Sasa kama alivyopendekeza mwanzoni Rev . Kishoka kuhusiana na Waislaam kuwa na chombo chao kama Wakristu hilo lingekuwa na usawa zaidi lakini serikali ndio imeshatufunga kamba za shingo siku nyingi.. Kelele za Waislaam mnaziona kama kelele za mlalahoi - Kikwete husema kelele hizo hazimzuii kulala. ..
Mkandara,
KUmekuwa na hili suala la kusema EAMWS ilifungwa na Nyerere. Inasemekana Bakwata ni chombo cha Serikali.
Swali langu ni hili, ikiw andani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunadai kuwa Waislamu hawana uhuru wa kuunda vyombo vyao, kuwawakilisha kwa kuwa EAMWS ilifungwa na Nyerere 1968, je kwenda OIC kutasaidia nini ikiwa ndani ya nchi hakuna mshikamano na kuna woga wa mzuka wa Nyerere?
Mimi ningefikiri na kufanya hivi kama ningekuwa ni Muislamu.
Kwanza ni kuleta msukumo wa kuundwa upya wa chombo cha kuwawakilisha Waislamu. na hili ningelianza kwa kutumia mkao wa madhehebu, kwanza, kila dhehebu liwe na chombo kikuu, iwe ismailia, Sunni, Shia, Ahmadiya au wenginewe.
Kisha vyombo vikuu hivi vya madhehebu, ndivyo viongoze wafuasi wao kiroho, vimiliki mali za misikiti na dhehebu.
Baada ya hapo, ndipo kuundwe baraza kuu la kuunganisha madhehebu haya kwa kutokana na viongozi wa vyombo vikuu vya madhehebu. Chombo hiki kikuu, ndicho kiwe mstari wa mbele kama vile TEC au CCT zilivyo na ndipo chombo hiki iwe ni Bakwata au EAMWS mpya kishike hatamu za kujiunga katika jamii na jumuiya nyingine za Kiislamu duniani, huku madhehebu yakiwa huru kujiwakilisha.
Ikiwa Ummah wa Sunni wataungana na jamaa wao wa Saudi na kujiwakilisha, hilo liwe ruksa, ikiwa wa Shia watasema sisi vijana wetu tunawapelea Iran kujifunza kwenye seminari, hilo liwe ruksa.
Kubwa zaidi ni kwa jumuiya hizi kuwa huru na kuondokana na kuitegemea Serikali ya Jamhuri katika maamuzi ya kila siku.
Inaelekea mgongano ndani ya Bakwata ni mkubwa kukiwa na pande mbili, wale ambao ni makuwadi wa Serikali na wale ambao ni huru wenye kutaka EAMWS irudi.
Sasa jambo la kujiuliza ni lini jamii hii itakaa chini na kuondokana na tatizo la uongozi ndani ya jamii na Baraza la uongozi?
Tanzania kama nchi kujiunga OIC, bado hakutakuwa suluhisho kumkomboa Muislamu ikiwa dhana ni kuwa kukimbilia nje ya nchi kupata misaada ndiyo suluhisho wakati kazi ya kwanza ya kumkomboa Muislamu inapaswa ianze ndaniya nchi kwa kuiunda upya Bakwata nakuifanya iwe huru na iwe na nguvu kuisukuma serikali kama vile inavyoonekana kuwa KKKT, CCT na TEC wanafanya.
Jukumu la kuiunda upya Bakwata na kuwaunganisha Waislamu wa Tanzania ni la Waislamu wa Tanzania na si OIC au Serikali ya Tanzania.