Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Naomba kuuliza jamani hivi wakati wa sensa huwa hawaulizi dini za watu .....?Nadhani mara ya mwisho ilifanyika 2002.

1.If yes ....kwa nini?
2.Kama wanauliza kwanini hizo statistics huwa hazitolewi sehemu yoyote?

Watu tunabaki tuki-guess tu hizi statistics
 
Logically speaking, Maaskofu walisema Kikwete ni chaguo la Mungu, na Membe ni chaguo la Kikwete, which implies Membe ni chaguo la Mungu. Kutofautiana na chaguo la Mungu ni kutofautiana na Mungu.
 
Kuweka takwimu sawa Islam population in Tanzania as of 2007, is about 35% of the population of the mainland (Tanganyika) and more than 99% of the population in Zanzibar are Muslims.

Source : Wikipedia

najua kuwa waislamu ni wachache hapo tanganyika ila wapo idadi kubwa hapo dar nadhani ni nusu kwa nusu..lindi, mkoa wa pwani, kondoa-dodoma, singida sina,urambo tabora, kidogoma ujiji, mtwara, but the rest naona wapo wachache sana..
 
Ushirombo alikuwa akijibu posting yangu kuhusiana na population ya moslems in Tanzania as the country.
Sentence yake ya kwanza ilikuwa kama anaelekea kusema hivyo...Then akasema mainland na Zanzibar..Kukawa na subdivisions...So nilichosema ni kuwa kama kuna mwenye overall percentage.
Other than that...Kabla hatujajadili kuhusu kujiunga na OIC ama la...Then tujiulize kama Muungano ni muhimu.
Ikiwa bado tunautaka Muungano..Then wengi watapewa.
 
Habari zilizonifikia sasa hivi Maaskofu wa CCT na TEC wametoa kauli kali kuhusu kampeni ya Serikali ya Tz kuiepeleka nchi OIC na wamemtaka Membe ajiuzulu kwa kuchukua msimamo kuhusu Tanzania kujiunga na OIC. Wamemshutumu kuwa ametoa msimamo kabla Baraza la Mawaziri kukaa na kuamua kuhusu hilo.

Mwenye data zaidi atupe, mimi ntapata BBC jioni na magazetini kesho. Mwenye nakala (soft copy) atuwekee hapa.

Hivi hawa wazee wetu wameshaanzisha chama chao nini?

Inaelekea ukimya wa watanzania makini kuamua kuwaacha wakijitwika jukumu la uanasiasa na kujitwalia uongozi wa nchi kutoka kwa MSWAHILI aliyepigiwa kura na watanzania unawafanya wajisahau na kuanza kuvuka mistari......

Taratibu jamani msiliingize taifa kubaya halafu mkamlaumu RAIS MSWAHILI.....

Tanzanianjema
 
Umesema population ya Tanzania halafu then uka merge na kuhamia kwenye mainlanda vs Zanzibar.
Mimi nilitaka uweke ya Tanzania kama Tanzania na si Tanzania kama Bara ikiwa na percentage yake na Zanzibar ya kwake.
Otherwise ungesema tu Tanganyika ina 35 percent ya Muslims na Zanzibar 99%.

zanzibar ina watu wasiozidi 1,000,000.sensa ya 2002 hawakuzidi laki 9, so idadi yao ni ndogo kuliko wananchi walio wilaya ya kinondoni.
so hata kama ukiwajumlisha wazenj kwenye popolation remember wanamake up 2.5% of the totoal population ya watanzania wote. so tukiwa add hapo unaona watakuwa 35% + 2.5% = 37.5% kama tutachukulia stats hizo hapo juu ni kweli..
 
Logically speaking, Maaskofu walisema Kikwete ni chaguo la Mungu, na Membe ni chaguo la Kikwete, which implies Membe ni chaguo la Mungu. Kutofautiana na chaguo la Mungu ni kutofautiana na Mungu.

Watu na maaskofu wakiwemo walinyeshwa mvinyo ule uliyoiva haswa wakawa wanaongea bila kujua kwa undani ni kitu wanasema au kukishabikia.
 
Logically speaking, Maaskofu walisema Kikwete ni chaguo la Mungu, na Membe ni chaguo la Kikwete, which implies Membe ni chaguo la Mungu. Kutofautiana na chaguo la Mungu ni kutofautiana na Mungu.
hahahahhhhhah nimeipenda hii..
 
From wikipedia


Religion in Tanzania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search

TanzaniaCurrent statistics on religion in Tanzania are unavailable because religious surveys were eliminated from government census reports after 1967.[1] Religious leaders and sociologists estimate that the Christian and Muslim communities are equal, each accounting for 30 to 40 percent of the population, with the remainder consisting of practitioners of other faiths, indigenous religions, and atheists.[1]

Muhimu hapa je hiyo sensa ya mwaka 1967 ilisemaje?
 
Hivi hawa wazee wetu wameshaanzisha chama chao nini?

Inaelekea ukimya wa watanzania makini kuamua kuwaacha wakijitwika jukumu la uanasiasa na kujitwalia uongozi wa nchi kutoka kwa MSWAHILI aliyepigiwa kura na watanzania unawafanya wajisahau na kuanza kuvuka mistari......

Taratibu jamani msiliingize taifa kubaya halafu mkamlaumu RAIS MSWAHILI.....

Tanzanianjema

bado unaishi enzi za ujima zile za "zidumu fikra za mwenyekiti". Unamawazo mgando sana ndugu Tanzanianjema wewe, eti anayepaswa kuzungumzia masuala ya mstakabali wa Taifa ni mwenye chama cha siasa tu! LOL
 
From wikipedia




Muhimu hapa je hiyo sensa ya mwaka 1967 ilisemaje?

pamoja na hayo yoote ukweli huu haupingiki kuwa wanzanzibar ambao 98% ni waislamu ..wanamake not more than 3% ya popolation ya nchi nzima..

sensa ya 2002 wakatoliki peke yake ni zaidi ya 15,000,000 nchi nzima.na hiyo ni karibu 27% ya wananchi woe wa tanzania.ndio maana kanisa katoliki lina nguvu kubwa ya kiuchumi na kiasiasa hapa nchini likifuatiwa na lutheran na anglikana. then madhehebu mengineyo..
so nadhani idadi ya waislamu nchini inaweza kuwa sawa na wakatoliki wote...hapo bila madhehebu mengine ambayo nayo ni mengi pia.
 
Umesema population ya Tanzania halafu then uka merge na kuhamia kwenye mainlanda vs Zanzibar.
Mimi nilitaka uweke ya Tanzania kama Tanzania na si Tanzania kama Bara ikiwa na percentage yake na Zanzibar ya kwake.
Otherwise ungesema tu Tanganyika ina 35 percent ya Muslims na Zanzibar 99%.

Nadhani umeelewa overall is less than 36% of the population are muslims na si 60% kama ulivyokisia awali, tupo pamoja

USHI
 
Waziri Membe apigia debe OIC

2008-10-24 09:56:58
Na Muhibu Said


Azma ya Tanzania kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC), imezidi kupata nguvu, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwataka Watanzania waondokane na woga wa kuiogopa jumuiya hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Membe alipozungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya wizara hiyo, jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku moja baada ya Naibu wake, Balozi Seif Ali Iddi, kukaririwa na gazeti hili jana akiweka bayana kuhusu azma hiyo.

Alisema anawashangaa baadhi ya Watanzania kutoa kauli zinazoashiria kuiogopa OIC na baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Iran, wakati wanasifika kuwa ni watu jeuri na majasiri wanaoweza kumudu kukabiliana na mambo makubwa, mazito na ya kutisha.

Membe alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa wanahabari, ambaye katika maelezo yake, alionyesha wasiwasi kuhusu msimamo wa serikali kuwa na uhusiano na Iran na azma yake ya kutaka kujiunga na OIC.

Mwandishi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, moja ya nchi za Kiislamu iliwahi kuingiza nchini msaada wa mchele, huku vifurushi vyake vikiwa vimewekwa juu yake misahafu ya Kurơni Tukufu kwa nia ya kuwasilimisha Watanzania.

Leo pia, katika utawala wa Rais Muislamu tunaelezwa kuwa Tanzania inataka kujiunga na OIC, kitu ambacho mimi nitakipinga hadi dakika ya mwisho,?isema mwanahabari huyo.

Wasiwasi wa mwanahabari huyo ulikuja baada ya Membe kueleza hatua nzuri iliyofikiwa katika mazungumzo kati yake na Rais wa Iran, Mahmoud Ahmednejad ambayo yalilenga kuiomba nchi hiyo kufuta madeni inayoyadai Tanzania yapatayo zaidi ya Sh bilioni 200.

Membe aliitisha mkutano huo kwa lengo la kuipongeza nchi ya Uganda kwa kuwa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kusema kuwa kuingia kwa nchi hiyo kutasaidia katika utatuzi wa migogoro inayolikumba Bara la Afika.

Kauli ya mwandishi huyo, ilimfanya Waziri Membe ambaye awali katika mkutano huo na waandishi wa habari alizungumza kwa upole, umahiri na kwa ufasaha wa hali ya juu, abadilike na kuanza kuzungumza kwa ukali.

Kwa nini tunashikwa na uoga? Tukipewa msaada na Marekani tunaambiwa kuna mkono wa mtu, tukipewa na Iran tunaambiwa hivyo.

Niambieni mimi kama Waziri wa Mambo ya Nje niende wapi?, alihoji Membe na kumtaka mwandishi huyo amtajie japo nchi mbili duniani ambazo ni takatifu kwa asilimia mia moja ili Tanzania ijenge uhusiano nazo na iachane na nchi nyingine.

Alisema kwa mfano Uganda, ambayo ni mwanachama wa OIC, asilimia 66 ya wananchi wake ni Wakristo, asilimia 10 tu ndio Waislamu na asilimia iliyosalia ni ya watu wasio wa dini hizo na pia, mapapa watatu wamewahi kwenda nchini humo.

Hata hivyo, Membe alisema pamoja na Uganda kujiunga na OIC, idadi ya Waislamu wala misikiti haijaongezeka nchini humo.

Kutokana na hali hiyo, alisema haoni ubaya mtu kunufaika na fedha za shetani na kwamba, kitendo cha Watanzania kuiogopa jumuiya hiyo na Iran, ni kujivua sifa yao ya ujeuri na ujasiri na pia ni kushindwa kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye hakuwa anaogopa hata kitu kimoja.

Kama unakuta shetani mahali ana hela si uchukue. Ujeuri wetu uko wapi?

Kwa nini tunaiogopa Iran. Ukiona mchele umewekwa Kur`ani, hiyo Kur`ani si unaitupa tu, halafu unakula mchele?`` alisema Membe.

Hata hivyo, Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake katika miaka ya 1990 aliwahi kukemea hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kwa kuwa ilkuwa ni ukiukaji wa katiba, licha ya maelezo kwamba ingevinufaisha visiwa hivyo kiuchumi.

Katika makemeo yake, Mwalimu Nyerere alisema hawezi kukaa kimya kuruhusu Zanzibar inufaike kwa kuvunja Katiba ya nchi.

Hata hivyo, Waziri Membe jana alisema suala la Tanzania kujiunga na OIC au la, litaamuliwa na wananchi wenyewe na kusisitiza kuwa aliposema bungeni Agosti 22, mwaka huu kwamba, kujiunga na OIC hakuna madhara hakumaanisha kuwa Tanzania imeshajiunga na jumuiya hiyo.

``Tuiache Israeli iiogope Iran. Tuna ubalozi wa Iran, hatukuwafukuza. Kwa nini tunaogopa na jeuri zetu. Uamuzi huu utafanywa na Watanzania wote, serikali kazi yake ni kutoa changamoto. Naomba Watanzania tujiamini.

Hata Tanzania tunachukiwa kwa kuishambulia Uganda, lakini tulikuwa na sababu. Kama (serikali) tungekuwa na woga tusingejiunga na Marekani kwa sababu hawa (Marekani na Iran) ni maadui`` alisema Membe.

Jana gazeti hili lilimkariri Balozi Iddi akisema kwamba mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC unatarajiwa kuanza wakati wowote na kwamba, hatua ya mwanzo ya mchakato huo.

Alisema viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano watakutana na wenzao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa ajili ya kupata msimamo wa pamoja kuhusu suala hilo.

Naibu Waziri huyo alisema hayo alipoulizwa na Nipashe kama mchakato kwa Tanzania kujiunga na jumuiya hiyo umeshaanza au la tangu Waziri Membe atoe kauli hiyo bungeni, mjini Dodoma, Agosti 22, mwaka huu.

Alisema mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC ni mrefu, ambao unatarajiwa pia kulishirikisha Baraza la Mawaziri kufikia maamuzi.

Balozi Iddi alisema hatua nyingine ya mchakato, ambayo serikali inatarajia kuichukua, ni kutoa elimu kwa umma ili kuwaondoa uoga wote walioonyesha hofu iwapo Tanzania itajiunga na jumuiya hiyo.

Agosti 22, mwaka huu Waziri Membe wakati akifunga mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake, alisema hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na IOC.


SOURCE: Nipashe
 
Hao maaskofu mawazo yao yanawakilisha kundi moja la watanzania kwahiyo wasituburuze tutaingia oic kwa manufaa ya hao maaskofu na vizazi vya pia

Shy you always boring my friend........ you better stay quite
 
Waziri Membe apigia debe OIC

Kwa nini tunashikwa na uoga? Tukipewa msaada na Marekani tunaambiwa kuna mkono wa mtu, tukipewa na Iran tunaambiwa hivyo.

Niambieni mimi kama Waziri wa Mambo ya Nje niende wapi?, alihoji Membe na kumtaka mwandishi huyo amtajie japo nchi mbili duniani ambazo ni takatifu kwa asilimia mia moja ili Tanzania ijenge uhusiano nazo na iachane na nchi nyingine.

MEMBE USITAKE NICHEKE MIE KHA! ITS VERY SIMPLE RUDI KWA WANANCHI, MBONA YA ZANZIBAR MLIVYOONA YANAWASHINDA MKAFIKIA MUAFAKA WA KUYARUDISHA KWA WANANCHI ILI WAAMUE WENYEWE KWA KUPIGA KURA?? HOW COMES THIS ONE LIKUCHANGANYE KICHWA........ AMKA SHITUKA HUKO MNAPOTAKA KUTUPELEKA HATUTAKI KABSAAA NA MSHINDWE NA MLEGEE KWA JINA LA YESU


[COLOR="red"]Kwa nini tunaiogopa Iran. Ukiona mchele umewekwa Kur`ani, hiyo Kur`ani si unaitupa tu, halafu unakula mchele?`` alisema Membe.


HATA WAMERAKANI WANAIOGOPA IRAN NDO MAANA HAWAISHI KUISEMA SEMA, NA PIA HAPA UNAENDANA NA IMANI ZA WAISLAMU HOW COMES UTUPE MAANDIKO WANAYOYAAMINI WAO??
 
