ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,478
- 41,419
- Thread starter
- #141
Karibu ☺️Asante!
Karibu ☺️Asante!
KaribuAsante!
Ahaa sawaHapana sio Mwanza!
Wizi na utapeli vimelala huko kwenye chaka la uchawi.So, unataka kufanyiwa practical 😂
Ni kua makini na haya mamboWizi na utapeli vimelala huko kwenye chaka la uchawi.
Sahihi kabisa.Nimewekea rejea ya vitabu vya dini kwa kutaka kuonesha kua hii dhana ya uchawi ni ya kale
Sio kweli. Fuatilia huko Denmark utafahamu kwamba kila tarehe 21 - 22 June kila mwaka huwa kuna zoezi la "kuwafukuza" au "kuwinga" wachawi na wanaamini kwamba wachawi konki wanatoka Ujerumani(Germany). Na shughuli hiyo ya kuwafukuzia wachawi warudi Germany walikotoka hufanyika usiku 21-22 June kwa kulipua fataki. Je, huko si ndiko Imani ilianzia au?Ajabu yake huko vitabu vya dini na imani vilipoanzia hawajishughulishi na hii dhana ya
Uchawi haukuundwa bali "ulifundishwa". Kama itakupendeza kajisomee kitabu cha Enoch(Henoko)sura ya 9 -12. Inaelezea habari ya Malaika walioasi na kushuka duniani n.k.n.k wakazaliana na mabinti wa Binadamu...uchawi kama huku africa
Kama unaweza kufanya mtu akupende na akakupenda je hakuna namna mzazi anaweza kufanya kutumia huo uchawi mtoto akashika no moja darasani
Yaani kwa faida maana umesema wanafaika wa uchawi ni wachawi wenyewe
Alieunda uchawi alikua hopeless kaunda kitu hakina manufaa zaidi ya uharibifu tu
Uchawi unaweza kuupata kwa kujinunulia, kurithishwa au kwa kupewa kwa "upendeleo" maalum. Ni wewe tu unatakaje - ila ujue kuna gharama.Mimi binafsi nikitaka kujiunga na wa chawi ili nipate hiyo cheap ya usafiri nawezaje?
Kikundi cha kikuda hiki hakina faida yoyote
Karibu brotherAsante mleta mada. Hii ni mada pana sana ambayo inahitaji fikra pevu, utulivu wa akili na utayari wa kusikiliza mitazamo tofauti ili kupata maarifa, ufahamu na elimu
Kaka nimeelewa visa vyako vyoteKwa mtazamo wangu, uchawi unaweza kueleweka kama imani au vitendo vinavyodhaniwa kutumia nguvu zisizo za kawaida ili kuleta matokeo fulani, kama kumdhuru mtu, kumlinda, kumshawishi au kubadilisha jambo fulani.
nimewahi kushuhudia na kusikia matukio ambayo, hata leo, yanaweza kuibua maswali mengi.
Mtu niliyemwona mlimani usiku
Kuna kipindi nilikuwa nasafiri kwenda Kahama. Ilikuwa usiku, karibu saa 7. Tulipopita eneo lenye milima, kwa macho yangu nilimuona mtu akiwa juu ya mlima. Alikuwa amevaa kaniki nyeusi, ameshika fimbo mkononi, na niliona macho yake kana kwamba yanatoa moshi.
Tukio hili lilinifanya nijiulize maswali mengi mpaka leo.
Je, nilichokiona kilikuwa kweli mtu? Je, mazingira ya giza, umbali na mwanga mdogo vilifanya macho yangu kutafsiri kitu fulani kwa namna tofauti? Au kulikuwa na jambo ambalo sikuweza kulielewa?
Mzee aliyedaiwa kuzuia mvua
Tukio jingine nililiona nikiwa bado mdogo kijijini.
Kulikuwa na Mzee ambaye watu walidai kwamba alikuwa na uwezo wa kuzuia mvua isinyeshe kwenye mashamba ya watu wengine, wakati mvua ilikuwa ikinyesha kwenye shamba lake.
Watu walipompelekea zawadi kama kuku, mchele au mbuzi, ndipo ilidaiwa mvua inaanza kunyesha kwenye mashamba ya wengine.
Mtoto nikiwa niliona tukio hili na kwa mtazamo wa wakati huo lilionekana kuwa jambo la ajabu sana.
Lakini leo najiuliza: Je, kweli Mzee huyo alikuwa anazuia mvua? Au kulikuwa na sababu nyingine za kimazingira ambazo watu hawakuzijua? Je, muda wa mvua kunyesha ulilingana tu na wakati zawadi zilipotolewa? Au kulikuwa na imani ya jamii iliyofanya watu waunganishe matukio hayo?
Tukio la Bibi mwenye nyumba
Kama miaka 12 iliyopita nilikuwa sehemu fulani kwa rafiki yangu. Tulikuwa tumekaa kwenye kochi baada ya kuangalia mpira, ilikuwa mechi za UEFA.
Baada ya mechi kuisha, ghafla nilianza kupitiwa na usingizi. Kichwa kikawa kizito, ndani kukawa na joto na nikajikuta nimelala pale pale kwenye kochi. Nilihisi kama napumua kwa nguvu na kwa shida.
Nilipofumbua macho, nilimuona Bibi mwenye nyumba akiwa amevaa baibui jeusi, jipya, amejipaka make-up na midomo yake ilikuwa imekolea rangi, huku macho yakiwa yamepakwa wanja.
Kwa mshtuko nilimtukana na kusema:
"Wewe mchawi! Huwezi..."
Ghafla, nikasema kana kwamba nilimwona akipotelea kwenye ile kona aliyokuwa amesimama.
Hili nalo ni tukio ambalo kwa mtu aliyelipitia linaweza kuwa la kutisha sana.
Lakini kuna uwezekano wa tafsiri mbalimbali. Inaweza kuwa nilikuwa katika hali ya mpito kati ya usingizi na kuamka, ambapo mtu anaweza kuona au kuhisi vitu kwa uhalisia mkubwa sana. Inaweza pia kuwa nilikuwa nimechoka sana baada ya muda wa usiku, na hali hiyo ikaathiri namna nilivyotambua mazingira.
Hivyo, tukio hilo ni la kweli kwa maana kwamba nilipitia uzoefu huo, lakini sababu yake haiwezi kuthibitishwa kwa kusema tu kwamba ilikuwa uchawi.
Dereva aliyepoteza uwezo wa kuona
Tukio jingine lilitokea maeneo ya Kakola, karibu na Mgodi wa Bulyanhulu, wakati fulani mwaka 2009.
Kulikuwa na jamaa aliyekuwa dereva wa daladala/baiskeli ambaye ghafla alipoteza uwezo wa kuona kwa macho yote; aliona giza.
Mke wake alikuwa Msabato, hivyo waliitwa watu wa kanisa na wakamuombea. Licha ya maombi hayo, hali yake haikubadilika wakati huo.
Baadaye zikaja taarifa kwamba kulikuwa na mganga wa jadi upande wa pili wa mlima. Jamaa huyo akapelekwa huko kwa baiskeli. Alipofika, akafanyiwa matibabu ya kimila na kuwekewa bangili mkononi. baada ya hapo alianza kuona tena.
Jamaa huyo mpaka nilipoondoka eneo lile hakutaka kusikia habari za Mungu; yeye aliamini zaidi kile alichokiita "Wakubwa".
Tukio hili pia linazua swali kubwa:
Je, kupona baada ya kwenda kwa mganga wa jadi kunathibitisha kwamba ugonjwa huo ulisababishwa na uchawi?
Katika kujadili huu mjadala kuna haya mambo matatu tuyaangazie na kuyaangalia
1. Tukio:
"Nimeona kitu."
2. Tafsiri:
"Nilichokiona kilikuwa uchawi."
3. Ushahidi:
"Naweza kuonyesha kwa namna inayoweza kuchunguzwa kwamba sababu ilikuwa uchawi."
Mara nyingi tunakuwa na namba 1, tunatoa namba 2, lakini tunakosa namba 3.
Ni vyema watu au binadamu tufike mahali tuwe wanynyekevu -tukubaliane kwamba pamoja na kuwa tunadhani kisayansi tumeendelea sana sana; lakini tukubali kwamba bado yapo mengi hatujaweza kumaliza katika Maarifa yote -bado yapo mengi sana hatujayagundua au kuyavumbua.ShesRise_1 Mi naamini tatizo itakuwa ni jina na ile dhana, kuna mambo yanayofanya uone kuwa huenda ikawa ishu ya kisaikolojia, mfano kuna ugonjwa mmoja wa kisaikolojia unaitwa (DID) dissociative identity dissorder au split personality hali hii inamfanya mtu anakuwa na personality zaidi ya moja ila ukiangalia kwa makini dalili zake kwa hapa africa tunasema ni kama mtu mwenye majini, hapo je ni wazungu wapo sawa kwamba huu ni ugonjwa tu na sio majini au sisi ndio tupo sawa kuwa yale ni majini na sio ugonjwa
Kitu chengine ni power ya energy na vibration ambayo kuna baadhi ya viungo hupona just kwa vibration ya mwili hii mpaka paka wanatumia ule muungoromo wanaotoa kama vibration fulani ni hali ya kujitibu au hata kuna kutuliza stress kuna kama hypnosis ya brain wave ambayo ni kama vibration ni inafanya kazi, hivi ndivyo ulimwengu unavyofanya kazi ni kucheza na frequency ya vibration pia hivyo ndivyo wachawi wanavyotumia ni frequency na vibration kwa kutumia maneno na nyimbo hii inakuwa the same ila moja tunaita ni imani za jadi ni ushamba ila nyingine ni sawa, mi naamini uchawi upo ila mapokeo yake ndio yanakuwa tofauti na approach zake ni tofauti ila conclusio ni moja, utumie maneno maalum (spelling,chants) au utumie meditation au utumie mathematics calculation hizi zote ni njia za ku utambua ulimwengu unavyo fanya kazi
Wewe tena short and clearHakuna uchawi.
Hakuna Shetani.
Sanahatari hii
We acha usanii unaelewa kabisa uchawi upo mpk ulitungiwa sheria. Biblia imeandika malengo ya uchawi ni kutesa, kuharibu na kuua.Hello jamii intelligence 👋
Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an
Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:
Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi
Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi
kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana
Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje
Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.
Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla
Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa
Sasa najiuliza...
Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?
Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?
Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?
Kuna hii pia👇
Ooh, wachawi wanapaa usiku...
Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?
Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa
Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?
Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?
Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu
Basi kuna mtu akamwambia mama:
Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔
Heh! 🤔
Nikastuka
Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?
Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine
Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.
Usiku naogopa kulala mwenyewe.
Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja
Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo
Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha
So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo
Mara nione hiki...
Mara nisikie kile...
Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?
Asieee!
Nikakaa nikasema:
Hapana, hizi mbona kama fix?
Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win
Nikaacha kabisa huo upuuzi
Nikaamua ku-clean akili yangu
Kuanzia hapo nikiambiwa
Njoo kwenye visomo
Nawaambia
Mimi sina tatizo lolote
Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu
Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku
Nikatumia zangu dawa nikawa fresh
Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu
Sioni mauza mauza wala nini
Naishi vizuri kabisa
Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu
Wala hakuna cha uchawi wala nini
Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake
Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...
Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?
Mashetani wana migodi yao huko?
Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi
Je, uchawi ni nguvu halisi?
Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?
Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...
Kwanini usitumike kinyume chake?
Au kama wachawi wanaweza kupaa...
Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?
Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?
ShesRise_1 ✋️
Mimi kwa mchango wangu ninaweza kushuhudia hiyo #1.Karibu brother
Kaka nimeelewa visa vyako vyote
Umesema kua hua kuna mambo ma 3
1 Tukio
2 Tafsiri
3 Ushahidi
Hiyo no 3 kimsingi ndiyo yenye mantiki
Tunaohoji kuhusu uchawi hua tunataka Ushahidi strong lakini ushahidi unakosekana mwisho mtu unaambiwa haya ni mambo ya rohoni
Kama wewe sio wa rohoni huwezi kuelewa
na hapo ndipo mjaadala unaanza kua mgumu na kukosa mvuto
Sasa nikuulize wewe una elewa vipi maana hapo ni kama umeongea kwa ujumla sana bro
So wewe hapa upo upande gani Dosho12 kwa wazungu au kwenye utamaduniShesRise_1 Mi naamini tatizo itakuwa ni jina na ile dhana, kuna mambo yanayofanya uone kuwa huenda ikawa ishu ya kisaikolojia, mfano kuna ugonjwa mmoja wa kisaikolojia unaitwa (DID) dissociative identity dissorder au split personality hali hii inamfanya mtu anakuwa na personality zaidi ya moja ila ukiangalia kwa makini dalili zake kwa hapa africa tunasema ni kama mtu mwenye majini, hapo je ni wazungu wapo sawa kwamba huu ni ugonjwa tu na sio majini au sisi ndio tupo sawa kuwa yale ni majini na sio ugonjwa
Sawa naweza kukubaliana na wewe kwamba uchawi upo na unaweza kutumika kwa hizi njia ulizozitajaKitu chengine ni power ya energy na vibration ambayo kuna baadhi ya viungo hupona just kwa vibration ya mwili hii mpaka paka wanatumia ule muungoromo wanaotoa kama vibration fulani ni hali ya kujitibu au hata kuna kutuliza stress kuna kama hypnosis ya brain wave ambayo ni kama vibration ni inafanya kazi, hivi ndivyo ulimwengu unavyofanya kazi ni kucheza na frequency ya vibration pia hivyo ndivyo wachawi wanavyotumia ni frequency na vibration kwa kutumia maneno na nyimbo hii inakuwa the same ila moja tunaita ni imani za jadi ni ushamba ila nyingine ni sawa, mi naamini uchawi upo ila mapokeo yake ndio yanakuwa tofauti na approach zake ni tofauti ila conclusio ni moja, utumie maneno maalum (spelling,chants) au utumie meditation au utumie mathematics calculation hizi zote ni njia za ku utambua ulimwengu unavyo fanya kazi
Mkuu, naomba hivyo vifungu vya malengo ya uchawi kwenye Biblia nijisomee tafadhali.We acha usanii unaelewa kabisa uchawi upo mpk ulitungiwa sheria. Biblia imeandika malengo ya uchawi ni kutesa, kuharibu na kuua.
Imani zilianzia Denmark?Sahihi kabisa.
Sio kweli. Fuatilia huko Denmark utafahamu kwamba kila tarehe 21 - 22 June kila mwaka huwa kuna zoezi la "kuwafukuza" au "kuwinga" wachawi na wanaamini kwamba wachawi konki wanatoka Ujerumani(Germany). Na shughuli hiyo ya kuwafukuzia wachawi warudi Germany walikotoka hufanyika usiku 21-22 June kwa kulipua fataki. Je, huko si ndiko Imani ilianzia au?
Uchawi ulifundishwa kwa manufaa gani?Uchawi haukuundwa bali "ulifundishwa". Kama itakupendeza kajisomee kitabu cha Enoch(Henoko)sura ya 9 -12. Inaelezea habari ya Malaika walioasi na kushuka duniani n.k.n.k wakazaliana na mabinti wa Binadamu...
Unauzwa wapi uchawi na gharama zake ni zipi?Uchawi unaweza kuupata kwa kujinunulia, kurithishwa au kwa kupewa kwa "upendeleo" maalum. Ni wewe tu unatakaje - ila ujue kuna gharama.
Huo uchawi ulianzishwa na nani?We acha usanii unaelewa kabisa uchawi upo mpk ulitungiwa sheria. Biblia imeandika malengo ya uchawi ni kutesa, kuharibu na kuua.