Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kalenge,
uzuri wa Uislaam sii watu ni dini na mafundisho nachofanya mimi sio lazima kiwe Uislaam.. Ungekuwa Muislaam ungeyajua hayo..
 
Katika hili muheshimiwa Mkandara lazima ukubali umechemka, maelezo unayoyatumia kupinga hoja yanakupinga wewe mwenyewe. Ni bora ulivyoaga kuwa unaachana na mada hii, kwani inatoa sura nyingine kabisa. Sio yule Mkandara anayeona mbali, mwenye mchango wa hekima tena. Bora upumzike tu, uiache hii hoja.
 
Shedafa,
Mkuu naomba unionyeshe wapi nimechemka ama sikusema ukweli.. nambie wewe ukweli, bila shaka nitakubali kuchemsha......maanake sasa naona wataka kunivua nguo!
 
Wala hawakuvui nguo mkuu, ktk hoja ya msingi wenzio wamekazania kuwa ni sawa kwa taasisi au jumuia ya Kiislamu kujiunga na wala si nchi. Na ndio nimeona wote walioupande wa pili waliposimamia, wewe umesimamia nchi. Lakini nikichukulia mathalani mfano ulioutuoa wewe mwenyewe wa Tz kujiunga na jumia za makanisa utaona unawaunga mkono, kwa sababu hayo makanisa yalianzishwa aidha na waumini au taasisi zao kufuata sheria za nchi. Baadaye ni hizo taasisi au makanisa yaliomba uanachama katika jumuia zinazowahusu, lakini kule wanajulikana ni Tz. Hii inawapa haki hata kama kuna nafasi ya kuchaguliwa ktk uongozi wanaweza kuchaguliwa na kutambulika kuwa Tz ni m/kiti au katibu na kujiunga kwao pia lazima kufuate sheria za nchi. Hiki ndio wenzako wamekuwa wakikueleza toka point ya mwanzo, kuwa ni sawa jumuia au taasisi ya kiislamu kujiunga kwa niaba ya Tz na wala si serikali. Naomba niishie hapo, nimekuwa msomaji mwisho imebidi nijaribu kuingia kwani naona mzee mwenzangu zile hekima zako hapa hatuzioni kwa sana. Pole mzee!
 
NINAMSHANGAA Askofu Kilaini kutoa haja ya Tanzania kutojiunga na na IOC eti kwa sababu ni suala la dini na sio kijamii na kiuchumi kwa faida angalau ya sehemu moja ya Watanzania.

Hili si kweli, maana wanaoomba Tanzania ijiunge na IOC ni wale wanaotaka kuona Watanzania wanafaidika na programu za shirika hilo ambalo ni mipango kabakaba ya kuwanufaisha watu kiuchumi na kijamii kupitia benki zake na taasisi zingine za kifedha.

Sisi Wakatoliki si haba tunanufaika na fedha za Vatican kila mwaka kiasi ambacho viongozi wetu wa dini wameanza kukufuru. Huu ni wivu tu toka kwa viongozi wetu kwa ndugu zetu Waislamu.

Kama ndivyo kwamba IOC ni dini basi serikali itakuwa inawadhulumu Waislamu kwa kuendelea kuwa na Ubalozi wa Vatican hapa nchini jambo ambalo dhahiri ni la kidini na sio la kisiasa.

Tusiwe wanafiki Watanzania ili tujenge udugu na amani ya kweli kati yetu sisi Wakatoliki, Waislamu na wenzetu wa madhehebu nyingine hapa nchini.

Mkatoliki anayekataa unafiki,
 
Ndugu Changamoto, kwanza kabisa unaonyesha hukuelewa alichosema Kilaini ila umeeleza jinsi wewe ulivyomwelewa. Kilaini alisema "kabla ya kujiunga na OIC wananchi washirikishwe kuhusu faida (au hasara zake)".

Mimi nadhani ni vizuri kujadili kitu kwanza kuliko kujiunga bila kujua chochote. Kwani tatizo liko wapi kama OIC ikijadiliwa kuona jinsi gani tutafaidkika? Kufanya hivi sidhani kama ni unafiki!

Yaani, wewe unataka kitu kikisemwa leo basi watu wasihoji waingie mikataba tu? Hukumbuki kuwa mikataba kama hiyo ndiyo imetuletea matatizo hapa nchini?
 
Wakuu,waislamu wajiunge na IOC kupitia taasisi zao,na sio jina la Tanzania kutumika ktk umoja huo.

Wakristo walio members wa jumuhiya za kidini,hawatambuliki kama Tanzania,bali hutambulika kama wanachama wakristo kutoka Tanzania.

Naomba nieleweke,wakristo hatuko tayari kupokea misaada ya waarabu,kwa migongo ya waislamu,lazima misaada hiyo iwafaidishe waislamu,kwani wao ni walengwa wakuu,ivo basi Membe+ waislamu acheni kukurupuka,tafuteni kitambulisho chenu mtakachotumia kujitambulisha ndani ya IOC.

Lazima mtambue kuwa,hatuko tayari kula hiyo misaada yenu,kama ni bei ya mafuta kushuka,munaweza kufanya utaratibu wa kuhakikisha dini nyinginezo hazifaidi hayo mafuta.

Sisi wakristo hatuchanganywi sana na hayo mafuta,neno linasema "Mtu haishi kwa mkate tuu,bali kwa kila neno litokalo ktk kichwa cha MUNGU",tunaamini ivo na MUNGU wetu anazo NGUVU za kutupa alternative.

Waislamu jiungeni kama waislamu,si kama nchi ya Tanzania,otherwise ombeni kuunda nchi yenu ndani ya Tanzania ili iwe rahisi kutimiza adhma yenu.

Nawakilisha.
 
VIONGOZI WA DINI WENYE CHOYO NA HUSUDA!

UMEZUKA mtindo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini kuingilia masuala ya dini zingine kwa kisingizio hiki au kile. Ninadhani hiki sio kitu chema na mahusiano kati ya dini hiyo na watu wa dini nyingine yanaweza yakalikokota taifa kule tusikotaka.

Katiba ya nchi inasemaje kuhusu suala la Imani za watu? Hapa chini ni nukuu ya kifungu Na.19 ambacho ndicho kinachozungumzia suala la imani:

"19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
"

Uchaguzi hapa tunachukulia sio tu ni maamuzi bali utekelezaji wa yale yote muumini wa dini fulani anayoamini kwamba ni lazima yawepo ili aijenge imani yake kikamilifu.

Kwa mantiki hii Waislamu wana haki sio tu ya kudai haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi kama sehemu muhimu ya kukamilisha Uislamu wao bali pia na kushirikiana na wale wote ambao wanaweza wakasaidia kuupeleka Uislamu mbele ndani na nje ya nchi.

Hili liko wazi katika katiba: '20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi aukuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.'

Kama Wakatoliki nchini wanavyosaidiwa na Vatican ni muhimu vivyo hivyo kwa Waislamu kusaidia na vyombo kama IOC ili kuupeleka Uislamu wao mbele.

Ilivyo sasa ni kwamba serikali inaelekea kusema na kuendesha mambo yake kama vile Wakatoliki na madhehebu nyingine wana haki ya kupata misaada kutoka nje lakini eti Waislamu hawastahili kupata msaada wowote toka nje kwa sababu ya kusingiziwa kuwa wao Waislamu ni 'magaidi'!

Ieleweke kwamba katika nadharia za Uwezo na Mamlaka katika nchi vikundi mbalimbali vya watu vinahodhi kiasi fulani cha 'units of power' na hatari kubwa kwa nchi ni kikundi kimoja kupora 'units of power' za vikundi vingine au vikundi fulani kushisrikiana ili kupora vikundi vingine 'units of power'! Kinachotokea sio tu kwamba wanasiasa wanawapora Waislamu 'units of power'! bali pia Wakatoliki wanawapora moja kwa moja na vile vile kwa kushirikiana na serikali hiyo ambayo tayari inawapora Waislamu haki zao.

