Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

waislam waachwe waanzishe baraza/korti yao ya usuluhishi AKA kadhi ila wajue sheria za nchi ni superior kuliko hiyo ya kadhi na hiyo kadhi ni kwa ajiri yao na wala haimo kwenye katiba na gharama ni za wahusika sio tax payer money!
 
Chuma ,

Naona badala ya kujibu hoja nilizotoa umekimbilia kwenye " Name calling " , sijui umefikia vipi conclusion ya kuwa nina elimu ndogo ya ufahamu ya mahakama ya kadhi. Kama nilivyosema sipingi waislamu au dini yeyote ile kuwa na mahakama yao ! Mimi ninachopinga ni mahakama hiyo kuwa part ya serikali na zaidi kutumika kwa hela ya walipa kodi kuendesha hiyo mahakama . Hii sio fair hata kidogo kwa nini hela za walipa kodi zitumike kuiendesha hii mahakama , mimi ambaye siamini katika dini husika nitafaidika vipi na hii mahakama?

Pili , lazima tuangalie suala la katiba yetu . Kama kweli tunasema serikali yetu haina dini bali watu wake ndio wana dini , tutawezaje pia kusema serikali yetu ina sponsor mahakama ya kadhi na zaidi viongozi wa mahakama hiyo ni wafanyakazi wa serikali ? Vipi kuhusu mgongano wa kikatiba.... na jee itakuwaje kama dini nyingine just over a sudden zikaamua kuanzisha mahakama zao na kutaka mahakama hizo pia zitambulike kikatiba, are you going to stop them ?

Suala la kusema dini nyingine hazina mahakama ni weak , kwani mahakama ni suala ambalo dini yeyote inaweza kuanzisha especially wakiona kuna incentives hela za serikali. Ni muhimu kwa watu kuangalia hii issue katika three dimension na kujaribu kuondoa itikadi zao za kidini wakati tunapojadili.
 
Hivi majuzi Mahakama kuu imemzuia Kikwete na Wanasiasa wote kutozungumza lolote juu ya mahakama ya Kadhi hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na mahakama hiyo.

Huu unaonekana ushindi kwa mtikila aliyeahidi kuwasimamisha watu kuzungumzia hilo hadi Kesi yake imalizike.
 
Wana JF, sina uhakika kama BArua hii ya Mchungaji Mtikila iliwafikia hapa maana sikufanikiwa kuiona kwenye vyombo vya habari(redio na magazeti) labda waliogopa kuitoa; nawawekea tuipitie, tuichambua na tutoe maoni yetu.

Pia nitawawekea Press Statement ya Mtikila aliyoitoa baada ya kukamatwa na Polisi. Lakini pia naomba ushauri kwenu Je, niweke kesi aliyoifaili Mahakama Kuu kupinga Mahakama ya Kadhi hapa JF? Maana Mahakama Kuu imeamuru jambo hili la Kadhi lisijadiliwe hadi hapo itakapokuwa imeamu shauri hilo.

Wakatabahu
 
Ibra, suala la Mahakama ya Kadhi haliwezi kujadiliwa na Bunge au Mahakama siyo na watu wa kawaida. Mahakama haina uwezo huo wa kuzuia watu (raia) kutoa maoni yao nyumbani kwao au kwenye kigenge!
 
Lakini pia naomba ushauri kwenu Je, niweke kesi aliyoifaili Mahakama Kuu kupinga Mahakama ya Kadhi hapa JF? Maana Mahakama Kuu imeamuru jambo hili la Kadhi lisijadiliwe hadi hapo itakapokuwa imeamu shauri hilo.

Wakatabahu

...you are the man, that was no bullshit, straight to the point,Mtikila is one man army, i salute him, nilichopenda ni jinsi tu alivyowahabarisha hao wasanii wawili bila kuzunguka mbuyu. Peace
 
Nimeupitia kwa maini walaka wa Mtikila, the guy is so smart I salute him!

Kwakweli maoni/hoja zake ni za msingi sana, na pengine zinatisha kama kweli mpango ni mkubwa kiasi hichi!!!

