina mihimili 3, yaani Utendaji (Executive), Utunzi wa Sheria (Bunge) na Mahakama (Judiciary).

  Iwapo Mahakama ya Kadhi itaanzishwa kwa sheria ya Bunge, basi itakuwa ni sehemu ya Judiciary, yaani itakuwa ni mojawapo ya mihili ya serikali. Katika nchi ambayo serikali haifungamani na dhehebu lolote, kama ilivyo Tanzania, ni kosa la kikatiba kwa Bunge kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

  Kwa serikali kupeleka hili jambo kwa wananchi ina maana gani? Kama wanataka kubadilisha katiba ili dini ya Kiislamu iwe sehemu ya serikali, basi wafanye hivyo bila kificho. Waache kupoteza fedha za nchi na muda wa wananchi.

  Augustine Moshi
   
 10. Wiki iliyopita muhubiri maarufu wa dini ya kiisilamu nchini She yahaya aliingilia suala la kadhi mkuu , huyu yeye akawa anateta hoja ya waisilamu kuwa na kadhi wa kwa ajili ya kuwatetea katika mambo yao

  Hoja alizozitoa ni pamoja na kwamba eti , waisilamu wamegawanyika sana , kutokana na kuwa na misikiti mingi na madhehebu mengi kwahiyo mahakama ya kadhi itawaunganisha na kuwa na chombo chao sababu nyingine ni kwamba huu mgawanyiko unaifanya bakwata isiwe na nguvu katika maamuzi kwa waisilamu wengine kwa kuwa kuna baadhi ya watu hawaitambui bakwata .

  Pia alisema mahakama za kawaida zinashindwa kutatua matatizo mengine ya waisilamu mahakama ya kadhi ndio inatosha kwa zote hizi , mimi tangia nimezaliwa miaka 24 sijawahi kusikia kwamba mahakama imeshindwa kutoa hukumu kwa mtu wowote yule kwa misingi ya dini ?

  Kabla ya huyu pia siku chache mzee mwinyi nae alikuja na hoja za ukadhi , naye alitetea ukadhi , sasa najiuliza kwanini huyu mwinyi hakuleta ukadhi wakati yeye akiwa kiongozi wan chi enzi hizo alikuwa anamuogopa nani kwanini hakujadili enzi zake anazileta sasa hivi kama sio kuletea shida wengine ?

  Napenda kuwasihi vijana wa kiisililamu na waisilamu wote popote walipo wasigubali kutumiwa kisiasa na watu ambao wameshashiba mamlaka wameshaishiba hii dunia hawajali wanachosema wanasema tu ilimradi waonekane wameongea lakini kuongea kwao hakuna chachu yoyote katika maendeleo ya nchi hii na watu wake .

  Lazima mambo ya dini yaondolewe katika maisha ya kawaida ya mwadanamu haswa mtanzania kwanza hizi dini ni za kuja sio za asili yetu kwanini tunazingangania tangia zimeingia tumepata shida sana , tabu na majuto mengi na sasa hii mahakama ya kadhi inataka kutetenga watanzania .

  Viongozi wa dini nyingi walivyosema mahakama ya kadhi haitakiwi kujadiliwa hawakua wajinga na sio mbumbumbu wanajua ubaya wa mahakama hizo na wanajua kwa mifano kwa nchi zingine , hivi mfano waikrito nao wakiamua kuwa na kadhi wao itakuwaje ? wahindu nao je ?? kuna maana gani ya kuwa na katiba ya nchi kama watu wengine wataanzisha mahakama zao ?

  Inasemekana hizi mahakama zitakuwa zinapewa ruzuku na serikali kwasababu ni ilani ya CCM tangia wakati wa uchaguzi mkuu wamwaka jana , nashangaa hawa CCM nani alitengeneza ILani yao ? hii ni ilani ya kutupagawisha watanzania na kutugawa mafungu kama kule Sudan , kwanini katika Ilani kuwe na hoja kama hizo za kadhi ??

  Basi tuna haki ya kusema kwamba CCM ni chama cha kidini , kwa sababu katika Ilani zao za uchaguzi zina hiyo ishu ya kadhi , kadhi ni kuingilia masuala ya ndani ya dini ingine kuichokonoa .

  Kikwete alivyosema kutenganisha dini na siasa basi yeye awe muazo wa kubadilisha hivyo , Aondoe ilani ya ukadhi ndani ya katika ya CCM kisha tumuelewe , na pia atoa tamke rasmi kuhusu kadhi , sisi kaama wananchi tumuelewe sio anakimbia hoja hii

  Tumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Udini katika Nchi hii watu wananyamaza sasa hivi limekuja suala la ukadhi watu wananyamaza pia – tena inahusiana na siasa iko katika Ilani ya CCM taifa

  Tutambue kwamba nchi yetu ni nzuri na inapendeza kwa watu wake na mambo yake sasa haya mambo yasiharibu watu na kuwagawanyisha

  Hii maana yake nini kama sio kututenganisha watanzania ??
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Oct 6, 2006
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mh... Ni mawazo yako kaka... Hakuna asiye na hoja na kila hoja inategemea na mtoaji wake. Jamii hii ina mapana na naamini kuna wenye mtazamo hasi na uliyoainisha hapa. Suala hili upande wangu naona LIMENIZIDI kwakuwa si mwislam na sijui wao wananufaika vipi na Mahakama ya Kadhi. Lakini kumbuka Mrema alisisitiza kuwepo kwa kadhi mkuu Tanzania... Nae ana hoja...
   
 12. S

  Sindbad Member

  #12
  Oct 12, 2006
  Joined: Oct 12, 2006
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza natoa shukurani zangu kwa wana Jambo kwa maoni yao . Kuhusu swala la kadhi maoni yangu ni kua katika haki za raia moja wapo ni haki ya Imani yake, sasa Serikali ina wajibu wa kuheshimu haki hiyo kwa raia zake na huku ikihakikisha kua haki hiyo haitumiwi vibaya, sasa mimi naona sio haki wala jambo la busara kuhukumu jambo kabla hata hilo jambo halijafanya kazi zake , la muhimu ni kua Serikali itafakari na kulitazama kwa kina na kuweka sheria ambazo zitakua na manufaa kwa wenye Imani hiyo BILA kuhatarisha au kuharibu haki za wenye Imani tofauti, maana haki ya kuabudu ni ya kila raia bila kuhatarisha haki za wengine, na katika kila Imani kuna sheria zake sasa kuamini bila kufuata sheria zake inakua Imani haijakamilika .

  No one is above the law:confused:
   
 13. f

  freemind Member

  #13
  Oct 27, 2006
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SINDBAD, naomba unisaidie katika suala hili la kadhi.
  1. Kwani hamuwezi kuweka hao makadhi bila ya bunge kuidhinisha?????
  2.Hiyo mahakama ya kadhi itatoa adhabu gani?? na je kuna magereza ya Kadhi yatakayoanzishwa????

  Wasiwasi wetu ni kuwa mahakama hizo ndio mwanzo wa kuwa na taifa la kiislamu ambalo sharia za kukata watu mikono zitakuwa ninatawala.
   
 14. S

  Sindbad Member

  #14
  Oct 29, 2006
  Joined: Oct 12, 2006
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mr Freemind,

  Kwanza Kumbuka Serikali raia zake ni wa Imani tofauti na pia kama kuna viongozi wa Imani fulani wataka kufanya jambo ktk nchi lazima iwakilishe maoni yao ktk Serikali sasa kwa kujibu swali lako la kwanza ni kua hawawezi fanya jambo bila kuiomba Serikali ombi lao na Serikali lazima ikae na kutafakari jambo hilo ikizingatia haki na usalama kwa wote.

  Pili ni kua Makadhi sio wanataka kua na Jela zao wenyewe hapana ila wanataka kama watu wa Imani yao wakiwa na matatizo yao basi wanaweza tatua kwa kutumia sheria za Imani yao sasa hapo ni juu ya Serikali kukubali au kukataa na mm siwezi sema lolote maana Serikali kila mara husema haina dini.

  lakini ktk mambo haya kuna sababu zilizofanya haya labda mimi na wewe hatujui.
   
 15. S

  Sensee New Member

  #15
  Dec 4, 2006
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ninavyojua Serikali yetu haina dini. Ukitaka kila imani iwe na jinsi yake ya kuamua kesi basi unakaribisha dini ndani ya serikali na wewe ni hatari sana kuliko hata Shekh Osama Bin Laden na haufai katika jamii. Habari ya Imam ni mpang mkamilifu kutoka nchi za Kiarabu na mpango wa OIC. Tuliyoyasikia Nigeria yatakuja kwetu. Kwa nini tusiamini mahakama zetu? Kama zina matatizo basi turekebishe na sio kuingiza kitu cha imani fulani, hili halifai kabisa.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jan 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Bila ya shaka Vatican ni nchi kamili ndio maana tuna uhusiano nao wa kibalozi. Binafsi sioni jambo kubwa hapo. Lakini wale ndugu zetu wenye hisia za udini wanasema nini kwa Rais wa Tanzania, Muislamu kualikwa na Serikali ya Vatican inayoongozwa na Papa?
   
 17. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2007
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Let him go.
   
 18. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2007
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kwangu habari ni hii hapa:
  Kwa hiyo Dk Migiro hakukosea au kuzungumza kwa bahati mbaya kuhusu msimamo wa Tanzania kuhusu Iran na nyuklia.
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  JK aende kisha awaeleze idadi ya WATANZANIA WAKATOLIKI ambao wamekufa kwa sababu ya msimamo wa VATICAN kuwaambia wafuasi wao wasitumie CONDOM hilo la MAPADRE WALAWITI awaahie hao waamerika watadela na vatican
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jan 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  je serikali ya Tanzania inafikiri vipi kuhusu maneno ya Rais wa Iran ambaye anataka kutengeza silaha za Nyuklia za "kuifuta Israel kutoka katika Ramani ya Dunia?"
   
Loading...