JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Maisha ni yako,we endelea kuogopa midomo ya watu...
Fanya kinachokufurahisha na kukupa amani ya moyo
 
04:20 I was here

Labda mwezi unavutia sababu uko mbali!

Labda nyasi huwa za kijani sana zikiwa ni fake!
 
Mazungumzo ya usiku



WAJIBIKA KWA MAKOSA YAKO


Mara nyingi au kama sio mara zote huwa hatupendi kuwajibika kwa makosa yetu ila huwa tunapenda kuwalaumu wengine kwa makosa yetu,kwa kufanya hivyo tunadhani tunajifariji kumbe tunajidhuru wenyewe

Ebu soma mfano huu,bwana Etugrul bey baada ya kuachwa na mpenzi wake ambaye aliamua kuanzisha mahusiano mengine,Etugrul bey alimlaumu sana ex wake kuwa ndio sababu ya kuvunjika kwa uhusiano huo

Na kibaya zaidi akaenda mbali zaidi kumlaumu kwa maumivu ya kuachwa anayoyapata,akamlaumu kwa kukosa furaha,amani na utulivu

Lakini baadae baada ya kukaa chini na kutafakari kwa kina,Etugrul bey akagundua kwamba kumbe hata yeye alichangia sana mahusiano yake kuvunjika,na bahati mbaya zaidi hakusoma mapema alama za nyakati au kugundua viashia ambavyo ex wake alivionyesha kuashiria kwamba hakuwa na furaha katika mahusiano hayo

Baada ya Etugrul bey kuchimba na kuchimba zaidi akagundua hakuwa akimjali ex wake kama alivyopaswa kujali,alikuwa na majivuno na hakumpa ex wake attention ambayo alipaswa kumpa,hapo akatambua moja kwa moja kumbe nae ni sababu ya mahusiano hayo kufa

Lkn aligundua kwamba pamoja na kuachwa,ex wake hakuwa ni sababu ya yeye kukosa amani na furaha,hakuwa sababu ya yeye kukosa usingizi usiku na hakuwa sababu ya yeye kuwa na stress

Baada ya kufikiria kwa undani zaidi akajua kwamba pamoja na kuachwa,kumbe ilikuwa ni wajibu wake kufikiri na kuyachukulia mambo katika namna ambayo ingekuwa na manufaa kwake,angechukualia kuachwa huko kama namna moja ya kujifunza na kujua mapungufu yake next time awe mtu bora zaidi

Kwahiyo baada ya kuyajua hayo yote,bwana Etugrul bey ameamua sasa kuwajibika kwa yote yaliyotokea,ameamua kuwa mtu bora zaidi na amejifunza kutoyachukulia mahusiano poa,na atakuwa tayar kuhakikisha makosa ya zamani haya jirudii tena.

Watu wengi huwa tunadhani tunapaswa kuwajibika kwa mafanikio na furaha yetu tu, lakini hatujui kwamba tutapo wajibika kwa matatizo yetu itatupa nafasi ya kujifunza zaidi na kua watu bora,na istoshe matatizo hutuimarisha zaidi

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom