Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

nimeona kwamba Zanzibar na hata Tanzania zinaweza kujiunga na muungano huo iwapo zitabadilisha katiba yake na kuwa nchi za kiislamu.

Mkuu Kithuku,

Heshima mbele mkuu, ninajua kuwa wewe ni mmoja wa the brain katika hii JF, hivi hayo maneno ni kweli? Sasa Uganda na Mozambique walibadili katiba zao au?

Binafsi sioni tatizo kwa Zanzibar au Bara, kujiunga na hii kitu, lakini ukweli uwekwe wazi kwanza, kuanzia hiyo kitu yenyewe, wanachama wake maana lazima tujue tunajiunga na nani, faida na hasara zake, na pia tuwekewe mifano ya nchi zilizojiunga na zilivyonufaika, wote tunajua yaliyotupata kwenye EAC, tukaishia kuisaidia Kenya kiuchumi, huku sisi tukizama kwenye umasikini!
 
Mtu wa Pwani,

wawakilishi wangependekeza Tanzania ijiunge na OIC, siyo Zanzibar peke yake. Uamuzi mzito kama huo unapaswa utolewe IDODOMYA.

wawakilishi wanawakilisha serikali ya zanzibar si ya muungano kule tunao wbunge wanaowakilisha serikali ya muungano.

pili wawakilishi wanaangilia jinsi gani kuinua uchumi wa serikali ya smz na kuleta maisha bora kwa wananchi wa zanzibar na si jukumu lao kuangalia tanzania maana wenye jukumu hilo tunao.

pia nnaamini tanganyika hawako tayari kujiunga na mambo haya maana ss tulisimamisha ili kuwapa nafasi wao kujiunga lkn wako kimya inaonyesha hawako tayari au udini inaumung'unyua muungano.

mahakama ya kadhi tu mmepiga kelele mpaka choka mbaya, sasa tunaona tukuombeni mturuhusu ss tujiunge na tunajiunga kwa lengo la kiuchumi zaidi n hilo tumeliweka wazi, na hata yakija mambo ya dini kwetu sio tatizo ni waislamu weng.

wakisema watatusaidia nafasi kumi za kuhiji kila mwaka kwetu fine, wakiamua kutuletea misahafu fine, wakiamua kutujengea misikiti na vyuo fine. ila nnaona nyny kwa haya hamyataki.


kila lenye mwanzo lina mwishowe
 
Li-muungano limekuwa irrelevant na Zanzibar imekuwa nuance. Yengele kama hili ni dalili za mke aliyechoka na yu tayari kwa talaka, kuendelea kumbembeleza ni kujitakia dhahama za bila sababu. Itafutwe a way out of this bs, walioleta muungano wameshajifia na huu muungano mie naona bora uwafuate huko walipo.
Hili nalo ni miongoni mwa mengi ya matatizo Marehemu Julius alotuletea na kutuachia wa-Tanganyika!!!. Enuff is enuff, let 'em go.
 
nimeona kwamba Zanzibar na hata Tanzania zinaweza kujiunga na muungano huo iwapo zitabadilisha katiba yake na kuwa nchi za kiislamu.

Mkuu Kithuku,

Heshima mbele mkuu, ninajua kuwa wewe ni mmoja wa the brain katika hii JF, hivi hayo maneno ni kweli? Sasa Uganda na Mozambique walibadili katiba zao au?
Binafsi sioni tatizo kwa Zanzibar au Bara, kujiunga na hii kitu, lakini ukweli uwekwe wazi kwanza, kuanzia hiyo kitu yenyewe, wanachama wake maana lazima tujue tunajiunga na nani, faida na hasara zake, na pia tuwekewe mifano ya nchi zilizojiunga na zilivyonufaika, wote tunajua yaliyotupata kwenye EAC, tukaishia kuisaidia Kenya kiuchumi, huku sisi tukizama kwenye umasikini!

Mkuu Field Marshal ES,

Sina uhakika na walichofanya Uganda na Mozambique hadi wakajiunga OIC, lakini wangebadili katiba za nchi zao kuwa za kiislamu nadhani isingekuwa siri, tungesikia zikiitwa Jamhuri za Kiislamu. Uwezekano mkubwa ni kwamba viongozi waliohusika "walikiuka" katiba hizo kwa makusudi (au kutokujua, labda) ili wafaidike na hayo waliyoambiwa yako huko. Ukisoma hiyo link niliyoweka ya OIC charter, article zote 14, na composition ya nchi wanachama, na malengo ya muungano, utaona kuwa nchi isiyokuwa ya kiislamu (kiitikadi na kikatiba, na si tu kuwa na waislamu nchini) haiwezi ku-fit katika umoja huo. Ndio maana baada ya kuisoma hiyo charter nikawa nashangaa kuwa hizi nchi kama Uganda, Sierra Leone, Mozambique nk ambazo si za kiislamu, zinashirikije umoja huo? Katika mkutano wa Wakuu wa nchi za OIC, Yoweri Museveni na Armando Guebuza wanahudhuria au la? Na Foreign Affairs Ministers wa nchi hizo wanahudhuria vikao vya Foreign Ministers wa OIC? Ikitokea OIC kutoa misimamo fulani, hawa jamaa wanaitekeleza vipi kwenye nchi zao ambazo si za kiislamu? Hapo nikadhani labda uanachama wao ni passive, pengine wakiwa active wananchi wao wataanza kuhoji ilikuwaje hadi wakaingia, what other explanation can we offer? Nadhani kwa kuwa passive members si rahisi wananchi wa kawaida kuanza kuhoji kuhusu uvunjwaji wa katiba.

Mwalimu Nyerere aliipinga hoja hiyo ya Zanzibar kujiunga huko OIC kwa msingi kwamba katiba ilikiukwa. Mimi sikumwelewa wakati ule, niliona ni sawa kwa waislamu wa Zanzibar kujiunga na wenzao popote walipo duniani. Kumbe mzee yule alikuwa anafahamu mengi zaidi, nadhani alishaisoma hii charter na alikuwa anaufahamu umoja huu vizuri.

Ni wazi tukijiunga OIC kwa katiba iliyoko sasa tutakuwa tunavunja katiba. Na suala la kuibadili ili tuwe na nchi ya kiislamu nadhani ni gumu zaidi. Kama tunayataka ya huko OIC, pengine kuna faida ya kujiunga huko hata kama tunavunja katiba? Twaweza kujadili pia, je kuna hasara gani tukajiunga tu hata kama tunavunja katiba, ili tufaidike mambo fulani fulani? Tuwe opportunistic tu, tujiunge "kisanii" hivyohivyo, yafaa? Hao kina Uganda na Mozambique wanapata nini na wanaathirika vipi? Je zipo athari za muda mrefu za kuvunja katiba kwa mtindo huo? Wenye majibu ya maswali haya watuwekee hapa, yatatusaidia kuchangamsha akili zetu kwenye mjadala huu.
 
Nchi za afrika hazitakaa ziendelee kama zitaendelea na hii mentality ya kutegemea misaada oka kwa wafadhili. Ukiwauliza watu wengi kuwa Tanzania itabenefit kwa kujiunga na hiyo jumuiya watakuambia misaada ! This is ridiculous , in this day and age people still rely on misaada ....
 
Kithuku mtaalamu wa kutoa address za website, tuoneshe website zinazoonyesha mabadiliko ya katiba ya Uganda na Mozambique zilizozifanya nchi hizo 'kuruhusiwa kujiunga na OIC' KWA SABABU NI ZA KIISLAM!!!!!.
 
Hao tulishawachoka, tatizo nafikiri hao wananchi wenzetu wa visiwani bado hawajaelewa ni masuala yapi yako chini ya Muungano na yapi yapo chini ya SMZ.

Kwataarifa yako anayengangania muungano si Zanzibar BALI ni watu wa bara na serikali ya bara...hivi unajua kwa nini Salmin Amour alifanyiwa fitna alipotaka kubadili katiba ya
ZNZ?


Zanzibar, some time I am getting little tired to hear anything from yakhe side. Plz save it

Sijakuelewa unamaana gani na hilo neno YAKHE lakini inaonekana umelitumia as a derogatory term. Hivi unajua kama msomi kuliko wote katika serikali ya muungani ni DR SHEIN? je yule naye YAKHE? lete issue mzee kama huna hoja kaa kimya


Li-muungano limekuwa irrelevant na Zanzibar imekuwa nuance. Yengele kama hili ni dalili za mke aliyechoka na yu tayari kwa talaka, kuendelea kumbembeleza ni kujitakia dhahama za bila sababu. Itafutwe a way out of this bs, walioleta muungano wameshajifia na huu muungano mie naona bora uwafuate huko walipo.Hili nalo ni miongoni mwa mengi ya matatizo Marehemu Julius alotuletea na kutuachia wa-Tanganyika!!!. Enuff is enuff, let 'em go.

Lets have some perspective here.Nakumbuka back in 1990's Halmashauri Kuu ya Maaskofu ya Baraza la Kanisa la Pentekoste la Tanzania(PCT), lilitoa kitabu kilichoitaka serikali iitishe kura ya maoni kwanza, kabla ya kuamua kujiunga na J(OIC), ili kupata ridhaa za Watanzania. Kitabu hicho, kama sikosei kilichopewa jina la "Amani katika Tanzania italindwa kwa:kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi", zaidi ya mengi nakumbuka kile kitabu kilieleza kuwa kuwa kitendo cha serikali ya Tanzania kutaka kujiunga na OIC si jambo dogo. Nijambo linalowahusu Watanzania wote, Waislamu na wasiokuwa Waislam, na hata wale wasiokuwa na dini yo yote.

Inshort Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, katika kitabu hicho, walitilia mashaka uhusiano huo kama utaanzishwa na walidai kuwa lengo la misaada inayotolewa na taasisi hiyo ni kwa ajili ya kutaka kueneza imani ya dini hiyo katika nchi wanachama. Maaskofu hao wamesema kuwa kama Tanzaniaitajiunga na taasisi hiyo basi itakuwa ni sawa na kuwasilimisha Watanzania bila ya nidhaa yao! na naona huu ni msimamo wa baadhi ya members wa JAMBO FORUMS katika kulijadili hili.


Sasa basimindhali hili suala limerudi tena hapa basi tutalijadili na asiye na muda basi arejee baadae.Kwa haraka haraka its fair kusema kuwa baadhi ya mitazamo humu JAMBO FORUMS pamoja na ule ya MAASKOFU umekosa uadilifu na inshort ni mtazamo ulioelekezwa katika kuuangalia upande mmoja tu wa shilingi na kuupuuzia upande wa pil waswahili wanaita ni MTYIZAMO CHONGO! kwa maneno mengine ni sawa na mtu mwenye macho mawili lakini akaamua, kwa makusudi, kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho moja.


Kama serikali ya Zanzibar au Tanzania hazifai kujiunga na OIC, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! uhusisano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikan, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo!


Kama mtakumbuka Mzee Aboud Jumbe, katika kitabu chake alichokiita, "The Partner-ship" alisema,kuwa kuwepo kwa ubalozi wa Vatican nchini Tanzania hakukupata kuhojiwa, pamoja na kuwa serikali yetu inadai kuwa si ya kidini. Kanisa, CCM na serikali, vyote vimekaa kimya huku vikijua kutendeka kwa hilo lakini vitazibwa mdomo hichi kitabu ninacho hapa na kama kuna mtu anataka basi asome (Ukurasa.126).

Cha ajabu basi huuu mjadala wa ZANZIBAR kujiunga na OIC kila unapokuja huwa unajadliwa kwa JAZBA na of course maneno ya kejeli toka wa vyombo vya habari ambavyo kusema ukweli vinamilikiwa na wasio WAZANZIBARI na specifically WABARA na more likely ambo si waislam na labda kwa mbali gazeti la RAI LA ZAMANI lilikuwa liko wazi kutoa maoni ya pande zote mbili sasa hebu niambieni hao wazanzibari au waislam wataacha kuona kuwa wako UNDER SIEGE?


Bunge letu nalo kama kawaida yake ni RUBBER STAMP bunge ambalo halitaki kujadili kitu lakini msishangae haka kama hili jambo likienda bungeni kuona wale wabunge waliokuwa wanalala wakati wa MIKATABA YA MADINI wakitumia jazba na ukereketwa wao kukwamisha mswada wa ZANZIBAR kujiunga na OIC, na kama mnabisha rejea mjadla wa Bunge in 1990's kupinga suala la wanafunzi wa kike katika mashule kuvaa sare zinazoendana na maadili ya dini zao!


Of course kila kukicha watu wanaambiwa wasichanganye dini na siasa lakini wanasiasa wako radhi kuwafuturisha watu IKULU na kuhost ma Padre IKULU kila kukicha.Sasa leo hii waislam wanaona wenzao wa ZANZIBAR wanavyokuwa short changed katika suala la ZNZ kujiunga na OIC wataambiwa wao hawaitakii nchi mema! MTAKE MSITAKE 99.99% ya waislam wa Tanzania wanaamini kuwa kuna CONSPIRACY kubwa inayofanywa na wakristo kwa kutumia vitengo vyao vya Kanisa kuwakwamisha kwenye mambo yao na moja wapo ni hili la OIC.



Hivi mshawahi kujiuliza kwa nini waislam wako obsessed n a PADRE SIVALON ambaye ni Padre wa Kikatoliki? Jibu ni kuwa Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA -1953 HADI 1985"ambacho nacho ninacho hapa ameeleza; "Mwishowe, SSY ilitoa msisitizo juu ya jukumu la walei katika jamii. Haya yalitokea wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 1970. "Ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuonyesha uhusiano kati ya SSY na wabunge waliochaguliwa, mmoja kati ya watu waliohojiwa alidaikuwa: SSY na Baraza vimeleta msisimko huu ambao umewaamsha Wakatoliki kupigania viti katika uchaguzi wa Wabunge na mimi nikiwa mmoja wao."Padre huyo anaendelea kusema, "Baadaye huko Bungeni tulifanya utafiti usio rasmi na kugundua kwamba asilimia 75 ya waliochaguliwa walikuwa Wakristo, na kati ya hao asilimia 70 walikuwa Wakatoliki"(Uk.49).

Nadhani mwenye akili hapo ataelewa SIVALON alikuwa anasema nini na waislam kila wanapoulizwa kuhusu mambo ya Zanzibar kujiunga na OIC reference yao huwa ni page 49 ha cho kitabu!



Sasa kwa nini tufikishane mpaka kwenye kuandaa kura ya maoni? Kwa nini tuvutane? Jambo liko wazi na kigezo WAZANZIBARI WANACHO! Ikiwa muasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanzisha uhusiano wa kibalozi baina ya serikali yake na taasisi ya kidini ya kanisa Katoliki duniani, Vatikano, vipi sisi, tunaojifanya tunafuata nyayo za kiongozi huyo, na kudai kuwa tunayaenzi mema yake, tupinge serikali kujiunga na taasisi ya kidini ya OIC? Au ni kwa sababu mtazamo chongo umetulevya mpaka tukaona uhusiano na taasisi ya Kikristo ni sawa lakini uhusiano na taasisi ya Kiilslamu ni dhambi? Kwa nini hatufunui macho yote mawili tukaona sawasawa?

MKEWE BUSH IN QATAR
aaaaa.JPEG



Aidha, misaada inayotolewa na OIC si ya kidini na wala haina lengo la kuwaingiza watu katika uislamu. Kama taasisi ya kidini inapotoa misaada huwa lengo lake ni kuwavuta watu waingie katika dini hiyo basi na misaada inayotolewa na Vatikano, kwa kupitia kanisa Katoliki nayo itakuwa inalenga kuwaingiza Watanzania katika Ukristo. Kanisa Katoliki limejenga shule, zahanati na hospitali na zinatumiwa na Watanzania wote bila ya kujali tofauti zao za kidini, jee kanisa hilo nalo nia yake ni kuwabatiza wanaopata huduma hizo?


OIC inatoa misaada ya kijamii tu. Inajenga mashule, mahospitali, barabara, madaraja na mfano wa hayo, kwa ajili ya faida ya jamii nzima na siyokuwa Waislamu tu. Misaada hiyo haitolewi kwa vikudni binafsi, inatolewa kwa nchi nzima, ndiyo maana taasisi hiyo ikataka nchi inayotaka ifaidike na misaada hiyo ijiunge na taasisi hiyo.

Uganda na Mozambique si nchi za Kiislamu, na wala hazina Waislamu wengi; lakini serikali za nchi hizo zimejiunga na OIC na zinafaidika na misaada inayotolewa na taasisi hiyo, bila ya kulazimishwa nchi hizo kufuata imani ya Kiislamu. Chuki za kuuchukia Uislamu zisiwe ndiyo sababu ya kutowatendea uadilifu Waislamu.


Sasa tusitake kulikimbia hili jini..mindhali WATAWALA wetu walishakuwa cozy na viongozi wa kidini na wadini basi tena hawana namna ila kuwakubalia tuu wazanzibari na matakwa yao
 
GM

Hivi unapata wapi muda wa kufanya hayo ma cross reference kama hayo? ama kweli Jf kuna mambo...
 
