Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Huyu anaota anataka kuamka tajiri sio! ila uwezekano upo maana Zitto hatabiriki sasa!
 
Chadema will you donate Zito to NCCR-Mageuzi? Will you do that for free?
If you will need money, how much do you think you have to be paid?
OR YOU WILL DONATE HIM FOR FREE AND also PAY NCCR ACCEPTANCE FEE?

A woman can be strong, confident and sexy
 
Zitto Zuberi Kabwe, mshamba kutoka Kigoma kwenye udongo mwekundu uliojaa viroboto vinavyosababisha funza. Amekuja tukampandisha chart, akawa mwanasiasa celebrity, akalanawili, akajulikana, tukadhani atatutumikia kuleta mageuzi, maskini ya Mungu, sasa amenunuliwa na mafisadi kwa milion 900!
Will we trust hawa 'marveric, firebrand, excitinf, intelligent opposition again?
1. Dr Lamwai
2. Dr Kabouru
3. Hiza Tambwe
4. Ngwaiya, etc.

The society full of betrayors cannot look into the future, period!
 
Mbatia alipelekwa nje kusoma na kugharimiwa na Rostam, Kuhusu Zitto kugharimiwa na Rostam, sina uhakika lakini ni kawaida kwa RA kumwagilia miche yote maana hana hakika na utakao chipua!! Lipumba, Mrema, Mtikila,Mbatia nk wote wako kwenye payroll yake.[/QUOTE]

Kuna mmoja umemsahau hapa. Na mkiendelea na huu ujinga, uvumulivu una mwisho.....

omarilyas

Kaka Omar nani huyo ambae amesahauliwa...? Mtaje wajulikane mapema... Wengine wanajulikana humu wao hupuliza, then wanaenda kwa mafisadi kuchukua mzigo...!!!
 
Kuna mmoja umemsahau hapa. Na mkiendelea na huu ujinga, uvumulivu una mwisho.....

omarilyas

Omar sema ... sema usiogope sema

Omar sema ... sema usiogope sema

Omar sema ... sema usiogope sema

Omar sema ... sema usiogope sema

Omar sema ... sema usiogope sema
 
Edward Kinabo

WATANZANIA wenzangu, kwa kawaida huwa sipendelei sana kujadili watu na inapotokea nikafanya hivyo, basi anayejadiliwa ni mtu ambaye kwa majukumu ya cheo chake, ana dhamana kubwa katika ama kuboresha au kuangamiza mustakabali wa taifa hili maskini.

Leo nimelazimika kumjadili Zitto Kabwe kwa minajili hiyo.

Kama si wote, basi wengi wenu mnamfahamu Zitto. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho.

Nikiri kuwa mimi ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa kijana huyu. Mbali ya kuwa kijana mwezangu na mwanaharakati mwenzangu, nimekuwa nikiguswa na uwezo wake wa kujenga hoja pamoja na misimamo yake katika baadhi ya masuala ya kitaifa, kabla na baada ya kuwa mbunge. Kama Watanzania wengine wengi, nami nilisisimka sana, pale aliposimamia ile hoja ya mgodi wa Buzwagi iliyompatia umaarufu baada ya kusimamishwa ubunge.

Kwa nafasi yake kama kiongozi wa juu wa moja ya vyama vikubwa vya upinzani nchini (CHADEMA), nimekuwa nikiitazama karama yake ya kisiasa, kama nyenzo ya kukiimarisha chama chake, ili kuwapatia Watanzania chama imara kabisa cha upinzani, kinachoweza kuwatetea na kuwapigania dhidi ya ufisadi na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, kwa umri wake kama kijana (33), nimekuwa nikimuona Zitto kama mfano wa kuigwa (role model) na vijana wenzake, katika kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya kisiasa, si tu kwa kugombea ubunge kama yeye (Zitto), lakini pia kwa kushiriki kujiandikisha, kupiga kura na kuzilinda kura hizo, ili kujipatia viongozi bora wanaoweza kutatua matatizo yaliyopo kwa haraka, likiwamo lile tatizo maarufu la vijana - ukosefu wa ajira.

Hata hivyo, ndani ya kipindi cha miaka miwili hivi au zaidi, nimekuwa nikishindwa kuielewa baadhi ya misimamo inayotolewa na mwanasiasa huyo, hususan ile inayotofautiana kabisa na kauli za viongozi wenzake pamoja na mwelekeo wa chama hicho, ambacho pasipo shaka yoyote ninakijua vema. Leo nitagusia machache.

Matukio ya hivi karibuni ya aliyekuwa kada wa CHADEMA, David Kafulila, kuondolewa katika nafasi ya uofisa habari wa chama hicho na baadaye kujivua uanachama wake na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi, pasipo kutarajia, yamenifanya nishindwe kumuelewa Zitto. Ndiyo, simwelewi Zitto Kabwe!

Ni matukio yanayomhusu Kafulila, lakini nimeshindwa kumwelewa Zitto, kwa kutilia maanani yafuatayo:

Kwanza, izingatiwe kuwa Kafulila aliondolewa katika nafasi hiyo kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Utovu wa nidhamu wa Kafulila ulijionyesha dhahiri katika vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti, pale alipokiita kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na wakurugenzi kilichoketi Dodoma mwezi uliopita, kwamba si kikao rasmi, hakitambuliki kikatiba - ni kikao cha ghetto. Ghetto kumezoeleka kuwa ni makazi ya vijana wasio na hulka njema – ni pango la wahuni.

Kukiita kikao cha viongozi wa juu wa chama kuwa ni kikao cha ghetto, hakuhitaji digrii kujua kuwa huo ni utovu wa nidhamu.

Mbali na utovu huo wa nidhamu, Kafulila pia hakuwa mkweli alipodai kuwa kikao kile hakikuwa rasmi. Kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa CHADEMA, kama zilivyobainishwa katika Katiba ya chama hicho toleo la mwaka 2006, viongozi wa sekretariati ya chama hicho wana uhuru wa kukutana kila inapobidi, iwe ni kwa utaratibu wa kawaida, kwa mahitaji au kwa dharura.

Wakati Kafulila akiwa ameondolewa katika nafasi hiyo na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kwa sababu ya utovu wa nidhamu ulio dhahiri, tena baada ya kuitwa na kupewa fursa ya kujitetea, Zitto ambaye kiutawala ni msaidizi wa Dk. Slaa alinukuliwa na vyombo vya habari akipinga uamuzi huo.