Hili haliashirii mema katika kuendelea kuwepo umoja na amani katika taifa hili.

Roho mbaya ya baadhi ya viongozi wa dini inawafanya washinikize serikali kuwanyima watu wa dini zingine haki zao za msingi na ushiriki wao katika kulea 'balance of power' ambayo ndiyo inayowezesha nchi kuwa na umoja na amani ya kweli.

Kinachoonekana hapa kwa kuwa kuna dini ina uongozi mkuu wa kimataifa na inasimamiwa katika misingi bora ya menejimenti na utawala; ina hazina kubwa inayotoka ndani na nje ya nchi; ina uwezo wa kifedha hata kurubuni viongozi wa kisiasa na serikali; ina waumini wake wengi kwenye nfafasi za maamuzi ya fedha, uchumi na maendeleo; ina taasisi zenye uwezo wa kujenga na kubadili fikira za wananchi; ina Ubalozi wa Kidni unaosaidia mambo yake; una mashirikiano na wenye fedha ndani na nje ya nchi kufanya mambo yao yaende vyema; na una wasomi na wataalamu wa kuweka misingi ya kuhodhi uwezo na mamlaka zaidi siku zijazo BASI DINI HIYO HAITAKI DINI NYINGINE nazo zipate fursa kama hiyo. Hii ni husuda, huu ni wivu, hii ni choyo na wala hakuna ajenda yoyote ya kidini kuingiliana na siasa hapa. Bali walio nacho wanataka wasio nacho waendelee kutokuwa nacho!

MIMI sina dini. Lakini kwa uchungu uliosababishwa na unafiki wa viongozi wa Kanisa la Katoliki imebidi niseme lile ninaloliona ndilo kwa hakika la ukweli na haki na sio vinginevyo!
 
Magobe T, kama hatuuigi...tuweke week end Jumatatu na Jumanne, then siku zilizobaki zote tufanye kazi...otherwise ujue TUNAIGA....na sijui umwiga mnyama gani...

Chuma, unajua shida ya kuiga? Yaani, kufanya kitu 'solely' kwa vile umeona wengine wanfanya hivyo? Shida ni hii: siku wakiacha hicho ulichoiga wewe, je, utaendelea nacho au utaacha pia? Na tuseme, utaacha pia. Je, wakirudia kufanya hivyo? Je, utafanya tena?

Mimi sitafanya kitu kwa kuiga. Nitafanya tu nikiona kina faida kwangu (yaani, kama kitu hicho ni 'constructive'). Shida ya kuweka Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba itaathiri mambo mengi sana. Mfano, je, tutakubali mtazamo wa waislamu kwa wanawake (kuwa 'infeior') kuwa swala la kikatiba?

Kuhusu uhuru wa kuabudu Katiba yetu iko wazi. Kitu kizuri kingekuwa kila dini na dhehebu wafanye yote yale wanayoamini na yanayofundishwa na dini zao mradi tu wasivunje sheria.

Lakini kuifanya dini fulani mambo yake yawe kwenye Katiba na nyingine hapana, hapo tunajitakia matatizo tu. Na kusema eti Mahakama ya Kadhi iwepo kwa vile iko Kenya na Uganda, kwangu siyo hoja kwa sababu mtu mwingine angeweza kusema mbona DRC, Rwanda na Burundi hakuna?
 
Soma kwanza na uelewe. Kabla ya hilo uliliona niliisha sema yafuatayo:

Wakatoliki si wanachama wa World Council of Churches na wala hawajawahi kuomba kuwa wanachama.

Fundi Mchundo, samahani sana. Ni kweli sikukuelewa. In fact, sikuwa na hakika kama hayo niliyoandika yalikuwa kujibu hoja yako au la.
 
NINAMSHANGAA Askofu Kilaini kutoa haja ya Tanzania kutojiunga na na IOC eti kwa sababu ni suala la dini na sio kijamii na kiuchumi kwa faida angalau ya sehemu moja ya Watanzania.

Hili si kweli, maana wanaoomba Tanzania ijiunge na IOC ni wale wanaotaka kuona Watanzania wanafaidika na programu za shirika hilo ambalo ni mipango kabakaba ya kuwanufaisha watu kiuchumi na kijamii kupitia benki zake na taasisi zingine za kifedha.

Sisi Wakatoliki si haba tunanufaika na fedha za Vatican kila mwaka kiasi ambacho viongozi wetu wa dini wameanza kukufuru. Huu ni wivu tu toka kwa viongozi wetu kwa ndugu zetu Waislamu.

Kama ndivyo kwamba IOC ni dini basi serikali itakuwa inawadhulumu Waislamu kwa kuendelea kuwa na Ubalozi wa Vatican hapa nchini jambo ambalo dhahiri ni la kidini na sio la kisiasa.

Tusiwe wanafiki Watanzania ili tujenge udugu na amani ya kweli kati yetu sisi Wakatoliki, Waislamu na wenzetu wa madhehebu nyingine hapa nchini.

Mkatoliki anayekataa unafiki,

Mimi nafikiri anayefananisha suala la OIC na kuwepo kwa ubalozi wa Vatican nchini hajui historia ya kwani kumekuwepo ubalozi huo. Mimi napata wasiwasi ni kwa vipi suala hili lipiganiwe na waislam zaidi na wala lisiwe la kitaifa?,kwa nini wanaojitokeza zaidi ni waislam?(tukiacha wachache ambao si waislamu).Ukisoma malengo ya OIC utapatajibu jibu kuwa imekusudiwa kunufaisha zaidi nchi wanachama ambazo ni za kiislam. Ifike wakati sasa tuwe makini na maamuzi tutakayoyachukua tusije jikuta tunavunja katiba yetu eti kwa kisingizio tu kuwa katiba si msaafu.Mimi nafikiri suala lolote linalohusu udini na ukabila hata kama linamaslahi vipi kwa taifa liogopwe kama ukoma!!Wana siasa jamani msitupotoshe kwa tamaa ya kubakia madarakani!!
 
WAKATI mwingine huwa najishangaa sisi Waislamu. Hivi kwa jambo kama hili pamoja na jitihada zote tunakumbuka dua na sura za kusoma toka kwenye Quran ili Mwenyezi Mungu atupe wepesi wa mafanikio?

Ninaamini wengi wetu hatujatambua umuhimu wa kuisoma Quran ili iturahisishie mambo. Basi kuanzia leo kwa wale wanaojifanya wasomi [bila kujua Quran] tuwaambie Usomi wao sio lolote sio chochote bila Quran. Soma Quran na mtaelimika mara mia zaidi!

Haya basi kina nani na nani pale na kule tuanze kwa kurejea tena na tena sura ya Al Falak ili kumkabidhi Mungu wale wenye hiana, tandi, inda, choyo na husuda naye atawashughulikia punde si punde. Ili mradi tusome kwa dhati ya akili na moyo:

Na wakati huu mambo yanapokucha kwa Waislamu basi kilichobaki ni kuwaombea viongozi wa dini wenye nyingine wenye choyo na husuda dua ifuatayo mara kadhaa kila siku :

"In the name of God,
Most Gracious, Most Merciful

113:1 Say: I seek refuge with the Lord of the Dawn
113:2 From the mischief of created things;
113:3 From the mischief of Darkness as it overspreads;
113:4 From the mischief of those who practise secret arts;
113:5 And from the mischief of the envious one as he practises envy. " Na kisha tusubiri majibu ya Muamuzi wa siku ya mwisho!
 
NINAMSHANGAA Askofu Kilaini kutoa haja ya Tanzania kutojiunga na na IOC eti kwa sababu ni suala la dini na sio kijamii na kiuchumi kwa faida angalau ya sehemu moja ya Watanzania.

Hili si kweli, maana wanaoomba Tanzania ijiunge na IOC ni wale wanaotaka kuona Watanzania wanafaidika na programu za shirika hilo ambalo ni mipango kabakaba ya kuwanufaisha watu kiuchumi na kijamii kupitia benki zake na taasisi zingine za kifedha.

Sisi Wakatoliki si haba tunanufaika na fedha za Vatican

Kama ndivyo kwamba IOC ni dini basi serikali itakuwa inawadhulumu Waislamu kwa kuendelea kuwa na Ubalozi wa Vatican hapa nchini jambo ambalo dhahiri ni la kidini na sio la kisiasa.

,

Ubalozi wa Vatican uko Tanzania kwa sababu Vatican ni nchi kama zilivyo nchi nyingine.
 
Mimi nafikiri anayefananisha suala la OIC na kuwepo kwa ubalozi wa Vatican nchini hajui historia ya kwani kumekuwepo ubalozi huo. Mimi napata wasiwasi ni kwa vipi suala hili lipiganiwe na waislam zaidi na wala lisiwe la kitaifa?,kwa nini wanaojitokeza zaidi ni waislam?(tukiacha wachache ambao si waislamu).Ukisoma malengo ya OIC utapatajibu jibu kuwa imekusudiwa kunufaisha zaidi nchi wanachama ambazo ni za kiislam. Ifike wakati sasa tuwe makini na maamuzi tutakayoyachukua tusije jikuta tunavunja katiba yetu eti kwa kisingizio tu kuwa katiba si msaafu.Mimi nafikiri suala lolote linalohusu udini na ukabila hata kama linamaslahi vipi kwa taifa liogopwe kama ukoma!!Wana siasa jamani msitupotoshe kwa tamaa ya kubakia madarakani!!

Sikubaliani nawe kuwa suala la kidini unaliogopa bali nahisi unalishabikia. Ivyo hujatafakari na kuona kuwa wanaopinga nao kwa upande mmoja ni tofauti na waislamu? Nawe kwa nini unapinga?
Kwani mwenzangu misingi ya dini zetu sote si Amani na manufaa ya binaadamu? sasa una wasi wasi gani na uislamu? Hivyo misaada inayoletwa na dini nyengine ikajenga Mahospital, mashule, na taasisi nyengine za Kijamii si hunufaisha Watanzania wote? Au kuna aina nyengine ya misaada ambayo haitokuwa kwa manufaa ya nchi ambayo itatolewa na OIC? Watanzania tuna utamaduni wa kufuata huduma bila ya kujali dini na hata kama huduma hizo ni za dini fulani si tutakuwa tumeshapiga hatuwa fulani kwa huduma hata kama wanaopata ni wananchi wa dini husika? Kwa mfano tunapotaja Vyuo vikuu si tunahesabu vyuo vya kikirsto na vya Kiislamu na kila mmoja anakuwa na uhuru wa kuchagua wapi apate huduma? Bado nafikiri jinamizi la udini na kuogopa kuwa dini fulani itapata maendeleo ndio inatawala majadiliano haya kwani suala la misaada na katiba hatujawahi kuijadili huko nyuma. Hata suwala la maoni ya mwananchi mmoja mmoja hayajawahi kutafutwa katika kuamuwa mambo yetu iweje kwa hili tu kunani?.
 
Ubalozi wa Vatican uko Tanzania kwa sababu Vatican ni nchi kama zilivyo nchi nyingine.

HAWA WENZETU WA DINI HII kidogo wana ajenda yao nyingine, ndo hawa hawa walosema ZANZIBAR NI NCHI ( shehe ponda anzibar hivi karibuni)
eti swala la zanzibar sisi wabara makafiriiii...!
KAMAIOC NI NCHI NA IEKE UBALOZI WAKE, NA KAMA VATICAN SI NCHI IONDOE UBALOZI WAKE....!
ENYI WASOMI WA SOMO LA URAIA KATIKA DINI HIYO ILIYOJAA MALUMBANO HAMLITAMBUI HILI....?

IRAN ni nchi na pia inayo ubalozi wake
VATICAN ni nchi nayo inayo ubalozi wake
KKKT, IOC, TAMPRO, UKWATA, CASFETA, TYCS, hizi si nchi haziwezi kuwa na ubalozi....!
 
Mkatoliki anayekataa unafiki,[/QUOTE][/B]
hee maajabu haya....!
haya hebu tuambie kama unakula ile nyama yetu tamu sana (MBUZI KATOLIKI)
na kama unakula umekula mara ngapi?
Na pia hebu kiri kuwa YESU NI MUNGU.....!
Na vile vile andika tuone kuwa aliyetabiriwa na YESU ni ROHO MTAKATIFU na si vinginevyo.
haya na mengineyo yatatufanya tuamini ni MKATOLIKI na si mtoto wa mama mdogo au wa nje ya ndoa au wengine husema wa haramu ISHMAEL.....!
 
Wakuu,waislamu wajiunge na IOC kupitia taasisi zao,na sio jina la Tanzania kutumika ktk umoja huo.

Wakristo walio members wa jumuhiya za kidini,hawatambuliki kama Tanzania,bali hutambulika kama wanachama wakristo kutoka Tanzania.

Naomba nieleweke,wakristo hatuko tayari kupokea misaada ya waarabu,kwa migongo ya waislamu,lazima misaada hiyo iwafaidishe waislamu,kwani wao ni walengwa wakuu,ivo basi Membe+ waislamu acheni kukurupuka,tafuteni kitambulisho chenu mtakachotumia kujitambulisha ndani ya IOC.

Lazima mtambue kuwa,hatuko tayari kula hiyo misaada yenu,kama ni bei ya mafuta kushuka,munaweza kufanya utaratibu wa kuhakikisha dini nyinginezo hazifaidi hayo mafuta.

Sisi wakristo hatuchanganywi sana na hayo mafuta,neno linasema "Mtu haishi kwa mkate tuu,bali kwa kila neno litokalo ktk kichwa cha MUNGU",tunaamini ivo na MUNGU wetu anazo NGUVU za kutupa alternative.

Waislamu jiungeni kama waislamu,si kama nchi ya Tanzania,otherwise ombeni kuunda nchi yenu ndani ya Tanzania ili iwe rahisi kutimiza adhma yenu.

Nawakilisha.

Kila taasisi inakuwa na ngazi zake na imetokea kuwa OIC ni jumuiya ya nchi sio Taasisi na hivyo ni mambo mawili tu . Aidha Tanzania ijiunge kwa niaba ya raia zake wanaofuata dini ya Kiislamu au kuacha kuingia kama nchi kwa kufuata matakwa ya baadhi ya raia wa Tanzania wenye choyo cha kuona husuda kwa wananchi wenzao watapata faida. Naamini Watanzania wengi hawako hivyo na wanahisi kuwa faida kwa wananchi wa dini nyengine, maadam haileti dhara ni jambo la kukubalika.
Si fikiri kuwa katika Tanzania hii bado wapo watu wenye mawazo kama yako. Ajabu unamtanguliza Mungu na huku kuwakatalia wenzio kumtambua Mungu kwa wanavyomtambuwa wao. Tuna uhuru wa kuabudu na hivyo Waislamu wana haki kuabudu na kuamini vyao. Ni bora ukakaa pembeni na kuacha kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini.
 
Ukitaka kuona jazba ya wabongo taja mambo yanayohusu dini, utashangaa katika mada nyingine wanajenga hoja vizuri lakini ikifika dini tatizo. Punguzeni jazba na zijengwe hoja kama kukubaliana au kupingana basi hoja ndio ziamue na si jazba wala uchoyo.