GM

Hivi unapata wapi muda wa kufanya hayo ma cross reference kama hayo? ama kweli Jf kuna mambo...

Sie tumeambiwa kuwa watu wanataka perspective wakati tunajadili mambo humu...sasa lets look at both sides of the coin kabla ya kuanza kuongea au sivyo?

sasa nawasubiri waje tujadiliane based on hoja nilizozitoa
 
GAMETHEORY, Masatu na wadau wengine- huu mjadala sasa unanoga!

1. Kwani Zanzibar kwa sasa iko ktk Jumuia z(ipi) za Kimataifa yenyewe kwa sasa? Na kumbuka waliomba kujiunga na FIFA wakatataliwa kwa kigezo kuwa hawatambuliki kama Visiwani ila ni sehemu ya Jamhuri! Ila bado wako CECAFA na CAF!

2. Ni kitu gani kinafanya URT kutojiunga na OIC hadi leo? Kama URT wangejiunga haya maneno sii yataisha- kama ni misaada itagawanywa tu kwa kutumia fomula ya URT ya sasa ya 5%!

3. Rufiji ameongea vizuri hapo juu- Tanzania au nchi nyingine ya Afrika hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada tu! Kama kigezo Zanzibar kujiunga na IOC ni kupata misaada- mbona tangu 1964 Visiwani wamepata misaada kibao- je leo imewaindoa ktk umaskini?
 



Kama serikali ya Zanzibar au Tanzania hazifai kujiunga na OIC, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! uhusisano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikan, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo!


Hapana Game Theory, mfano uliotoa hauendani na mjadala huu. Tungekuwa tunajadili kuanzishwa kwa ubalozi wa jumuiya ya kiislamu, hapo mfano wako ungekuwa sawa. Tanzania ina mahusiano mazuri tu na jumuiya za namna hii, hata miezi michache H.H. Prince Aga Khan alipata mapokezi makubwa sana Tanzania. Hatuwezi kuvunja ubalozi na nchi ati kwa sababu tu ya dini yake, maana ukisema hivyo itabidi pia tuvunje ubalozi na nchi zote za kiislamu, na zile nyingine zitakajizotangaza kuwa ni za kidini, sasa sijui hiyo itakuwa diplomasia ya aina gani. Ushirikiano wa kibalozi ni tofauti sana na kujiunga na jumuiya za nchi zenye malengo fulani. Sisi tuna uhusiano wa kibalozi na Misri, Iran nk, lakini Tanzania si mwanachama wa Arab League ambayo nchi hizo ni wanachama. Tanzania pia ina uhusiano wa kibalozi na Marekani, Uingereza nk, lakini bado Tanzania si mwanachama wa NATO. Tutofautishe mambo haya.Kinachojadiliwa hapa ni suala la nchi ambayo kikatiba si ya kidini kujiunga na umoja wa kidola ambao charter na objectives zake ni za kidini, na zimewekwa wazi. Tutawezaje kuyatekeleza makubaliano na misimamo inayofikiwa katika jumuiya hiyo bila kuwaathiri wasio waislamu? Kama ni suala la "misaada" kama wengine wanavyodai, hiyo jumuiya inaona taabu gani kuwasaidia waislamu wenzao wa Tanzania bila nchi yetu kuwa mwanachama? Hiyo inatupa mashaka wengine na kutusababisha tuhisi kuna kitu kinafichwa hapa. Kumsaidia mwislamu mwenzako kupata maendeleo, si lazima nchi yake ijiunge na jumuiya yako, waweza kuzisaidia taasisi zake zikapata nguvu zaidi ya kufanya maendeleo.
 
Hapana Game Theory, mfano uliotoa hauendani na mjadala huu. Tungekuwa tunajadili kuanzishwa kwa ubalozi wa jumuiya ya kiislamu, hapo mfano wako ungekuwa sawa. Tanzania ina mahusiano mazuri tu na jumuiya za namna hii, hata miezi michache H.H. Prince Aga Khan alipata mapokezi makubwa sana Tanzania. Hatuwezi kuvunja ubalozi na nchi ati kwa sababu tu ya dini yake, maana ukisema hivyo itabidi pia tuvunje ubalozi na nchi zote za kiislamu, na zile nyingine zitakajizotangaza kuwa ni za kidini, sasa sijui hiyo itakuwa diplomasia ya aina gani. Ushirikiano wa kibalozi ni tofauti sana na kujiunga na jumuiya za nchi zenye malengo fulani. Sisi tuna uhusiano wa kibalozi na Misri, Iran nk, lakini Tanzania si mwanachama wa Arab League ambayo nchi hizo ni wanachama. Tanzania pia ina uhusiano wa kibalozi na Marekani, Uingereza nk, lakini bado Tanzania si mwanachama wa NATO. Tutofautishe mambo haya.Kinachojadiliwa hapa ni suala la nchi ambayo kikatiba si ya kidini kujiunga na umoja wa kidola ambao charter na objectives zake ni za kidini, na zimewekwa wazi. Tutawezaje kuyatekeleza makubaliano na misimamo inayofikiwa katika jumuiya hiyo bila kuwaathiri wasio waislamu? Kama ni suala la "misaada" kama wengine wanavyodai, hiyo jumuiya inaona taabu gani kuwasaidia waislamu wenzao wa Tanzania bila nchi yetu kuwa mwanachama? Hiyo inatupa mashaka wengine na kutusababisha tuhisi kuna kitu kinafichwa hapa. Kumsaidia mwislamu mwenzako kupata maendeleo, si lazima nchi yake ijiunge na jumuiya yako, waweza kuzisaidia taasisi zake zikapata nguvu zaidi ya kufanya maendeleo.

SASA HEBU SOMA HIZI CORRESPONDENCE MBILI BTN WAISLAM NA BEN MKAPA IN 1999



HALMASHAURI KUU YA WAISLAMU.
c/o Islamic Club, P.O Box 11392. Tel.: 185258/0511 613422, Dar es Salaam.

26/08/1999.

Mhe. Benjamin William Mkapa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu, Dar es Salaam


YAH: MASHAURIANO KUHUSU MADAI YA WAISLAMU.



Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa tunaomba uhusike na kichwa cha maneno; na urejee mazungumzo yetu ya awali pamoja nawe yaliyofanyika nyumbani kwako, hapo Ikulu, jioni ya jumatano, tarehe 7 july 1999.

Awali ya yote halmashauri inatoa shukurani za dhati kwako kwa kitualika kukutana nawe siku hiyo na kutukirimu. Mkutano huo ulitupa matumaini makubwa juu ya uwezekano wa kipatikana na ufumbuzi wa kudumu wa madai ya waislamu ambayo tuliyawasilisha rasmi kwako mwazoni mwa mwaka huu, wakati wa baraza la Eid el Fitri. Madai hayo kwa ufupi yanahusu:

* Ubaguzi uliojitokeza dhidi ya waislamu katika baadhi ya vyombo vya dola ambao unafanywa na naadhi ya watendenaji walio katika serikali. Mfano wa hili umejitokeza katika:
o Kuwepo kwa idadi ndogo ya waislamu katika vyuo na maofisi ya serikali ukilinganisha na iwiano halisi ulivyo katika jamii yetu ya watanzania; na
o Kuwepo kwa idadi kubwa ya waislamu "wazururaji" na "wahalifu"katika magereza;
* Suala la Mwembechai kupatiwa utatuzi;
* Suala la Mahkama za Makadhi na
* Suala la nchi yetu kujiunga na "organization of Islamic conference" (OIC) na kiboresha uhusiano wake na nchi za Kiislamu.

Tulipokutana siku hiyo, kama tulikuelewa vjema, ulitueleza kwamba:

* Serikali inatambua kuwepo "imbalances" dhidi ya waislamu katika jamii yetu ya Watanzania;
* Sio lengo wala njama za serikali au hata sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa na hizo "imbalances"
* "Imbalances" hizo zipo tu kwa sababu ya kihistoria na ubinafsi ya baadhi ya watu katika CCM na Serikali; na
* Serikali bado inajukumu na wajibu wa kuondoa hizo "imbalances" kama inavofanya na maeneo mengine.

