JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya usiku


UNAPOPATA MATATIZO HUWA UNAKIMBIA AU HUWA UNAPAMBANA NAYO


Mwaka 2008 Taliban walichukua utawala wa pakistani kimabavu na kuweka utawala wao wa sheria,ikiwemo kuzuia matangazo ya television,hakuna sinema,hakuna wanawake kutoka nje ya nyumba zao bila kuongozana na mtu wake wa karibu kama baba au kaka

Na istoshe wakazuia wanafunzi wa kike kuendelea na elimu,lakini binti mmoja anaitwa Malala mwenye umri wa miaka 11, yeye alipinga uamuzi huo,na kuamua kuhudhuria shule kama kawaida,na alikuwa mstari wa mbele kupaza sauti na kupigania haki ya watoto wa kike kwenda mashuleni

Mnamo mwaka 2012 akiwa anatoka shule na wenzake,mara paap wakasimamishwa na askari wa taliban,akiwa amebeba silaha au bunduki,na kuwauliza abiria waliokuwa mle ndani ya basi,kwamba nionyesheni Malala

Kwa mshangao mkubwa na ujasiri Malala akajitambulisha mwenyewe,na hapo hapo yule gun man akampiga Malala risasi ya kichwa,na wakasema kwamba kama binti huyo atapona basi watamuua yeye pamoja na baba yake

Lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu alipona na kuendelea na harakati zake kama kawaida,kwa hali ya kawaida tungetegemea angeogopa na kuacha harakati zake,lakini binti wa watu kwa ujasiri mkubwa kabisa,ndio kwanza alipata hamasa na nguvu mpya ya kupigani haki wa wanawake na kuwa msemaji wao

Kutokana na jitihada zake mnamo mwaka 2014 alipata Tuzo ya Nobel na kutambuliwa mchango wake katika jamii

Je wewe ni aina ya watu kama Malala ambao huwa hawa quit pale wanapo kutana na changamoto Au ndio changamoto kidogo unakata tamaa na kukimbia

Ngoja nikwambie kitu msomaji wangu,hii dunia inahitaji watu ambao wapo strong enough to fight back,watu ambao huwa wanasonga mbele daima na kurudi nyuma kwao ni mwiko

Hata wewe pia unaweza kuwa imara na madhubuti kama Malala.

Mlinzi wa zamu!
 
00:15
02nd May, 2025 I was here 🙂



"She asked me when can we meet again? I answered when the war is over. She asked when will the war be over, I answered when we meet again.
 
00:37 I was here 😉

"We we're only lovers before the love came in"

Ayra Starr & Omah Lay - Beggie
 
01:00 I was here 🙂

Dondoo
1. Usipolala/ukikosa usingizi kwa siku 10 mfululizo inaweza kupelekea kifo!

2. Unaweza kupatwa na hali ya kuamka huku ukiwa umelala, hivyo unakuwa umeamka lakini huwezi kufanya chochote hali hii huitwa sleep paralysis!

3. Tunatumia zaidi ya 25% ya maisha yetu kulala, tunalala muda mrefu ili kurejesha sehemu ya nishati iliyopotea, kupumzisha viungo muhimu mf. macho, kutoa nafasi ubongo na mwili utengeneze seli mpya!
 
01:11 I was here 🙂

Healing energy
Healing energy
All I really need is one thing
Healing energy on me
When it's 01:11 🙂
 
01:22 I'm blessed 🙂

Tumaini la wanyonge, kwamba ipo serikali,
Ile nchi ya mazonge, ya wenye meno makali,
Wanyang'anyao matonge, wanyonge hawana hali,
 
02:20 I was here 🙂

Kitu chenye ladha mbili, kitamu kuliko vyote na kichungu kuliko vyote nilivyowahi kuvionja ni kimoja tu, MAPENZI!

signing out until we meet again.
 
Back
Top Bottom