JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Kalamu ya bey [zamani mazungumzo ya usiku]

IF YOU DO ME I DO YOU

Duniani pote ipo hivyo kile utachomfanyia mwenzako ndicho atachokufanyia pia.

Lakini bahati mbaya Sana huwa tunapenda kuwafanyia watu ubaya huku tukitarajia wao watufanyie vizuri kitu ambacho hata asili inakataa kabisa.

Formular ni moja tu, ukinifanyia jema nitakufanyia pia,ukinipenda nitakupenda pia,ukini dharau nitakudharau pia na listi inaendelea.

Uungwana ni kuwafanyia watu kile ambacho tungependa kufanyiwa Sisi pia, Kwa kufanya hivyo tutajihakikishia furaha na Amani siku zote.

Utakuta mtu anataka mke awe romantic kwake wakati yeye hajawa romantic Kwa mke wake! Je unarajia kupata nini sasa?

Na wanawake hivyo hivyo unataka Mme wake awe romantic kwako wakati wewe hujawa romantic Kwa Mume wako,je unarajia nini?

Always remember if u do me I do you

Unataka kuishi vizuri na majirani zako basi show love kwao na watashow love kwako pia, unataka kazini kwako kuwe sehemu nzuri ya kuishi wajali co workers wako nao watakujali pia.

Unaona mambo ni rahisi Sana lakini sijui kwanini tunapenda kuyafanya yawe magumu?

Ebu tuanze Leo kuifanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi na kumbuka mabadiliko siku zote yanaanza na wewe.

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom