JamiiForums Usiku wa manane
Mastory ya Bey

NDIO MAANA WANAUME TUNAKUFA MAPEMA



Tangu tukiwa wadogo tumekuwa tukiambiwa wewe ni mtoto wa kiume Acha Kulialia jikaze, tangu lini umeona mtoto wa kiume analalamika hovyo! Haya na mengine mengi yamemjenga mtoto wa kiume kumeza machungu yake yeye mwenyewe pasina kuomba msaada Kwa watu wengine,kumemfanya kupambana na mitihani mbali mbali pasina kupata ushauri au muongozo toka Kwa watu wengine.

Na Hali hii tunakutana nayo huku ukubwani na kuendelea na mambo Yale Yale ambayo tumekuwa tukiambiwa tangu tukiwa wadogo. Matokeo yake vifua vyetu vimejaa mizigo mizito ivunjayo mbavu zetu,tumejawa na misongo ya mawazo,na hatujui wapi PA kupata msaada na ushauri,kwasababu nafsi zetu zinatusuta Kwa kutuambia Sisi ni wanaume hatupaswi kuomba msaada wala ushauri toka Kwa watu wengine.

Matokeo yake tunapata maradhi ya moyo na mengineyo kutokana na mizigo ambayo tumeibeba katika vifua vyetu,tunajikuta kutwa kucha Sisi ni watu WA stress Tu.

Sasa ukikuta mwanaume anaomba ushauri WA changamoto Fulani ambayo anakutana nayo basi jua kweli anahitaji msaada,kwahiyo sio Busara na sio vizuri kumwambia wewe ni mwanaume tatua changamoto zako mwenyewe au huo sio uanaume pambana na Hali yako.

Hapa tunakosea Sana,ifike kipindi tujue nasi ni wanadamu pia tuna hisia na tunapata changamoto pia,hivyo tuachane na zile fikra za kusema kuwa mwanaume inabidi ugangamale,mwanaume unatakiwa ukomae na shida zako,hapana tuna feli Sana tena Sana.

Ukiona mwanaume ima anatuma post humu na kuomba ushauri basi ujue yupo ktk changamoto kubwa Sana na kapambana mwenyewe na hakupata suluhu,kwahiyo na wewe usiwe sehemu ya kumuongezea tatizo.

Tofauti na wanawake wao ni watu ambao wanashea Sana mambo Yao na hivyo kuwafanya vifua vyao viwe vyepesi na kupata msaada pia,unajua wakati mwingine unacho hitaji ni kusikilizwa Tu,Kwa kufanya hivyo unakuwa umepunguza stress kiasi Kikubwa,sasa wanaume mambo hayo hatuna na ndio yanayo tupelekea kupata msongo WA mawazo na hatimaye kufa kabisa.

Kuwa wanaume haimaanishi kuwa tuishi kama robot au tupambane wenyewe Tu Bila kuomba au kupata msaada toka Kwa wengine laa hasha!
Nasi pia inafika kipindi data kichwani zinazima na kushindwa kutatua changamoto mbali mbali.

Nimekuwa inspired kuandika haya maudhui baada ya kuona baadhi ya wanaume humu kuwasemea kauli mbovu wanaume wenzao pale wanapokutana na changamoto mbali mbali nakutaka ushauri .

Tubadilike na kumfanya mwanaume aondokane na Mila na desturi mbaya ambayo huchangia anguko lake hapa duniani.
 
2309

NUKUU YA LEO:


"The measure of intelligence is the ability to change."
Albert Einstein

This quote emphasizes adaptability as a key sign of true intelligence—being able to adjust your thinking and actions in response to new information or situations.
 
LEO KATIKA HISTORIA

Leo, Mei 18, ni siku ambayo imejaa matukio muhimu ya kihistoria duniani. Hapa kuna baadhi ya matukio ya kipekee yaliyotokea siku kama ya leo:

---

🌋 1980 – Mlima St. Helens Wazuka Nchini Marekani
Mnamo Mei 18, 1980, Mlima St. Helens huko Washington, Marekani, ulizuka kwa nguvu kubwa baada ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 5.1. Tukio hili lilisababisha vifo vya watu 57 na kuharibu maeneo makubwa ya misitu na mazingira ya karibu. [1]

---

⚖️ 1896 – Uamuzi wa Plessy v. Ferguson
Mahakama Kuu ya Marekani ilitoa uamuzi maarufu katika kesi ya Plessy v. Ferguson, ikihalalisha sheria za ubaguzi wa rangi chini ya kauli mbiu ya "separate but equal" (tofauti lakini sawa). Uamuzi huu ulihalalisha ubaguzi wa rangi hadi ulipobatilishwa na kesi ya Brown v. Board of Education mwaka 1954. [2]

---

☢️ 1974 – Jaribio la Nyuklia la Kwanza la India
India ilifanya jaribio lake la kwanza la silaha za nyuklia, lililojulikana kama "Smiling Buddha," katika jangwa la Pokhran, Rajasthan. Tukio hili lilifanya India kuwa taifa la sita duniani kumiliki silaha za nyuklia. [3]

---

🌠 1910 – Dunia Yapita Katika Mkia wa Kometi ya Halley


Mnamo Mei 18, 1910, Dunia ilipita kupitia mkia wa Kometi ya Halley. Tukio hili liliibua hofu na msisimko miongoni mwa watu, huku wengine wakihofia sumu kutoka kwenye mkia wa kometi hiyo. Hata hivyo, tukio hilo halikusababisha madhara yoyote na lilisaidia wanasayansi kuelewa zaidi kuhusu kometi. [4]

---

🎂 Watu Maarufu Waliozaliwa Mei 18
  • 1920 – Papa John Paul II, kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Poland.
  • 1957 – Ai Weiwei, msanii na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka China.
  • 1970 – Tina Fey, mchekeshaji na mwandishi maarufu wa Marekani.
  • 1955 – Chow Yun-Fat, muigizaji mashuhuri kutoka Hong Kong. [5]

---
 
Back
Top Bottom