Inasikitisha sana kuona Udini ulivyojengwa Tanzania. na kibaya zaidi ni pale unaposikia viongoizi wa dini hizi hasa waislaam na Wakristu wakirushiana madongo bila hoja za msingi..yaani kweli hawa ni watu wa Mungu au wachawi tu.
Binafsi nimelifuatilia swala hili kwa makini na hakika nimegundua kwamba Washeikh na Maaskofu, wote ni wadini wa kutupa! wote hawaoni nje ya kabati la Udini inapofikia swala lolote linaloweza kujanga jamii moja..huweiz kupata maendeleo kwa watu wote kwa pamoja ila maendeleo huanza na kila mmoja wetu pale aliposimama iwe ktk dini, kazi au mchango wowote ktk jumuiya hii ya Kitanzania..
.
Kwanza nitaanza na upande wa Masheikh..
Kweli mahakama ya kadhi ni sehemu ya Ibada yao kama ilivyo kwa Wakristu na Parokia..lakini vyombo hivi vyote vinahitaji baraka za serikali kuweza kuchukua maamuzi ya mahakama au parokia kuwa ndio haki ya wahusika.
Tofauti ya Parokia na Mahakama ya kadhi ni maswala wanayoshughulikia ktk ibada hizi. Kwa Waislaam maswala mazito ya Kijamii (Personal matters) hutolewa settlement na mahakama hizi wakati wakristu maamuzi ktk maswala haya tayari yamekwisha jengwa ktk mfumo wa Kisheria tunaoufuata..inakuwa vipi vigumu kwa Maaskofu kuliona hilo!
Hivyo, inawezekana kabisa serikali yetu kuchukua baadhi ya sheria kama zilivyo za wakristu ndani ya sheria na maamuzi ya mahakama za Madai ambazo zimebeba maamuzi mengi kulingana na jamii hii nikiwa na maana WATU na MAZINGIRA..
Zipo sheria ambazo zinakubalika kwa Wakristu na wasiokuwa na dini, ila Magistarte court Act, inapo Indetify dini moja kuwa sheria zake zimekuwa restricted ndipo utata unapoanzia. Kwani hiyo Act haikusema kutoitambua mahakama ya kadhi isipokuwa kutotambua na kuzuia matumizi ya yoyote ya sheria za kiislaam..
Hii ndio point wangesimama nayo kuonyesha kwamba sii swala la mahakama ya kadhi isipokuwa MCA kuwqeka wazi kwamba ina restrict matumizi ya sheria za kiislaam hivyo hata wakiunda baraza lao wenyewe kama Parokia halitaweza kutambulia kama inavyotambuliwa Parokia..
Upande wa pili wa shilingi inasikitisha sana kusoma Asokofu akisema kwamba:-
Waislamu kama wanataka, wanaweza kuanzisha Mahakama ya kadhi bila ya kuihusisha Serikali." Wana uhuru wa kuendesha mambo yao kwenye taasisi zao yanayoendana na masuala ya kiroho bila kuishirikisha Serikali.
Maneno haya ni dharau ya wazi kabisa...kwa sababu kuna maamuzi mengi ya Kidini yamefikiwa kwa kuihusisha serikali kaa vile sisi sote tunachukua Jumamosi na Jumapili kama siku ya Mapumziko kwa sababu ni siku ya ibada za Kikristu.. waislaam hawajadai kuondolewa kwa haki hilo ya ibada ama kutoihusisha serikali ati waktaka kwenda kusali wakasali kama sisi waislaam tunavyokwenda siku ya Ijumaa ambayo inatambulika kama siku ya kazi na Waislaam hulazimishwa kwenda kazini (kikatiba) hata wakati wa Ibada zao.
Wakristu wanasherehekea siku ya kuzaliwa na kufa kwa Yesu na serikali imeifanya kuwa Public Holiday lakini Waislaam hawawezi kuzua madai kwa misingi ya kufananisha kila kesi na Wakristu wakati vitu hizi vina uzito topfauti ktk kila dini au shehebu.. Kila dini ina umuhimu wa maswala la siku zake tofauti na dini nyingineyo huwezi kusema kama sisi tuna Parokia basi waislaam nao waanzishe parokia wakati hivi vyombo havifanani kabisa.. Parokia sii part ya ibada ya Kikristu ila ni sehemu ya utawalka wa Kikatoliki..
