Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

...
...
the secretary-general of the organization of the islamic conference, prof. Ekmeleddin ihsanoglu, received in his office today 30 august 2008, his excellency mr. hussain shihab, ambassador of the republic of maldives to the kingdom of saudi arabia, who presented his credentials as the permanent representative of his country to the organization of the islamic conference.

The ambassador of maldives conveyed to the secretary-general the compliments of the maldivian leadership. He also assured of his determination to further enhance oic-maldives relationship during his tenure.

On his part, the oic secretary general welcomed the new maldivian ambassador and expressed the hope that maldives would play a more proactive role in the organization.

views on various ways to further improve bilateral relations between maldives and oic were also exchanged in the meeting.

...

...
 
Jokakuu,
Mkuu hapa unajaribu kusema kitu gani maanake kusema kweli siwafahamu kabisa wewe na mwanakijiji kuhusiana na Balozi.... Maldives ni member wa OIC kwa hiyo kinachosukuma hoja hii ni kipi hasa!..Hata UN nafikiri zipo nchi wanachama bado hawana balozi wao wa kudumu pale New York. Hii sio ajabu kabisa...
Kisha huko nyuma nimeona ukiandika kwamba OIC imeshindwa kutatua migogoro ya Somalia Sudan na sijui wapi hata sielewi unachojaribu kusema hapa... Hiyo UN imeshindwa sehemu ngapi si wao ndio baba iweje hili swala liwe la OIC. Sisi wenyewe tulishindwa kutatua mgogoro wa Rwanda, Burundi na Kongo una maana tufanywe kitu gani?..Au unachanganya OIC hii na ile international security body (OIC) inayojaribu kutatua migogoro ya nchi husika!.

Jamani nashindwa hata kufuatilia mjadala huu maanake nimeshauliza maswali zaidi ya 20 na hakuna maibu isipokuwa watu mnakuja na maswali mengine mapya! maswali yangu aaah!...aaah!...
 
Mkandara said:
Jokakuu,
Mkuu hapa unajaribu kusema kitu gani maanake kusema kweli siwafahamu kabisa wewe na mwanakijiji kuhusiana na Balozi.... Maldives ni member wa OIC kwa hiyo kinachosukuma hoja hii ni kipi hasa!..Hata UN nafikiri zipo nchi wanachama bado hawana balozi wao wa kudumu pale New York. Hii sio ajabu kabisa...
Kisha huko nyuma nimeona ukiandika kwamba OIC imeshindwa kutatua migogoro ya Somalia Sudan na sijui wapi hata sielewi unachojaribu kusema hapa... Hiyo UN imeshindwa sehemu ngapi si wao ndio baba iweje hili swala liwe la OIC. Sisi wenyewe tulishindwa kutatua mgogoro wa Rwanda, Burundi na Kongo una maana tufanywe kitu gani?..Au unachanganya OIC hii na ile international security body (OIC) inayojaribu kutatua migogoro ya nchi husika!.

Mkandara,

..nadhani ili nchi iwe na Permanent Representative/Balozi huko OIC inapaswa kwanza kuwa mwanachama.

..kuna hoja imeletwa kwamba tuwe na Balozi OIC kana kwamba kitendo hicho kitaepusha sisi kuwa wanachama wa OIC.

..siyo mimi niliyeandika kuhusu OIC na Somalia au Sudan. hapo naona umenionea kidogo.

..mimi naona tujiunge tu ili nchi isonge mbele tuweze kujadili mambo mengine yanayolihusu taifa letu.
 
JokaKuu.. usidhani; soma Katiba ya OIC.. huitaji kuwa mwanachama ili uwe na representative. Marekani ina Balozi OIC na si mwanachama. Hivi kuna ugumu gani wa kuisoma hiyo Katiba ya OIC?

Mkandara, watoto wa Yakobo na OIC?
 
1216456174.gif
 
faida za kujiunga na OIC:

a. Tutapata misaada
b. Jamii ya Waislamu wataridhika kuhusiana na chombo cha Kiislamu na hivyo itakuwa rahisi kupata misaada.
c. Tutakuwa tumejiunga na nchi nyingine ambazo nazo ni wanachama wa OIC na hivyo kuwa karibu katika kusaidiana na wanachama wenzetu.
d. OIC itasaidia kujenga vyuo kama kile cha Uganda
e. OIC kwa vile ina nchi nyingi zinazozalisha mafuta itatusaidia kupunguza bei ya mafuta na hilo litawanufaisha watu wote siyo waislamu tu.
f. Itatatusaidia kuchukua msimamo wa pamoja katika masuala ya kimataifa hasa katika kutetea haki za Wapalestina ili wawe na nchi yao ambapo Al Quds al Sharrif (Yerusalemu) ni makao makuu.
g. Itatusaidia kushiriki katika kulinda maslahi ya jamii ya Kiislamu popote duniani.
h. Itatusaida kuwa katika mchakato mzuri wa hatimaye kuwa sehemu ya Soko la Uchumi la Nchi za Kiislamu ambapo hatimaye tutakuwa katika Jumuiya ya Uchumi wa Nchi za Kiislamu. Hili litakuwa na faida kubwa sana za kiuchumi kama masuala ya kodi, kusafirisha bidhaa, mikopo isiyo na riba n.k


Kuna niliyosahau?

i.

Denial.png
 
Rev Kishoka, Kuna tatizo kubwa hapa. Kubwa ambalo nchi inalifunika. Na watanzania tukicheza litalipuka vibaya manake vimpipuko vidogovidogo ndio kama hivi.
Waislamu wana hasira na (upendeleo) uliokuwapo tangu tupate uhuru.
Kwa kuwa maswala ya imani ukimwachia mtu asiye na imani akayaongoza hayafiki mbali au yanawarudisha nyuma waumini, mimi naona kuingia kwa SERIKALI YA TANZANIA kwenye jumuiya hii ni makosa makubwa.
Serikali/watendaji hawataweza kulipa hili swala msukumo wa kiimani kama inavyohitajika katika maswala yote ya kiimani.
Kuikabidhi serikali iendeshe na kugharimia mipango yote ya uanachama itakuwa na conflict of interest.
Kila siku waislamu wanalalamika serikali inaingila BAKWATA. Hii ni uthibitisho kuwa mkono wa serikali ukiingilia maswala ya dini inaleta mtafaruku na kutokuelewana sikuzote kwa waumini wenyewe.
Kwa upandea wangu bajeti ya nchi kutumika katika swala la dini yoyote mimi naona si haki.
Serikali itoe kibali na masharti, dini na waumini wake wafanye wanachofikiria wenyewe. Lakini si serikali kuajiri watu wa kufanya mambo ya dini, bali kusimaina tu kama wanafuata sheria za nchi.

Hapa ni kwa dini yoyote mpya au ya zamani. hata za kimila.
Nadhani hii itajumuisha mahakama ya kadhi kuingizwa serikalini.
Sidhani kama kuna makosa yaliyofanyika huko nyuma, ni budi tuongeze makosa mengine, bora turekebishe hayo makosa kwanza.
 
Hivi huko Uganda mafuta ni bei chee kwa sababu wamejiunga na OIC?
 
Mkandara,

..nadhani ili nchi iwe na Permanent Representative/Balozi huko OIC inapaswa kwanza kuwa mwanachama.

..kuna hoja imeletwa kwamba tuwe na Balozi OIC kana kwamba kitendo hicho kitaepusha sisi kuwa wanachama wa OIC.

..siyo mimi niliyeandika kuhusu OIC na Somalia au Sudan. hapo naona umenionea kidogo.

..mimi naona tujiunge tu ili nchi isonge mbele tuweze kujadili mambo mengine yanayolihusu taifa letu.

Ni mimi niliyeongelea kuhusu nchi za somalia na zingine zenye migogoro.Kimsingi nilitaka kubainisha hasara ya taifa ambalo limekumbatia fikra za kimaskini na kutojiamini.Mataifa niliyoyataja kwenye post yangu yanakabiriwa na tatizo kubwa la umaskini na ujinga.Simanishi kuwa ukijiunga na OIC ndio utakaribisha umaskini la hasha,natoa angalizo kwa watetezi wa hoja hiyo kuwa sio kweli kuwa ukijiunga na OIC ni njia pekee ya kufungulia neema ya misaada.Kwa maana hiyo, nchi nilizozitaja ni wanachama lakini bado zimebaki na migogoro mikubwa ya kijamii na kiuchumi kwa sababu wamekosa njia sahihi za kujumuisha maamuzi ya wananchi wao kwa njia shirikishi ya kidemokrasia.
Nitoe mfano wa nchi ya kiislaam ya Turkey,wananchi wake wanaenjoy mfumo wa kidemokrasia wa ulaya na nchi yao inasonga mbele katika nyanja za kisiasa,kiuchumi na kijamii.Ukilininganisha nchi za kiislaam zenye migogoro utaona utashi wa wananchi kujiamulia mustakabali wao unadhibitiwa na wakiritimba aina ya kina Kingunge.Eneo la demokrasia shirikishi ni muhimu sana kufikia maendeleo endelevu kuliko kufikiria kutafuta suluhu ya matatizo nje ya jamii husika.Natoa mwito kwa watz tufungue fikra zetu ya kutafuta suluhisho kwa kushirikisha wadau wote tusimuachie Kingunge,Nchimbi nk kutuamulia mustakhabari wetu.
Natoa shukrani za dhati kwa michango ya kifikra kwa Rev.Kishoka.Mwanakijiji,Field Marshal,Ben,Zitto,Asha,Kitila,Mnyika,Dr Slaa na orodha ni ndefu ambao wameamua kutoa fikra zao kwa umma mpana wa Tanzania kwa faida za wote.
 
Mwanakijiji,
Watoto ya Yakub na OIC?

Alaah! nimekuuliza swali jibu kwanza kwani sio wewe uliyeandika faida za kujiunga na OIC au mtu mwingine..
Kuhusiana na katiba ya OIC, Marekani wana mwakilishi lakini sio wanachama hivyo hawahitaji msaada wowote toka OIC..Ndio maafa kama ya Katrina waliwaacha weusi wajijue wenyewe..

Jokakuu,
samahani mkuu nimesema nilishindwa kukuelewa...na sababu ni kwamba uliandika tu kuhusiana na balozi lakini hukuandika zaidi kama ulivyoandika sasa hivi..Huo ndio ukweli ambao Mwanakijiji anajaribu kuutungia ngonjera...

Mkuu, binafsi nimechukua muda wote huu kuzungumzia swala la OIC ili jamaa zangui mpate kufahamu zaidi ya wasiwasi na hofu zao kuhusiana na Uislaam. najua miaka yote Uislaam umekuwa tishio kubwa la wakristu hali haijawahi kutokea ktk historia dini hizi mbili kuwa maadui zaidi ya Watawala hasa Wazungu na Waarabu kuzitumia dini hizi ili kuongeza mapana ya Tawala zao... Sisi sote tunafahamu hili na kamwe halkiwezi kupewa nafasi..
Ni ajabu naposikia watu wakisema waislaam wana hasira! sielewi kama hasira hiyo ipo kwa serikali ama wananchi wa madhehebu mengine lakini pamoja na yote hayo huu ni uzushi na propadanda kwani kama kweli waislaam wangekuwa na hasira tungeisha ingia msituni against serikali au kusikia mfarakano kati yetu na kanisa ama dhehebu fulani. Isipokuwa waislaam tunajenga hoja zetui na kuziwakilisha ktk vyombo husika, maneno yetu yamekuwa chachu kwa wasomaji wengine ambao badala ya kutafakari hoja iliyopo wanataza hawa ni kina nani?... Waislaam! then haitusaidii sisi waumini wa dini nyingine..
Ndio haya haya yanatokea ktk siasa kiasi kwamba Chadema wanaposimama kulalamikia kitu mathlan EPA imekuwa swala la kutazama hizo fedha ni za nani?... sio za serikali kwa hiyo hakuna tatizo hata kama zimeibiwa kupitia chombo muhimu nchini BoT..
Ni katika ufinyu wa fikra hizi ndio maana tumeshindwa kabisa kuweza kusonga mbele kwa sababu kila tatizo nchini huwa lipo ktk jumuiya moja ama chache ambazo kwa ujumla wake ndio hulifanya tatizo zima kuwa la TAIFA.
Tanzania watu tumekwisha kubali kuwa kila mtu na Mzigo wake, hivyo siii rahisi kwa watu kuelewa matatizo yanayohusu kundi la watu fulani.. wanachotaka ni tatizo ambalo lipo Tanzania nzima kwa watu wote ili lipate sauti..na kwa hali hii haiwezekani na hakuna tatizo la Tanzania nzima isipokuwa ni ktk mafungu mafungu ndipo unapopata ukweli. Matatizo ya Umeme yapo Dar na baadhi ya mikoa wapo watu walishindwa kuelewa kwa nini tatizo la Richmond liwe la kitaifa hali linahusiana na mikoa ya Pwani, swala la Sangara lilihusu wakazi wa Mwanza kwa hiyo haikuwepo sababu wala umuhimu kwa wananchi kuilaumu serikali, haiwahusu wala hawana uchungu..Buzwagi, Kiwila na mengine yote yanakosa umuhimu kwa wananchi kwa sababu yanahusu sehemu fulani ama kundi la watu..Hivyo ni shauri yao haoi wahusika.. Kuna msemo wa waswahili wanadai kwamba Umasikini Tanzania haupo ila upo kwa baadhi ya watu - Kama wewe ni maskini sema wewe ni maskini lakini usiseme watu wote (Tanzania) ni maskini...

Kwa hiyo mkuu wangu nimejaribu sana kutoa mchango wangu lakini inakuwa vigumu sana kwa ndugu zangu kuelewa kwa sababu ya utengano tuliokwisha ujenga kutokana na Umaskini..CCM wameweza kututenga vizuri sana kwa kutuwekea hilo sinia la Pilau mkekani na hivyo kila mmoja wetu anaangalia maslahi yake kwanza... Tunapiga kelele sana kuilaumu serikali kutoweka maslahi ya Taifa mbele wakati sisi wenyewe ni replica ya viongozi hao hao..Yote hii imetokana na sinia la pilau mkekani...
Hata ndugu yako unaweza kumputa ganja la mkono kwa sababu ya pande la nyama....
 
Mwanakijiji, swali lako ni zuri.

Ningependa nikujibu kwamba, kabla hatujapima "uwingi wa faida, dhidi ya uwingi/uchache wa hasara" ni bora tukaambiwa au tukachambua hizo hasara na faida kwanza. Hili bado hatujalifanya.

Kwa maoni yangu, ningependa kwanza nijuwe hasara tutakazopata kwa kujiunga na umoja huu. Ingawa sina uelewa mpana, sina shaka kwamba OIC ina faida nyingi ambazo zimefanya nchi nyingine kujiunga. Wala sitakaa nishawishike kwamba nchi zilizojiunga na zinazoendelea kujiunga zinaumia kwa namna moja au nyingine.

Hivyo basi, kwa haraka naweza kuhitimisha kwamba OIC ina practical/theoretical benefits, otherwise kusingekuwa na wanachama. Nisichoweza kuelewa ni hasara zake kwa watanzania as a whole au segment ya watanzania (e.g wakristo, wamatumbi, wapagani, etc). Kama kwa kujiunga na OIC Tz au baadhi ya watanzania wataumia kiuchumi, kimaendeleo nk, hapo ndipo tunapoweza kupima impact ya faida vs maumivu.
 
