MAZUNGUMZO YA USIKU
HISIA ZINAPEWA UZITO SANA
Hili ni tatizo kubwa,tujue kwamba hisia zipo kwa ajili ya kutupa mrejesho wa mambo na kutufanya tujisikie vizuri kwa kipindi fulani,kwa maana hauta jisikia vizur mda wote
Hisia huwa hazidumu ndio maana unaweza kujisikia vizur sasa hivi lkn baada ya mda fulani ile furaha au hisia za furaha uliyokuwa nayo inapotea,na unaweza ukawa na hisia za huzuni sasa hivi na baaada ya masaa kadhaa hiyo huzuni ikapotea
Na hisia ni kama kiashiria cha kutuambia kitu fulani kiko sawa na kitu hakiko sawa,ambacho hakiko sawa ukitafutie ufumbuzi na ambacho kiko sawa endelea kukiboresha zaidi
Mfano katika mahusiano ,hisia mbaya huwa ni ishara inayo kwambia kwamba haya mahusiano sio mazuri,ndio maana kila mara unapata hisia ambazo hazikupi furaha,maana yake unapewa ujumbe ebu tatua hili tatizo ambalo linakufanya ujisikie huzuni au vibaya katika mahusiano yako
Na hisia nzuri katika mahusiano zinakupa ishara kwamba huu uhusiano ni wa kuupigania kwasababu unakufanya ujisikie vizur,kwahiyo kama ulikuwa unauchukulia poa basi ebu jitahidi kuuboresha zaidi
Kama vile ambavyo unapata maumivu baada ya kidole chako kugusa moto,hayo maumivu yanakwambia next time uwe muangalifu zaidi,na hisia za huzuni zinakwambia just try to fix something chap
Kwahiyo kwakuwa hisia ni zenye kubadilika badilka basi usifanye maamuzi tu kwa kutumia hisia peke yake utafeli amigo,bali fanya maamuzi kwa kutumia akili pia,na kwa kufanya hivyo utafanya maamuzi sahihi siku zote
Anayehitaji kufanya maamuzi kwa hisia tu ni mtoto wa miaka mitatu au mbwa,unajua kwanini kwasababu hawana cha kufanya zaidi ya kushit katika kochi au kitanda
Kwahiyo jua kwamba hisia hubadilika,na haimaanishi kitu kinachokufanya uhisi vibaya sasa hivi ni kibaya,bali unaweza hisi vibaya lkn kitu hicho kikawa kizuri,na unaweza kuwa na hisia fulani juu ya kitu fulani kuwa ni kizuri lkn ukweli wa mambo kitu hicho sio kizuri
Ndio maana inasisitiwa fanya maamuzi kupitia hisia pamoja na reason
Mlinzi wa Zamu!