Nina hakika kabisa kama mahakama ya kadhi ingeitwa jina jingine mathlan - Baraza la Usuluhishi, wakristu wasingekuwa na tatizo kabisa wakati hoja ya msingi sio jina la chombo hiki isipokuwa sheria zinazotakiwa kutumika..
Hivyo ukisoma maelezo yote ya Askofu hakuna sehemu ameeleza kwa nini anapinga matumizi ya mahakama ya kadhi nje ya kuona Uislaam ukihusishwa na serikali. Kihs madai kwamba wao wana mahakama zao kuanzia ngazi ya Parokia hadi Roma.. je kuna Mkristu gani alipeleka madai yake kwa Parokia na akakata rufaa hadi Roma.
Utaratibu wa kanisa Katopliki hauwezi kutumika kote sii kwa Wakristu wote wala wananchi wote..kwani Waislaam hawana Roma yao hawana kesi inayoweza kwenda nje ya mipaka ya nchi wanayoishi.. Uislaam ni dini sio nchi au taasisi inayowaongoza waumini kwani mwongozo kwao ni Kuran.. Tofauti hizi ndizo zinazotupa sisi maamuzi ya kuchagua dini uitakayo, na laukama Uislaam wangekuwa na Roma au Pope, mimi nisingekuwa Muislaam...Ikiwa Mkrisdtu anaweza kwenda kizimbani kanisani akatubu akasamehewa hapa duniani na Akhera hii sii mfano mzuri kwa Muislaam au Mkristu mwenye imani tofauti na kutii nguvu ya Parokia na Roma kiroho..
Ndoa, mirathi na mengineyo ya part ya ibada ya Waislaam.. Kufanya lolote kinyume cha walivyoamriwa ni kupotoza ibada. Kufanya lolote kinyume cha matakwa ya dini kunaweza kumtoa muumini ktk Uislaam akawa hana tofauti na kafir..Ni muhimu sana Askofu huyu aelewe kwamba Muislaam asiyefuata sheria za ndoa na Mirathi hukiuka matakwa ya dini ktk ibada hiyo, na haiwezekani kabisa Bakwata au chombo chochote kutoa maamuzi mazito ambayo hayatambuliwi kisheria..Kuna faida gani?
Mwisho msingi wa kutokubaliana na mahakama ya kdhi ungejengwa kulingana na Jamii yetu na sio dini zetu..Je, Waislaam wanafuata ibada hizi? jibu lake ni hapana. Ndoa nyingi za wananchi ni kinyume cha mafundisho hivyo huwezi kuchukua part ya Ibada ktk usuluhisho ukasahau au kupuuza kilichotangulia.. hata kama ni Kusali Muislaam anatakiwa apate udhu kwanza kabla hajaingia msikitini hivyo ibada yake ipate uzito wa kupokelewa. Ni part ya ibada ya sala kwa Muislaam hatuwezi kusema waingie tu kama wakristu au vinginevyo kurahisisha matakwa yetu...
Waislaam nchini wana wake toka madhehebu mbali mbali wengine hata hawana dini..Waislaam nchini hawana Udhu ktk maswala ya ndoa mirathi na kadhalika hivyo huwezi ku settle matatizo ambayo kwanza hayakufuata misingi ya dini. na hao hao Mashekh wanafungisha ndoa hizi, wana vimada na watoto nje ya ndoa zao... Na hata yule Sheikh anayekataa kufungisha ndoa mtu anakwenda Halamashauri na ndoa ikakubalika..Je, hii mahakama ya kadhi itakuwa na kazi gani na itamhukumu nani haswa?.
Mara zote mahakama ya kadhi itafanya kazi tu kwa waumini wa kweli na hili haliwezekani nchini isipokuwa linawezekana tu ikiwa mwongozo unatngulia ndoa halali za kiislaam ambazo zinatambua uzito wa ibada hiyo.