Ni kweli Tanzania haina dini lakini watanzania wana dini na serikali inaowajibu wa kuwasaidia wananchi kuabudu katika dini wanazotaka, serikali pia ni watu. Kama katika ibada na sikukuu za kidini serikali inatoa ulinzi kuhakikisha waumini wanaabudu kwa imani zao basi ni sahihi kusema serikali inasaidia waumini kuabudu kwa gharama za walipa kodi bila kujali imani za walipa kodi.

Sidhani kama kuna tatizo lolote katika hili la serikali kusaidia waumini wa dhehebu fulani. Kama Membe amesema ruksa kujiunga OIC kwa faida ya waislamu wa Tanzania na haitaathiri uhuru wa dini zingine hiyo safi, hata kama ingekuwa Wasabato pia ingekuwa safi hakuna haja ya kuogopa.

Labda tu siku hizi kinachoonekana kuna baadhi ya dini lazima zitoke na misimamo yao baada ya serikali kuamua jambo. Hii sio safi, waacheni watu waabudu wanavyoona wao sahihi na halivunji sheria za nchi hata kama linawakera. Haikutokea na haita tokea watu wote tukawa na imani sawa, na dunia inapendeza zaidi watu wakawa na imani tofauti.

Tukumbuke pia dini zenyewe tumeletewa kwa malengo na madhumuni ya walio tuletea, kubeba bango na kuona wengine hawako sahihi sio poa tujenge hoja maisha yaendelee, kwa wasio waislamu mnapoteza nini Tanzania ikijiunga OIC. Isijekuwa mtu mwenyewe anachukia kusikia dini flani na anatumia dini yake kusema hisia zake.

Kauli mbiu ya Forum Hii izingatiwe katika kila jambo linaloletwa mbele, acheni woga wa kujadili dini zenu na viongozi wa dini zenu. Inapojengwa hoja nao wanapata mwongozo wa kwenda mbele na wenyewe ni binadamu na wanakosea pia, sio kila wanalo sema basi ndio msimamo wenu.
 
Naanza kupoteza imani na uongozi wa sasa

Uwepo wa JK ktk siasa uliwekewa misingi mizuri na Mwinyi.

Mwinyi huyuhuyu ndiye alietaka kubadilisha jina la Tanzania kuwa "The United Islamic Republic Of Tanzania".

Leo hii JK kupitia Membe anataka kutumiza adhma ya Mwinyi kwa mgongo wa OIC.

Wakristo ni muhimu sana tukawa makini na siasa za TZ+viongozi wake.

Migogoro mingi ya kidini,na favor nyingi kwa waislamu zisizo na kichwa wala miguu,tumezishuhudia ndani ya uongozi wa Mwinyi na JK.

Wateule tuwe macho.

No nooooooo OIC.
 
Kila taasisi inakuwa na ngazi zake na imetokea kuwa OIC ni jumuiya ya nchi sio Taasisi na hivyo ni mambo mawili tu . Aidha Tanzania ijiunge kwa niaba ya raia zake wanaofuata dini ya Kiislamu au kuacha kuingia kama nchi kwa kufuata matakwa ya baadhi ya raia wa Tanzania wenye choyo cha kuona husuda kwa wananchi wenzao watapata faida. Naamini Watanzania wengi hawako hivyo na wanahisi kuwa faida kwa wananchi wa dini nyengine, maadam haileti dhara ni jambo la kukubalika.
Si fikiri kuwa katika Tanzania hii bado wapo watu wenye mawazo kama yako. Ajabu unamtanguliza Mungu na huku kuwakatalia wenzio kumtambua Mungu kwa wanavyomtambuwa wao. Tuna uhuru wa kuabudu na hivyo Waislamu wana haki kuabudu na kuamini vyao. Ni bora ukakaa pembeni na kuacha kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini.

International Islamic Court of Justice
Article 14
The International Islamic Court of Justice established in Kuwait in 1987 shall, upon
the entry into force of its Statute, be the principal judicial organ of the Organisation (OIC).
 
Back
Top Bottom