Wapo vizuri sana kwa maana ya uharaka wa kusafirisha parcels na gharama nafuu bila complications kama za wazungu ambao kuna restrictions nyingi mno za kusafirisha (complications za wauzaji)..

Lakini customer care yao Siku za nyuma ilikuwa shida kidogo maana hakukuwa na namba za simu,email wala system mail hivyo ilikuwa shida kidogo kujua mustakabali wa mzigo wako in case haujafika, kwa sasa sijui ipoje...ila jamaa wako poa sana kwa kutokuwa na complications.. On eBay refunds in uhakika, hakunaga longolongo ila shida no wazungu kuleta complications za kusafirisha
 
Natakaga kuagiza laptop na camera lakini huwa naogopa sana sijui kwa nini! Mkuu nibembeleze basi ili niweze kuagiza!!
 
Huo ni mtazamo wako kutokana na experience yako na hao......

Nimekutana na watu hawataki hata kuusikia huo mtandao....
 
wadau vp kuhusu wizi wa posta zetu? Bd upo?

Mikoani hakuna shida kabisa ila Posta ya Dar bado kuna element za wizi, kuna mzigo niliwahi kutumiwa kituo cha kupokea kikawa Tanga sasa nilipotrack nikauona umefika Tanzania (Dar) lakini kuanzia hapo kukawa hakuna update na ofisi ya Tanga ukawa haujafika.

Ikabidi kufuatilia Dar ofisi kuu ya posta ndio nikgundua ulipigwa hapo, walisema kuwa kweli mzigo ulifika lakini ndani ya box kulikuwa empty hivyo wakaamua kuurudisha ulikotoka kitu ambacho so kweli na hata kingekuwa kweli bado haikuwa kazi yao, ikabidi seller abebe mzigo kwa kunirefund.

Generally wizi umepungua siku hizi save for changamoto hizo chache hapo Dar (ingawa mizigo yote ya mikoani ili ifike ni lazima ipitie Dar)
 
Nilikua mtumiaji mzuri sana wa eBay ila niliongiwa na ukakasi mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuagiza drone kwa pesa ndefu kweli kweli nimesubiri mwezi naingia kucheki status naambiwa "seller suspended"

Kuhangaika kusumbuana na eBay mwisho wa siku nikachoka nikaachana nao mpaka sasa sitaki tena masuala ya kununua vitu online kuna ufala mwingi
 
Natakaga kuagiza laptop na camera lakini huwa naogopa sana sijui kwa nini! Mkuu nibembeleze basi ili niweze kuagiza!!

Nunua wala hutojuta, posta pia wako vizur kama uko dar
Unapewa track number au posta ukifika mzigo wanakupigia.
 
Naomba nikiri kwa kinywa changu kwamba aliexpress inazipiku hizo eBay na hata amazoni
-
Kwanza aliexpress ni rahisi kununua


Pili ni fastest shipping compare to ebay or amazon


Cha tatu wanarefund haraka na ni wa uhakika zaidi

Cha NNE bidhaa zao ni cheap na affordable


Cha tano sana customer care nzuri sana


Cha sita packages za bidhaa wanapack vizuri


Sijaona cha kunishawishi kunitoa aliexpress kiukweli naenjoy sana hata juzi ijumaa nimetoka kupokea parcel zangu Posta ya Arusha


Jamaa wapo vizuri changamoto ni Posta zetu hazijakaa kidigital hapa ndo tatizo

Nyingine ongezeeni wakuu
Nimenunua fast charge tangu 26/3/2018. Mpaka leo hakuna taarifa
 
Nilikua mtumiaji mzuri sana wa eBay ila niliongiwa na ukakasi mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuagiza drone kwa pesa ndefu kweli kweli nimesubiri mwezi naingia kucheki status naambiwa "seller suspended"

Kuhangaika kusumbuana na eBay mwisho wa siku nikachoka nikaachana nao mpaka sasa sitaki tena masuala ya kununua vitu online kuna ufala mwingi
refund jee?
 
129 Reactions
Reply
Back
Top Bottom