Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Uchawi upo kama ukiamini kuna uchawi pia uchawi haupo kama huamini kuna uchawi.
Kuhusu uchawi kuna aina mbili za uchawi, uchawi mweupe na uchawi mweusi.
Uchawi mweusi ni nguvu inayotokana na mashetani,majini wabaya, mizimu n.k
Uchawi mweupe ni nguvu ambayo inatokana na asili, akili n.k
Kupata uchawi mweupe ni ngumu inahitaji kuanzia miezi 6 na kuendelea ila uchawi mweusi ni rahisi siku moja tu unakuwa na nguvu hizo
nimecheka sana. kuna Mengi duniani
 
siamini katika uchawi na pia siamani katika story za dini. kuishi hivi hakujawahi kunisababishia tatizo lolote katika maisha. sijawahi kurogwa au dalili yoyote ya kuwa anayeitwa mungu ananiadhibu. naishi maisha yenye furaha.
Enjoy mkuu 😊
 
Watu wa imani ndio watu gani?

Suala la watoto kuchelewa kutembea na hadi kuchanjiwa dawa ili waweze kutembea lipo sana katika jamii zetu, sasa mie napotoa mifano kama hiyo ili tuijadili unakuja kusema sie watu wa imani.

Watu wa imani ni watu gani? Hebu elezea ni kwa vp wewe unaishi kwa uthibitisho tu katika maisha yako ya kila siku.
Watu wa IMANI ni watu mnaomini katika MIUJIZA aka Superpower kama Mungu, Malaika, uchawi, majini na vitu kama hivyo ambavyo HAMUWEZI kuthibitisha uwepo wake

Unapotoa mfano toa mfano kwa kutumia LOGIC(akili) na sio IMANI
Yaani wewe ukisikia tu mtu karopoka kuhusu UCHAWI unaamini pale pale na kuja nao hapa JF kama ndio USHAHIDI wa hoja yako………,tuna jadili vipi sasa?

Mkuu nikikwambia leo nimekula Pilau naweza kuwa nakudanganya LAKINI uwezekano wa mimi kula pila upo kwa 100%…………… Nitofauti kabisa na nikikwambia leo nimekutana na paka akaanza kuongea……….

Swala fulani kuwepo kwenye jamii sio UTHIBITISHO kwamba ni la KWELI
Jamii ya Wachina zaidi ya Bilioni wanacho amini kuhusu Miungu yao ni FACT?
Ni KWELI Yesu ni Mungu kisa jamii ya wakristo wana amini hivyo? Vipi kuhusu jamii ya Vikings, Islam, Hindu nk?
Hivi unajua jamii ya kimasai ilikua inaamini nini kuhusu watoto wanaozaliwa na ulemavu wowote ule? Imani yao Ilikua ni kweli na sahihi?
Unajua Imani za jamii za kale zilivyokua KATILI Mkuu?
 
Mkuu mimi naishi kwa kutumia fact/logic/sayansi/uhalisia

Nikitaka jambo langu liende na push kulingana na UHALISIA na sio kumuomba Mungu wala mizimu kwa mganga wala kutafuta miujiza kufanikisha

Nikiumwa nakwenda hospitali siendi kuombewa wala kuaguliwa
Ili kunidhuru mimi ni ama unipe sumu na sio uvunje nazi njia panda au uchukue nyele zangu halafu nidhurike…NOPE

Nikipata/fanikisha jambo itakua ama juhudi zangu au coincidence na sio baraka kutoka kwa Mungu au mizimu

Nikipatwa na changamoto ni coincidence za maisha na sio laana ua kutorogwa
Nadhurika kwa vinavyo ingia mwilini direct na sio kuvunja nazi Chanika nikadhurika Sinza, au kunilaani nk

Nikisikia jambo nalipima kwa logic na sio IMANI ili kulikubali, kulitilia shaka au kulikubali
 
HIvi unafahamu hata meditation zamani watu walikataa kuwa ina faida kwa sababu ilikuwa haijathibitishwa kuwepo hizo faida kwenye meditation ila sasa hivi faida za meditation zimeweza kuthibitishwa kisayansi?
Hii inahusiana nini na UCHAWI
BTW moja ya mambo yaliokuja kifanya watu wengi kuachana na IMANI za supernatural ni sayansi kuja kujibu

Zamani mambo yote ambayo binadamu alikua hajui yamefanyikaje alikua anaamini Kuna nguvu kuu ambayo inafanya hayo, na nguvu hiyo ilikua ni Mungu au uchawi

Taratibu mambo yakaanza kubainika pale sayansi ipoanza kubaini yanafanyikaje na kuonekana sio miujiza tena
 
Huoni kama hiyo sababu ya mtoto kucwanjwa ni nyepesi sana kuthibitisha uchawi ?

Kama asingechanjwa unadhani asingetembea?

Kawaida watoto wanatofautiana sana
Kuna wale wanaowahi kutembea na kuna wale wanaochelewa kutembea

Wazazi wengi wanaenda kwa waganga mtoto ameshafikia kutembea

Akipewa dawa baada ya week
Mtoto akatembea anaona mganga kamsaidia 😅
Kwahiyo hao wazazi huwa wanaenda kwa mganga ikiwa imebaki wiki tu ili mtoto aweze kutembea mwenyewe?
 
Mimi nakuuliza kuhusu hoja ya uliyoileta ndio tunaijadili, wewe kuamini au kutokuamini uchawi hilo ni jambo lako binafsi.
Haja yako sikubaliani nayo mkuu
Nadhani pia nimekueleza kwanini
 
Hii inahusiana nini na UCHAWI
BTW moja ya mambo yaliokuja kifanya watu wengi kuachana na IMANI za supernatural ni sayansi kuja kujibu

Zamani mambo yote ambayo binadamu alikua hajui yamefanyikaje alikua anaamini Kuna nguvu kuu ambayo inafanya hayo, na nguvu hiyo ilikua ni Mungu au uchawi

Taratibu mambo yakaanza kubainika pale sayansi ipoanza kubaini yanafanyikaje na kuonekana sio miujiza tena
Hiyo inahusu uthibitisho na ukweli, meditation imekuwepo kwa miaka mingi pamoja na faida zake(ukweli) kabla hata sayansi hajaweza kueleza chochote kuhusu meditation na faida zake(uthibitisho).

Wakati huo watu walipinga hizo faida za meditation kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kisayansi, ndio maana nasema kukosekana kwa ushahidi sio ushahidi wa kutokuwepo.
 
Haja yako sikubaliani nayo mkuu
Nadhani pia nimekueleza kwanini
Na mimi nimehoji pia katika sababu ulizoeleza.

Halafu mkuu hapa tunajadiliana tu wala hatulazimishani kukubaliana au ndio ukubali nachoamini mimi. Kwahiyo hapa tunajadili tu wewe baki na msimamo wako na wengine tunabaki na misimamo yetu hii ni misimamo ambayo tumeikuta mkuu imekuwepo kabla hata wazee wetu hawajazaliwa.
 
Hiyo inahusu uthibitisho na ukweli, meditation imekuwepo kwa miaka mingi pamoja na faida zake(ukweli) kabla hata sayansi hajaweza kueleza chochote kuhusu meditation na faida zake(uthibitisho).

Wakati huo watu walipinga hizo faida za meditation kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kisayansi, ndio maana nasema kukosekana kwa ushahidi sio ushahidi wa kutokuwepo.
Mkuu hii hoja haina uhusiano wowote na IMANI ya uchawi.

Turudi kwenye hoja………. Wewe binafsi ukiachana na porojo za kusikia kwa wengine, je umewezaje KUJIHAKIKISHIA uchawi upo?
 
Na mimi nimehoji pia katika sababu ulizoeleza.

Halafu mkuu hapa tunajadiliana tu wala hatulazimishani kukubaliana au ndio ukubali nachoamini mimi. Kwahiyo hapa tunajadili tu wewe baki na msimamo wako na wengine tunabaki na misimamo yetu hii ni misimamo ambayo tumeikuta mkuu imekuwepo kabla hata wazee wetu hawajazaliwa.
Sawa mkuu 👍
 
Watu wa IMANI ni watu mnaomini katika MIUJIZA aka Superpower kama Mungu, Malaika, uchawi, majini na vitu kama hivyo ambavyo HAMUWEZI kuthibitisha uwepo wake

Unapotoa mfano toa mfano kwa kutumia LOGIC(akili) na sio IMANI
Yaani wewe ukisikia tu mtu karopoka kuhusu UCHAWI unaamini pale pale na kuja nao hapa JF kama ndio USHAHIDI wa hoja yako………,tuna jadili vipi sasa?

Mkuu nikikwambia leo nimekula Pilau naweza kuwa nakudanganya LAKINI uwezekano wa mimi kula pila upo kwa 100%…………… Nitofauti kabisa na nikikwambia leo nimekutana na paka akaanza kuongea……….

Swala fulani kuwepo kwenye jamii sio UTHIBITISHO kwamba ni la KWELI
Jamii ya Wachina zaidi ya Bilioni wanacho amini kuhusu Miungu yao ni FACT?
Ni KWELI Yesu ni Mungu kisa jamii ya wakristo wana amini hivyo? Vipi kuhusu jamii ya Vikings, Islam, Hindu nk?
Hivi unajua jamii ya kimasai ilikua inaamini nini kuhusu watoto wanaozaliwa na ulemavu wowote ule? Imani yao Ilikua ni kweli na sahihi?
Unajua Imani za jamii za kale zilivyokua KATILI Mkuu?
Hakuna watu ambao wanaamini hivyo vitu kwa pamoja hadi uwaite kuwa ni watu wa imani,watu hutofautiana katika kuamini hivyo vitu. Wapo wenye kuamini Mungu ila hawaamini kuwepo kwa majini,uchawi wala mizimu na wapo wasioamini Mungu wala malaika ila wanaamini mizimu au uchawi n.k

Lakini pia watu hawaamini kila kitu kama usemavyo et kisa wao ni watu wa imani, watu hutofautiana wanavyoamini na si kwamba wanaamini kila kitu, watu wana sababu zao tofauti za kuamini na ndio maana hutofautiana hata huo uchawi wapo wenye kuamini uchawi ila hawakubaliani na kwamba uchawi unaweza kusaidia katika mapenzi au kupata pesa kama ambavyo wengine wanaamini.

Hivyo suala la watoto kuchanjwa ni jambo ambalo hufanyika na matokeo hupatikana ambayo yaliyokusudiwa. Sasa mimi nimelileta hili ili tujadili hayo matokeo yanayopatikana baada ya mtoto kuchanjwa je ni nini hasa? Ni saikolojia tu au ni kitu gani?
 
Mkuu mimi naishi kwa kutumia fact/logic/sayansi/uhalisia

Nikitaka jambo langu liende na push kulingana na UHALISIA na sio kumuomba Mungu wala mizimu kwa mganga wala kutafuta miujiza kufanikisha

Nikiumwa nakwenda hospitali siendi kuombewa wala kuaguliwa
Ili kunidhuru mimi ni ama unipe sumu na sio uvunje nazi njia panda au uchukue nyele zangu halafu nidhurike…NOPE

Nikipata/fanikisha jambo itakua ama juhudi zangu au coincidence na sio baraka kutoka kwa Mungu au mizimu

Nikipatwa na changamoto ni coincidence za maisha na sio laana ua kutorogwa
Nadhurika kwa vinavyo ingia mwilini direct na sio kuvunja nazi Chanika nikadhurika Sinza, au kunilaani nk

Nikisikia jambo nalipima kwa logic na sio IMANI ili kulikubali, kulitilia shaka au kulikubali
Ni kwa sababu hujui kwamba imani si issue za Mungu,mizimu,miujiza,uchawi na mfano wa hayo tu ndio maana unadhani kwamba hayo uliyoeleza hapo juu umeipuka imani katika maisha yako.

Halafu pia unasema unadhurika na vinavyoingia mwilini mwako direct na kutaja sumu, sijajua hiyo ni sayansi ipi ikiwa kwamba nocebo effect na stress vinaweza kumsababishia mtu madhara pasina kuingia kitu mwili. Tafiti za kisayansi zilizofanywa kuhusu vifo vya watu kutokana na laana wameona kuwa chanzo cha vifo ni hofu ndio yenye kupelekea kifo.

Unaweza ukaacha kuamini mambo ya dini,Mungu, uchawi n.k ila sio kutokuamini kabisa hakuna mtu huyo.
 
Mkuu hii hoja haina uhusiano wowote na IMANI ya uchawi.

Turudi kwenye hoja………. Wewe binafsi ukiachana na porojo za kusikia kwa wengine, je umewezaje KUJIHAKIKISHIA uchawi upo?
Hiyo hoja inahusu uthibitisho na uthibitisho ndio wimbo mnaoimba sana hapa, sasa unaanzaje kusema niachane nayo wakati nakuonyesha tofauti ya uthibitisho na ukweli?

Wewe unatuambia hakuna uchawi kisa tu hakuna uthibitisho kwa maana umefanya kukosekana kwa huo uthibitisho ndio uthibitisho wa kutokuwepo huo uchawi, mimi nakwambia kukosekana kwa uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo na kwamba ukweli na uthibitisho ni vitu viwili tofauti.

Ndio maana nimetoa mfano wa meditation, sasa unaniambiaje haina uhusiano?

Halafu mimi sijaleta habari za kusikia kwa wengine bali naleta hoja hapa za mambo ambayo yana matokeo halisi ili tujadili kwa pamoja ili wote tuonyeshe ni kwa vp tumejiridhisha kuwa uchawi upo ama haupo.

Sasa ajabu watu mmekariri neno uthibitisho tu na wengine wanaonyesha wazi hawataki kabisa challenge kwenye msimamo wao wa kudai hakuna uchawi, wao washaamua tu kuwa hakuna uchawi basi.
 
Je uchawi upo au n saikolojia, jibu n uchawi upo ila ni saikolojia.
Uchawi sio jambo la kiroho, uchawi n kama kuogopa giza kwan kwenye giza kuna nn, au kuogopa ndoto kwan kwenye ndoto kuna nn, au kuogopa sanam kwan sanam ina uwezo wakukufanya nn, au bundi paka panya mjusi au mende ana athari gan kwa binadam au n stori za kubun zinazorithishwa kizazi had kizazi.
Mauzauza tunayohadithiwa anaye kuhadithia nae kahadithiwa na yanayoonekana n utukutu tu wakawaida kabisa au n vipaji akili au ujuzi wakawaida kabisa usio ujua ukaita uchawi.
Na madhara n hofu yako inayokudhuru mwenyewe.
Kuamin uchaw n kuchelewesha maendeleo, Ulaya wameanza kufuta iyo iman miaka ya 1400 had 1717,hapo ndio rasmi wakaanza kuendelea.
Ata iyo mifano ya kwenye bibilia ule sio uchawi yale n mazingaombwe yanayofundishwa vyuoni. Enz izo chuo kilikuwepo Misri ndo mana wakajiuliza Yesu mtoto wa Selemala hawez kwenda kusomea sasa kapata wap uwezo wa maajabu.
 
Shukran sana mkuu🙏
 
Back
Top Bottom