JamiiForums Usiku wa manane
Bado kuna terminology nyingi sana kule Jeshini. Kuna moja inaitwa all fire available. Huwa inatolewa pale ambapo unagusa maslahi ya maisha yao na wakati hawana namna ya kufanya zaidi ya kujiokoa. Usiombe siku hiyo ikuangukie!

Pale ambapo utamteka unaweza ukapata hasara usiyoihitaji. Kwa hiyo basi "Usilitaje bure jina la Maserati, maana siku ukimteka ghadhabu na adhabu zitakuwa juu yako!"
 

Mwanafunzi wako mzembe kweli kweli, tangu nimpe chemsha bongo ndio katoweka kabisa na hataki kukusanya, anakuja kuchungulia na kuondoka. Tena akiniona ni nduki kama Usain Bolt
Hahaha tatizo lako siku ya kwanza ulikua na mikwara mingi, Mara umeingia darasani na rundo la bakora
Mwanafunzi wangu ni kichwa sana usipomtishia na bakora
 
df6cf741dc379255d94920e8823ae81e.jpg
 
alafu sio xmas
CHRISTMAS ni MUUNGANO wa maneno mawili yaani *CHRIST + MAS.*

Hapo zamani, siku ya Tarehe 25 December, ilikua siku ya Kusherehekea MATAMBIKO YA KIPAGANI kabla MWANA WA MUNGU, YESU KRISTO hajazaliwa.

Baadae mwaka 533 AD, Mtakatifu Constantine, aliyekua Mkuu wa Kanisa la WARUMI, ambalo siku hizi linajulikana kama Kanisa la Katoliki (Kanisa la kwanza), aliibadili siku hiyo isiwe tena ya MATAMBIKO YA KIPAGANI badala yake siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa MKOMBOZI MWANA WA MUNGU YESU KRISTO na kuiita *Siku ya kusanyiko la KRISTO* yaani *CHRISTMAS.*

1. *CHRIST* ni neno la kiingereza ambalo tafsiri yake ni KRISTO yaani MASIA au MPAKWA MAFUTA au ALIYETENGWA KWA KAZI MAALUMU.

2. *MAS* ni neno la KIYUNANI ambalo maana yake ni *KUSANYIKO.*

Kwa hiyo maana ya neno CHRISTMAS ni *KUSANYIKO la KRISTO.*

Kwa *WAKRISTO* wanaoamini siku hiyo, wawe makini sana na neno *X-MASS!.*

Inaaminika kuwa, baada ya siku hiyo ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO, kupata umaarufu, neno X-MASS, lilikuja baadae sana na lililetwa na wapinga KRISTO ambao waliamua kufuta neno *CHRIST* kwa kuweka alama ya *“X”* yaani hakuna KRISTO.

Hiyo ilibadili maana kwa kusomeka *X-MASS.*

X-HAKUNA na MASS-KUSANYIKO, hivyo X-MASS, maana yake ni HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO! Yaani HAKUNA CHRISTMAS!
Sasa, Kama wewe ni Mkristo hutakiwi kutumia neno X-MAS, badala yake tumia neno CHRISTMAS

MUNGU awabariki muwe na maandalizi mema ya *CHRISTMAS* na sio *“X-MASS!”*
 
Back
Top Bottom