Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 12,981
- 25,624
Mazungumzo ya usiku
TUJENGE TABIA YA KUWASHUKURU NA KUWAPA SIFA WATU WETU WA KARIBU
Ni mara nyingi sana kama sio zote huwa tunawapa hongera na kuwakubali sana wanasiasa na watu mashuhuri kwa mambo wanayo yafanya iwe ya kisiasa au kijamii na mambo kama hayo
Pamoja na kuwakubali na kuwasifu kwa namna moja au nyingine ila wao hawatufahamu wala hawatujui,wanatuona ni watu tu miongoni mwa kikundi cha watu,kwahiyo kuna haja gani ya kuwapa kipaumbele sana
Lakini bahati mbaya sana,kuna watu ambao wapo kwenye maisha yetu ya kila siku,na wanamchango mkubwa kwetu lakini huwa hatuwapi sifa wanazo stahili
Dada wako wa kazi anasafisha nyumba yenu,anawapikia chakula,saa nyingine huwatayarisha watoto kwa kwenda shule,lakini haijatokea hata siku moja,ukampa sifa anayo stahili akajisikia vizuri na kuona mchango wake unatambulika
Wale wenye walinzi,mnajua jinsi kazi ya ulinzi ilivyo ngumu na ina risk kubwa,je mmeshawi walau mara moja moja kuwaambia ni kiasi gani mnajivuna kuwa nao hapo nyumbani?
Madereva wa serikali ni watu ambao kutwa kucha wapo na maboss wao tu,saa nyingine hadi wikiend,je nyie maboss mmeshawahi walau kuwapa maneno mazuri ya kushukuru kwa huduma yao?
Mlinzi wa zamu ninachotaka kusema ni kwamba,tujenge tabia ya kuwapenda na kuwapa sifa pia watu ambao wanatuzunguka na ambao wana mchango mkubwa sana katika maisha yetu
Tukiwaonyesha kwamba tunajivunia kuwa nao na tunatambua mchango wao,hakika itawapa hamasa kubwa sana ya kujituma zaidi na kufurahia majukumu yao
Mlinzi wa zamu!