Nimefungua uzi huu kutokana na kuwa na janga la kukata usingizi usiku. Kama na wewe ni mmojawapo naomba tuungane pamoja hapa kwa kuandika ulipo na unafanya nini kwa wakati huo baada ya kukosa usingizi.
Muda wa jukwaa ni kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 asubuhi. Mimi hapa leo tangu nimeamka nimeamua KUFANYA IBADA Tuuuu!
tatizo la kukosa usingizi isomnea husababishwa na mambo yafuatayo
mawazo :msongo wa mawazo hufanya mtu kukosa usingizi hivyo hutumia muda mwingia kuchanganua baadhi ya mizunguko na changamoto za maisha. mawazo ni adui mkubwa sana kwenye afya ya akili mpka ya mwili na tabia kwa ujumla
matumizi ya computer ama simu: matumizi ya simu ya muda mrefu ni tatizo kwa kuipa kazi kubwa macho pupil na cornea ya jicho kucontrol mwanga ivo basi kukaa kwa muda mrefu kwny screaan ama tv huleta changamoto kubwa kumaintain muda wa kulala
Madawa/chemical : zipo dawa amabazo husabisha mtu kutokupata usingizi nazo n mirungi , caffein ,kahawa energy drink hizo humfanya mtu kutopata usingizi na kufanya misuli kuwa active wakati ili mtu alale anahitaji misuli irelax na mwili kuwa at rest ndo hupata usingizi
Maumivu makali /pain:Yapo magonjwa yanayoleta maumivu makali muda wote mfano cancer ,dental diseases ... maumivu makali hufanya mtu kutopata usingizi
Upweke |sonona huu n ugonjwa mkubwa kwa wali waliozoea kulala pembeni mwa wenzi wao wanapokua mbali hupata shida kupata usingizi
Makelele : kelele ni sauti ambazo hazipo kwenye mpangilio maalumu hivyo bac huleta sauti mchanganyiko ambazo huumiza ngoma ya sikio na kuleta kuchanganyiwa distabance
mwisho usingizi n bora kwa afya ya ubongo