Mazungumzo ya usiku
KUWA MAKINI NA UNACHO KIAMINI
Mwaka 1988 akiwa katika chumba cha matibabu ya kisaikolojia mwandishi wa habar na mwanaharakati wa haki za wanawake Meredith Maran alimshutumu baba yake mzazi kuwa alimnyanyasa kingono
Wakati huo ndio huduma mpya ya repressed therapy ilikuwa imegunduliwa,ni huduma ya kutatua changamoto za kisaikolojia kwa kujaribu kuchambua au kupekenyua kumbukumbu ambazo zimejificha
Sasa iko hivi ubongo wetu huwa hauna jipya zaidi ya kuyafanyia kazi mambo ambayo tayar unayajua au ambayo yameshawahi kukutokea hapo zamani,kwahiyo mambo yoyote mapya ambayo yatakutokea sasa hivi katika maisha yako,basi ubongo wako utajaribu kutafuta data za zamani ambazo zinaendana na uzoefu mpya
Sasa toka awali mwanamama Meredith Maran hakuwa na uzoefu mzuri na baba yake,kwakifupi hawakuwa na mahusiano mazuri katika ukuaji wake
Pili,mahusiano yake na wanaume wake hayakuwa mazuri hivyo alikuwa na kila sababu kuwachukia wanaume
Na kibaya zaidi akiwa mwandishi wa habari alifanya utafiti kuhusiana na unyanyasaji wa watoto wadogo ambao watuhumiwa walikuwa ni wanaume
Na kwa miaka ile ya 1980's kulikuwa na kesi nyingi sana za unyanyasaji wa watoto,lakini kumbe hofu na kumbukumbu ambazo hazikuwa sahihi zilizo sababishwa na aina mpya ya matibabu ya repressed therapy ndio zilisababisha kuibuka kwa imani ambazo sio za kweli kuhusiana na unyanyasaji wa watoto
Ikagundulika kuwa kesi nyingi hazikuwa za kweli na matokeo yake kila mtoto alipofanyiwa hiyo therapy alisema alinyanyaswa kingono,baadae hao wataalamu wa hizo therapy walifungiwa leseni zao na wengine kufungwa kabisa
Tukirudi kwa Meridith Maran akajiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja na mwanamke mwenzake ambaye ni victim wa unyanyazaji wa watoto huko miaka ya nyuma,basi ndio akaathirika vibaya na kuamini Baba yake alimnyanyasa kingono
Ila baadae alikuja kujua amefanya makosa,na wakati huo tayar uharibifu mkubwa ulishatokea katika familia,alitumia karibia miaka miwili kuomba msamaha kwa baba yake na bahati mbaya baba yake alikufa kabla hajamsamehe
Kwahiyo kuwa makini sana na kile unachokiamini huenda sio kweli!
Mlinzi wa zamu!