JamiiForums Usiku wa manane
Mazungumzo ya usiku

HAUNA HAJA YA KUJIFAHAMU SANA AU KUJIELWA SANA

Usipo jifahamu wewe ni nani,inakupa nafasi ya kuwa huru wa kufahamu zaidi kuhusu wewe binafsi,hautakuwa na mipaka ambayo kwa namna moja au nyingine itakuwa kikwazo kwako kujifunza zaidi na kujua mambo mengi zaidi

Kuna mambo mengi tunashindwa kuyafanya na kuya experience kwakuwa tayar tumeshajipa lebel kwamba sisi ni watu wanamna gani au wa hadhi gani

Matokeo yake lebel hizo tulizo jipachika zinakuwa mwiba kwetu kufanya mambo mengine kwenye maisha hata kama ni mambo ya kawaida tu

Mfano mtu maarufu,kwakuwa amejipa lebel ya umaarufu,basi kwa lebel yake hii,anaogopa kuonekana amepanda dala dala,au anaogopa kwenda restaurant za hadhi ya chini kwakuwa amejipa lebel ya umaarufu na ukubwa,matokeo yake anashindwa kuishi maisha mengine tofauti na yale ambayo lebel yake inataka aishi

Wakati mwingine watu wanashindwa kuacha maisha fulani ambayo wamechoka kuyaishi au hawayapendi tena kwa kuogopa kuacha lebel zao ambazo wamekuwa nazo katika maisha yao yote

Mfano,mtu labda amekuwa mlevi sana na anapenda wanawake,sasa kuna kipindi anataka ayaache maisha hayo,anaanza kuwaza ataanza vipi kuacha pombe ambayo ameizoea,je akionekana kaacha pombe,huenda ataonekana kafulia,je marafiki ambao hukutana nao kwenye ulabu si ndio atawapoteza kabisa!

Kwahiyo anaamini kabisa hapaswi kuacha ulabu kwakuwa anastahili kuwa na marafiki zake walevi,hii ni lebel ambayo amejipachika,hivyo lebel inakuwa pingu kwake ya kushindwa kubadilika na kuwa mtu bora zaidi

Hizi lebel ambazo huwa tunajipachika na kuziamini zinatufanya tushindwe kufanya mapya katika maisha yetu,zinatufanya tushindwe kupata uzoefu mpya katika maisha

Mfano naamini kabisa kuna watu ambao wanashindwa kutia maguu katika Mtaa wa Usiku wa manane kwakuwa wao wanaamini wapo kwa ajili ya nyuzi serious tu,au wanahisi kuwepo mtaa huu kutawafanya waonekane wanastress au hawana usingizi

Huenda wanatamani hata kukomenti kitu ila wanahofu na lebel zao ambazo wamejiwekea,ambazo zinawakumbusha mda wote kwamba "wewe kwa hadhi yako ambayo unajulikana huku jukwaani haupaswi kuwepo katika uzi wa usiku wa manane

Endeleeni hivyo hivyo na lebel zenu zinazo wafanya mshindwe kuishi maisha yenu halisi na kuexperience mambo tofauti katika maisha,wakati mwingine it's all about having fun and al that!

Team nzima ya Mtaa wa Usiku wa Maneno sisi tuendelee kuishi maisha yetu and let's enjoy kila moment ambayo tunakutana nayo katika maisha maadamu hatumuumizi wala kumkera mtu yoyote yule

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom