JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Nipo macho dakika chache zilizopita manjuu masoud masoud alikuwa akielezea historia ya muziki wa uud wa zain al abedeen,mzaliwa wa lamu
 
04:55 I was here 🙂

I swear to my dead body
simwamini rafiki anaenilipia kodi
huenda anafurahi mi kumpigia hodi
Akinipenda MUNGU inatosha!
 
Mazungumzo ya usiku

WOTE HUWA TUNAPITIA NYAKATI NGUMU

Wakati mwingine unaweza kujihisi ni mtu ambaye una mikosi sana,kila unalopanga haliendi na kila unalo litaka haliwi vile unavyotaka wewe

Kumbuka kwamba wewe unapanga na Mwenyezi Mungu nae anapanga,hakika maamuzi ya Mungu yana hekima zaidi anajua lipi lina manufaa na wewe na kwa wakati gani


Wahenga waliamini zaidi katika mipango ya Mola wetu,pale wanapoomba kitu fulani wakapata hufurahia mara moja,na pale wanapoomba na kukosa walichotaka walifurahi mara mbili,kwakuwa wanajua Mwenyezi Mungu ana mipango bora zaidi

Tambua kwamba ambalo lilipangwa ulikose usingelipata na lile ambalo lilipangwa ulipate usingelikosa kamwe

Kwahiyo endelea kuomba,kuna msemo mwingine unasema ukiwa unaomba na hukupata bado basi tambua mda wa maombi bado hauja kwisha kwahiyo endelea kuomba

Na unapoomba kuna code moja,ukiomba usitie shaka juu ya rehma ya Mwenyezi Mungu,pale itakapopita moyoni mwako tu,kwamba hivi kweli Mungu atajibu maombi yangu?,basi hapo umebatilisha maombi yaani kama ni simu basi ni wrong number

Issa bin Mariam alisema lau mtu angekuwa na chembe ndogo ya imani basi angahamisha milima

Endelea kujipa moyo na ipo siku moja kitaeleweka,kumbuka Prince Charles alisubiri kiti cha ufalme kwa miaka 70,sasa hivi ni mfalme


Trump alisubiri awamu nyingine ya Uongozi na sasa hivi ni raisi ingawa anaendelea kutunyoosha

Etugrul bey kaomba awe verified tangu mwaka jana mwezi august 2024 na aka update tena november 5 2024,lakini mpaka leo hakijaeleweka hahaha,naendelea kusubiri kama King Charles

Kwahiyo msomaji wangu trust me wakati wako unakuja kikubwa kuwa na imani,subir na endelea kuamini ndoto zako zitatimia

Mlinzi wa zamu!
 
03:00 I was here 🙂

When life gives you lemons, make orange juice and surprize everyone!
 
Back
Top Bottom