Mkuu hapana mimi sii hatari isipokuwa nipo kijiweni na hapa ni mahala pa kuangalia pande mbili za shilingi kisha unapima uzito wa hoja zote..Bila kuwakilisha upande wa pili itakuwa hatujadiliani isipokuwa tunafanya ushabiki mtupu..we Mkandara ni mtu hatari sana (sorry to say that) ukweli ndiyo huo. umh...
Kumbuka hili swala ni zito sana na linaweza tikisa nchi na kinachotakiwa ni kuelimisha Umma pande zote mbili, mazuri na mabaya yake (kama vile swala la mahakama ya kadhi OIC na MOU)
Taratibu na haki za ibada hizi kwani ndizo zinazofanya tofauti ya dini hizi. kama sote tungekuwa tunakubaliana basi sidhani kama tungekuwa na dini au madhehebu mengi..Kinachotushinda kuelewa ni hizi tofauti ambazo ndizo chanzo cha sisi kutengena ktk imani ya dini lakini tunajariobu kufikiria sawa mahala pasipokuwa na usawa huo..
Utasherehekea kuzaliwa/Kufa kwa Yesu kwa sababu ni ibada kubwa ya Mkristu, na sio lazima iwe pia ya Muislaam wala Muislaam kuweka shaka juu yake. Waislaam nao wanasherehekea Idd kwa taratibu zao kwa sababu ndiyo part ya ibada yao ktk mafundisho yao ukianza ku question wakati jibu lake ndilo lilikufanya usiwe Muislaam itakuwa kazi mpya..
Hizi zote ni ibada (sherehe) zinazokubalika kikatiba lakini huwezi kulazimisha ibada moja ya dini utumike ktk dini nyingine ukitumia reasoning ya mafundisho yako.