JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya usiku

UKIAMUA KUWA MWANAHARAKATI BASI WAFIKIRIE WAPENDWA WAKO


Tupo kwenye wimbi kubwa la kisiasa hapa nchini,wimbi ambalo linaweza kumsomba yeyote ambaye atajaribu kuvuka mbele yake

Ukiwa na tahadhari yamkini unaweza kuvuka salama lakini ukijafanya jabari na mwenye kujiamini zaidi huenda usivuke salama kwakuwa hakuna ajuaye kina cha bahari kikoje

Hapa tulipo fikia haijulikani wanao fanya kazi kwa niaba ya dola ni wapi na wanao jifanya wao dola ni wapi,hivyo hala hala na nafsi yako


Kunguru muoga huficha mbawa zake,najua kwa baadhi yenu Etugrul bey anaweza kuonekana ni muoga,lakini ni bora aonekane muoga ili familia yake na watoto wasimkose baba,kwani hakuna aliye shujaa mbele ya dola

Kwahiyo wakati unafanya harakati zako ebu wafikirie walio nyuma yako,je wataathirika kiasi gani baada ya kukumbwa na wimbi hilo ambalo mda wowote lipo mawindoni

Kuna maisha baada ya siasa,kuna wapendwa ambao wanakutegemea na wanakuhitaji uwepo nao kuwa ongoza na kuwalea ili nao siku moja watimize ndoto zao

Kumbuka uhai wako una thamani zaidi kuliko siasa za msimu,walikuwepo mashujaa wengi lakini leo hawapo tena kwa kile kinachoitwa siasa

Kumbuka siku zote kunguru muoga huficha mbawa zake

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom