Hata mimi nataka kujua zaidi,kuna kitu nataka kuagizia kama sio leo ni kesho asubuhi..
Hii link pia itakusaidia: Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
1. usalama wa fedha apo hakuna tatizo sana.
Iwapo utatumia njia rasmi ya kufanya malipo, Ni salama.
2. Uhakika wa bidhaa. (Picha vs real product)
Kwanza hakikisha unafanyia utafiti bidhaa husika, kutoka site zingine kwa kuangalia reviews za wanunuaji wengine walio tangulia. Mfano: Waweza kuwa umeiona bidhaa ALIBABA, kabla ya kufikiria kununua kwanza ingia site kama AMAZON, tafuta hiyo bidhaa, na angalia sehemu ya maoni ya walio nunua. Kwa utaratibu huu lazima utapata bidhaa yenye ubora.
Kumbuka china zipo bidhaa zenye ubora na zisizo na ubora, hivyo ni jukumu lako kufanya utafiti kwanza
3. Bidhaa inachukua muda gani mpaka kunifikia
Inategemea na njia ya usafirishaji uliyokubaliana na muuzaji.
- Zipo njia za haraka, Huchukua siku 5 hadi 9 kwa mzigo kufika nchini. Changamoto wa njia hii (a) Ghalama ya usafirishaji (b) Agent and handling fees - baada ya mzigo kufika nchini (c) Kodi/ VAT
- Njia isiyo ya haraka; Mzigo unachukua kati ya siku 11 hadi 21, Ghalama ya usafirishaji huwa ni ndogo.
Unaweza kuta gharama yake ikawa kubwa kuliko ata ya bidhaa uliyo inunua
Ndio, mfao waweza nunua earphone kwa dola 5, ila ukataka zikufikia ndani ya muda mfupi, seller atatumia DHL/ FEDEX na utajikuta unalipia freight cost ya Dola kati ya 15 hadi 22, Chukua umelipa dola 15
Hapo utaona bidhaa hadi inakufikia unakuwa umetumia USD20
4. Refund procedures endapo mzigo sijaupata, au sijarishika nao.
N.k
Karibuni
Njia uliyotumiakufanya malipo ndio njia utakayotumia kupokea refund.
Hivyo epuka njia zisizo rasmi katika kufanya muamala, fuata taratibuza site husika.

Iwapo bado unashaka basi waweza kutumia huduma yangu hapa: Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
 
Why Amazon or Ebay ? When we havie Jumia and Kivuko in Tanzania. Its better to go for a local store than waiting for an international store to do our shipments.
 
Mifumo yote ni salama.

Alipay na Amazon Pay - Ni mifumo salama itumiwayo na aliexpress (alipay) na Amazon (amazon pay) kufanya manunuzi.

Ambapo mnunuzi unaweka taarifa zako za card na malipo yanafanyika kiusalama kabisa.

Kwa mifumo yote miwili, Seller hapewi fedha hadi pale wewe mnunuzi utakapo thibitisha kuwa umepokea mzigo
  • Iwapo mzigo hujapokea REFUND hufanyika na fedha inarudishwa kwenye kadi husika.
Naomba nionyeshe sehemu ya kuthibitisha umepokea.
Vp usipothibitisha umepokea inakuaje?
 
Naomba nionyeshe sehemu ya kuthibitisha umepokea.
1533550435058.png
Hapo nilipo zungushia
Vp usipothibitisha umepokea inakuaje?
1533551097822.png

Bila shaka KakaJambazi nimeeleweka
Huo muda ukiisha, Automatic muuzaji anapewa fedha yake. Hata bila ya wewe kutoa taarifa.

Ila kwanza utatumiwa EMAIL ya kukupa taarifa kuwa inatakiwa uthibitishe kuwa mzigo umekufikia
1534240374046.png
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: http://comgateway.com/ - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
Brother hongela nahangaik sana namna ya kununua gali mtandaoni hasa nchi za wenzetu nataka nipate kupitia website ya Amazon ndo nmeipenda bt wana mawakala hapa Tanzania??????
 
wakuu hawa tra wanakata asilimia ngap ya thaman ya mzigo kama kodi? (mzigo ulionunuliwa kupitia mtandao)
 
Wapendwa habari za jioni?

Baada ya mizunguko yangu ya Leo nimepata wazo la kununua bidhaa mtandaoni. Lakini wakati naendelea kutafakri nikagundua sijui chochote kuhusu hili, wakati naendelea kuwaza zaidi nikakumbuka ipo JF na ninaweza kupata msaada huku.

Swala la msingi ninaomba kufahamishwa jinsi ya kununua bidhaa mtandaoni taratibu na kwa mapana na marefu tangu unachagua bidhaa, jinsi ya kulipia bidhaa, namna bidhaa inavyosafirishwa gharama za kusafirisha bidhaa kodi na jinsi ninavyoweza kufikiwa ba hiyo bidhaa.

Ikumbukwe tu mpaka Sasa hivi sijui chochote kuhusu hili kwa hiyo naomba naomba nielekezwe hatua Moja baada ya nyingine kwa unasahau.

Ahsante na mbarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapendwa habari za jioni?

Baada ya mizunguko yangu ya Leo nimepata wazo la kununua bidhaa mtandaoni. Lakini wakati naendelea kutafakri nikagundua sijui chochote kuhusu hili, wakati naendelea kuwaza zaidi nikakumbuka ipo JF na ninaweza kupata msaada huku.

Swala la msingi ninaomba kufahamishwa jinsi ya kununua bidhaa mtandaoni taratibu na kwa mapana na marefu tangu unachagua bidhaa, jinsi ya kulipia bidhaa, namna bidhaa inavyosafirishwa gharama za kusafirisha bidhaa kodi na jinsi ninavyoweza kufikiwa ba hiyo bidhaa.

Ikumbukwe tu mpaka Sasa hivi sijui chochote kuhusu hili kwa hiyo naomba naomba nielekezwe hatua Moja baada ya nyingine kwa unasahau.

Ahsante na mbarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama una VISA card au MasterCard iliyiverified kwa ajili ya online purchases,nenda play store download Ali Express fanya mambo kuwa rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wadau habari za muda

ningependa kufahamu mchanganuo wa biashara kupitia Alibaba, nahitaji kununua bidhaa kutoka china.

natamani kufanya biashara ya alunium foil ana apo baadae niwe na kiwanda ila kwa sasa. nikijarbu kuwasliana na kampuni za china nakuta bei zao zko juu ama tofauti ndogo. so nkipga maesabu nakuta ntawafaidisha watu wa shipping an tra na mimi stopata ktuy.

mwenye uelewa zaid naomba aniwezeshe kimchanganuo wa makato ama kujua kampuni za be nafuu na ubora mzuri
 
Kuna bidhaa nahitaji kununua katika mtandao wa Alibaba ila seller kunambia nimlipe kwa TT je ni njia salama kwa pesa yangu?
 
Back
Top Bottom