Unajua wengine tunaona yanatendeka na kama kawida yetu watanzania tunachukulia mambo ya kawaida/kirahisi tu!! duuu.. inatesha kama mamabo yako hivo.. napata wasi wasi kwamba tunako elekea siko!! MUNGU TUNUSURU!!
 
Nimejaribu kuiweka hii kwenye RTF ili isomeke hapa. Sijui kama itakaa vizuri.

The Full Salvation Church
Kanisa la Wokovu Kamili


P. o. Box 3885
Phone 2180725
Dar es Salaam


"Salvation for Body, Soul and Spirit"
"Wokovu wa Mwili, Nafsi na Roho"

01 Novemba 2007

Ndugu Edward Lowasa
Waziri Mkuu,
Ikulu
DAR ES SALAAM

USALITI WAKO WA KUMSAIDIA KIKWETE KUSILIMISHA NCHI
KWA MBINU YA MAHAKAMA YA KADHI


*Ukiwa kiongozi uliyeajiriwa na wananchi kwa Katiba ya Jamhuri uliyoapa kuitii na kuilinda na kuitetea kwa moyo wako wote, ukaweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kwa kumwinulia Biblia Takatifu, na

*hali ukijua kwamba ki-Katiba ni mwiko kabisa uongozi wa Taifa hili ambalo ni secular kujihusisha na dini fulani, ambapo dini inabaki kuwa uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wake hivyo kwamba jukumu la serikali ni kulinda tu Haki ya Msingi ya uhuru wa kuabudu (Ibara ya 19 na 20(1)
ya Katiba ya Jamhuri), na

*huku ukijua kwamba Katiba ya Nchi inakupiga marufuku wewe na
mamlaka yoyote ya Nchi hii kutunga sheri a au kuweka taratibu au kanuni yoyote yenye ubaguzi au upendeleo wa aina yo yote ile ama kwa dhahiri au kwa taathira yake:

  • 1. Umekiri wakati ukiwa mkoani Mbeya siku ya Jumamosi tarehe 20 Octoba 2007 kwamba kwa vipande thelathini vya fedha? wewe na wenzako katika serikali ya awamu ya nne mmeikanyaga Katiba ya Nchi kwa kuipa Tume ya kurekebisha Sheria (Wizara ya Sheria na masuala ya Katiba) kuandaa utaratibu wa kisilimisha Nchi yetu kwa kubadili Katiba ili kuanzisha "Sharia" ya mahakama ya Kadhi, kwa kutumia Bunge la Jamhuri ya Muungano! Na wewe ndiwe uliyewezesha kuzungumzwa Bungeni suala hili la kigaidi, na kuridhia azma hii ya hatari ifanyiwe kazi na Wizara ya Sheria, ukimjali zaidi rafiki yako Jakaya mnayemaliza naye nchi yetu kwa ufisadi wa klltisha, kliliko Bwana Yesu aliye na hatima yako ya milele!

    2. Umeshiriki mkakati huu wa Jihad hali ukijua kwamba mahakama ya Kadhi ni nyenzo ya kusilimishia nchi kwa upanga iwe lamhuri ya . Kiislamu, yaani kufuta Hald ya Msingi ya Binadamu ya Uhuru wa Kuabudu na kuuangamiza Ukristo nchini, kuwaua watu wasioikubali qini ya Kiislamu, kuwaua Waislamu watakaoiacha dini hiyo na kujiunga na imani zingine wanazozipenda n.k, majukumu ya kigaidi ambayo kwa mujibu wa Kurani na Hadith za Mtume (s.a.w) ndiyo yanayopaswa kutekelezwa na Kadhi!

    3. Umeasi kiapo chako cha ajira na Katiba ya Nchi kwa kusimamia utekelezaji wa Jihad hii kwa kiwango kilichofikiwa, hali ukijua kwamba mahakama ya Kadhi ni taasisi ya kigaidi iliyo ndani ya Kurani, ambayo ni msahafu wa dini ya Kiislam. Unajua kwamba
    kutumia Bunge na Serikali kuhalalisha matakwa au lengo la dini fulani ni njia dhahiri ya kuifanya dini hiyo kuwa ya lazima kwa watu wote! Hii ndiyo njia ya mkato ya kusilimisha nchi, aliyoichagua jemadari mjanja sana wa Jihad, lakaya Kikwete! Lakini mbali ya kuwa mapinduzi hatari ya Katiba ya Nchi, unajua kwamba huku ni kumaliza kabisa amani ya Nchi na umoja wa Taifa hili!

    4. Ulipaswa kuitetea Katiba ya Nchi ilipoanza Jihad hii katika chama chenu CCM, ambamo kwa udini na ufisadi mlipenyeza hiyo mahakama ya Kadhi katika Ilani yenu ya Uchaguzi, kichaa ambacho kimepigwa marufuku na Ibara ya 20 (2) (a) (i) ya Katiba ya lamhuri! Ukiwa Waziri Mkuu ilikupasa kuhakikisha kwamba Msajili wa vyama vya siasa anafuta usajili wa chama hicho kwa sababu ya wendawazimu huu!

    5. Umeusaliti Ukristo kiasi kwamba hata ulipojua kwamba Kesi ya Katiba Na. 80 ya mwaka 2007 ipo Mahakama Kuu ili kukomesha Jihad ya kusilimisha nchi yetu kwa kuanzisha mahakama ya Kadhi, wewe ulitangaza kule Mbeya kuendelea na Jihad kwa kutumia Tume ya kurekebisha Sheria, ili hatimaye mtumie Bunge la Nchi kuupa
    ugaidi nguvu ya Sheria nchini! Umefanya kosa hili wakati unajua kwamba ni mwiko kabisa kwa serikali au Bunge kushughulikia jambo lolote ambalo liko katika Mahakama Kuu! Unapouchukia Ukristo kiasi hiki tukuelewe kuwa umesilimu na kubaki na j ina tu la "Edward" kwa ajili ya kuhadaa Wakristo?


UGAIDI UNAOENDELEA DHIDI YA UKRISTO NCHINI

Papa Benedict XVI alishindwa kuuvumilia usanii wa Jakaya Kikwete
alipomdanganya kwa dakika 15 kwamba eti anadumisha uvumiliano wa
kiimani hapa nchini, wakati siyo siri kwamba katika utekelezaji wa maazimio ya Abuja ya Ole na IAO Kikwete ni jemadari wa kwanza wa Jihad aliyediriki hata kuuingiza ugaidi wa kuutokomeza Ukristo ndani ya Katiba ya Nchi kwa mbinu hii ya mahakama ya kadhi kwa kuwachukulia Wakristo wa nchi hii kuwa mataahira!


Kama vile gaidi la kimataifa Osama Bin Laden lilivyotangulia kuonya mara kadhaa kabla ya kulipua majengo ya WTO jijini New York kwamba lingeiadhibu Marekani kwa kudhamini dini ya makafir (Ukristo) duniani, ni ugaidi pia utekelezaji wa maazimio ya kigaidi ya Abuja uliothibitika kuendeshwa na Jakaya Kikwete kuanzia katika uteuzi wake wa mawaziri, makatibu wakuu, mabalozi, wakuu wa mikoa na wilaya, na viongozi wa Taasisi za umma, hata kama ni ugaidi wa baridi kuliko wa Al-Qaeda.


Kikwete na Saidi Mwema wanaendesha ugaidi wa kuuangamiza Ukristo
nchi nzima, kwa kutumia Jeshi la Polisi kuzuia kwa mabavu na kuvunjilia mbali mikutano ya hadhara ya kuutangaza na kuutetea Ukristo, huku likiilinda kwa silaha mihadhara ya Waislamu ya kuuangamiza Ukristo. Ustadh Saidi Mwema amerudisha kimya kimya utaratibu ,. uliopigwa marufuku ki-Katiba wa vibali vya Polisi kwa ajili ya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, kwa ajili ya kudhibiti wahubiri wa ki-Kristo wasieneze wala kuitetea lmani yao inaposhambuliwa hadharani na Waislamu kwa ulinzi wa Polisi.


Kwa agizo la Jakaya Kikwete na usimamizi wa Saidi Mwema mikutano ya Wakristo inavamiwa na Polisi kwa kisingio kwamba Wakristo hawana haki ya kuhubiri baada ya saa 12 jioni, ingawa kanuni tuliyowekewa na Bwana Yesu ni kukesha, kama Yeye mwenyewe alivyofundisha ule mkutano siku tatu mfululizo usiku na mchana. Lakini Waislamu wanaachiwa kuendesha mihadhara yao hadi saa saba za usiku, mbali ya mahubiri yao ya masaa 24 kwa vipaza sauti vya misikitini, bila kujali mateso ya wananchi wengine kwa bughudha hiyo!


Wameliagiza Jeshi la Polisi kutumia kisingizio kwamba mahubiri ya
Wakristo yanahatarisha amani kwavile eti Waislamu hawafurahishwi!
Yaani. Wakristo wanalazimishwa kuhubiri wanayopenda kusikia Waislam!
Hii ni kinyume kabisa na mhimili wa haki ya msingi ya uhuru wa kuabudu



ambao ni kuvumiliana kiimani yaani religious tolerance, ambapo mvunjaji wa sheria anayeshughulikiwa na Polisi duniani kote ni yule anayeshindwa kustahimili na kuheshimu imani na mafundisho ya
wengine, hata kama ni matusi au makufuru kwa mungu wake yeye!


Kielelezo muhimu ni ile hukumu ya Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Hassan Dibagula aliyefungwa Morogoro kwa kuutukana Ukristo kwamba Yesu si Mungu wala si mwana wa Mungu kwa sababu Mungu hakuoa wala hakuzaa. Mahakama ya Rufaa ilimpa haki Mwislamu huyo kwa sababu hayo matusi na makufuru dhidi ya Mungu wa Wakristo ndiyo imani yake yeye, na ni haki yake ya ki-Katiba ya uhuru wa kuabudu au kuamini hivyo.


Fafanuzi hiyo ya Mahakama ya Rufaa inasisitiza kwamba Polisi walipaswa kuwakamata Wakristo walioshindwa kumvumulia Hassan Dibagula, kwani hao ndio waliovunja kanuni ya uvumiliano wa kiimani au religious tolerance, ambayo ndio nguzo ya amani katilm mataifa yenye ustarabu wa kidemokrasi. Vivyo hivyo na Waislamu wanaoshindwa kustahimili mafundisho ya Wakristo ambayo na wao pia ndiyo imani yao na haki yao ya uhuru wa kuabudu, ndio wanaopaswa kukamatwa na Polisi na kufikishwa mbele ya Sheria!


Makamanda wa Polisi wanapolinda mahubiri ya Waislamu (ambayo ni
makufuru na matusi kwa Wakristo) kwavile ni haki ya Waislamu ya ki-katiba ya uhuru wa kuabudu kwa sababu ndiyo imani yao, huku
wakiwafanyia uharamia Wakristo wa kuvunja mikutano yao ya kueneza na kuitetea lmani yao na kuwatupa ndani wainjilisti nchini kote, huu ndio ugaidi wa OIC/IAO ulioazimiwa Abuja, unaotekelezwa kwa ujasiri na Kikwete na Saidi Mwema, ambao ni lazima utokomezwe kwa gharama yoyote! Wakristo wa kweli maana yake wahanga kwa ajili ya Kristo.


Kikwete na Saidi Mwema wanafahamu kwamba mtu anayehatarisha amani
kuhusu dini duniani kote ni yule asiye na ustarabu wa uvumiliano wa kiimani, na hii ndiyo mbegu ya ugaidi. Ndiyo maana watu wa jinsi hii sasa wanadhibitiwa kwa nguvu zote ulimwenguni. Lakini hapa kwetu ni kinyume, kwani Jeshi la Polisi ndilo linalotumika kuwanyang'anya Wakristo haki yao ya uhuru wa kuabudu, kwa kosa la kuhubiri yasiyowafurahisha Waislamu!