Akipinga uamuzi huo, Zitto alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (si Tanzania Daima), akisema maneno yafuatayo:

“Ninasikitika kuwa tunachukua maamuzi kama haya kipindi hiki ambacho nchi inahitaji chama imara cha upinzani.

“Kafulila ni mgombea mtarajiwa wa ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini ambalo CCM wamefanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuliko majimbo yote nchini. Uamuzi huu unaweza kuwashtua sana wanachama wetu Kigoma Kusini na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla.

“Kwangu mimi Kafulila ni kijana mahiri mwenye kukipenda chama chetu na ndiyo maana niliamua kumgroom (kumkuza) ili aje kuwa mgombea ubunge na baadaye mbunge katika Jimbo la Kigoma Kusini. Anakipenda chama chake, ana akili nyingi na mjuzi wa kujenga hoja katika kutetea chama bila woga.”

Kinachonifanya nisimwelewe Zitto ni kutoa kauli za moja kwa moja katika vyombo vya habari akipinga na kuonyesha kutoridhishwa na uamuzi wa kuondolewa Kafulila katika nafasi ya uofisa habari. Pengine ingelikuwa ni busara kwake kushauriana na viongozi wenzake kwanza juu ya mawazo yake, badala ya kulipuka kwenye vyombo vya habari akimtetea Kafulila aliyetenda kosa la dhahiri.

Kinachonishangaza ni kule kuona kuwa katika maneno yote aliyokaririwa, Zitto hajaonyesha kuguswa wala kushitushwa na utovu wa nidhamu ulionyeshwa na Kafulila kwa viongozi wa juu wa chama hicho wakiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake, Dk. Slaa.

Kitendo cha Zitto kupinga uamuzi huo, hakina tafsiri nyingine yoyote zaidi ya kubariki au kufumbia macho utovu wa nidhamu, eti kwa sababu tu Kafulila ana akili nyingi, anajua kujenga hoja na huenda akashinda Kigoma Kusini.

Kwa Zitto, kilicho muhimu kwake ni ubunge tu wa Kafulila na si nidhamu yake kwa chama.

Kwamba Kafulila ana akili nyingi sana na ni mjuzi wa kujenga hoja kama alivyosema Zitto, hilo si sehemu ya makala hii. Lakini sina hakika kama akili nyingi zisizokuwa na busara wala nidhamu ndizo ambazo mbunge anapaswa kuwa nazo na wala sijui kama hulka hiyo inaweza kumsaidia Kafulila katika harakati zake za kufanya kile alichokiita kuimarisha upinzani kupitia NCCR-Mageuzi.

Hiyo ni tafsida tu, harakati zenyewe ni za kutafuta ubunge Kigoma Kusini. Namshauri abadili tabia, awe mwaminifu na awe na msimamo mmoja tu wa kutafuta ubunge wake kwa haki na si kuutafuta kwa kuwachafua wengine kwa propaganda ili kujipatia umaarufu wa chee (cheap popularity). Kila la heri kamanda.

Ni hatari kuwa na upungufu wa wabunge wa upinzani, lakini ni hatari zaidi kuwa na maofisa wasio na nidhamu kwa chama wala kwa viongozi wa kitaifa wanaoheshimika na waliokijengea chama haiba njema hata kukubalika kwa Watanzania walio wengi.

Hivi kuna umuhimu gani kulinda utovu wa nidhamu wa ofisa wa chama, huku chama kizima kikiwa kimechafuliwa na ofisa huyo na kuvunjiwa heshima mbele ya umma wa Watanzania, kwa viongozi wake wakuu kudaiwa kufanya vikao ghetto?

Watanzania watakiungaje mkono chama ambacho viongozi wake wanafanya vikao vyao ghetto? Simuelewi Zitto Kabwe!

Pili, baada ya Kafulila kujivua uanachama wake na kujiunga na NCCR-Mageuzi, jana Zitto ameripotiwa na gazeti moja la kila siku (si Tanzania Daima) kwamba anamuunga mkono swahiba wake Kafulila kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya chama hicho (NCCR).

Kwa mujibu wa habari hiyo, kiongozi huyo wa CHADEMA ameamua kumuunga mkono Kafulila ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoka mikononi mwa CCM na kwenda upinzani.

Kwamba, Zitto ametoa ufadhili wa magari matatu kwa Kafulila wa NCCR-Mageuzi ili zimsaidie katika ziara ya jimboni kwake anayokusudia kuifanya hivi karibuni kwa lengo la kuwaeleza wanachama wa CHADEMA sababu za kujiondoa CHADEMA na hatima yake kisiasa.

Kwamba, Zitto anaamini Kafulila ndiye aliyejenga CHADEMA kama chama ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano na NCCR-Mageuzi katika maeneo ambayo chama hicho kina nguvu.

Kwamba, Zitto amekwisha kuweka bayana kuwa katika uchaguzi mkuu ujao upande wa jimbo hilo (Kigoma Kusini) anamuunga mkono Kafulila kwa kuwa anaamini atashinda na kuimarisha upinzani.

Naye Kafulila alipoulizwa (kwa mujibu wa habari hiyo) kuhusiana na ufadhili huo, alisema:

“Mimi na Zitto ni marafiki wa siku nyingi, tayari nimezungumza naye na amekubali kunisaidia kama rafiki yake wala sijakodisha. Amenipa magari yake kwa ajili ya usafiri kwa sababu nitaondoka na watu wangu huku Dar kwenda Kigoma”.

Habari hiyo sawa na ile iliyomkariri Zitto akipinga kuondolewa kwa Kafulila katika uofisa habari, hadi namaliza kuandika makala hii ilikuwa bado haijakanushwa. Jitihada zangu za kumpata Zitto kuthibitisha ufadhili wake kwa Kafulila na NCCR-Mageuzi hazikufanikiwa, kwani simu yake anayotumia huko Ujerumani ilikoelezwa kuwa yu masomoni, iliita bila kupokewa.

Hata hivyo, tukizingatia kile alichokisema Kafulila kuwa alimuomba Zitto na kukubali kumfadhili magari hayo, na tukitilia maanani kumbukumbu za Zitto kumtetea Kafulila mara kadhaa hata pale anapofanya makosa kama ya utovu wa nidhamu, basi nashawishika kuipa uzito habari hiyo, huku nikimshangaa Zitto kama ifuatavyo:

Ninamshangaa kwa kumfadhili kada wa chama kingine cha siasa (NCCR-Mageuzi), ambaye tangu ajitoe CHADEMA amekuwa akifanya kazi ya kukichafua chama hicho cha Zitto kwa propaganda za uongo na siasa za maji taka, kwa lengo la kujijengea umaarufu.

Hoja yake ya kumsaidia Kafulila ashinde ubunge ili kuimarisha upinzani inanishangaza. Ni kweli tunahitaji upinzani imara bungeni, lakini hatuwezi kuimarisha upinzani bila kuimarisha kwanza vyama na kuvilinda visiporomoke. Siasa zetu ni siasa za vyama, wabunge wote wa kuchaguliwa hutokana na vyama.

Kwa mantiki hiyo, si busara kuupa kipaumbele ubunge wa Kafulila bila kujali kuwa kijana huyo anaichafua CHADEMA, tena kwa maelezo ya uongo.

Hivi Zitto kwa nafasi yake kama Naibu Katibu Mkuu, atakuwa ameimarisha vipi upinzani kwa kumfadhili Kafulila na harakati zake za kujiongezea umaarufu kwa kuichafua CHADEMA? Kafulila ni mtu au kwa maneno ya Dk. Slaa ni sisimizi tu. CHADEMA ni chama.

Tunapozungumzia ubunge, Kafulila akishinda atakuwa ameshinda yeye tu kama Kafulila lakini tunapozungumzia hadhi na mwelekeo wa CHADEMA kama chama, watu wengi zaidi wanaweza kupata ubunge kupitia chama hicho.

Kwa mantiki hiyo, hatua ya Zitto kumsaidia Kafulila katika kuendeleza jitihada zake za kuichafua CHADEMA (safari hii huko Kigoma), haiwezi kuimarisha upinzani nchini kwani kijana huyo anachojali yeye ni kupata ubunge tu hata kama ni kwa kuichafua CHADEMA na viongozi wake, chama ambacho kina uwezo wa kutoa wabunge wengi zaidi kwa maslahi ya taifa.

Kumbe Zitto anaimarisha upinzani kupitia kwa mtu anayebomoa upinzani. Vituko vitupu.

Zitto ana marafiki wengi sana, hata mimi ni mmojawapo. Sina tatizo na urafiki wa Zitto na Kafulila wala mapenzi yao ya kupeana magari matatu.

Ni marafiki wema, wanaonekana kufaana wakati wa dhiki na faraja – wabarikiwe. Lakini kuna urafiki na kazi. Katika ofisi mbalimbali wafanyakazi wa ofisi husika wamekuwa wakikatazwa kuchanganya kazi na urafiki. Urafiki kazini ni sumu. Tukio la Zitto kumfadhili Kafulila na chama chake cha NCCR-Mageuzi ni tukio la kisiasa, linawahusu wanasiasa.

Linahusu kazi ya siasa na lina taathira (impact) ya kisiasa, iwe hasi au chanya.

Zitto kama Naibu Katibu Mkuu, kazi yake ni siasa na ofisi yake ni CHADEMA. Ana wajibu wa kulinda hadhi na mwelekeo wa ofisi yake hiyo.

Hapaswi kushiriki kuichafua wala kuwasaidia wengine waichafue au waidhohofishe.

Anapaswa kuipenda wakati wote na pale penye matatizo anapaswa kushiriki kuyatatua. Wakati mwingine ni busara zaidi kuhama ofisi yako kama imekuchosha kupindukia, kuliko kuichafua au kusaidia walioko nje waichafue kama anavyofanya Kafulila.

Kwamba Kafulila ameichafua CHADEMA, hilo ni suala lililo dhahiri. Amezungumzia ufujaji wa fedha za ruzuku aliodai unafanywa na Mbowe, amezungumzia ukabila na udikteta ndani ya CHADEMA. Hana jipya.

Kimsingi, yaliyosemwa na Kafulila juu ya CHADEMA ni yale yale yaliyokuwa yakisemwa na marehemu Chacha Zakayo Wangwe na kukuzwa sana na baadhi ya vyombo vyenye shauku ya kuona upinzani unakufa kwa masilahi ya mafisadi.

Madai hayo, Kafulila kwa nafasi aliyokuwa nayo kama ofisa habari alishiriki moja kwa moja kuyakanusha na kuonyesha ukweli halisi ulivyo.

Kama ni kujivua uanachama kwa sababu hizo, basi ningemwelewa kama angejivua wakati huo, vinginevyo yote anayoropoka sasa ni maneno ya mkosaji tu – hayawezi kuizuia CHADEMA kunywa maji.

Mathalani, Kafulila na mwenzake Danda Juju aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Bunge na Halmashauri kabla naye kujivua uanachama, wanaudanganya umma wa Watanzania kwamba Mbowe ndiye mtu pekee ndani ya CHADEMA anayetia saini kuidhinisha utoaji wa fedha za chama hicho kutoka benki.

Jibu la nani au kina nani wanaidhinisha matumizi ya fedha za chama hicho, limo pia kwenye katiba ya chama hicho.

Kwa bahati nzuri, Mbowe pia amekwisha kulitolea ufafanuzi mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama hicho, ni watu wanne ndio wanaohusika na utiaji saini, ambao ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho.

Kwa ufafanuzi huo wa Mbowe kama unavyojibainisha dhahiri katika kanuni na taratibu za chama hicho, ni vema ikazingatiwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA anaweza kuwa mtu yeyote, si lazima Mbowe – angeweza kuwa hata Kafulila (kama angewafaa).

“Wanasiasa wetu wanakosa hoja ya msingi katika suala hili. Hakuna ofisa hata mmoja wa CHADEMA wala Mbowe ambaye anasaini fedha peke yake, na huu ni utaratibu wa tangu chama kinaanzishwa, kwa hiyo hizi naweza kuziita ni fitna za kisiasa ambazo tunaelekea kuzizoea,” alisema Mbowe wakati akitoa ufafanuzi huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa upande mwingine, wakati Zitto Kabwe akiifadhili NCCR-Mageuzi kupitia kwa Kafulila, kumbukumbu zinaonyesha kuwa ushirikiano wa vyama vikuu vinne vya upinzani, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP na CUF ulishavunjika.

Ahsante kwa Zitto kama ameamua kuufufua ushirikiano huo lakini simuelewi pale anapoufufua uhusiano huo kupitia kwa Kafulila anayefanya kazi ya kuichafua CHADEMA kwa manufaa yake binafsi (umaarufu +ubunge).

Kafulila amejivua uanachama CHADEMA kitoto, alijiona hawezi kusimama dede bila kukichafua chama hicho maana bado anatambaa kisiasa.

Angehama kama Lwakatare alivyohama CUF ningemwona amekomaa katika kutumia haki ya kikatiba ya kuwa katika chama chochote cha siasa anachotaka. Lwakatare alihama CUF kwa ustaarabu, Kafulila amehama CHADEMA kwa matusi na kashfa (pima ukomavu wake mwenyewe).

Nasisitiza tena simwelewi Zitto Kabwe anayefadhili matusi na kashfa za Kafulila dhidi ya CHADEMA. Kwa sababu hiyo, namtaka atoe ufafanuzi haraka iwezekanavyo kuhusu kauli na misimamo yake hiyo, kabla sijaijadili mingine.

Anayemwelewa Zitto anisaidie. Tukutane Jumatano ijayo.
 
Maadam umeshasema humwelewi sidhani kama utakuja kumwelewa Zitto. Alosema ni mawazo yake ambayo binafsi ningechukia kama asingeyaweka wazi..Ni kazi yenu kutafakari maelezo ya Zitto na kutazama njia zipi zifanyike mkizingatia maneno hayo.

Ikiwa kweli Chadema wamefanya vizuri ktk jimbo la Kafulila na kuna madai hayo inabidi myatazame kwanza kabla ya kufikiria vinginevyo. Kama kuna Ukweli basi zitafutwe mbinu za kurejesha imani ya wananchi. Mbinu kama zile zilizofanyika Tarime baada ya kifo cha Wangwe na uchaguzi ulofuatia kwani pasipo kuzingatia maneno yaliyofuatia baada ya kifo chake, Chadema wangelipoteza jimbo hilo pia..

Ukweli usemwe daima hata kama unauma, ndio kujifunza na kukubali makosa hata kama yalikuwa muhimu kufanyika na ndio Demokrasia inavyotakiwa.

Hata mimi ukiniuliza nitakwambia kwamba kuna makosa yamefanyika pamoja na kwamba uamuzi huo ulikuwa muhimu sana ktk kukijenga chama lakini makosa haya yanaweza rekebishwa na sii kuamini tu kwamba Zitto is damn wrong..na Chadema watashinda uchaguzi ujao Kigoma pasipo Zitto ama Kafulila.
 
Hili ndo tatizo la watanzania kuamini kuwa siasa zenu ni watu na si system, linapotokea tatizo mnaanza kujadili watu na si mfumo uliozaa,kulea na kukuza watu wenyewe...ndo mana leo watanzani wanashindwa kujiletea mabadiliko kwa hiari zao kwa mazowea tu ya watu kuwapo madarakani na system kwao si tatizo, kwa hiyo, si mh. zitto tu wanasiasa wengi wa tanzania hawataeleweka.
 
Edward Kinabo

Kama si wote, basi wengi wenu mnamfahamu Zitto. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho.

Nikiri kuwa mimi ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa kijana huyu. Mbali ya kuwa kijana mwezangu na mwanaharakati mwenzangu, nimekuwa nikiguswa na uwezo wake wa kujenga hoja pamoja na misimamo yake katika baadhi ya masuala ya kitaifa, kabla na baada ya kuwa mbunge. Kama Watanzania wengine wengi, nami nilisisimka sana, pale aliposimamia ile hoja ya mgodi wa Buzwagi iliyompatia umaarufu baada ya kusimamishwa ubunge.

Kwa nafasi yake kama kiongozi wa juu wa moja ya vyama vikubwa vya upinzani nchini (CHADEMA), nimekuwa nikiitazama karama yake ya kisiasa, kama nyenzo ya kukiimarisha chama chake, ili kuwapatia Watanzania chama imara kabisa cha upinzani, kinachoweza kuwatetea na kuwapigania dhidi ya ufisadi na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, kwa umri wake kama kijana (33), nimekuwa nikimuona Zitto kama mfano wa kuigwa (role model) na vijana wenzake, katika kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya kisiasa, si tu kwa kugombea ubunge kama yeye (Zitto), lakini pia kwa kushiriki kujiandikisha, kupiga kura na kuzilinda kura hizo, ili kujipatia viongozi bora wanaoweza kutatua matatizo yaliyopo kwa haraka, likiwamo lile tatizo maarufu la vijana - ukosefu wa ajira.

Hata hivyo, ndani ya kipindi cha miaka miwili hivi au zaidi, nimekuwa nikishindwa kuielewa baadhi ya misimamo inayotolewa na mwanasiasa huyo, hususan ile inayotofautiana kabisa na kauli za viongozi wenzake pamoja na mwelekeo wa chama hicho, ambacho pasipo shaka yoyote ninakijua vema. Leo nitagusia machache.

Matukio ya hivi karibuni ya aliyekuwa kada wa CHADEMA, David Kafulila, kuondolewa katika nafasi ya uofisa habari wa chama hicho na baadaye kujivua uanachama wake na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi, pasipo kutarajia, yamenifanya nishindwe kumuelewa Zitto. Ndiyo, simwelewi Zitto Kabwe!

Ni matukio yanayomhusu Kafulila, lakini nimeshindwa kumwelewa Zitto, kwa kutilia maanani yafuatayo:

Kwanza, izingatiwe kuwa Kafulila aliondolewa katika nafasi hiyo kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Utovu wa nidhamu wa Kafulila ulijionyesha dhahiri katika vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti, pale alipokiita kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na wakurugenzi kilichoketi Dodoma mwezi uliopita, kwamba si kikao rasmi, hakitambuliki kikatiba - ni kikao cha ghetto. Ghetto kumezoeleka kuwa ni makazi ya vijana wasio na hulka njema – ni pango la wahuni.
Kukiita kikao cha viongozi wa juu wa chama kuwa ni kikao cha ghetto, hakuhitaji digrii kujua kuwa huo ni utovu wa nidhamu.

Mbali na utovu huo wa nidhamu, Kafulila pia hakuwa mkweli alipodai kuwa kikao kile hakikuwa rasmi. Kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa CHADEMA, kama zilivyobainishwa katika Katiba ya chama hicho toleo la mwaka 2006, viongozi wa sekretariati ya chama hicho wana uhuru wa kukutana kila inapobidi, iwe ni kwa utaratibu wa kawaida, kwa mahitaji au kwa dharura.

Wakati Kafulila akiwa ameondolewa katika nafasi hiyo na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kwa sababu ya utovu wa nidhamu ulio dhahiri, tena baada ya kuitwa na kupewa fursa ya kujitetea, Zitto ambaye kiutawala ni msaidizi wa Dk. Slaa alinukuliwa na vyombo vya habari akipinga uamuzi huo.

Akipinga uamuzi huo, Zitto alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (si Tanzania Daima), akisema maneno yafuatayo:
"Ninasikitika kuwa tunachukua maamuzi kama haya kipindi hiki ambacho nchi inahitaji chama imara cha upinzani.

"Kafulila ni mgombea mtarajiwa wa ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini ambalo CCM wamefanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuliko majimbo yote nchini. Uamuzi huu unaweza kuwashtua sana wanachama wetu Kigoma Kusini na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla.

"
Kwangu mimi Kafulila ni kijana mahiri mwenye kukipenda chama chetu na ndiyo maana niliamua kumgroom (kumkuza) ili aje kuwa mgombea ubunge na baadaye mbunge katika Jimbo la Kigoma Kusini. Anakipenda chama chake, ana akili nyingi na mjuzi wa kujenga hoja katika kutetea chama bila woga."

Kinachonifanya nisimwelewe Zitto ni kutoa kauli za moja kwa moja katika vyombo vya habari akipinga na kuonyesha kutoridhishwa na uamuzi wa kuondolewa Kafulila katika nafasi ya uofisa habari. Pengine ingelikuwa ni busara kwake kushauriana na viongozi wenzake kwanza juu ya mawazo yake, badala ya kulipuka kwenye vyombo vya habari akimtetea Kafulila aliyetenda kosa la dhahiri.

......

Kwamba Kafulila ana akili nyingi sana na ni mjuzi wa kujenga hoja kama alivyosema Zitto, hilo si sehemu ya makala hii. Lakini sina hakika kama akili nyingi zisizokuwa na busara wala nidhamu ndizo ambazo mbunge anapaswa kuwa nazo na wala sijui kama hulka hiyo inaweza kumsaidia Kafulila katika harakati zake za kufanya kile alichokiita kuimarisha upinzani kupitia NCCR-Mageuzi.

Hiyo ni tafsida tu, harakati zenyewe ni za kutafuta ubunge Kigoma Kusini. Namshauri abadili tabia, awe mwaminifu na awe na msimamo mmoja tu wa kutafuta ubunge wake kwa haki na si kuutafuta kwa kuwachafua wengine kwa propaganda ili kujipatia umaarufu wa chee (cheap popularity). Kila la heri kamanda.

Ni hatari kuwa na upungufu wa wabunge wa upinzani, lakini ni hatari zaidi kuwa na maofisa wasio na nidhamu kwa chama wala kwa viongozi wa kitaifa wanaoheshimika na waliokijengea chama haiba njema hata kukubalika kwa Watanzania walio wengi.

Hivi kuna umuhimu gani kulinda utovu wa nidhamu wa ofisa wa chama, huku chama kizima kikiwa kimechafuliwa na ofisa huyo na kuvunjiwa heshima mbele ya umma wa Watanzania, kwa viongozi wake wakuu kudaiwa kufanya vikao ghetto?

Watanzania watakiungaje mkono chama ambacho viongozi wake wanafanya vikao vyao ghetto? Simuelewi Zitto Kabwe!
Pili, baada ya Kafulila kujivua uanachama wake na kujiunga na NCCR-Mageuzi, jana Zitto ameripotiwa na gazeti moja la kila siku (si Tanzania Daima) kwamba anamuunga mkono swahiba wake Kafulila kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya chama hicho (NCCR).

Kwa mujibu wa habari hiyo, kiongozi huyo wa CHADEMA ameamua kumuunga mkono Kafulila ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoka mikononi mwa CCM na kwenda upinzani.

Kwamba, Zitto ametoa ufadhili wa magari matatu kwa Kafulila wa NCCR-Mageuzi ili zimsaidie katika ziara ya jimboni kwake anayokusudia kuifanya hivi karibuni kwa lengo la kuwaeleza wanachama wa CHADEMA sababu za kujiondoa CHADEMA na hatima yake kisiasa.

Kwamba, Zitto anaamini Kafulila ndiye aliyejenga CHADEMA kama chama ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano na NCCR-Mageuzi katika maeneo ambayo chama hicho kina nguvu.
Kwamba, Zitto amekwisha kuweka bayana kuwa katika uchaguzi mkuu ujao upande wa jimbo hilo (Kigoma Kusini) anamuunga mkono Kafulila kwa kuwa anaamini atashinda na kuimarisha upinzani.

Naye Kafulila alipoulizwa (kwa mujibu wa habari hiyo) kuhusiana na ufadhili huo, alisema:

"Mimi na Zitto ni marafiki wa siku nyingi, tayari nimezungumza naye na amekubali kunisaidia kama rafiki yake wala sijakodisha. Amenipa magari yake kwa ajili ya usafiri kwa sababu nitaondoka na watu wangu huku Dar kwenda Kigoma".

Habari hiyo sawa na ile iliyomkariri Zitto akipinga kuondolewa kwa Kafulila katika uofisa habari, hadi namaliza kuandika makala hii ilikuwa bado haijakanushwa. Jitihada zangu za kumpata Zitto kuthibitisha ufadhili wake kwa Kafulila na NCCR-Mageuzi hazikufanikiwa, kwani simu yake anayotumia huko Ujerumani ilikoelezwa kuwa yu masomoni, iliita bila kupokewa.

Hata hivyo, tukizingatia kile alichokisema Kafulila kuwa alimuomba Zitto na kukubali kumfadhili magari hayo, na tukitilia maanani kumbukumbu za Zitto kumtetea Kafulila mara kadhaa hata pale anapofanya makosa kama ya utovu wa nidhamu, basi nashawishika kuipa uzito habari hiyo, huku nikimshangaa Zitto kama ifuatavyo:

Ninamshangaa kwa kumfadhili kada wa chama kingine cha siasa (NCCR-Mageuzi), ambaye tangu ajitoe CHADEMA amekuwa akifanya kazi ya kukichafua chama hicho cha Zitto kwa propaganda za uongo na siasa za maji taka, kwa lengo la kujijengea umaarufu.

Hoja yake ya kumsaidia Kafulila ashinde ubunge ili kuimarisha upinzani inanishangaza. Ni kweli tunahitaji upinzani imara bungeni, lakini hatuwezi kuimarisha upinzani bila kuimarisha kwanza vyama na kuvilinda visiporomoke. Siasa zetu ni siasa za vyama, wabunge wote wa kuchaguliwa hutokana na vyama.

Kwa mantiki hiyo, si busara kuupa kipaumbele ubunge wa Kafulila bila kujali kuwa kijana huyo anaichafua CHADEMA, tena kwa maelezo ya uongo.

Hivi Zitto kwa nafasi yake kama Naibu Katibu Mkuu, atakuwa ameimarisha vipi upinzani kwa kumfadhili Kafulila na harakati zake za kujiongezea umaarufu kwa kuichafua CHADEMA? Kafulila ni mtu au kwa maneno ya Dk. Slaa ni sisimizi tu. CHADEMA ni chama.

Tunapozungumzia ubunge, Kafulila akishinda atakuwa ameshinda yeye tu kama Kafulila lakini tunapozungumzia hadhi na mwelekeo wa CHADEMA kama chama, watu wengi zaidi wanaweza kupata ubunge kupitia chama hicho.

Kwa mantiki hiyo, hatua ya Zitto kumsaidia Kafulila katika kuendeleza jitihada zake za kuichafua CHADEMA (safari hii huko Kigoma), haiwezi kuimarisha upinzani nchini kwani kijana huyo anachojali yeye ni kupata ubunge tu hata kama ni kwa kuichafua CHADEMA na viongozi wake, chama ambacho kina uwezo wa kutoa wabunge wengi zaidi kwa maslahi ya taifa.

Kumbe Zitto anaimarisha upinzani kupitia kwa mtu anayebomoa upinzani. Vituko vitupu.

Zitto ana marafiki wengi sana, hata mimi ni mmojawapo. Sina tatizo na urafiki wa Zitto na Kafulila wala mapenzi yao ya kupeana magari matatu.

Ni marafiki wema, wanaonekana kufaana wakati wa dhiki na faraja – wabarikiwe. Lakini kuna urafiki na kazi. Katika ofisi mbalimbali wafanyakazi wa ofisi husika wamekuwa wakikatazwa kuchanganya kazi na urafiki. Urafiki kazini ni sumu. Tukio la Zitto kumfadhili Kafulila na chama chake cha NCCR-Mageuzi ni tukio la kisiasa, linawahusu wanasiasa.
Linahusu kazi ya siasa na lina taathira (impact) ya kisiasa, iwe hasi au chanya.

Zitto kama Naibu Katibu Mkuu, kazi yake ni siasa na ofisi yake ni CHADEMA. Ana wajibu wa kulinda hadhi na mwelekeo wa ofisi yake hiyo.

Hapaswi kushiriki kuichafua wala kuwasaidia wengine waichafue au waidhohofishe.

Anapaswa kuipenda wakati wote na pale penye matatizo anapaswa kushiriki kuyatatua. Wakati mwingine ni busara zaidi kuhama ofisi yako kama imekuchosha kupindukia, kuliko kuichafua au kusaidia walioko nje waichafue kama anavyofanya Kafulila.

Kwamba Kafulila ameichafua CHADEMA, hilo ni suala lililo dhahiri. Amezungumzia ufujaji wa fedha za ruzuku aliodai unafanywa na Mbowe, amezungumziaukabilana udikteta ndani ya CHADEMA. Hana jipya.

Kimsingi, yaliyosemwa na Kafulila juu ya CHADEMA ni yale yale yaliyokuwa yakisemwa na marehemu Chacha Zakayo Wangwe na kukuzwa sana na baadhi ya vyombo vyenye shauku ya kuona upinzani unakufa kwa masilahi ya mafisadi.

Madai hayo, Kafulila kwa nafasi aliyokuwa nayo kama ofisa habari alishiriki moja kwa moja kuyakanusha na kuonyesha ukweli halisi ulivyo.

Kama ni kujivua uanachama kwa sababu hizo, basi ningemwelewa kama angejivua wakati huo, vinginevyo yote anayoropoka sasa ni maneno ya mkosaji tu – hayawezi kuizuia CHADEMA kunywa maji.

Mathalani, Kafulila na mwenzake Danda Juju aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Bunge na Halmashauri kabla naye kujivua uanachama, wanaudanganya umma wa Watanzania kwamba Mbowe ndiye mtu pekee ndani ya CHADEMA anayetia saini kuidhinisha utoaji wa fedha za chama hicho kutoka benki.

Jibu la nani au kina nani wanaidhinisha matumizi ya fedha za chama hicho, limo pia kwenye katiba ya chama hicho.

Kwa bahati nzuri, Mbowe pia amekwisha kulitolea ufafanuzi mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama hicho, ni watu wanne ndio wanaohusika na utiaji saini, ambao ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho.

Kwa ufafanuzi huo wa Mbowe kama unavyojibainisha dhahiri katika kanuni na taratibu za chama hicho, ni vema ikazingatiwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA anaweza kuwa mtu yeyote, si lazima Mbowe – angeweza kuwa hata Kafulila (kama angewafaa).

"Wanasiasa wetu wanakosa hoja ya msingi katika suala hili. Hakuna ofisa hata mmoja wa CHADEMA wala Mbowe ambaye anasaini fedha peke yake, na huu ni utaratibu wa tangu chama kinaanzishwa, kwa hiyo hizi naweza kuziita ni fitna za kisiasa ambazo tunaelekea kuzizoea," alisema Mbowe wakati akitoa ufafanuzi huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa upande mwingine, wakati Zitto Kabwe akiifadhili NCCR-Mageuzi kupitia kwa Kafulila, kumbukumbu zinaonyesha kuwa ushirikiano wa vyama vikuu vinne vya upinzani, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP na CUF ulishavunjika.

Ahsante kwa Zitto kama ameamua kuufufua ushirikiano huo lakini simuelewi pale anapoufufua uhusiano huo kupitia kwa Kafulila anayefanya kazi ya kuichafua CHADEMA kwa manufaa yake binafsi (umaarufu +ubunge).

Kafulila amejivua uanachama CHADEMA kitoto, alijiona hawezi kusimama dede bila kukichafua chama hicho maana bado anatambaa kisiasa.

Angehama kama Lwakatare alivyohama CUF ningemwona amekomaa katika kutumia haki ya kikatiba ya kuwa katika chama chochote cha siasa anachotaka.

Lwakatare alihama CUF kwa ustaarabu, Kafulila amehama CHADEMA kwa matusi na kashfa (pima ukomavu wake mwenyewe).

Nasisitiza tena simwelewi Zitto Kabwe anayefadhili matusi na kashfa za Kafulila dhidi ya CHADEMA. Kwa sababu hiyo, namtaka atoe ufafanuzi haraka iwezekanavyo kuhusu kauli na misimamo yake hiyo, kabla sijaijadili mingine. Anayemwelewa Zitto anisaidie. Tukutane Jumatano ijayo.

Mwandishi wa makala hii ni mchagga aliyeajiriwa kwa kigezo cha ukabila akiwa yeye na TEMBA.

AJIRA ZAO ZILILALAMIKIWA SANA NA WAFANYAKAZI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA AMBAO SIO WACHAGGA WENGINE WANA MIAKA MINNE WAKIWA VIBARUA TU.

PILI MWANDISHI UCHWARA HUYU ANAANDIKA KAMA MSEMAJI WA CHADEMA NA SI MWAJIRIWA WA MBOWE.

ANATOLEA MAELEZO UTIAJIA SAINI HUNDI WA MBOWE WAKATI MTU WA KUTOA JIBU HILO NI SLAA KWANI MBOWE HAWEZI KUSEMA UKWELI.

WEWE KINABO KIJANA WA KICHAGGA UNATETEA CHAKULA CHAKO HUNA KITU.

MCHAGGA KINABO NI MUONGO NA MZANDIKI LWAKATARE AMEHAMA KWA KUIKIASHIFU CUF KIASI CHA KUTUMA CONFIDENTIALS DOCUMENTS ZA CUF HUMU JF,NA AKASEMA ANATUNGA KITABU KUWASHTUMU CUF.

AIDHA UNAPOSEMA KUWA ZITTO AJIBU HARAKA KABLA HUJATOA MAKALA NYINGINE KWANI WEWE NI NANI?YAANI ZITTO AWAJIBIKE KWAKO WEWE KIBARUA WA MBOWE? BOSI WAKO MWENYEWE HAMUWEZI ZITTO UTAWEZA WEWE RIPOTA?

MWANDISHI AMBAYE MAANDIKO YAKO YAMEJAA MAKOSA KILA NUKTA.

KAFULILAH NA DUNDU WALIKUWA VIONGOZI WA CHADEMA ,WEWE NI KIBARUA TU LAZIMA SISI TUWAAMINI HAO KULIKO WEWE NDUGU WA MBOWE.

MWISHO WAMESHINDWA NA WAMELEGEA WENZAO KAANZA MHARIRI WAKO MTENDAJI KIBANDA,KAJA NGURUMO,AKAJA MCHAGGA MWINGINE,AKAJA KWAYU WA IPP NA SASA UMEKUJA WEWE, NYOTE KUMMALIZA ZITTO KABWE HAMUWEZI.ZITTO NI ZAIDI YA TAASISI.
 
Maadam umeshasema humwelewi sidhani kama utakuja kumwelewa Zitto. Alosema ni mawazo yake ambayo binafsi ningechukia kama asingeyaweka wazi..Ni kazi yenu kutafakari maelezo ya Zitto na kutazama njia zipi zifanyike mkizingatia maneno hayo.

Ikiwa kweli Chadema wamefanya vizuri ktk jimbo la Kafulila na kuna madai hayo inabidi myatazame kwanza kabla ya kufikiria vinginevyo. Kama kuna Ukweli basi zitafutwe mbinu za kurejesha imani ya wananchi. Mbinu kama zile zilizofanyika Tarime baada ya kifo cha Wangwe na uchaguzi ulofuatia kwani pasipo kuzingatia maneno yaliyofuatia baada ya kifo chake, Chadema wangelipoteza jimbo hilo pia..

Ukweli usemwe daima hata kama unauma, ndio kujifunza na kukubali makosa hata kama yalikuwa muhimu kufanyika na ndio Demokrasia inavyotakiwa.

Hata mimi ukiniuliza nitakwambia kwamba kuna makosa yamefanyika pamoja na kwamba uamuzi huo ulikuwa muhimu sana ktk kukijenga chama lakini makosa haya yanaweza rekebishwa na sii kuamini tu kwamba Zitto is damn wrong..na Chadema watashinda uchaguzi ujao Kigoma pasipo Zitto ama Kafulila.

Ni kweli kabisa. Nadhani sasa tuingie kiundani tujue nguvu ya CHADEMA Kigoma Kusini chanzo chake ni nini? Ni mtu au ni chama? tukishajua haya tutajua kwamba kuondoka kwa Kafulila ni pigo kwa CHADEMA ama kwake mwenyewe!.

Ngoja nitafute viongozi wa CHADEMA Kigoma wataweza kutuma facts halisi badala ya propaganda za Mwananchi ambazo zinatamkwa na Kafulila mwenyewe. Najua mihimili ya siasa za Kigoma ndani ya CHADEMA ni Zitto Kabwe, Mzee mmoja ainatwa Kasisiko, meya wa kule anaitwa Shaban Mambo, na Mama Shida Salum. Mwenye kuweza kuwapata hawa awaulize maswali ya kina tujadili hali ya mambo huko!

Asha
 
Mwandishi wa makala hii ni mchagga aliyeajiriwa kwa kigezo cha ukabila akiwa yeye na TEMBA.

AJIRA ZAO ZILILALAMIKIWA SANA NA WAFANYAKAZI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA AMBAO SIO WACHAGGA WENGINE WANA MIAKA MINNE WAKIWA VIBARUA TU.

PILI MWANDISHI UCHWARA HUYU ANAANDIKA KAMA MSEMAJI WA CHADEMA NA SI MWAJIRIWA WA MBOWE.

ANATOLEA MAELEZO UTIAJIA SAINI HUNDI WA MBOWE WAKATI MTU WA KUTOA JIBU HILO NI SLAA KWANI MBOWE HAWEZI KUSEMA UKWELI.

WEWE KINABO KIJANA WA KICHAGGA UNATETEA CHAKULA CHAKO HUNA KITU.

MCHAGGA KINABO NI MUONGO NA MZANDIKI LWAKATARE AMEHAMA KWA KUIKIASHIFU CUF KIASI CHA KUTUMA CONFIDENTIALS DOCUMENTS ZA CUF HUMU JF,NA AKASEMA ANATUNGA KITABU KUWASHTUMU CUF.

AIDHA UNAPOSEMA KUWA ZITTO AJIBU HARAKA KABLA HUJATOA MAKALA NYINGINE KWANI WEWE NI NANI?YAANI ZITTO AWAJIBIKE KWAKO WEWE KIBARUA WA MBOWE? BOSI WAKO MWENYEWE HAMUWEZI ZITTO UTAWEZA WEWE RIPOTA?

MWANDISHI AMBAYE MAANDIKO YAKO YAMEJAA MAKOSA KILA NUKTA.

KAFULILAH NA DUNDU WALIKUWA VIONGOZI WA CHADEMA ,WEWE NI KIBARUA TU LAZIMA SISI TUWAAMINI HAO KULIKO WEWE NDUGU WA MBOWE.

MWISHO WAMESHINDWA NA WAMELEGEA WENZAO KAANZA MHARIRI WAKO MTENDAJI KIBANDA,KAJA NGURUMO,AKAJA MCHAGGA MWINGINE,AKAJA KWAYU WA IPP NA SASA UMEKUJA WEWE, NYOTE KUMMALIZA ZITTO KABWE HAMUWEZI.ZITTO NI ZAIDI YA TAASISI.
Kanda2,
Tatizo lako ni nini? Mwenye ukabila ni wewe. Badala ya kujadilia issues unajadilia messenger. Tafuta viatu.
 
Zitto ana hoja ya msingi ya kujibu hapa ili atuweke sana - ni kweli ametuchanganya kabisa huyu kiongozi

Tusubiri majibu yake.
 
Ni kweli kabisa. Nadhani sasa tuingie kiundani tujue nguvu ya CHADEMA Kigoma Kusini chanzo chake ni nini? Ni mtu au ni chama? tukishajua haya tutajua kwamba kuondoka kwa Kafulila ni pigo kwa CHADEMA ama kwake mwenyewe!.

Ngoja nitafute viongozi wa CHADEMA Kigoma wataweza kutuma facts halisi badala ya propaganda za Mwananchi ambazo zinatamkwa na Kafulila mwenyewe. Najua mihimili ya siasa za Kigoma ndani ya CHADEMA ni Zitto Kabwe, Mzee mmoja ainatwa Kasisiko, meya wa kule anaitwa Shaban Mambo, na Mama Shida Salum. Mwenye kuweza kuwapata hawa awaulize maswali ya kina tujadili hali ya mambo huko!

Asha

Kule ni chama na siyo Mtu, kama una kumbukumbu ya Dr Kaburu itakusaida kujua kule kuna watu wa aina gani - Chadema Kigoma si Zitto wala Kafulila wa NCCR. kajimaliza mwenyewe. nafikiri yu mbioni kurudi UVCCM
 
Zito ni mwanasiasa na pia ni philosopher,itakuchukua muda mrefu sana kumuelewa hasa kama uwezo wako wa kuelewa ni mdogo,Nakushauri mtoa hoja ukaacha kumjadili Zitto badala yake tujadili matatizo yetu ya msingi yanayotukabili Watanzania.
 
Mimi naona CHADEMA na huyo Mh ZITTO ni ngoma ivumayo sana .............

Ni vigumu sana kwa wanaCHADEMA ku admit matatizo yao. wanajifanya wamefumba macho na kusonga mbele. UKANDA, UKABILA na Dr Slaa ni sumu na mwiba mkali sana kwa ustawi wa Chadema.

Kumbukeni kuwa panapofuka moshi ...............
 
Zito ni mwanasiasa na pia ni philosopher,itakuchukua muda mrefu sana kumuelewa hasa kama uwezo wako wa kuelewa ni mdogo,Nakushauri mtoa hoja ukaacha kumjadili Zitto badala yake tujadili matatizo yetu ya msingi yanayotukabili Watanzania.

Hivi kweli Zitto ni philosopher? una uhakika na hilo? muulize mwenyewe Zitto kama yeye ni Philosopher.

Mimi ninavyojuwa Zitto ni mwanasiasa mchanga sana na anahitaji muda sana katika kupata uzoefu wa mikiki ya siasa.

Tukumbuke kuwa kuwa Mbunge sia lazima uwe mwanasiasa inawezekana watu tu walimpenda katika utendaji na uwajibikaji wake.

Sasa ni wakti muafaka kwa Zitto kutumia nafasi zake katika chama chake kujifunza siasa na mikiki yake. Asije akalewa sifa anazopewa na watu bali ajitahidi sana kufata nyendo za wakongwe wa siasa katika kujiimarisha.
 
there must be something very big behind the name zitto and the man called zitto, haiwezekani ukipita huku zitto,ukikaa kidogo tu humu zitto,ukiongelea chadema tu,zitto,
aaaaahhhhh the zitto kingdom
 
hivi kwa nini tusijadili namna ya kuwezesha kusonga mbele , wanaharakati wakaanzisha mjadala wa wagombea binafsi/huru haya yote hayatakuwepo manake tatizo hapa ni ulafi wa fedha na madaraka umaarufu kila mtu anataka ajiposition mahali akiisi anazidiwa anatafuta sababu watatupotozea muda zitoo chademaa kafulila kila siku jamni ?
 
there must be something very big behind the name zitto and the man called zitto, haiwezekani ukipita huku zitto,ukikaa kidogo tu humu zitto,ukiongelea chadema tu,zitto,
aaaaahhhhh the zitto kingdom

Zitto pole sana... naamini unapita katika kipindi kigumu sana. Una a very bright future kisiasa.. lakini mwenendo wa matukio ya hivi karibuni na kama utashindwa kuonyesha ukomavu wako kisiasa... huenda aliyosema Kabanda yakatimia... kama analiona anguko lako.

Waswahili walisema ngoma ikivuma saana hupasuka.. sikuombei mabaya ila kila ni kimkumbuka Bi Amina almarhuum na wengi ambao walivuma mno na wakazimika ghafla kisiasa... remember about Salum Msabaha yule Mbunge wa CUF Mkunazini na hekaya zake za kutekwa nyara..the listis endless sheikh.

Ushauri wangu..usikurupuke kujibu jibu...kaa kimya na ukitafakari if possible omba ushauri kwa watu wazoefu na siasa. Kwa mfano nimesikitishwa na majibu yako juu ya ile makala ya mahojiano kati ya Kubenea na mama yako na reaction kutoka kwa Kubenea mwenyewe.

Ikishindikana achana na Siasa na endelea na mambo yako mengine ya kitaaluma unaweza kuwasaidia watanzania hata bila kuwa mwanasiasa kama lengo lako ni hilo..

Kila lakheri mdogo wangu.

Kingwele.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom