Unazijua sababu zilizopelekea ikateuliwa? Na mzozo mkali uliofuatia?
Ipo hoja kwamba lahaja ya Kiunguja iliteuliwa na Waingereza ili kukiharibu Kiswahili kwa makusudi na kukiondolea ubantu wake hasa katika msamiati. Lahaja hii ndiyo ilikuwa imeathirika zaidi na maingiliano na Kiarabu kuliko lahaja zingine zote (Unguja yalikuwa makao makuu ya himaya ya Mwarabu). Kama lahaja za huko Lamu zingeteuliwa Kiswahili leo kingekuwa na sura tofauti sana kuliko hiki Kiunguja kilichosheheni maneno ya Kiarabu mpaka kupelekea wengine kuhoji kama Kiswahili kweli ni lugha ya Kibantu.