Isitoshe, Jakaya Kikwete anaendesha Jihad wazi wazi katika lkulu yetu, ambako milolongo ya wajahidina wanakwenda kugawiwa mapesa ya umma kwa ajili ya kuimarisha Dislam. lkulu imegeuka msikiti mkuu wa nchi ambao sasa unagharamia Waislamu kwenda hija, unalisha waumini futari na kudhamini mihadhara ya Waislam ya kuuangamiza Ukristo nchini, kwa bajeti kubwa sana ya serikali aliyojipangia Kikwete. Kama huku siyo kusilimishwa Taifa letu kimya kimya ni kitu gani?


Lakini Kikwete alijiweka wazi katika hotuba yake- ya kwanza Bungeni, aliponena kwamba hataifuata Katiba ya Nchi kama msahafu, bali katika mambo mengine atatumia busara yake mwenyewe, yaani uwezo usio na mipaka anaoutumia sasa kuipeleka nchi pabaya sana!


Ugaidi wa Kikwete ni pamoja na ule anaoufanya kimya kimya kule Mbeya anakotumia dola kutesa Wachungaji, kwa kisingizio kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita eti walifikiwa na vipeperushi vya wapinzani wake vilivyoanika maovu yake na kushawishi wananchi wasimpe kura, ili Taifa lisiangamie kwa ufisadi unaomaliza nchi hivi sasa. Hii si Jihad ya kawaida bali utawala wa kigaidi yaani rule of terror.


Wewe Edward ni Mkristo unayefahamu jinsi inavyotekelezwa mikakati ya kuufisha Ukristo nchini tangu awamu ya Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Unajua jinsi magaidi walivyochoma mota shule ya Shauritanga na - kuteketeza watoto wetu 43, Scotland Yard wakaletwa kuchunguza ugaidi huo, lakini Alhaj Ali Hassan Mwinyi na mamluki Lyatonga Mrema aliyemtumia kupigia debe mahakam a ya Kadhi wakakataa kutangaza taarifa ya uchunguzi wa ugaidi huo na kuwachukulia hatua maadui hao wa Ukristo! Leo una taka kuupa ugaidi nguvu ya sheria!


Unajua kwamba mpaka sasa makanisa zaidi ya 16 yamechomwa mota
nchini, lakini kwavile ugaidi unadhaminiwa na vigogo wenye dhamana ya dola hata mtuhumiwa mmoja hajakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria! Unakumbuka jinsi makanisa ya S1. Joseph's Cathedral na St. Peter's yilivyoponea chupuchupu kuteketezwa. Tena unajua jinsi yalivyovunjwa makanisa makubwa kwa amri ya watawala Waislamu kwa visingizio vya kipuuzi, kama lile la Pemba lililokuwa kama la Mkunazini Zanzibar lenye thamani ya mabilioni ya fedha, lakini Wakristo walipolialia wakalipwa "fidia" ya shilingi elfu kumi na nne (Sh. 14,000/-)


Kitendo cha Rais Kikwete na Saidi Mwema cha kunyamazia uchochezi wa Radio Kurani wa kukatwa kichwa Mchungaji Mtikila, na kuzuia askari wasiwafikishe mbele ya sheri a Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake wa msikiti wa Mtambani kwa hukumu yao ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2007 ya kumteka nyara Mchungaji Mtikila na kumkata kichwa, ni ushahidi kwamba wameubariki ugaidi, ndiyo maana walitaka kuupa nguvu ya kisheria kwa mahakama ya Kadhi.


Kuna taarifa za kuendeshwa kimya kimya zoezi" zito la kuhojiwa vikali na kutishiwa kuondolewa kazini walokole katika Jeshi la Ulinzi, kwa amri ya Mnadhimu Mkuu mpya ambaye anaonyesha kutaka. kuunda Jeshi la Kiislamu kwa malengo hatari ya Jihad.


Kwa ugaidi huu nchini mwetu na ari mpya, nguv~ mpya na kasi mpya ya Jakaya Kikwete ya kutekeleza maazimio ya Abuja ya OIC/IAO ya Jihad, hotuba aliyoitoa Italia ni usanii wa kuhadaa ulimwengu, ili usielekeze macho kwenye maangamizi ya Ukristo anayoendesha katika nchi yetu. Lakini Wakristo wa nchi hii ni Mwili mmoja wa Kristo, kwahiyo mikakati yote ya Jihad dhidi ya Ukristo haitafanikiwa. Hata majengo ya Morogoro yaliyogeuzwa kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu anzeni utaratibu wa kuyarudisha TANESCO.


Mwisho, mpendwa Lowasa unajua kwamba kwa maagizo ya'Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu la Torati (17:14-20) wewe na rafiki yako
Kikwete pamoja na mtandao wenu hamnayo kabisa sifa ya kuongoza nchi. Ufisadi na ushirikina hauwezi kuwakinga na Mkono wa Mungu unapoinuka kuangamiza kabisa uchafu katika nchi hii. Kwahiyo mnaIo jambo moja tu Ia kufanya, naIo ni kutengeneza na Mungu upesi juu ya ugaidi, ufisadi, na uporaji wa nchi yetu mlioufanya kwa kasi mpya na nguvu mpya.


Kwa ajili Haki, Amani na Hatima ya nchi yetu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.


Mchungaji C/Mtikila,
MW ANGA(IZI WA KANISA


Nakala kwa :Viongozi wa Makanisa yote nchini
: Mitandao ya Kikristo
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete
: Vyombo vya habari
6
 
Huyu Mtikila sikubaliani naye katika mengi ila nimeanza pia kuogopa ukali wa maneno yake.

Sijui ni watanzania wangapi wataamini hiki. MUNGU tusaidie na hiyo nchi yetu inayoonekana kama imelaaniwa.
 
Sijapenda hata kidogo tone + pathos katika hiyo barua, Mtikila you are better than that !
 
As bad as I dislike Islamic fundamentalism, I dislike a counter that is rooted in fundamentalism even more.

Mtikila amefuja nafasi nzuri ya kumkosoa Lowassa.Kwanza kaanza vizuri kwa kueleza umuhimu wa viongozi kudumisha maadili ya secularism.Halafu akapoteza command yote ya issues kwa ku-introduce extremism na unsubstantiated claims.

Watu kama Mtikila ni wa kuogopwa sana kwa sababu wana potential ya kufanya kitu chcchote kiwe combustible.

Nawaweka Mtikila ma Mrema katika kundi moja la sensationalist politicians.Mtikila's brand of extremism is even worsened by the fact that from his command of the central issues he ought to know better, it's not like he is talking at the level ya mchungaji wa mtaani au ustaadh aliyekosa ilmu dunia.

To me, fundamentalism is dangerous, period, be it Christian,Islamic or Atheistic.
 
hakuna kitu kibaya kama hoja za woga! Hoja zinazotishia woga au zinazotokana na woga ni hoja zinazolenga hisia badala ya akili. Ningepata muda ningechambua udhaifu wa hoja za Mtikila, natumaini wenye kuangalia kwa karibu wataweza kuuona udhaifu huo kiurahisi tu.
 
na Mohammed Abduralhman, Zanzibar



BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi visiwani humu, wameifufua hoja ya Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya OIC, na kusema kuwa wakati umefika sasa kwa Zanzibar kujiunga na jumuiya hiyo kwa vile sera ya mambo ya nje imebadilika.
Waliyaeleza hayo wakati walipokuwa wakichangia mada katika semina ya siku mbili kujadili sera mpya ya mambo ya nje, iliyofunguliwa juzi na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha.

Mwakilishi wa Ziwani, Rashid Seif, alisema Zanzibar hivi sasa inayo nafasi ya kujiunga na OIC kwa vile sera ya mambo ya nje imebadilika kutoka kuwa ya kisiasa na kuwa ya kiuchumi.

Alisema kwamba kubadilika huko kwa sera, sasa kunaiwezesha Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na OIC, kwa vile awali ilizuiliwa kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo kwa sababu za kisiasa.

Mwakilishi huyo alisema kwamba, kwa kuwa sera ya mambo ya nje imezingatia diplomasia ya uchumi, basi Zanzibar iruhusiwe kujiunga na jumuiya hiyo kwa vile itaweza kunufaika kiuchumi.

“Zanzibar ipo tayari kuruhusiwa kuingia OIC kwa vile ilizuiwa kujiunga kwa sababu za kisiasa, lakini sasa sera imebadilika kutoka sera ya kisiasa na kuwa ya kiuchumi,” alisema mwakilishi huyo.

Akizidi kujenga hoja hiyo, Mwakilishi wa Jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk, alisema kwamba muungano wa Tanganyika na Zanzibar una serikali mbili, ambazo uchumi wake unatofautiana.

Alisema kwamba ni jambo la kushangaza hadi suala la kujiunga na OIC halijapatiwa ufumbuzi wakati serikali ya Muungano iliahidi kulishughulikia baada ya Zanzibar kutakiwa kujiondoa.

“Bahati mbaya hadi sasa suala hili lipo kimya, wakati Serikali ya Muungano iliahidi kulishughulikia, lakini matokeo yake tunaona Uganda inaendelea kunufaika na jumuiya hii,” alisema mwakilishi huyo.

Aidha, alisema kwamba ili Zanzibar iweze kupiga hatua kiuchumi, lazima kero za ndani za Muungano zitatuliwe, hasa katika mfumo wa kodi, kwa vile hivi sasa wafanyabiashara wa Zanzibar wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika suala la ulipaji kodi kutokana na viwango vyake kutofautina kati ya Tanzania Bara na Zanzibar wakati mamlaka inayosimamia mapato (TRA) ni moja.

Katika hatua nyingine, Wawakilishi hao walidai kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado una matatizo mengi hadi hivi sasa kwa sababu uundwaji wake uliharakishwa.

Walisema kuundwa kwa muungano huo haukwenda hatua kwa hatua, na kushauri suala hilo lizingatiwe wakati wa kuingia kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Hassan Diria, ndio walioruhusu Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kusababisha mgogoro mkubwa nchini.

Hata hivyo, baadaye hatua hiyo ilipingwa kwa madai kuwa Zanzibar haina haki ya kujiunga na jumuiya za kimataifa, kwa vile utaifa wake ulikufa kama ulivyokufa wa Tanganyika mwaka 1964, baada ya kufikiwa kwa Muungano.

Hata hivyo, akijibu hoja hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, alisema suala la Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na OIC, bado linazungumzika na linahitaji mjadala kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.

“Si kama Serikali ya Muungano haipendelei Zanzibar ijiunge na jumuiya hiyo, lakini bado kunahitajika baadhi ya mambo ya msingi yakaangaliwa kati ya pande zote mbili, ili utekelezaji wake usiathiri katiba ya nchi,” alisema Waziri Membe.

Alisema kwamba wakati suala hilo lilipoibuka lilionekana linagusa masuala ya dini, lakini tayari limekuwa likitekelezwa na nchi za Afrika, ikiwemo Uganda na Msumbiji ambazo ni wanachama katika jumuiya hiyo.

“Jambo la msingi ambalo Serikali ya Muungano itapaswa kuliangalia ni kuona Zanzibar iwapo itajiunga na jumuiya hiyo haitaweza kuvuruga katiba ya nchi katika mambo yanayohusu Muungano,” alisema.

Kwa upande mwingine, Membe alisema serikali mbili zimeshapiga hatua kubwa katika kutatua kero za Muungano tangu kuundwa kamati iliyotokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete na kuwashirikisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha.
 
Hao tulishawachoka, tatizo nafikiri hao wananchi wenzetu wa visiwani bado hawajaelewa ni masuala yapi yako chini ya Muungano na yapi yapo chini ya SMZ.
 
Hao tulishawachoka, tatizo nafikiri hao wananchi wenzetu wa visiwani bado hawajaelewa ni masuala yapi yako chini ya Muungano na yapi yapo chini ya SMZ.

aliemchoka mwenziwe ni nani?

nani hajaelewa yapi masuali ya muungano? mwenzetu uko mbali kubwa nnakupa pole.


uelewa juu ya muungano zanzibar ni mkubwa sana. na hili ni suala ambalo karibu kila mzanzibari linamuuma na kumgusa kwa sana. ni kitu nyeti kwetu hiki.

huenda upande wa pili hata hawajui hasa kuhusu huu muungano, na hawajui vipi uliunganishwa.

tuzungumze kwa uwazi au litote tugawane mbao
 
Mtu wa Pwani,

wawakilishi wangependekeza Tanzania ijiunge na OIC, siyo Zanzibar peke yake. Uamuzi mzito kama huo unapaswa utolewe IDODOMYA.
 
Zanzibar, some time I am getting little tired to hear anything from yakhe side. Plz save it
 
acheni wajiunge tuu kwani shida ni nini?na ukweli Zanzibar 90% au zaidi ni waislam, lakini wajue sheria za nchi na katiba ni ile ile,ila wasituletee mambo ya sharia hapo ndani ya nchi la sivyo itakuwa marufuku
 
Kuwasaidia uelewa zaidi ili muweze kujadili mada hii mkiwa na taarifa za kutosha, hebu someni kwanza ile CHARTER iliyoanzisha OIC mwaka 1972. Charter hiyo ina articles 14, nazo zinajieleza wazi, inapatikana hapa: http://www.oic-oci.org/oicnew/page_detail.asp?p_id=53
Baada ya kuisoma kawa makini, nimeona kwamba Zanzibar na hata Tanzania zinaweza kujiunga na muungano huo iwapo zitabadilisha katiba yake na kuwa nchi za kiislamu. Muungano wa OIC umetamkwa wazi kwamba muungano ni wa nchi za kiislamu (na si wa makundi tu ya kiislamu), na hii inamaanisha kwamba waislamu wa Tanzania wakitaka umoja huo inabidi wajiunge kama nchi, na si kama kundi. Na muungano si wa nchi "zenye waislamu" bali ni wa nchi "za kiislamu". Hii sio NGO, (wala hauwezi kulinganishwa na vyombo kama FIFA) ni muungano rasmi wa dola (states) (kama tunavyozungumzia AU, Commonwealth nk), wenye baraza la wakuu wa nchi na wafalme, kamati ya mawaziri wa mambo ya nje, sekretariat, nk. Wakiitisha kikao cha "Kings and Heads of State and Governments" inatarajiwa rais wa nchi mwanachama ahudhurie, na msimamo unaofikiwa pale unachukuliwa kama msimamo pia wa nchi husika, kwa hiyo rais anarudi nao nyumbani kuutekeleza. Je hii inawezekanaje kwa nchi ambayo kikatiba si ya kiislamu? Hapo ndio ninapoona matatizo mengi, na ndilo linalowapa mashaka wasio waislamu. Sina uhakika wa uimara (au "uhai") wa uanachama wa nchi kama Uganda na Sierra Leone (ambazo kikatiba si za kiislamu)kwenye umoja huo, lakini logically mtu yeyote anaweza akahisi kwamba hawa hawawezi kuwa active members, maana sielewi wanatekelezaje maazimio ya mikutano hiyo nchini mwao, na sijui kama Museveni huwa anahudhuria vikao vya wakuu wa nchi za kiislamu au huwa anawakilishwa na nani? Kama kuna watu kwenye forum hii wenye details juu ya hili watugee na siye tutafakari kwa pamoja.

Huu ndo mchango wangu kwenye hili suala, wengine karibuni.
 
Back
Top Bottom