Mwanakijiji said:
JokaKuu.. usidhani; soma Katiba ya OIC.. huitaji kuwa mwanachama ili uwe na representative. Marekani ina Balozi OIC na si mwanachama. Hivi kuna ugumu gani wa kuisoma hiyo Katiba ya OIC?

Mwanakijiji,

..nitaiangalia katiba ya OIC kwa undani zaidi.

..siyo kwamba hoja zako hazina msingi. nafikiri kuna watu wengi tu ndani ya jamii yetu wanayafahamu hayo unayojitahidi kuyaeleza.

..lakini kwa hali ya KIJAMII ilipofikia sasa hivi, ni busara kuwasikiliza WAISLAMU na kujiunga na OIC. Zaidi tujiunge on their[Muslims] terms.
 
Jokakuu,
..lakini kwa hali ya KIJAMII ilipofikia sasa hivi, ni busara kuwasikiliza WAISLAMU na kujiunga na OIC. Zaidi tujiunge on their[Muslims] terms.

Mkuu wangu hapa ndipo mnapokosea mnapoandika vitu kwa rangi zake...U have to come out of that box kuweza kunielewa...kwa sababu message inayokwenda kwa wasomaji inaonyesha dhahiri kuna kinyongo kati ya waislaam na wakristu kiasi kwamba Wakristu wakubali OIC kwa sababu hawana jinsi...

Binafsi siwalaumu Wakristu/Waislaam, hata kidogo kwa sababu hii hulka imejengwa na baadhi viongozi wa dini zote mbili ambao wamekuwa msitari mbele kunyoosha vidole na kutoa dosari upande wa pili ambao unapigania haki sawa na wao. Ni mchezo mchafu ambao hivi sasa umekwisha ota sugu na wananchi tumeshindwa kabisa kutofautisha maamuzi yetu ktk maswala ambao yanatinga ktk kundi la MATATIZO na MAFANIKIO...

Kwa mfano binafsi siwezi kutenganisha matatizo ya Mwanakijiji ikiwa matatizo hayo yanahusu jamii yetu bila kutazama dini ya Mwanakijiji au wahusika..Kama unavyofahamu Mwanakijiji anaendesha site yake ya KLH News na mara nyingi amepata matatizo ambayo yanahusiana na kijiwe chake. Wachache sana wamekuwa msitari wa mbele kumsaidia kwa mawazo hali na mali kwa sababu tumejenga ile tabia ya kusema haya ni matatizo ya Mwanakijiji hayawezi kunisaidia mimi zaidi ya kwamba Mwanakijiji atatajirika ama kupata Umaarufu. Kwa ufinyu huu wa kutazama tumeshindwa kuelewa ama kupima Mafanikio ya kijiwe cha Mwanakijiji ktk mzani wa FIKRA ambazo ameweza kuzisambaza Tanzania nzima kwa wananchi wote isipokuwa kipimo ni fedha dhahabu inayoweza kuwa exchanged.. Kwa hiyo maamuzi mengi kwamba siwezi kumsaidia Mwanakijiji kwa sababu he will be successful, while I'm down here struggling to make ends meet!..
Ni kwa upana wa fikra hizi ndio maana binafsi nimekuwa tofauti na utazamaji wa hoja ama mada inayowasilishwa.. na kama unakumbuka niliwahi kumwambia mchangiaji mmoja kuhusiana na Tarime kwamba hoja ya Tarime ni nzuri kama ataiweka Kitaifa kwa sababu nawafahamu Wabongo.. wataanza kujiuliza faida ya Tarime kwao, kisha watai crush vibaya hata kama malengo yake ni kuamsha Umma...Lakini kama swala hilo hilo litakuja kitaifa kidogo litabeba uzito kwani linaweza kuwa defenced na fikra mpya kupandikizwa na watu wakaelewa ingawa sii wote..

All in all hapakuwepo haja kabisa ya kutazama swala la OIC kama ni swala la Waislaam kwa sababu hao waislaam ni kiungo cha jumiya nzima ya Watanzania. na kama tutafikia kusema maswala ya Waislaam yaamuliwe na Waislaam basi tutakuwa tunapoteza nguvu ya serikali na pengine jumuiya nzima ya Watanzania.. UMOJA wetu utakuwa dhaifu na rahisi kwa maadui wa Uhuru wetu kupenyeza..

Tuna mwendo mkubwa sana kuweza kuuelimisha Umma kwani tumekwisha jengwa tabia mbaya ya utengano na kila kitu kina rangi zake kiasi kwamba hata ajira hazipatikani bila kujulikana . na kujulikana kwenyewe ndio huko - Kabila lako, dini yako, mtoto wa nani? na kadhalika, hivi vyote ni kichwa cha resume ya mtu kabla ya maswala mengine yote..
Hii sio tabia nzuri na hakika imeturudisha nyuma sana ktk maswala mengi muhimu na maadui wetu wamekuwa wakitumia hila hizi kuonyesha uchovu wa mapendekezo ambayo ukiyatazama kwa makini MAFANIKIO ya huyu mtu mmoja ama kundi yataweza kujenga jamii nzima..hakika mkuu wangu sisi siku zote hupongeza chombo ama kiongozi ambaye ataweza kutunufaisha sisi wote badala ya kufikiria kwamba chombo kile au Kiongozi huyo mtaweza vipi kumtumia ili kuboresha maisha yenu..
Kennedy alisema:- Ask what U can do for Ur Country, not What a Country can do for You...
Kwa wabongo na hasa watu maskini tunasema - What have you done for me lately!
 
Last edited:
Kulikuwa na thread ya Tanzania kujiunga na OIC, hata hivyo naiweka hii hapa inaweza kuunganishwa baadaye.

Nimepata hii OIC Charter na unaweza kuisoma hapa http://www.oicun.org/categories/The-OIC/About-OIC/OIC-Charter/

Pia dhima mpya ya OIC (New Vision of OIC) unaweza kuisoma hapa http://www.oicun.org/articles/37/3/New-Vision-of-the-OIC/3.html

Naamini mjadala utanoga na kuendelea mbele kama ni lazima TZ ijiunge na OIC
Nashukuru makala ya MMMJ kwenye TZ Daima ya wiki ameliongela vizuri sana.


Asante sana Ngereja kwa charter hii muhimu.
Siku zote kumekuwa na mjadala kuhusu Tanzania kujiunga au kutokujiunga na OIC.Sikupenda sana kujiingiza ktk mjadala ila nilichangia kwa kuwaqtaka wana JF na watanzania wote kuweka itikadi za kidini pembeni na kujadili suuala hili katika sura ya kitaifa ili kuona:
- Nini hasa OIC kwa maana ya malengo, mtizamo n.k
- Nini faida za kujiunga na OIC kama taifa kwa ujumla wetu na siyo kikundi fulani tu
- Nini zimekuwa hasara kwa upande wetu kwa muda wote ambao hatujawa wanachama waOIC.
n lazima iwepo tafakari yakinifu juu ya kujiunga OIC.Tusiyumbishwe na imani ya mtu kwa namna yoyote ile.

Kwa kuitazama charter hii naona kuna haja kujiuliza kama kweli Tanzania ya waislamu,wakristo ,wabudha,wahindu na wale wote wenye dini na wasiokuwa na dini wanabebwa katika vipengele hivi vya charter ya OIC.

RESOLVED to preserve Islamic spiritual, ethical, social and economic values, which will remain one of the important factors of achieving progress for mankind;

DETERMINED to consolidate the bonds of the prevailing brotherly and spiritual friendship among their people, and to protect their freedom, and the common legacy of their civilization restoring particularly on the principles of justice, tolerance and non-discrimination;A) Objectives:
The objectives of the Islamic Conference shall be:

* to promote Islamic solidarity among Member States;
* to consolidate cooperation among Member States in the economic, social, cultural, scientific and other vital fields of activities, and to carry out consultations among Member States in international organizations;
* to endeavor to eliminate racial segregation, discrimination and to eradicate colonialism in all its forms;
* to take necessary measures to support international peace and security founded on justice;
* to coordinate efforts for the safeguarding of the Holy Places and support of the struggle of the people of Palestine, to help them regain their rights and liberate their land;
* to back the struggle of all Muslim people with a view to preserving their dignity, independence and national rights;* to create a suitable atmosphere for the promotion of cooperation and understanding among Member States and other countries

Kwa mtizamo wangu nashawishika kusema kuwa mambo niliyoyaweka rangi ya dark brown hayagusi ustawi wa watanzania wote bila kujali mipaka ya dini zao.Tupendetusipende OIC kama chombo kinavyojieleza ni jumuiya ya nchi za Kiislamu na inatambua uanachama wa nchi nyingine zisizokuwa za kiislamu kwa kigezo cha kuwepo kwa waislamu katika nchi hizo.

Tanzania kama taifa hatuna sababu ya msingi kujiunga OIC na vilevile hatuna sababu ya kujiunga na jumuiya ya nchi za kikristo au za kihindu kama zipo.Umoja wetu na mshikamano wetu unajengwa na utadumishwa hata kama hatupo OIC.

Ndugu zetu waganda wanazo sababu za kujiunga OIC na wala hazina uhusiano na misaada ya kiuchumi.Ni suala la kihistoria na iliwalazimu kufanya hivyo kwa wakati ule.

Tukijadiliana kwa fikra pana tutafika,tusishupE
 
Tuelimishane zaidi kuhusu katiba ya nchi yetu inasemaje kuhusu masuala ya dini na kama kujiunga kwa Tanzania kama nchi katika OIC kutakiuka katiba ya nchi au hapana.
 
Bila kutafuna maneno hii jumuiya si muafaka kwa Tanzania yetu. Huku ni kutafuta matatizo mengine zaidi ya tuliyonayo tayari! Huu ni mkataba mwingine wa kifisadi serikali ya awamu ya nne inataka kutuingiza!
 
Sasa jamani hivi viongozi wetu wanasema tujiunge tu ili tuwe tunasaidiwa sasa mbona hawa member wa oic wanapata taabu na hiyo oic inatuambia sisi wenye will ili tusaidie na sio oic kuchukua hatua.
Jamani tunadanganywa kuhusu hili jambo.

Wangerekebisha amani Somalia ningeona kweli hawa ni msaada maana Somalia ipo oic lakini kama wanapigana waokwa wao na kule wakristo tuseme 1 kwa maelfu. sasa haya sijui tunaenda wapi nimesoma hii habari nikashangaa.


Source

It has been brought to my knowledge that over 14 million people have been suffering from various forms of malnutrition in several Eastern African countries out of which three are Member States of the Organisation of the Islamic Conference, namely Somalia, Uganda and Djibouti.

According to UN sources, half of the population of Somalia is faced with acute food shortages due to prolonged instability, rising high food prices worldwide, coupled with long-term prevailing drought.

Likewise, Uganda and Djibouti are also facing food deficits due to persistent rain failures which have rendered nearly two million people dependent on international aid in the arid Karamoja area in Uganda while 149,000 Djiboutians are completely relying on food provided by the international community and various agencies. By the same token, the situation is no different in non-OIC member countries in Eastern Africa, such as Ethiopia and Kenya where millions of people are in need of urgent food assistance.

In this blessed and holy month of Ramadan, I solemnly appeal to all OIC Member States, Philanthropists, NGOs and all people of good-will, to generously come to the rescue of the needy people living the affected countries to avert the possibility of mass starvation, if bold steps are not taken to complement the laudable efforts deployed by various stakeholders.

 
Back
Top Bottom