JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya usiku

MARA ZOTE HUWA TUNAFANYA MAAMUZI


Leo hii ukilazimishwa kufanya mazoezi na mzazi wako,hakika utaona ni maumivu makubwa na utajihisi unaonewa ingawa ni kwa faida yako mwenyewe

Lakini

Ukiamua kwa hiari yako kufanya hayo mazoezi utajituma na utafurahia kwa kuwa umechagua mwenyewe kufanya hivyo

Kwahiyo siku zote huwa ni watu wenye kufanya maamuzi ya kutafsiri mambo hata kama yametokea nje ya uwezo wetu au maamuzi yetu,mfano ule mfano wa mazoezi,pamoja na kwamba umelazimishwa kufanya na mzazi wako,lkn una maamuzi ya kuyatafsiri kwa namna mbili

Ama utafsir kwamba ni jambo zuri la kiafya ambalo mzazi wako anataka uwe na afya nzuri au utafsiri kwamba ni adhabu kwako

Ebu twende katika mfano wa maisha halisi:

Anaitwa William James,ametoka katika familia bora yenye kujiweza kiuchumi,lkn pamoja na hayo,huyu mwamba alizaliwa akiwa na changamoto nyingi za kiafya

Alikuwa na tatizo la macho ambalo lilimpa upofu wa mda,akawa na matatizo ya kusikia,alikuwa na changomoto ya uti wa mgongo kiasi kwamba wakati mwingine alishindwa kukaa au kutembea kwa siku kadhaa


Alishindwa kuendelea katika masomo,alishindwa kufanya jambo lolote,alionekana lazy katika familia,kibaya zaidi mdogo wake Henry James alikuwa mwandishi wa riwaya alifanya vizur sana katika kazi yake

Mdogo wake Alice James nae alikuwa mwandishi,alifanya vizur na kuishi kwa kutegemea kazi yake

Baba yake na William kwakuwa ana connections na maguru,basi akamfanyia mpango akajiunge na shule ya masomo ya utatibu pale Havard,na akaambiwa kwamba akifeli this time atajijua yeye mwenyewe

Baada ya miaka kadhaa pale Chuoni,alishindwa na kurudi mtaani,akiwa hana hili wala lile,na alikata tamaa na kutaka kujiua kwakuwa alijiona amefeli maisha

Siku moja usiku akiwa anasoma lectures za profesa mmoja,akakutana na somo ambalo linasema lolote linalo mtokea mwanadamu ni kutokana na maamuzi yake

Rejea mfano kule nyuma nilisema ni kwa namna gani tunafanya maamuzi ya kutafsiri matukio kwa yale yanayo tutokea ndio itatufanya tuwajibike kwa namna moja au nyingine

Basi akaamua afanye majaribio ya somo lile,akadhamiria kwamba ataishi kwa mwaka mmoja akiamini kwamba yote yalitokea katika maisha yake lilikuwa ni kosa lake,na baada ya huo mwaka mmoja kama hali haitabadilika basi atakatisha maisha yake

Mwisho wa siku William James alijulikana kama Baba wa Filosofi nchini Marekani,alipewa heshima kama msomi,mwanasaikolojia,mwanafilosa

Alienda kutoa lecture Havard University,na Vyuo mbalimbali Marekani pamoja na Ulaya

Tambua kwamba siku zote huwa tunafanya maamuzi,hata kwa yale mambo ambayo yapo nje ya uwezo ila bado tunafanya maamuzi

Ni kwa kiasi gani utatafsiri yale yanayo kutokea na kuchukua maamuzi ambayo yatakuathiri au laa iko juu yako

Mfano umeachwa na mpenzi wako,una mambo mawili ama uchague kulialia na kupata msongo wa mawazo na kushindwa kufanya majukumu yako ya kila siku

Au

Utafsiri kwamba huyo hakuwa mtu wako wa kudumu alipita kwako akupe uzoefu fulani kisha utakutana na mwenza wa maisha yako

Hapo utaona kwamba always huwa tunafanya maamuzi

Mlinzi wa zamu!
 
00:40
Wanachama wenzangu naomba mnisamehe kwa kutoroka kwa mda kwenye hili jukwaa la usiku wa manane.
Nakili kosa na sitorudia tena kupotea kwenye jukwaa hili.
ASANTENI.
 
Back
Top Bottom