Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Naona thread nyingi humu JF ni za zitto/chadema/wapinzani. Mimi naona kama kweli hivi vyama vya upinzani vina nia ya dhati ya kuikomboa nchi toka mikoni mwa mafisadi wa CCM, basi waache maliumbano yasiyo na tija. wakianza kufitiniana haitakwa shuluhisho la matatizo yao.
Naona hivi vyama vya upinzani wenyewe hawana umoja na hakuna anaye taka mwenzake afanikiwe kuichukua nchi.
Wajue wanavyolumbana, ndo neema kwa CCM, na itafanya juu chini hata kama ni ku support wapinzani ili wajimalize wenyewe.
 
Zitto yuko huru kutoa msaada wowote anaoona unafaa kwa Kafulila na urafiki wao hauwezi kutenguliwa na yeyote. lakini kwa mazingira aliyojenga Kafulila mwenyewe, sioni kama tamaa ya chama chake cha NCCR ya kushinda ubunge jimbo la Kigoma kusini itatimia. Na kwa takwimu za kuanzia uchaguzi mkuu wa 2005, CHADEMA na NCCR wote wanaonekana kuwa na nguvu jimboni humo. Kwa mazingira aliyojenga Kafulila, nani atamwachia mwenzake? Naona CCM wakilichukua jimbo kilaini!
 
Mbatia ukiona vyaelea vimeundwa! unda vyako pia.
Akija huko mkitofautiana hatutaki kusikia oooh zito mamluki, amekuja kutumaliza! kauli uliyoitoa leo itakuhukumu. Usikae chini kusubiri migogoro ikuletee wanachama makini....rudi kwenye historia ya chama chako ujifunze kitu fulani.

A woman can be strong, confident and sexy
 
umenena vyema kapwani anamuona mzuri kwa vile bado hajachanganyika nae na kuona mazuri na mabaya yake
 
Mbatia hajajifunza somo la kuporomoka kwa NCCR MAGEUZI, Mrema alipokelewa kama Mungu Mtu, kisha akakisambaratisha kwa faida ya Usalama wa Taifa na kwa maslahi binafsi.
leo anatamani mamluki wa KUTOKA VYAMA VINGINE, ameshidwa kuijenga NCCR Mageuzi , ameshidwa kuisisimua, anatamani ustawi wa CHADEMA, hajipi muda kujenga chama toka kwa wanachama waaminifu.
Anapaswa ajifunze toka CHADEMA, wamejenga Chama chao taratibu ila kwa uhakika.
kina Zito wamelelewa pale, NCCR IMESHIDWA kuwajenga kina Bahati Tweve kua vijana IMARA kisiasa.
Mbatia amekua kama Mchawi anaeua mtoto wa jirani yake wakati hamli nyama, Anadhani utawi wa NNCR unategemea udhaifu wa CHADEMA. Lazima aijenge NCCR kama chama cha siasa na si NGO yenye kutoa taarifa za utekelezaji pale Habari maelezo.
 
Mbatia alipelekwa nje kusoma na kugharimiwa na Rostam, Kuhusu Zitto kugharimiwa na Rostam, sina uhakika lakini ni kawaida kwa RA kumwagilia miche yote maana hana hakika na utakao chipua!! Lipumba, Mrema, Mtikila,Mbatia nk wote wako kwenye payroll yake.

Basi tumekwisha
 
Mbatia alipelekwa nje kusoma na kugharimiwa na Rostam, Kuhusu Zitto kugharimiwa na Rostam, sina uhakika lakini ni kawaida kwa RA kumwagilia miche yote maana hana hakika na utakao chipua!! Lipumba, Mrema, Mtikila,Mbatia nk wote wako kwenye payroll yake.[/QUOTE]

Kuna mmoja umemsahau hapa. Na mkiendelea na huu ujinga, uvumulivu una mwisho.....

omarilyas
 
mbatia alipelekwa nje kusoma na kugharimiwa na rostam, kuhusu zitto kugharimiwa na rostam, sina uhakika lakini ni kawaida kwa ra kumwagilia miche yote maana hana hakika na utakao chipua!! Lipumba, mrema, mtikila,mbatia nk wote wako kwenye payroll yake.

fisadi,mwongo mkubwa!
 
. Lazima aijenge NCCR kama chama cha siasa na si NGO yenye kutoa taarifa za utekelezaji pale Habari maelezo.
Na CHADEMA aijenge CHADEMA kama chama cha siasa na si Family Corporate Company. Bora kuwa kwenye NGO kuliko kwenye Family Private comapny au?
 
Mbatia hajajifunza somo la kuporomoka kwa NCCR MAGEUZI, Mrema alipokelewa kama Mungu Mtu, kisha akakisambaratisha kwa faida ya Usalama wa Taifa na kwa maslahi binafsi.
leo anatamani mamluki wa KUTOKA VYAMA VINGINE, ameshidwa kuijenga NCCR Mageuzi , ameshidwa kuisisimua, anatamani ustawi wa CHADEMA, hajipi muda kujenga chama toka kwa wanachama waaminifu.
Anapaswa ajifunze toka CHADEMA, wamejenga Chama chao taratibu ila kwa uhakika.
kina Zito wamelelewa pale, NCCR IMESHIDWA kuwajenga kina Bahati Tweve kua vijana IMARA kisiasa.
Mbatia amekua kama Mchawi anaeua mtoto wa jirani yake wakati hamli nyama, Anadhani utawi wa NNCR unategemea udhaifu wa CHADEMA. Lazima aijenge NCCR kama chama cha siasa na si NGO yenye kutoa taarifa za utekelezaji pale Habari maelezo.

Mnanikumbusha hadithi ya watu wawili waliotumbukia kwenye shimo, badala ya kusaidiana wakaanza kutambiana, wewe uko chini zaidi, mimi nina nafuu siko kwenye sakafu ya shimo. Mwenzake akamwambia, sote tuko shimoni, atakayetoka humu ndo kidume.
Nasema hivi, wapinzani nyote hamchekani!!
Atakayemg'oa CCM ndo atakuwa kidume. Concentrate on that mission comeon!
 
Mbatia anafilisika kimawazo. Wenzao ccm wameshawatuma kina Kilango wanamobilize wanawake mikoani kwa ajili ya uchaguzi ujao wewe umekua kama fisi kusubiri mkono udondoke!! Mbatia acha kuzurura ughaibuni nenda kajenge mtandao mikoani.

Zito atakisaidia nini NCCR hata mkipata hilo jimbo moja halafu mkaanza kutwangana mangumi.
 
Hivi hawa wanasiasa wanaingia tu kwenye chama mradi apate cheo au wanasoma katiba za vyama vyenyewe na sera zao na kuona kama zinaendana na imani zao kisiasa???

Kama NCCR na CHADEMA sera zao hazifanani basi mwogope kama ukoma anaehama kimojawapo kwenda kingine, ni opportunist tu huyo hana lolote kichwani la kusaidia taifa.
 
Nilikuwa fisadi zamani, ndiyo maana nawajua Mafisadi na njia zao. Huo ndio ukweli na unauma
 
Huyu Kafulila sijui Kafufuka inabidi awe makini sana tena mno mpaka hapa inaonyesha hana pesa za kuweza kushindana na hawa CCM ila kitendo cha kutokuwa na msimamo ndo kimemshishia hadhia awe makini sana anaweza jikuta mwakani anadondokea utosi hivi hivi asijitengenezee umaarufu wa kilaisi laisi kupitia kwa Zitto.
 
Zitto anakwenda, zitto anakwenda, zitto anakata chenga, zitto anachanja mbuga, zitto anamvisha kanzu beki yule, zitto sasa anaelekea golini, zitto hakamatiki, zitto anarudi nyuma, zitto anawalamba chenga mabeki wote, zitto huyoooo...

Mpira wa kizamani huo. Haichoshi masikioni?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom