Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Matusi haya kama ningekuwa muislamu ningeandamana kwa hili

Yaani inaonekana uislamu unafanywa kama wale watoto wa vipofu barabarani, wanatumika kuomba hela, this is shame siyo swala la kujisifu! Kikwete anatumia divide and rule, ameshindwa kutataua matatizo anajificha kwenye mwanvuli wa dini!


waberoya
 
Matusi haya kama ningekuwa muislamu ningeandamana kwa hili

Yaani inaonekana uislamu unafanywa kama wale watoto wa vipofu barabarani, wanatumika kuomba hela, this is shame siyo swala la kujisifu! Kikwete anatumia divide and rule, ameshindwa kutataua matatizo anajificha kwenye mwanvuli wa dini!


waberoya


...mimi marafiki zangu wengi kuanzia shule za chini hadi chuo kikuu hadi sasa ni waislamu kama walivyo wakristo ,wahindi nk.....kati ya vitu tangu nikiwa mdogo nilikuwa vinanikera ni tabia ya baadhi ya wazazi waislamu kuwahimiza watoto wao waende ijumaa madukani na kwenye mageti ya matajiri [waislamu] kusubiri kugawiwa swadaka...hilko liliniumiza sana....niliona ni kama kujenga tabaka la omba omba au kujenga tabaka la wanyonge ambao daima watawasujudu matajiri....niliwaeleza marafiki zangu ambao kwa bahati walijaliwa kuzaliwa kwenye familia za kati [working class] kama mimi..na tulikubaliana kwa pamoja kuwa ni jambo la kukemea na tusikubali ndugu zetu wawe miongoni mwa wanaaounga foleni kwenye mageti ya matajiri kusubiri sadaka...tena matajiri wengi kwa dharau...watu watasubiri wee yeye atatoka saa 10 na kuanza kuwagawia shilingi elfu moja moja.....

MYTAKE..kama mtu umejaliwa si lazima utake watu waje kukusujudu getini kwako wakipigwa na juwa ndio uwape visenti vyako...unaonaje ukiwafuata nyumbani kwao? unaonaje ukiwajengea kisima?unaonaje ukiwafungulia saccos!!!

HAPA NAMAANISHA TUSIJENGE TAIFA LA OMBA OMBA...WATOTO WA AINA HII WANAOPANGA FOLENI KWENYE MAGETI YA MATAJIRI HATA WAKISOMA WAKIPATA MAMLAKA WANABAKI NA INFERIORITY COMPLEX NA HATA AKIKABILIWA NA TATIZO LINALOTATULIKA KWA KUFANYA KAZI OPTION YA KWANZA KICHWANI KWAKE ITAKUWA NI KUTAFUTA TAJIRI ILI AMUOMBE MSAADA...HATUTAWEZA KUWAFANYA WATOTO WETU WAJITEGEMEE KWA AINA HII YA MALEZI...

HADI LEO HII MARAFIKI ZANGU WOTE WAISLAMU WAMEKATAZA JAMAA ZAO KWENDA KUJIPANGA FOLENI KWA MATAJIRI.....

HADIDHI HII YA KWELI NIMEITOA KAMA KUJENGA MAUDHUI YA SISI KAMA TAIFA.....JE TUMEONA SULUHISHO LA MATATIZO YETU NI KUJIPANGA JUANI KUSUBIRI SWADAKA ZA OIC?????...AU NI MATOKEO YA VIONGOZI WALIOZEZETWA UTOTONI NA MAZOEA YA KUJIPANGA KWENYE MAGETI YA WAKUBWA KUOMBA CHOCHOTE....

TUSIKUBALI KUWA WATUMWA WA AKILI ....BORA TUKAKOPE BENKI YA DUNIA NA IMF ..NA TUTALIPA KWA JACHO...LAKINI SI KWENDA KUJIUNGA MAHALI KWA KUTEGEMEA KUPEWA BURE BURE.,.......

KWANI IMEELEZWA KUWA MWANAMUME ATAKULA KWA JASHO NA MWANAMKE ATAZAA KWA UCHUNGU!!!
 
Mzee Philemon, kwani sasa hivi hakuna misaada nchi yetu inayopokea kabla ya kujiunga na OIC?

Acheni hizo wazee na machuki yenu ya kidini. Ndio maana taifa hili haliwezi kupiga hatua kwasababu kuna watu vipaumbele vyenu ni: Imani zenu, Matumbo yenu kisha ndio Taifa.

Acha ngonjera za kashfa!

NN
 
Asilimia kubwa ya watanzania ni Waislamu na ni haki yetu kujiunga na OIC...kama ilivyokuwa haki yetu kuwa na mahakama ya Kadhi itaesuluhisha matatizo ya kifamilia, ya kibinafsi na ya kibishiara kwa waislamu...nchii hii ni huru na sisi sote tuna uhuru wa kuamua. Tafadhali tusilete chuki za dini, sisi wote ni watanzania na kama viongozi wetu wameona kwamba tutapata manufaa kutokana na kujiunga na umoja huu basi RUKHSA!
 
Acheni hizo wazee na machuki yenu ya kidini. Ndio maana taifa hili haliwezi kupiga hatua kwasababu kuna watu vipaumbele vyenu ni: Imani zenu, Matumbo yenu kisha ndio Taifa.

Acha ngonjera za kashfa!

NN

....alaaa kumbe OIC inahusu dini....mimi nilifikiri unataka kunishawishi kwa sababu za kiuchumi...ukinipa na mifano hai namna uganda na mozambique...zilivoweza kuondoka kwenye list ya nchi masikini duniani....

..ndio narudi pale pale ..malezi tuliyopata yanatofautiana ...mimi binafsi sijafundishwa kumpigia yeyote goti ili nipate mkate wangu....nimefundishwa kutumia uwezo wangu binafsi wa akili,mazingira yanayonizunguka.....msaada niliofundishwa kuupokea ni wa mbegu....huo unaniwezesha kuotesha ili nikivuna mwakani nisipewe tena msaada ...bali nami nitoe...

sijafundishwa kunyenyekea mwanadamu.....wala sijafundishwa kumdhalilisha mwanadamu....kwa kutaka anisujudu ...na eti badala ya kumpa mbegu na jembe ili kesho asije kuniomba tena ..nampa pilau na senti chache ili na kesho tena nione fahari wakinijalia upenuni mwangu kusuburi tena msaada wa tumbo...

ninatoa wito tuwafunze watoto wetu kujitegemea na kujiamini...hilo ni muhimu sana hawa ndio viongozi wa kesho ,iwapo tutawalea kwenye mazingira ya kujipanga foleni kusubiri matajiri.....kesho wakiwa viongozi hawataona hatari kuuza uhuru wetu .tu kwa ajili ya jumuia fulani ambayo inatoa sadaka .....tutakuwa na tofauti gani kama taifa na watoto,kinamama na kinababa wazimaa wanaosubiri nje ya mahekalu ya matajiri kusubiri walau watoke wawapatie fedha kidogo za tumbo.....matajiri wa aina hii katu hawatataka ujikomboe ..kwani ukishajikomboa hutakaa tena nje ya majumba yao kusema yalaah msaada....na fahari yao itakwisha!

tanzania ijiunge na jumuia za kiuchumi....tunao uwezo wa kukopa na kulipa ......hatutaki makombo ya waarabu......

waarabu waliowachukua babu zetu na kuwahasi ...na kuwafanya wanawake....waarabu wanaoendekeza kujenga ukoloni mamboleo miongoni mwetu la kujenga tabaka ambalo kwao unyonge na umaskini na kutumikia wao huona kuwa ndio majaliwa yao ....na kuwaona waarabu kuwa ni halali yao kusujudiwa.....naaam wapo waarab weusi wanaonea fahari utamaduni wa kunyenyeakewa.....

HATUTAKI HIYO OIC ....AU CHOCHOTE CHA AINA HIYO....TUNA AKILI NA MIKONO IMARA......

OIC NI HOJA ILIYOSHINDWA INAYOLETWA NA VIONGOZI WALIOSHINDWA KAZI...ILI KUTAKA SYMPATH YA TABAKA LA WATANZANIA.....KWA KUJUWA WATAWAPA ...HAWAWEZI ASILANI!!!!....NA ITABAKIA KAMA HADIDHI YA FISI NA MWANADAMU...MKONO HAUTADONDOKA ....MWAKA 2015 UTAFIKA MTAJIKUTA MMEKOSSA OIC,MAHAKAMA YA KADHI,....NA MAISHA BORA VILE VILE......

NA HUYU MEMBE..ANATAKA HURUMA YA KUNDI FULANI AKIJUWA KUWA MWAKA 2015 UTAFIKA OIC HAITAPATIKANA .....NA AKIJUWA WATAMPA YEYE ILI AWAPE OIC.......

NASHAURI KUWA KAMA ZANZIBAR WANATAKA OIC ,...WARUHUSIWE KUJIUNGA KAMA INSTITUTION MEMBER.....
 
Huyu Membe kama anatembeleaga JF ajue kuwa Watanzania na hasa ambao si Waisalamu hatuko tayari kukubali hilo na kama alikuwa anota Uras siku za usoni ni vema ajue kuwa ndo imeshatoka na haiwezekani labda apate kura za Waislamu. Inaonekana ni kama OIC na Mataifa ya Kiislamu yaliusaidia mtandao wao kupata madaraka maana kutoa mifano ya Uganda na Marekani inahusiana vipi na sisi TZ na kujiunga OIC? Nchi na Katiba zinasema Nchi hii haina dini na OIC ni taasisi ya kidini na jina lenyewe linajionyesha hivyo- ORGANISATION OF ISLAMIC COUNTRIES (OIC) sasa kujidanganya huku kwatoka wapi? Yaani Membe anataka kutufanya Watanzania wote Mabwege! Mbunge mmoja alishawaonya Wanaotaka kutufnaya sisi mabwege na akawaambia- Watanzania si Mabwege Tena! na huo ndo ukweli, enzi za kuburuzwa aimeisha!
 


Katika mazungumzo yake hayo Membe alionyesha kushangazwa na woga wa baadhi ya watu baada ya Tanzania kutangaza kuanzisha mchakato wa kujiunga na jumuiya hiyo.

“Woga wa Watanzania unatoka wapi kujiunga na OIC? Mbona tunaaminiwa duniani, iweje leo tuogope kitu hiki?” alihoji Membe na kuongeza; [COLOR="DarkRed[COLOR="Red"]"]“Kama kuna shetani ana fedha zake kwa nini tusiende kuzichukua?
“Hata kama wewe ni Mwislamu una njaa na kuna nyumba ambako kuna nyama ya nguruwe na ng’ombe, iweje ugome kuingia, kwa nini usiingie uchukue nyama ya ng’ombe na kuondoka?[/COLOR]” alisema.

size][/color]


Membe katoa jibu la msimamo wa serikali kwa uwazi kabisa kuwa wao katika serikali hawaogopi kuchukua hela za shetani kama wana njaa.

Anahimiza watu kutoogopa kuchukua hela za shetani yeyote awe wa EPA au Richmond kama wana njaa.

Nimekuelewa Membe kumbe ndiyo maana hamuwachukulii hatua mashetani wa EPA na RICHMOND kumbe pesa zao huwa mnazila kwa kuwa mna njaa.

Na mko tayari hata kupokea hela za Shetani wa OIC ili muingize udini na mambo ya kadhi kwenye katiba tumekuelewa.

Watu wazima tumekusikia na tumekuelewa msimamo wako na serikali kuwa mkiwa na njaa ya pesa hamjali chochote.Hata imani zenu za dini zinazokataza dhambi mko tayari kuzitupilia mbali ili mradi mpate pesa zikiwemo za kifisadi.
 
Mkuu.

Pongezi kwako kwa hili.
Unajua mawazo ya kibaguzi huwa hayaletwe na mtu ila ni sisi wenyewe.Nyinyi wachangiaji wenzangu hapo juu,mngeweza hata kufanya uchambuzi tu kidogo wa hayo malalamiko yenu alafu ndio mlete hapa.

sasa ona hata Nigeria imo kwenye hii organisation,kama wafatiliaji wa mambo mnakumbuka Nigeria ndio BIAFRA ilipo,hiyo ndio hata ilimfanya Nyerer agombane na Amin lakini agalia hata wao leo wamo kwenye OIC.
tufikiri kwanza kabla ya kuleta UBAGUZI wetu kwa wenzetu
But Mr . Bauer , we need schematics for that building called OIC.So as once we are in ,we should not get lost.We do not have Chloe O'brian to guide us as a nation.Chloe is DEAD , JACK.
 
Nafikiri mtazamo mkubwa walionao viongozi wetu ni kwamba tukijiunga na OIC basi nchi itafaidika na misaada kutoka katika jumuiya hiyo. Hebu waachane na fikira potofu za kila mara kufikiria jinsi ya kupata misaada. Nchi haiendelei kwa misaada bali ni jitihada binafsi na utashi wa kisiasa wenye malengo ya kukwamua hali duni ya kiuchumi. Na isitoshe kila jumuiya ina masharti yake je tupo tayari kuyatekeleza hayo?
Tafakari - je Uganda ambao wamejiunga na OIC ni bora kuliko sisi? Ni kipi kipya walichopata ambacho TZ cant live without it? Membe na wenzake waonyeshe na watafsiri sera zao na jinsi zitakavyoleta mapinduzi ya kiuchumi na si kutegemea misaada.
 
Asilimia kubwa ya watanzania ni Waislamu na ni haki yetu kujiunga na OIC...kama ilivyokuwa haki yetu kuwa na mahakama ya Kadhi itaesuluhisha matatizo ya kifamilia, ya kibinafsi na ya kibishiara kwa waislamu...nchii hii ni huru na sisi sote tuna uhuru wa kuamua. Tafadhali tusilete chuki za dini, sisi wote ni watanzania na kama viongozi wetu wameona kwamba tutapata manufaa kutokana na kujiunga na umoja huu basi RUKHSA!

Hii ndo hatari iliko na ndo tunajua hili shinikizo linatokea wapi na kwa nini limekuwa shinikizo kubwa wakati viongozi wa nchi wakiwa Waislamu i.e Mwinyi na sasa JK lakini kumbuka sio Waisalmu waliompa kua nyingi JK na tena ni Maaskofu ndo waliompigia chepuo bila kujua kuwa 'JK ni chaguo la Mungu'.

Ukweli ni kuwa Waislamu hupiga kura kwa mgombea ambaye wanaamini atakubaliana na matakwa yao ya kidini kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu. Naamini uchaguzi ujao (kwa kuwa Waislamu walianza hivyo) Wakristo nao watapiga kura kwa kuzingatia hilo na mwisho tutakuwa na Jamhuri mbili-moja inayotambua na kukubali misingi ya Kiislamu kutumika katika nchi hiyo na Jamhuri nyingine ambayo labda itabaki kuwa secular.

[QUOTE]Asilimia kubwa ya watanzania ni Waislamu na ni haki yetu kujiunga na OIC[/QUOTE]

Uongo mwingine wa mchana kweupe. Sijui hizo takwimu umezipata wapi. Tumia kigezo kuangalia mikoa ya Tanzania na angalia predominant religion halafu base hata hiyo conclusion yako kwa kualngalia hili.
 
Wewe Philemon acha UNAFIKI.

Kwanza mwambie jamaa yako MBOWE aache kwenda kuomba misaada huko Marekani na Ulaya.

Kinachowaudhi watu wenye chuki za kidini kama wewe ni hilo neno Islamic kwenye hiyo OIC. Hampo tayari kuona lolote lenye alama ya Uislam/Uarabu (OIC, Iran, nk) linapata nafasi Tanzania hata kama ni kwa maslahi ya Taifa zima.

Hizo hadithi nyingine tumeshazizowea.

NN.
 
Asilimia kubwa ya watanzania ni Waislamu


hiyo sensa ulifanya nini?
na ni haki yetu kujiunga na OIC...

Haki yenu "waislamu" au haki yenu kama Watanzania? Kama ni haki ya Waislamu tu kwanini Bakwata isijiunge yakaisha?

kama ilivyokuwa haki yetu kuwa na mahakama ya Kadhi itaesuluhisha matatizo ya kifamilia, ya kibinafsi na ya kibishiara kwa waislamu...

Kwani kuna mtu kakataza hilo; Waislamu wakitaka kuwa na Mahakama ya Kadhi waanzishe (wasilipiwe wala kuendeshwa na kodi ya watanzania wote unless kuwe na kodi maalumu ya Waislamu tu inayokusanywa na serikali)

nchii hii ni huru na sisi sote tuna uhuru wa kuamua.

isipokuwa uhuru wa watu wengine kuamua kutoingia OIC au kutokuwa na Mahakama ya Kadhi? Kwanini uhuru huo wa kuamua ni uhuru kwenu tu na kwa wengine siyo uhuru?

Tafadhali tusilete chuki za dini, sisi wote ni watanzania na kama viongozi wetu wameona kwamba tutapata manufaa kutokana na kujiunga na umoja huu basi RUKHSA!

Yaani mtu hawezi kupinga kati isipokuwa kwa chuki..
 
Asilimia kubwa ya watanzania ni Waislamu na ni haki yetu kujiunga na OIC...kama ilivyokuwa haki yetu kuwa na mahakama ya Kadhi itaesuluhisha matatizo ya kifamilia, ya kibinafsi na ya kibishiara kwa waislamu...nchii hii ni huru na sisi sote tuna uhuru wa kuamua. Tafadhali tusilete chuki za dini, sisi wote ni watanzania na kama viongozi wetu wameona kwamba tutapata manufaa kutokana na kujiunga na umoja huu basi RUKHSA!

Hizo data mwenztu umezitoa wapi? Kampeni mpaka humu. May be Membe atupe data kamili, maana kama kaweza kutupa za Uganda nafikiri zetu hazitakuwa tatizo.

Ushauri wa bure: Tufikirie kwa kutumia akili, siyo hisia!!!!!!!
 
Habari zilizonifikia sasa hivi Maaskofu wa CCT na TEC wametoa kauli kali kuhusu kampeni ya Serikali ya Tz kuiepeleka nchi OIC na wamemtaka Membe ajiuzulu kwa kuchukua msimamo kuhusu Tanzania kujiunga na OIC. Wamemshutumu kuwa ametoa msimamo kabla Baraza la Mawaziri kukaa na kuamua kuhusu hilo.

Mwenye data zaidi atupe, mimi ntapata BBC jioni na magazetini kesho. Mwenye nakala (soft copy) atuwekee hapa.
 
Hao maaskofu mawazo yao yanawakilisha kundi moja la watanzania kwahiyo wasituburuze tutaingia oic kwa manufaa ya hao maaskofu na vizazi vya pia
 
Habari zilizonifikia sasa hivi Maaskofu wa CCT na TEC wametoa kauli kali kuhusu kampeni ya Serikali ya Tz kuiepeleka nchi OIC na wamemtaka Membe ajiuzulu kwa kuchukua msimamo kuhusu Tanzania kujiunga na OIC. Wamemshutumu kuwa ametoa msimamo kabla Baraza la Mawaziri kukaa na kuamua kuhusu hilo.

Mwenye data zaidi atupe, mimi ntapata BBC jioni na magazetini kesho. Mwenye nakala (soft copy) atuwekee hapa.

kazi ndio kwanza inaanza
 
Membe alifananisha Uganda kujiunga na OIC licha ya kwamba wana asilimia 10 tu ta waislam ukilinganisha na Tanzania ambayo kama sikosei ina wasilam asilimia kama 60 ya population yake.
Sasa kuna habari kuwa ni Idi Amin ndiye aliyei ingiza Uganda kwenye OIC na inasemekana bado kuna mgogoro kuhusu uwepo wa mkataba huo.
So tusiwadanganye wananchi..Nyie mnadai kuwa eti tunasaidiwa na tunapata misaada kwa kujiunga na OIC..Kwasababu mko out of touch nyie viongozi wetu..Bado mnafikiri watanzania ni wajinga.
Mmekosea..Watu weshajuwa wao ni matajiri ila nyie ndio Babylon wenyewe...Mnawadanganya na huku mna mabilioni kwenye benki za nje na mnaishi kama wafalme.
Shida ni kwamba tuna tabaka tayari la watawala na watawaliwa na hivyo watawala kwa kipindi kirefu wamedhani kuwa wao ndio wameteuliwa na Mungu kututawala wao na vizazi vyao....Huku wakituamulia mambo based on their assumptions kuwa sisi ni masikini na kwahivyo basi ni lazima tuwasikilize hao tunaowamba.....Na kukubaliana nao kwa kila kitu kwasababu hatujui tutalipaje.

Hiyo siyo shida, Shida ni kwamba hakuna uzalendo...Mbona China walikuwa na uongozi wa Dynasty lakini bado walijitahidi kuwasaidia wananchi na wanasonga mbele?

Sisi undumila kuwili na kutaka ubosi na madaraka zaidi ya kulitumikia Taifa na kujuwa kuwa uongozi ni dedication ya kuwatumikia wananchi na si kuwasikilizisha unachotaka wewe ama unachoona ni sawa kwa manufaa yako wewe na watu wako na mabwana zako.
Akili ya kitumwa tutaifuta na tutalikomboa Taifa letu...GOD WILLING.

NB:Membe alidai kuwa pesa za shetani ni za kwenda kuchukuwa...Hakusema ama hakuweka wazi kuwa pesa hizo za shetani kama alivyodai..Zina mkataba...Kwahiyo ni kwamba yuko radhi kuingia mkataba na shetani.
Hayo aliyasema yeye...Na mimi namwambia hivi..Kama ni kweli wanawatayarisha hao magraduates huko bongo...Je ule usemi wa there is nothing as such as a free lunch mnawaambia?
Nadhani mgefanya hivyo wananchi wangeleezwa kwamba kwenye makubaliano hayo kuna nini.
 
Membe alifananisha Uganda kujiunga na OIC licha ya kwamba wana asilimia 10 tu ta waislam ukilinganisha na Tanzania ambayo kama sikosei ina wasilam asilimia kama 60 ya population yake.

Kuweka takwimu sawa Islam population in Tanzania as of 2007, is about 35% of the population of the mainland (Tanganyika) and more than 99% of the population in Zanzibar are Muslims.

Source : Wikipedia
 
Kuweka takwimu sawa Islam population in Tanzania as of 2007, is about 35% of the population of the mainland (Tanganyika) and more than 99% of the population in Zanzibar are Muslims.

Source : Wikipedia

Umesema population ya Tanzania halafu then uka merge na kuhamia kwenye mainlanda vs Zanzibar.
Mimi nilitaka uweke ya Tanzania kama Tanzania na si Tanzania kama Bara ikiwa na percentage yake na Zanzibar ya kwake.
Otherwise ungesema tu Tanganyika ina 35 percent ya Muslims na Zanzibar 99%.
 
Back
Top Bottom