Kauli hii ilitupa faraja na imani kwamba viongozi wa CCM na Serikali sio tu hawapaswi kufuata sera hiyo potofu za kibaguzi dhidu ya Waislamu, bali pia wako pamoja nao katika kutetea usawa. Tunashukuru pia kwamba siku hiyo ulitudokezea kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa kasoro hizo. Miongoni mwa hatua ulizozitaja ni:

* Maelekezo uliyokwisha kuyatoa juu ya kutatuliwa kwa matatizo ya Waislamu yanayohusu "hijabu" na kuwepo kwa mabaa (bars), nyumba za wageni (gest houses), ufugaji ovyo na uchuuzi wa nguruwe na mabucha yake.
* Ofisi yako ina "update human resources bank" yake, ikiwa ni pamoja na kutafuta waislamu wenye taaluma za kushika nyadhifa mbali mbali; na
* Katika masuala ya utoaji wa vyeo, serikali imeanza suala la kuzingatia uwiano baina ya waumini wa dini tafauti.

Pamoja na maelezo hayo ulitoa tahadhari kwamba:

* Utatuzi kamili wa matatuzi ya Waislamu utachukuwa muda;
* Masuala ya OIC na Mahkama za Makadhi bado yanahitaji utafiti, matayarisho na kuelimishana; kwa vile baadhi ya watu bado wanadhana au khofu kuwa kukubali masuala haya ni sawa na kukubali kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Kiislamu; na
* Kuwapa Waislamu nafasi zote wanazostahiki kunataka busara na hekima kubwa kwa vile inabidi kwanza baadhi ya nafasi hizo wanyimwe au wanyanganywe watu wengine.

Mwisho ulishauri kuwa:

* Badala ya Waislamu kudai kwenye majukwaa, ni vyema madai hayo kuletwa kwako moja kwa moja kwa vile uko tayari kuyapokea na kuyashughulikia.

Mhe Rais, Halmashauri ilikubaliana nawe kwa hayo yote; na uliongeza kwa kusema kwamba:

* Siyo muhimu sana kwa Waislamu hivi sasa kujua nani amesababisha hizo "imbalances", bali muhimu zaidi ni serikali kutambua kwamba "imbalances" hizo zipo na inapaswa kuziondoa.
* Suala la ku "update human resource bank" ya serikali ni suala muhimu sana kwani inawezekana Waislamu kukosa baadhi ya nafasi kwa sababu ya Serikali kutojua kama kati yao wamo wenye taaluma za kushika nafasi hizo.
* Waislamu hawataraji miujiza ya kutatuliwa matatizo yao yote kwa usiku mmoja; bali wanahitaji kuona kuwa hatuwa thabiti zinachukuliwa za kutatua matatiza hayo ikiwa ni pamoja na:
o Kuundwa kwa tume huru za kuchunguza suala la Mwembechai;
o Kuanzishwa kwa mpango, hata kama ni wa muda mrefu, na ratiba ya kuondoa hizo "imbalances" na
o Kukemewa na kukomeshwa kwa propaganda potofu dhidi yao.

Halmashauri, Mhe Rais, ilikudokezea kwamba takriban imeshamaliza kufanya utafiti wake; na, pamoja na mambo mengine, matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kwamba:

* Imbalances zipo kwa vile hakuna "mechanism" ya kuzuia kuwepo kwake; na zipo kwa sababu takwimu zote takriban zinaonesha hivyo.
* Ilikuwa ni kinyume na Katiba kuondoa Mahkama za Makadhi kwa vile Katiba ya Tanzania inadhamini uhuru wa kuabudu na Waislamu kuwa na Mahakama hizo ni sehemu ya ibada.

Kwa kumalizia, Halmashauri yetu ilikuhakikishia kwamba:

* Haifanyi haya yote kwa sababu ya choyo, uroho au maslahi ya ubinafsi ya Waislamu peke yao; ila inafanya hayo kwa maslahi ya Taifa zima na kwa nia safi ya uzalendo na kutaka kuimarisha demokrasi na uadilifu.

Hapa tunapenda kutoa taarifa, Mhe Rais, kwamba siku chache kabla ya kikao hicho pamoja nawe,
na baada ya kuona muda mrefu umepita tangu Halmashauri yetu kukupatia Madai ya Waislamu, tulikuwa tumejiandaa kulieleza Baraza la Maulid siku ya tarehe 10 julai 1999 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kuwa Serikali inachelewa kushughulikia Madai hayo. Lakini, kutokana na mazungumzo hayo ya tarehe 7 julai 1999, Halmashauri kwa furaha ilibidi ibadilishe risala yake na kutoa tamko rasmi kwamba madai hayo sasa yameanza kushughulikiwa na Serikali ipasavyo.

Mhe Rais, pamoja na mkutano wetu huo nawe hapo Ikulu, kumetokea mambo mengine kadhaa ambayo tunapaswa kuyazingatia kwa vile yana uhusiano mkubwa na masuala yetu.

* Mosi, kumekuwa na tamko la CCT la kutaka Serikali iache mara moja fikra ya Tanzania kujiunga na OIC kwa hoja kwamba OIC ni jumuiya ya Kiislamu na nchi hii ina Waislamu na Wakiristo


o Tamko hilo ambalo tunatarajia kuwa limetolewa kwa nia nzuri linathibitisha kauli yako kwamba baadhi ya wananchi wana dhana kuwa Tanzania ikijiunga na OIC itakuwa nchi ya Kiislamu. Ndio maana Halmashauri inakubadiliana nawe kuhusu kuelimishana ili kuondoa dhana hii. Ni muhimu wenzetu wajue kuwa nchi zisizo za Kiislamu ambazo zimejiunga na OIC kama vile Uganda na Mozambique, zinaendelea kuwa si za Kiislamu. Tangu kujiunga na OIC bado hatujasikia hizo nchi kutakiwa au kushauriwa kuwa za Kiislamu. Badala yake nchi hizo zinashiriki kikamilifu kakika shughuli za OIC kwa sababu ya maslahi yake. Aidha, kwa maoni yetu, nchi kuwa yenye Waislamu na Wakiristo ndio sababu nzuri zaidi ya nchi hiyo kujiunga, na sio kutojiunga na jumuiya hizo za kimataifa ama za Kiislamu au za Kikristo. Hivi sasa kwa mfano nchi yetu tayari ni mwanachama wa jumuiya ya madola (ya Commonwealth) ambayo kiongozi wake lazima awe Mkristo na mkuu wa Kanisa la Kianglikana; na hii haifanyi Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria n.k kuwa nchi za Kianglikana.

o Bali hata ingalikuwa Tanzania haijajiunga na jumuiya kama hizo, isingekuwa vibaya kuanza kwa kujiunga na OIC. Kwani Watanzania tunajiamini na tunajulikana kwa utamaduni wetu mkubwa na mzuri wa kuvumiliana katika masuala ya itikadi. Mfano nzuri ni kwamba katika Tanzania Waislamu na Wakristo wanapumzika Jumamosi na Jumapili, na sio Ijumaa na wanasherehekea mwaka mpya wa Kikristo, na sio wa Kiislamu. Aidha Vatican inayo mwakilishi wake hapo nchini ambae amepewa hadhi na anatambuliwa na kuheshimika kama Balozi. Ikiwa haya na mengi mengine ya aina hii yanafanyika hapa Tanzania kwa usalama na amani, ni dhahiri kwamba hakutakuwa na tatizo nchi yetu ikiboresha uhusiano wake na nchi za Kiislamu au ikijiunga na OIC.

o Zaidi ni kwamba tunataka Tanzania iboreshe uhusiano wake na nchi za Kiislamu kama invyoboresha uhusiano wake na nchi za Kikristo, na ijiunge na jumuiya za kimataifa za kidini sio tu kwa maslahi ya kiroho, bali pia kwa maendeleo ya kidunia. Ikijiunga na OIC, nchi yetu itastahiki misaada na mikopo kama ile ya Islamic Development Bank (IDB) ambayo ni nafuu zaidi kuliko mingi tuipatayo kutoka jumuiya au nchi nyingine. Aidha, kwa kufanya hivyo nchi yetu itakuwa imejipatia jukwaa jengine ambalo ni muhimu kwa harakati zake za kidiplomasia.

* Pili, kulitokea upinzani mkubwa katika Bunge, wakiwemo baadhi ya Mawaziri, dhidi ya Waziri wa Elimu na Utamaduni, Mhe. Juma Kapuya, kwa sababu ya kutangaza baadhi ya yale mambo ambayo wewe umeagiza yatekelezwe. Katika maelezo yake Mhe. Kapuya alizungumzia:


o Haki ya wanafunzi wa itikadi mbali mbali ya kuabudu nyakati za sala, na kuvaa mavazi yanyokubalika katika maadili yao.
o Wajibu wa wanafunzi wa kuendesha miradi yao ya uchumi kwa kuzingatia tafauti za udini zilizopo bila ya kuleta bughudha kwa kundi au dhehebu lolote.
o Jukumu la Wizara la kuhakikisha kwamba suala la udini halijitokezi wakati wa kujaza fomu za maandalizi ya kujiunga na Kidato cha 1, cha V pamoja na kujiunga na mafunzo ya ualimu.

Maneno haya, ambayo yangelisaidia sana kuonesha kwamba serikali haiko dhidi ya dini, Waziri Kapuya alilazimishwa sio tu kuyafuta, bali pia kuomba radhi kwa kuyatamka. "Kama anahitaji kubaki waziri", Mbunge mmoja alimwambia, "basi aondoe suala la udini kwenye bajeti". Jambo ambalo, pamoja na kufanya Serikali ionekane kuwa dhidi ya dini, limesababisha Waislamu kuandamana na baadhi yao kupigwa na kutiwa ndani.

Tunashukuru kuwa kwa upeo wako mpana, ulibainisha hivi karibuni kwamba:

o Wapo wanasiasa au viongozi wengine wa jamii wanaozungumza wazi wazi lugha ya udini, ukabila na majimbo. Tusiwapuuze na wala tusiwaonee haya.

Tunakubali kauli yako hiyo kwa ukweli wake; kwani hata katika tukio hili baadhi ya viongozi wa aina hiyo wamejitokeza. Akiashiria Mhe. Kapuya, Mbunge mmoja alifika kusema kwamba: "Al-Haji hafai kuwa Waziri". Ila, kinyume na maagizo yako, viongozi hawa sio tu hadi sasa wamepuuzwa, bali pia walishangiliwa na wabunge wenzao Wakristo wa chama tawala na vile vya Upinzani. Wabunge Waislamu wa chama tawala walioomba kuchangia katika mada hii wakati huo walinyimwa nafasi na Mhe. Spika. Mawaziri waliokuwepo pia walihiari kukiuka maadili ya "collective responsibility" kuliko kumuunga mkono waziri mwezao. Kauli za aina hii hazikusikika kabisa wakati Mhe. Rev Simon Chiwanga alipokuwa Waziri wa wizara hiyo!

* Tatu, kumetokea teuzi mbali mbali za viongozi wa Chama, Serikali na Mashirika ya Umma. Wahusika wa teuzi hizo hawakuonekana kuzingatia suala la uwiano baina ya waumini wa itikadi tofauti; jambo ambalo linaonesha sio tu kupuuza Madai ya Waislamu, bali pia kutokujali maelekezo yako. Katika chaguzi ndogo zilizofanyika Temeke na Ubungo hivi karibuni, kwa mfano, CCM iliteuwa wagombea wote wawili kutoka dini moja. Aidha katika bodi la ya Wakurugenzi wa shirika la PPF walioteuliwa hivi karibuni wote ni kutoka dini moja; na wale watatu ambao walikuwemo kabla wa dini nyingine wametolewa kwa mpigo. Mifano ya aina hii ni mingi na hapa hatuwezi wala hatuhitaji kuitaja yote. Ila ni muhimu kutanabahi kwamba Waislamu wanaangalia kwa makini sana teuzi zote zinazofanywa hivi sasa katika CCM, Serikali na Mashirika ya Umma.

* Nne, kumekuwa na Mkutano Mkuu wa Bakwata ambao umefanyika Dodoma mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 29/07/1999. Ukihutubia katika ufunguzi wa mkutano huo kama mgeni rasmi ulisema kuwa:

Uko tayari, na kwa kweli, umeshaanza kuyashughulikia matatizo ya kitaifa yanayohusu Waislamu.

Halmashauri inakupongeza kwa ujasiri huo wa kuweza kuwatangazia wananchi kwa jumla yale ambayo ulitueleza sisi kabla. Kauli hii sasa imeweka wazi kuwa, pamoja na kutambua kuwepo kwa "imbalances" kadhaa dhidi ya Waislamu, umekubali kubeba jukumu la kuziondoa. Ila kutokana na hutuba hiyo, masuala mengine yamejitokeza ambayo tunahitaji, na kwa hiyo, tunaomba ufafanuzi wake:

o Kwanza, kuna suala la "machanism" ambayo itatumika kusawazisha hizi "imbalances". Ukizungumzia suala hili ulisema:

+ Serikali haitasuta kumchukulia hatua kali mtu yeyote atakae bainika akimbagua mwengine katika masuala ya elimu, ajira, upandishaji vyeo na utoaji wa leseni au hati mbali mbali kwa misingi ya jinsia, dini, kabila au eneo anakotoka mtu.
+ Serikali haiwezi kuweka kanuni ya kudumu ya kugawa vyeo kwa misingi hiyo ya udini, ukabila na jnsia.
+ Kwa faida ya taifa ni vizuri tugawe vyeo kwa vigezo vya ujuzi, uwezo na upimaji makini wa matokeo ya kazi.

Kuhusiana na suala hili sisi tuna maoni tafauti na, kwa hiyo, ni vyema kukutana na kubadilishana mawazo. Sisi tunaona kwamba:

o Haitakuwa rahisi kuwachukulia hatuwa wabaguzi bila ya kuwa na vituo vya kutosha vyenye taratibu madhubuti na uwezo wa kupokea na kufuatililia madai ya wanaobugudhiwa.
o Itakuwa vigumu kukomesha ubaguzi na kuhukumu wabaguzi kama hakutakuwa na sheria maalumu, hata kama ni ya muda ya kufanya hivyo.
o Katika kuomba au kutoa nafasi za elimu au ajira, utaratibu wa kutumia nambari badala ya majina ni vyema utumike; kwani usipo saidia kuinua wanyonge, utasaidia kuondoa zana ya upendeleo.
o "Affirmative action" au "positive discrimation" tayari inatumika hapa nchini na inasaidia kuinua wanyonge wa jinsia; kwa hiyo ni bora pia ijaribiwe katika kuinua wanyonge wa dini, kabila na maeneo, n.k.

Hii sio kwamba tunapendekeza kuwa wanyonge hao wapewe nafasi hata kama hawafai. Halmashauri inakubaliana nawe moja kwa moja kwamba ugawaji wa vyeo ni lazima uzingatie ujuzi na uwezo. Ila tunaomba kuwa kuna haja vile vile ya njia ya kuhakikisha kwamba wanyonge wenye uwezo na ujuzi hawakoseshwi vyeo kwa misingi ya dini au kabila; na wale wanaopewa vyeo miongoni mwao hawasumbuliwi kwa maneno; kama vile: "Al-Haji (au Reverend, hata kama ni Profesa) hafai kuwa Waziri". Kukiwa na njia hiyo, wanyonge hawatapendelewa ila kutakuwa na uhakika wa wao kupata haki yao, bila ya kudhulumu au kudhulumiwa.

Kwa maneno mengine, sisi tunaona kuwa si vyema uwezo na ujuzi kuwa ndio vigenzo pekee vya kuzingatiwa katika kugawa vyeo. Kuna haja pia ya kuwa na "mechanism" ya kuzuia watu wa dini, kabila au jinsia moja kuchukua vyeo vyote au (vingi mno) mpaka wenzao wa dini, kabila au jinsia nyengine wakakosa kabisa (au wakapata vichache sana) hali nao wanafaa. Kwa hiyo, badala ya kuchagua baina ya vigezo vya kabila, jinsia na dini kwa upande mmoja, na vigezo vya ujuzi, uwezo au uzalishaji kwa upande mwengine, ni muhimu vigezo vyote hivi vitumike kw wakati mmoja.

* Kisha, kuna suala la matokeo ya utafiti ambao sote tumefanya. Hotuba yako imetupa hisia kwamba sasa Serikali imemaliza kufanya utafiti wake juu ya Madai ya Waislamu; na ndio maana iko tayari kuyashughulikia. Ila pia hotuba hiyo imetupa wasiwasi kuwa labda "conclusion" ya utafiti huo ni tofauti ba ile ya utafiti wa Halmashauri. Wasiwasi huu umekuja baada ya kusikia kauli yako kwamba:


o Hakuna mchujo wowote katika kuandikisha watoto shule, kwenda sekondari, au vyuo vikuu, au katika ajira, unaofanywa kwa msingi wa kuwabagua watu wa dini fulani. Hiyo nawahakikishia kabisa.
o Na kama yupo mwenye ushahidi kwamba mwanafunzi fulani amezuiliwa kuendelea na elimu kwa sababu tu ya dini yake, jinsia yake au kabila lake basi wanaohusika wajulishwe.

Kama hii ndio "conclusion" ambayo Serikali imefikia baada ya utafiti wake, basi bila shaka inatofautiana na ile ya Halmashauri. Kwa hivyo, kuna haja ya kukutana ili kubadilishana "notes" na kufanya uchambuzi wa pamoja. Kinyume na uoni huo, sisi tunanona kuwa mchujo upo; ila labda mchujo wenyewe si rasmi, au haufanywi kwa makusudi. Ni maoni yetu pia kwamba, ili tuweze kuondoa mchujo huo, ni muhimu tukubaliane kwanza kwamba upo. Sisi tunaamini kuwepo kwake kutokana na hoja kadhaa. Baadhi ya hoja hizo ni kwamba:

o Ukosefu wa ushahidi wa kwepo kwa mchujo, si uthibitisho wa kutokuwepo kwa mchujo huo; kwani ushahidi unaweza kukosekana hata kama mchujo ukiwepo madhali unafanywa kwa siri au uangalifu wa kutosha.
o Ushahidi wa kesi za mchujo si rahisi kupatikana kwa kuwataka wanaobaguliwa waripoti kesi zao kwa wahusika au hata kwa Rais mwenyewe. Kwani mara nyingi hao wahusika huwa hawajulikani au wenyewe ndio wabaguzi. Aidha si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuwa na uwezo na ujasiri wa kufika Ikulu.
o Athari ya mchujo ipo, inaonekana, nayo ni hizi "imbalances" ambazo tunakubaliana kwamba zipo.
o Itakuwa ni kitu cha ajabu sama mchujo kutokuwepo; kwani kwa kawaida, binadaamu haachi kuchuja (kujipendelea yeye mwenyewe na kupendelea walio wake) kama hakuna cha kumzuia.
o Takwimu zetu zinaonyesha kwamba watoaji wa nafasi za masomo au ajira wengi, kama si wote, ni waumini wa dini moja; na wanaopewa nafasi hizo wengi, kama si wote, pia ni waumini wa dini hiyo; ila wakosaji sasa, kama si wote, wengi wao ndio waumini wa dini vyingine.

* Halafu kuna suala la kujenga badala ya kubomoa madaraja ya kijamii. Ni vyema umelitaja suala hili katika hotuba yako; na umesema kuwa:


o Mojawapo ya visingizio vinavyotumiwa na wanaotaka kuvunja madaraja ya umoja na utaifa wetu ni kwamba watu wa eneo fulani wameachwa nyuma, au watu wa dini fulanai hawapewi nafsi fulani katika uongozi wa nchi na jamii.

Ikizingatia suala hili, Halmashauri imeona ni muhimu vile vile kuwa hadhari sana watu ambao nao wanaweza kuvunja madaraja ya kijamii kwa kusingizia kwamba hakuna ubaguzi, hali upo; au hakuna watu wa dini, kabila, jinsia au eneo ambao wameachwa nyuma kimaendeleo au wamenyimwa au nyadhifa, wakati wapo.

Mheshimiwa Rais, huu ni muhtasari wa baadhi ya yale tulionayo moyoni ambayo tunapenda kushauriana nawe. Baada ya kukubaliana kuhusu kuwepo kwa "imbalances" dhidi ya Waislamu; ni muhimu sasa tukutane kujadili "mechanism" ya kusawazisha hizo "imbalances". Hapa tunajaribu kubainisha baadhi ya tofauti zilizopo baina yetu katika suala hili kwa kueleza rai yako na kutoa maoni yetu, ambayo kwa ufupi ni:

  • Kuwa na utaratibu wa nambari badala ya majina katika kuomba na kutoa nafasi za elimu;
  • Kutumia mpango wa "positive discrimination" au "affirmative action" katika kutoa nyadhifa na ajira;
  • Tanzania kuboresha uhusiano wake na nchi muhimu za Kiislamu kwa kufungua balozi zake katika nchi hizo na kujiunga na OIC;
  • Mahkama za Makadhi kurudishwa;
  • Serikali kukemea propaganda potofu na kukomesha ubaguzi dhidi ya Waislamu kwa:
o Kuanzisha tume ua kuchunguza kesi muhimu za aina hiyo, hususan Kesi ya Mwembechai;
o Kuanzisha vituo maalum na vya kutosha vya kupokea na kufuatilia kesi za ubaguzi.

Kwa hivyo, tunaomba kukutana nawe mapema, ikiwezekana, kuzungumzia kwa kina suala hili la "mechanism". Kwani, kama maradhi, matatizo huzidi kila yanapochelewa kutatuliwa na hayaondoki kwa kuondoa tu dalili (symptoms) zake. Kama tulivyokubaliana kuhusu kuwepo kwa "imbalances" dhidi ya Waislamu, tuna imani kwamba tutakubaliana pia juu ya "mechanism" ya kuzisawazisha. Aidha tunaomba kukutana nawe ili kupata ufafanuzi juu ya hi hali iliyojitokeza ya baadhi ya watendaji wa CCM na Serikali kufanya mambo kinyume na maelekezo yako. Hali hii imeonekana zaidi katika utekelezaji wa maelekezo yako kuhusu:

  • Kutatua matatizo ya Waislamu yanayohusu "hijabu", sala wakti wa ibada na kuwepo kwa mabaa (bars), nyumba za wageni (guest houses), ufugaji ovyo na uchuuzi wa nguruwe na mabucha yake.
  • Kuzingatia suala la uwiano baina ya watu wa itikadi tofauti katika uteuzi wa viongozi mbalimbali.
  • Kutozungumza lugha ya udini, ukabila na majimbo.
Tukiamini kwamba utatukubalia ombi letu, tunatanguliza shukrani.


Ahsante.

Al-Miskry, Saleh

Secretary.


MKAPA JINSI ALIVYOWAJIBU WAISLAM:


The President of the United Republic ofTanzania
The State House
Dar es Salaam

17 Desember, 1999


Ndugu Saleh Al-Miskry,
Halmashauri Kuu ya Waislamu,
C/o Islamic Club,
S.L.P. 11392,
DAR ES SALAAM.


Ndugu Al-Miskry,

NINAKIRI kupokea, kwa shukrani, barua yako ya tarehe 26 Agosti, 1999, pamoja na viambatanisho vyake. Imenichukua muda mrefu kukujibu kwa sababu mambo uliyoandika ni mazito, ya kitaifa na inabidi niyatafakari kwa kina, niyafanyie utafiti zaidi, na nishauriane na wenzangu serikalini kabla ya kuyajibu.

Leo ninakuandikia si kwa lengo la kujibu hoja moja baada ya nyingine, au kutoa jibu kwa kila swali. Katiba ya Jamhuri yetu inanipa mimi, kama Rais, wasaidizi wengi. Ninaye Makamu wa Rais, na ninaye Waziri Mkuu. Ninaye waziri wa kila sekta, na ninao wakuu wa mikoa na wilaya kwa kila eneo la nchi yetu. Nitakuwa siwatendei haki nikijibu maswali yanayowahusu wao. Ningeshauri, kama mlivyojenga mahusiano mazuri nami, mjenge pia mahusiano mazuri na mawaziri, wakuu wa mikoa, na kadhalika, ili kila jambo lisingoje mpaka lifikishwe kwa Rais.

Nina uhakika, kwa mfano, kwamba Waziri wa Elimu ana uwezo na madaraka ya kutosha kushughulikia masuala ya elimu, ambayo kwangu ni muhimu sana. Akikwama atayaleta kwangu. Hiyo itasaidia kufanya mawasiliano nami yawe yale yanayohusu mambo ya msingi, badala ya kujadili matukio. Misingi hiyo itasaidia kuwaongoza watendaji wa serikali, na kuniwezesha mimi na nyinyi kuwa na vigezo vya kupima tunafanikiwa kiasi gani katika kuhakikisha kila mwananchi anapata haki zake za msingi bila ubaguzi wowote kwa sababu za dini, dhehebu, kabila, jinsia, eneo analotoka, na kadhalika.

Msingi wa kwanza ni utawala wa sheria. Nchi yetu lazima iendelee kutawaliwa kwa msingi wa sheria zilizowekwa kwa njia za demokrasia. Hivyo napata taabu kidogo raia wa nchi hii anapofikiri matatizo aliyo nayo yanaweza kutatuliwa nje ya mfumo wa utawala wa sheria. Kila mwenye kero akichukua msimamo huo, nchi hii itakuwa haitawaliki tena, itakuwa vurugu tupu. Kazi ya msingi ya serikali yoyote ni kuhakikisha unakuwepo utawala wa sheria, ulinzi na usalama wa raia wote, wa aina na imani zote. Uhalali wa raia kudai haki nje ya mfumo wa utawala wa sheria unaweza ukakubalika penye utawala wa kikoloni, utawala wa ubaguzi wa rangi, au utawala wa kidikteta. Uhalali huo haupo hata kidogo katika nchi huru, inayoongozwa kwa misingi ya demokrasia kama ilivyo Tanzania.

Kwa sababu hiyo nimefadhaishwa sana na kauli za kuashiria shari za wale wanaojiita "Shura ya Maimamu Dar es Salaam". Pamoja na mambo mengine ya uchochezi wanasema, "Waislamu hatuna moyo tena na serikali ya nchi hii na vyombo vyake vyote likiwemo Bunge na Mahakama". Ninajua huu sio msimamo wa Waislamu walio wengi, lakini matamko yasiyokuwa na kiasi kama haya yasipokanushwa, na wanaoyatoa wanapopewa fursa na majukwaa ya kuyasema, hiyo inawapa silaha wale wachache wanaojaribu kupaka matope heshima na picha nzuri ya Waislamu. Mimi na ninyi tuna kazi ya kuwasahihisha wenye hulka ya aina hiyo, lakini matamko kama haya yatafanya kazi hiyo iwe ngumu zaidi.

Utawala wa sheria chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri. Katiba yetu imepiga marufuku ubaguzi wowote, kwa msingi wowote, ikiwemo dini, kabila, rangi, eneo analotoka mtu, na kadhalika. Katiba hiyo pia imetoa uhuru kamili, ndani ya uwigo wa sheria, wa imani za dini kustawi katika uhuru wa ibada. Isipokuwa kwa wale ambao hawana imani na vyombo vyote vya dola, mimi nina imani kuwa mahakama zetu zina uwezo na uhuru kamili wa kumpa haki hizi za msingi yule ambaye atakuwa amenyimwa kwa ubaguzi.

Narudia. Haki za msingi za kila raia zimo ndani ya sheria Mama - Katiba - ya Jamhuri yetu. Kama kweli upo ushahidi kwamba baadhi ya taasisi za umma, au viongozi wa umma, wamebuni mfumo wao wa kuhakikisha Waislamu wananyimwa haki zao, hao wala si wa kuchukuliwa hatua za nidhamu tu, bali ni wa kushitakiwa mahakamani. Wasionewe haya. Tusaidianeni washitakiwe!

Siwezi kushangaaa iwapo kuna mtu au kiongozi mahali ambaye ndani ya moyo wake ana chuki dhidi ya Wakristo au dhidi ya Waislamu, au ana chuki dhidi ya wanaume au wanawake, au ana chuki dhidi ya Wazaramo au Wahaya, au chuki dhidi ya watu warefu au wafupi. Ninachosema ni kuwa katika utafiti niliofanya hakuna mahali popote katika serikali hii ambapo upo mfumo rasmi wa kubagua au kumnyima haki za msingi mtu yeyote kwa msingi wowote.

Kweli, zipo tofauti kati ya idadi ya Waislamu na wasio Waislamu katika shule, vyuo, sehemu mbalimbali za kazi lakini huo si ushahidi wa mfumo wa ubaguzi. Sababu zake sote tunazijua - ni za kihistoria na za kijamii, kama ilivyo kwa tofauti kati ya idadi za watu wa kabila mbalimbali, au jinsia. Ingekuwa tofauti hizo peke yake zinatosha kuthibitisha mfumo rasmi wa ubaguzi wa Waislamu, kwanini tusiseme pia kuwa upo mfumo rasmi wa kubagua wanawake, au watu wa kabila fulani, au rangi fulani, au umbo fulani. Na ukweli ni kuwa si kila mahali Waislamu ni wachache. Kwa mfano nimejaribu kuhesabu ni mabalozi wangapi, tena kwenye zile ofisi za ubalozi muhimu sana, ambao ni Waislamu. Naomba na ninyi mfanye hesabu hiyo.

Lakini turudi kwenye masuala ya msingi. Si jambo zuri sana kuanza kujenga utamaduni wa kuhesabu watu kwa misingi ya kabila zao, dini zao, rangi zao, jinsia zao, au maeneo yanayotoka. Tangu uhuru tumejitahidi kujenga taifa ambapo haki na heshima ya mtu inatokana na utu wake, si dini yake, kabila lake, jinsia yake, na kadhalika. Siko tayari kujenga mfumo wa utawala ambapo sifa ya mtu kupata nafasi ya shule, au nafasi ya kazi, ni dini yake. Aidha, tukishaanza na dini tutawazuiaje wengine kudai nao wafikiriwe kwa misingi ya dhehebu la dini, jinsia na kadhalika. Hapo tutakuwa tumefumua misingi ya umoja, upendo, mshikamano na kuheshimiana waliyotuachia waasisi wa Taifa letu. Naomba sana tusitafute dawa ya ugonjwa mdogo itakayozua magonjwa makubwa zaidi yasiyokuwa na tiba.

Vile vile kuanzisha taasisi mpya ya kupokea na kuchunguza ubaguzi wa kidini kutazidi kutuvuruga tu kwa vile ni kukiri kuwa kweli upo ubaguzi uliojengeka ndani ya mfumo wa utendaji serikalini, jambo ambalo si kweli. Aidha, kama nilivyosema, ukianzisha taasisi ya kushughulikia ubaguzi wa kidini, huwezi kukataa wengine wakidai taasisi nyingine ya kushughulikia ubaguzi wa jinsia, ubaguzi wa kabila, rangi na kadhalika.

Tusijitose sana katika zoezi la kuhesabu watu kwa misingi ya dini. Tukifanya hivyo tutaimarisha, badala ya kufifisha, hali ya watu kujihisi kwanza kama watu wa dini fulani, badala ya kujihisi kwanza kama Watanzania. Mimi nilifikiri kuwa Tanzania ilishavuka hatua hiyo. Naomba tusirudi nyuma kwenye kutukuza udini, ukabila, au maeneo tunayotoka. Tukishajitumbukiza huko hatuwezi kutoka tena. Badala yake lengo letu liwe kuelekea mahali ambapo tutakuwa vipofu wa dini, vipofu wa rangi, vipofu wa kabila, na kadhalika. Na pia tusisahau kuwa Tanzania yetu hii ina hata Maaskofu wenye majina ya Ramadhani au Hussein, na wengine wengi ambao wana majina yasiyofichua dini zao au kabila lao.

Jambo jingine la msingi ni kuhakikisha kuwa Tanzania kama Taifa, na kama serikali au chama chochote cha siasa, inakuwa haina dini. Kwenye hili hakuna mjadala, maana ni hali hiyo ya kutoinamia upande wa dini yoyote ndiyo inayotupa nguvu ya kusimamia na kuhakikisha kila raia anapata haki zake za imani za dini na uhuru wa ibada bila hofu au wasiwasi.

Kwa hili serikali ni refa anayehakikisha kila upande una haki sawa, na uhuru sawa, na kuwa uhuru wa kuabudu au kutangaza dini kwa upande mmoja hauathiri haki ya uhuru wa ibada na kutangaza dini kwa upande wa pili.

Mimi ni Rais wa watu wa dini zote, na ni Rais pia wa wale wasiokuwa na dini, ni Rais wa kabila zote na rangi zote, jinsia zote na hulka zote.

Mimi ni Rais wa wanywa pombe na wasio wanywa pombe; wala nguruwe na wasiokula nguruwe. Si kazi yangu kuhukumu nani kati yao ni mwema na nani si mwema. Kunitaka nimkataze mmoja anachopenda ni kunitaka nifanye kazi ya kuhukumu juu ya imani za watu ambayo si yangu; hiyo mimi naamini ni kazi ya Mwenyezi Mungu mwenyewe.

Hiyo pia ndiyo inayonifanya nichelee kukubali haraka haraka hoja ya Tanzania kujiunga na Shirika la Waislamu (OIC). Nadhani si sahihi kuishinikiza serikali ikubali hoja hiyo kwa vile tu zipo nchi nyingine zilizojiunga. Kila nchi huangalia mazingira yake na sababu zake. Kwa vile ukijiunga unafanya hivyo kama Taifa zima, si kama sehemu ya Taifa, siwezi kupuuza kabisa maoni ya wale ambao si Waislamu. Hivyo huu si uamuzi ambao ninaweza kuufanya kwa wepesi; unahitaji mashauriano zaidi na pande zote na kuelimishana ili jamii yote ya Tanzania ielewane.

Kuhusu suala la Mwembechai mimi nilifikiri tulishaelewana kuwa haitasaidia sana kuunda Tume ya Uchunguzi, maana tunajua kilichotokea. Na tunajua kuwa zile fujo, ambazo hatimaye zilihitaji nguvu kubwa ya dola kuzizima, hazikuwa na uhusiano na mambo ya dini kabisa. Ndio maana miongoni mwa waliokamatwa walikuwapo watu ambao wala si Waislamu. Bado haja na hoja ya kuunda Tume sijaiona.

Tulipokutana tarehe 7 Julai, mwaka huu, mojawapo ya mambo tuliyozungumzia ilikuwa umuhimu wa kuwa na fursa ya mazungumzo ya kudumu baina ya waumini wa dini mbalimbali, (inter-faith dialogue), ili mradi wahusika wawe watu waliokomaa kimawazo, wenye busara na nia njema. Hii itasaidia kujenga maelewano baina ya waumini wa dini zote na hivyo kupunguza hisia za kibaguzi za kila upande, na kujenga msingi bora zaidi wa kufurahia uhuru wa imani katika mazingira ya kupendana na kuheshimiana, japo tuwe na imani tofauti za dini.

Mlango wangu bado uko wazi kwa majadiliano ya mambo ya msingi kama haya kila nikiwa na nafasi.

Tanzania ni nchi yetu sote, watu wa imani tofauti za dini. Tukiwa na busara, tutawajengea watoto wetu nchi nzuri ya kumcha Mungu kwa uhuru, amani na kuheshimiana kwa kuzingatia kwa dhati maneno haya.

Wasalaam,

Benjamin William Mkapa
 
Sasa basi tukirudi kwenye hiyo issue ya ZNZ kujiunga na OIC lazima uelewe kuwa huu ni mwaka 2007 na ungetegemea kuwa watawala wetu wangekuwa na progressive minds lakini wapi!

Whats be big deal na ZNZ kujiunga na OIC kwa maslahi yake ya kitaifa na kiuchumi?

Na kwa taarifa kwa wale wasiojua ni kuwa(OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam. Watendaji Wakristo katika Wizara ya Elimu walipiga vita mradi huo na mwisho chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda...na leo hii ni moja kati ya vyuo ambavyo vinaproduce ma graduates toka nyanja mabali mbali Africa ya Mashariki....

Vile vile usisahau kuwa wale wa Saudi Arabia walipotaka kujenga shule ya ufundi Kibaha na yale yaliyoikuta OIC na wao yaliwafika sawia.

Unajua mimi niko radhi hata hao ma Freemasons wafungue vyuo Tanzania lakini kwa taarifa yako hiyo itakuwa haiwezekani kwani bado kuna mentality ya kuamua nani ajenge chuo na nani asijenge chuo Tanzania na yote iko based on imani za kidini

Huu ndiyo ukweli wa nchi yetu,watawala wako mstari wa mebele kuwahutubia na kuwakemea waTanzania wasichanganye dini na siasa lakini wenyewe wamejaa udini halafu wanataka kumtafuta mzizi wa fitna ili hali huo mzizi wanao wao wenyewe!

In short nchi yetu bwana hakuna anayekubali kuwe na honest debate na kama huamini tazama ile thread ya WANAKAGERA humu. badala ya watu kuibebea bango serikali kwa nini imewatosa wana kagera tangu vita na Uganda watu wamerukia kujisifu na harambee na kuingiza cheap politics za CHADEMA v/s CCM!
 
Sasa basi tukirudi kwenye hiyo issue ya ZNZ kujiunga na OIC lazima uelewe kuwa huu ni mwaka 2007 na ungetegemea kuwa watawala wetu wangekuwa na progressive minds lakini wapi!

Whats be big deal na ZNZ kujiunga na OIC kwa maslahi yake ya kitaifa na kiuchumi?

Na kwa taarifa kwa wale wasiojua ni kuwa(OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam. Watendaji Wakristo katika Wizara ya Elimu walipiga vita mradi huo na mwisho chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda...na leo hii ni moja kati ya vyuo ambavyo vinaproduce ma graduates toka nyanja mabali mbali Africa ya Mashariki....

Vile vile usisahau kuwa wale wa Saudi Arabia walipotaka kujenga shule ya ufundi Kibaha na yale yaliyoikuta OIC na wao yaliwafika sawia.

Unajua mimi niko radhi hata hao ma Freemasons wafungue vyuo Tanzania lakini kwa taarifa yako hiyo itakuwa haiwezekani kwani bado kuna mentality ya kuamua nani ajenge chuo na nani asijenge chuo Tanzania na yote iko based on imani za kidini

Huu ndiyo ukweli wa nchi yetu,watawala wako mstari wa mebele kuwahutubia na kuwakemea waTanzania wasichanganye dini na siasa lakini wenyewe wamejaa udini halafu wanataka kumtafuta mzizi wa fitna ili hali huo mzizi wanao wao wenyewe!

In short nchi yetu bwana hakuna anayekubali kuwe na honest debate na kama huamini tazama ile thread ya WANAKAGERA humu. badala ya watu kuibebea bango serikali kwa nini imewatosa wana kagera tangu vita na Uganda watu wamerukia kujisifu na harambee na kuingiza cheap politics za CHADEMA v/s CCM!

hawa wee watizame tu, lkn ukweli daima hauwezi kukaa chini, utausinya wee sawa na kuzamisha boya utatumia nguvu zote ukichoka linakuja juu tu
 
GAME-THEORY,
Tanzania ingejiunga na OIC 1990 Nyerere angekuwa hana hoja. Kikatiba ZNZ haina mamlaka wa kujiunga na jumuiya kama OIC,OAU,UN,Commonwealth etc etc. Kimataifa ZNZ na TGK hazitambuliki kama dola au nchi.

sioni kwanini TANZANIA[ZNZ && TGK] tusijiunge na OIC. Hili jambo linatakiwa litolewe uamuzi sasa hivi. Yaani miaka zaidi ya 15 serikali inakuwa na kigugumizi?
 
Yaleyale ya Nyerere kuwazuia wananchi wake kusafiri na kuwanyang'anya mabaharia magari yao kuwa ilikuwa anasa!..Leo hii ndio kwanza tunaanza kutoka nje na wengine kupata elimu basi sio ushamba na Ulimbukeni huo wa Mdanganyika. Watu wanashindana ukubwa wa magari badala ya kuwekesha fedha zao ktk miradi utafikiri Wasomali walivyoingilia Umalaya walipofika Ulaya!..
 
GAME-THEORY said:
Sijakuelewa unamaana gani na hilo neno YAKHE lakini inaonekana umelitumia as a derogatory term.Hivi unajua kama msomi kuliko wote katika serikali ya muungani ni DR SHEIN? je yule naye YAKHE? lete issue mzee kama huna hoja kaa kimya

GAME-THEORY,
umetumia kigezo gani ku-conclude kwamba Dr.Mohamed Shein ni msomi kuliko wenzake "wote" hawa: Dr.Eng.Mwandosya,Dr.Athumani Kapuya, Dr.Eng.Kawambwa, Dr.Juma Ngasongwa, Dr.Cyrill Chami, Dr.Batilda Burian etc etc.
 
Zanzibar wajiunge tu na hiyo OIC na waanzishe sharia law itakuwa poa sana maana zenji kuna waislamu 99%.
 
Msikilize Mzanibari huyu anavyosema...Hata mimi nawashangaa hawa wawakilishi, baada ya kusema kwamba ZNZ iwe na mabalozi wake kila nchi na waweko mabalozi wa kigeni ZNZ ati wanaomba nafasi za afisa wa ubalozi. Wallah inasikitisha sana sana. Hatutaki nafasi ya afisa wa ubalozi, tunataka ZNZ kama nchi huru yenye mamlaka yake kamili,kama ilivyokua kabla ya ushetani wa 1964. Mwenyezi Mungu awashushie laana wale wote walioshiriki na ufuska huo na kuizamisha ZNZ,AMIN...!
Hawa Wazanzibari hawatutaki kabisa wanatuona ni maadui wa roho zao na vizazi vyao Muungwana tutaonekana na kudhalilishwa hivi mpaka lini ??? Bora tuwateke mambo na kero yajimalizikie.
 
Swali langu ni moja tuu hii jumuiya inatoa hii misaada wakiexpect nini in in return ? Mimi nashindwa kuelewa kitu kimoja kwa nini linapokuja kwenye suala la imani watu wako tayari kupinda sheria za nchi " Katiba " . Hivi kweli watu hawaoni conflict jambo hili litakalozua kama Zanzibar ikijiunga na hii jumuiya . Ni lazima watu watambue ya kuwa Zanzibar sion nchi pali ni part ya sehemu ya Jamhuri .

Mimi nadhani kama watu wangekuwa wanafuatilia katiba wala haya maswali yasingekuwepo .
 
Back
Top Bottom