Nina uhakika kwamba percent kubwa ya nchi hii ni waislamu na pia tuna haki ya kujiunga na OIC...kujiunga na OIC hakiwezi kuifanya nchi hii ya Kiislamu bali tutatambulika tu kwamba ni nchi ambaye ina waislamu wengi na imejiunga na umoja huu. Waziri Membe anachukua hatua hii kutokana na maslahi ya nchi, na pia nina uhakika kwamba referendum ikifanyika waislamu(ambaye ni majority) watashinda kwa hio tusibabaishane kwa swala ambalo ni obvious. Sisi wote tuna haki kama wananchi na tafadhali msilete udini au ukabila, tusonge mbele kama Wazawa wa nchi mmoja. UNITED WE STAND, DIVIDED WE FALL!
 
Mimi nashangaa hivi tulipoanzisha uhusiano na vatican nani alishauriwa.
 
Nationality:
noun: Tanzanian(s)
adjective: Tanzanian
Ethnic groups:
mainland - African 99% (of which 95% are Bantu consisting of more than 130 tribes), other 1% (consisting of Asian, European, and Arab); Zanzibar - Arab, African, mixed Arab and African

Religions:
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim


Languages:
Kiswahili or Swahili (official), Kiunguja (name for Swahili in Zanzibar), English (official, primary language of commerce, administration, and higher education), Arabic (widely spoken in Zanzibar), many local languages

SOURCE: CENTRAL INTELLIGENCE AGENCY(CIA) THE WORLD FACT BOOK.
Last updated October 23, 2008

Link: https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html
 
...ukiona mtu anafikiri dini yake ndio majority tanzania...basi huyo mtu jina lake ni MJINGA......

......NDIO MAANA MWALIMU HAKUPENDA KUWEKA DINI KWENYE SENSA MAANA KUNA AMBAO WANGEFIKIRI AMEPANGA.....

DISTRIBUTION YA NCHI HII IPO WAZI.......TANGA,DAR,LINDI MTWARA,...

NA "SLAVE ROUTE :" BAGAMOYO,TABORA,KIGOMA.......haya maeneo wazi yana asilimia kubwaa ya dini ya kiislamu.....

maeneo mengine yaliyobaki ya nchi.....asilimia ni ndogo sana ...kuna vijiji nchi hii watu hawajawahi kuona mwislamu[sitanii]...lakini hakuna kijiji amabacho hakina wakristo.....pia AMBAO HAWANA DINI NAO WAPO WENGI[WAPAGANI]

...SO POINT YA WINGI HAINA MAANA KWA KUWA HAUPO HUO....NI NADHARIA TU WANAPOKUTANA WAKIWA WENGI.....LAKINI PIA WAKRSITO WANAPOKUTANA WAKIWA WENGI WANAWEZA KUJIONA WAO NI MAJORITY...FOR WHICH ITS TOOO FULISHNESS....

......MEMBE TAMAA YAKE YA URAIS ATAFANYA LOLOTE ....LAKINI TUNAJUWA KINACHOWAPONZA NI PESA WALIZOCHUKUWA KUFANYIA KAMPENI.....YULE MWANDISHI WA UINGEREZA ALIPOTOBOA WAKASEMA WANAENDA MAHAKAMANI....HAWAKWENDA ...KWANI ALIKUWA NA USHAHIDI WA KIKWETE KUPEWA PESA ZA IRAN KWA MALENGO MAALUM.......NA BUSH ANAMTAIMU TU....

KIUKWELI KUJIUNGA NA OIC HAITAWEZEKANA TANZANIA...WANAOTAKA HII HOJA WAONGEE MENGINE.....WASIPOTEZE MUDA..KWA LISILOWEZEKANA ....KWANI KUNA NGUVU KUBWA YA KUPINGA HILI AMBAYO WASIPENDE KUJARIBU KUIONA.......WASTAARABU HUWA HAWANA MAKELELE....!!!
 
Date::10/24/2008
Maaskofu wakaripia matamshi ya Waziri Membe kuhusu OIC

please delete
 
Back
Top Bottom