Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

mazingaombwe ni nini

View attachment 3652526
View attachment 3652527
View attachment 3652528
+2

Mazingaombwe ni sanaa ya udanganyifu wa macho au vitendo vya ajabu vinavyofanywa na mtu ili kuburudisha, ambapo vitu vinaonekana kufanyika lakini kiuhalisia ni mbinu za kisayansi, wepesi wa mikono, au saikolojia badala ya uchawi wa kweli. [1, 2, 3]

Sifa za Mazingaombwe
    • Kiini macho: Huwafanya watazamaji kuona vitu ambavyo havipo au kutokea kwa namna ya tofauti na uhalisia.
    • Sanaa na Burudani: Hutumika kwenye maonyesho ya sarakasi, majukwaani, na televisheni.
    • Mbinu za Siri: Msanii hutumia vifaa maalumu au kasi ya mikono kuficha ukweli wa jinsi tendo linavyofanyika.
TOFAUTISHA SANAA ILIYOPO NYUMA YA MAZINGAOMBWE VS UCHAWI ILI KUTHIBITISHA HOJA YAKO KWAMBA VITABU VYA DINI VIMEANDIKA UONGO HUSUSANI KWENYE SEKTA YA UCHAWI
 
Magic ni myth
Waafrica mna matatizo sana
Kama unasema uchawi haupo kwa sababu hujawahi kuuona au kuuthibitisha mwenyewe kwa mantiki hiyo hiyo unawezaje kusema kwa uhakika kwamba haupo badala ya kusema tu kwamba hujapata ushahidi wa kutosha wa uwepo wake ?
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Tusiwe wagumu wa kufikiri kwa kina au kulazimisha kila kitu kiendane na mtazamo wetu Kama kuna utofauti wa mitazamo ndani ya jamii, hata kwenye masuala ya uchawi tunaweza kuwa na mitazamo tofauti.

Labda nikuulize hivi Hao wanaoitwa Freemasons au Illuminati, ambao wana mali na pesa nyingi, unaamini hawajawahi kutumia mambo wanayohusishwa nayo kama uchawi kwa namna wanayoiona kuwa nzuri au yenye faida? Na kuhusu chuma ulete, unaona haiwezekani mtu kuamini kwamba ameitumia kwa njia nzuri ili kupata mafanikio?

Si kwamba nasema hayo ni kweli moja kwa moja, bali tuache nafasi ya kuuliza na kuchunguza kabla ya kukataa kabisa.
 
Mimi pia kuanzisha huu mjadala ni kutaka kujua zaidi

Nimetoa rejea ya vitabu vya dini kuhusu uchawi unajua kwanini ?
Jibu ni kutaka kuonesha au kukubali hii dhana ya uchawi ni ya zamani (kale )

Na pia nikatoa mfano wa mimi mwenyewe na scenario niliyokutana nayo na namna nilivyoelewa

Nikasema pia kwa wale ambao mna amini uchawi kwamba unaweza kufanya kadha wa kadha tuseme ni kweli nakubali

Kwanini sasa hiyo nguvu ya uchawi isitumike kwa mambo ya faida zaidi
Nikatoa na mifano

Kwa mantiki hiyo wewe ukija kuchangia mjadala chagua upande wako kuungana na mimi au kuniponga kisha tujadili kwa fact sio jumla jumla
Hakuna kitu sipendi kama mtu anakichulia mjadala jumla jumla
 
kwenye mjadala lazima tuishie kwenye kukubali au kupinga tu? Hatuwezi kwanza kusimama katikati, kufikiria kwa kina, kuchunguza hoja zote, na kuangalia uwezekano mwingine kabla ya kuamua kukubaliana au kupingana ?

Ndio maana nilitanguliza tafakari kuhusu mada yako, kwa sababu mjadala haupaswi kuishia kwenye kukubaliana au kupingana tu. Kwanza tunapaswa kuchunguza hoja, kuangalia uwezekano mbalimbali, na kufikiri kabla ya kufikia hitimisho.
 
Baado sijajua hata unataka kusema nini
Nikiri tu kwamba nimeshindwa kukuelewa bro

Sijui unataka kusema je : nimeshindwa kukuelewa
 
Kwamba waganga hapa Dar wagonjwa zao hutoka sana mikoani kuliko Dar yenyewe?
Kuna special case hutokea pale mtu alilogwa akiwa mkoani kisha anahamia Dar akiwa mgonjwa tayari ila anakuja kushtukia mbeleni wakati yuko Dar maana Dar watu wanahamia kila siku
 
Baado sijajua hata unataka kusema nini
Nikiri tu kwamba nimeshindwa kukuelewa bro

Sijui unataka kusema je : nimeshindwa kukuelewa
Umesema kwenye kujibu maada yako nisije jumla maana ake nipinge au nikubali ndomana nmesema kwenye mjadala ni lazima tu kukubal au kupinga ?

Hatuwezi fikilia tofauti, au kuangalia sababu mbali mbali tofauti na kupinga au kukubali ?
 
Okay twende kwenye point
Kwenye hii issue ya uchawi ambayo mimi naichukulia kama dhana tu

Wewe unaamini uchawi upo na unafanya kazi?
 
Okay twende kwenye point
Kwenye hii issue ya uchawi ambayo mimi naichukulia kama dhana tu

Wewe unaamini uchawi upo na unafanya kazi?
Ndiyo naaminiuchawi upo, lakini bado ni sehemu inayo husishwa na uharibifu Kwa hiyo si rahisi kuuchukulia kama njia ya manufaa kwa jamii kwa sababu mara nyingi uchawi ni jambo la mtu binafsi na kila mtu anaweza kuwa na malengo yake yawe mazuri au mabaya.

Pia hata kama uchawi unatumiwa kumsaidia mtu kwa namna inayo onekana kuwa nzuri, bado kuna swali la msingi je huo uzuri haujajengwa juu ya jambo la madhara kama kafara au taratibu nyingine za kishirikina? Hivyo, kile kinachoonekana kuwa faida kwa mtu mmoja kinaweza kuwa na upande mwingine wa madhara kwa mtu au kitu kingine.
 
Ahaa sasa mpka ukafikia hitimisho na kusema unaamini
Ulitumia vigezo gani
Ukasema kwa hiki na hiki ama kweli uchawi sio dhana ila ni halisi
 
Ahaa sasa mpka ukafikia hitimisho na kusema unaamini
Ulitumia vigezo gani
Ukasema kwa hiki na hiki ama kweli uchawi sio dhana ila ni halisi
Kama jambo fulani limeelezwa na watu wengi tofauti, na kuna shuhuda nyingi zinazofanana kutoka kwa watu ambao hawahusiani, si rahisi kulipuuza kama jambo la kufikirika tu.

Shuhuda hizo zinaweza kuwa kigezo cha msingi cha kukubali kwamba jambo hilo linaweza kuwepo na linafanya kazi.

Mbali na hapo nmefanikiwa kuishi iringa kuna mambo mengi pia nmeyaona kwa uhalisia wa macho .
 
Ni kwa sababu wengi wenu humu uchawi ni kitu mnachokisikia zaidi kuliko kushuhudia, wengi humu mnazungumzia story za utapeli wa waganga, imani potofu ambazo mnazisikia zenye kuhusishwa na uchawi. Kwahiyo kama uelewa wako kuhusu uchawi ni kupitia hizo story za utapeli basi ni wazi lazima ushindwe kutenganisha.
Mazingaombwe tu.
 
Uliuona wapi, unafananaje huo uchawi.
Nilikuruhusu unifanyie huo uchawi. Alafu uje utoe ushuhuda humu
 
Kama jambo fulani limeelezwa na watu wengi tofauti, na kuna shuhuda nyingi zinazofanana kutoka kwa watu ambao hawahusiani, si rahisi kulipuuza kama jambo la kufikirika tu.

Shuhuda hizo zinaweza kuwa kigezo cha msingi cha kukubali kwamba jambo hilo linaweza kuwepo na linafanya kazi.
Kwangu mimi kwa jambo kama la uchawi ushuhuda wa watu wengine
Tena wenye mkanganyiko haunitoshi mimi kukubali hiyo dhana ya uchawi

But naheshimu uamuzi wako
Mbali na hapo nmefanikiwa kuishi iringa kuna mambo mengi pia nmeyaona kwa uhalisia wa macho .
Na mimi siku nikishuhudia kama ulivyoshuhudia wewe nitakuja na story nyingine
 
Uchawi hakuna asililimia kubwa ni psychology tu ya akili yako ikanza kukubali basi Matokeo yake yanakuwa positive
mawazo yako yana nafasi kubwa kuleta effect katk maisha yako
 
Hivi kweli watu wanaweza kufarakana kwa mtindo huo?
Sio kwamba kutokuelewana ndiyo chanzo kikuu cha mahusiano kuharibika ?
Mimi sizungumzii chanzo cha kuharibika mahusiano ya watu bali nazungumzia jinsi ambavyo uchawi unaweza kutumika kuharibu mahusiano, kuna watu waume zao wana mahusiano ya nje huko, hivyo moja ya mambo ambayo watu hutumia uchawi ni huko kuachanisha/kufarakanisha mahusiano kama hayo. Sasa kesi kama hiyo mganga anatumia saikolojia gani hapo kumdanganya mteja wake?
 
Umezungumzia swala la uchawi na majini, ni kweli kabisa kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uchawi na majini

Wachawi na majini ni wadau muhimu sana wa kufanikiwa kwa uchawi,kwasababu mmoja ni boss na mwingine ni mtumwa

Wachawi wanawatumikia Majini,ndio maana kwenye kitabu cha qur'an Allah anasema majini wanawapoteza watu wengi sana kwenye njia ya Mwenyezi Mungu

Kwasababu ukitaka ufalme wa uchawi, jini nae ana masharti yake,ikiwemo umkane Mwenyezi Mungu,ukufuru na mambo kama hayo

Utaambiwa ua mama yako au baba yao au mwanao,kifupi nao wana ile dhana ya no free lunch

Na wachawi wanapewa uwezo na majini kwa kufanikisha mambo yao,mathalani kupaa,kuingia kwenye nyumba kichawi na mambo kadha wa kadha

Kwahiyo ni sahihi kusema huwezi kutenganisha uchawi na majini
Uchawi ni taaluma ambayo inaweza kufanyika kwa msaada wa jini au bila ya uwepo wa jini.

Chukuliwa jini kama muuaji anayekodiwa kutenda mauaji...Haya mauaji ndio uchawi. Uchawi unaweza kutumia maneno, miti shamba n.k pia unaweza ukamtumia jini kufanya baadhi ya mambo ya kuleta madhara kama kuvunja ndoa,kuharibu biasharaau afya ya mtu n.k
 
Watu wengi wanadhani uchawi upo africa tu...ila hawajui kama wachawi walo dunia nzima, hadi wazungu wachawi wapo na wao si kitu cha kujificha, huwa wanafanya wazi wazi kabisa na magician unamkuta ana ofisi na yuko proud na kazi yake tofauti na huku Africa jambo linaloonekana ni la taboo na aibu sana.
 
Uchawi hakuna asililimia kubwa ni psychology tu ya akili yako ikanza kukubali basi Matokeo yake yanakuwa positive
mawazo yako yana nafasi kubwa kuleta effect katk maisha yako
Sawa bin shetani sema kwa hiyo username nilidhani utakuja kusema uchawi upo 😃
 
Back
Top Bottom